JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Katika Ukusanyaji wa Taarifa/Data za Watu miongozo mbalimbali inapaswa kuzingatiwa ikiwemo kuwepo kwa Sheria ya #UlinziWaData

Mkusanyaji wa Data/Taarifa anapaswa kuzingatia Faragha/Usiri wa wenye Data na kutekeleza Ukusanyaji kwa njia iliyo halali

Ni vema Mkusanya Data awe na kusudi maalum na lengo la kuendeleza ukusanyaji huo

Soma - https://jamii.app/UkusanyajiData

#DataProtection #DigitalRights
MABADILIKO YA KANUNI: CHANELI ZA KULIPIA RUKSA KURUSHA MATUKIO MUBASHARA

Ili kuboresha Huduma ya Mawasiliano nchini, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imerekebisha baadhi ya kanuni za Leseni za mwaka 2018

Kuanzia sasa, chaneli za kulipia zitaruhusiwa kurusha matukio mubashara (Live Events). Mabadiliko haya ni katika kanuni ya 29. Awali, chaneli zilizorusha matukio mubashara zilikuwa chaneli zisizolipiwa tu

#JamiiForums #DigitalRights
ALGOPHOBIA: Ni hali ya kuwa na hofu kali/isiyo ya kawaida kuhusu Maumivu ya Kimwili (Mf. kuchomwa Sindano)

Mwenye #Algophobia anaweza kupata shambulio la hofu (Panic attacks) akiwaza kuhusu Maumivu. Dalili zinaweza kujumuisha: Kizunguzungu, kutokwa Jasho, Kutetemeka, kubanwa pumzi, Mapigo ya Moyo kuongezeka au Tumbo kuvurugika ghafla.

Soma - https://jamii.app/Algophobia

#JFMaarifa
DR CONGO: WAKIMBIZI ZAIDI YA 50 WAUAWA NA WAASI

Waasi wa CODECO walijipenyeza kambi ya Savo iliyopo Ngujona Mkoani Ituri na kuwaua kwa kuwashambulia kwa visu wakimbizi waliokuwa wanaishi hapo

Hii si mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kutokea

Soma - https://jamii.app/50Wauawa
MDAU: NAMNA ZA KUPATA 'CONNECTION' ZA AJIRA

Anashauri kutumia Mitandao kutangaza ujuzi, Kujitolea na kushiriki shughuli za kijamii

Anasema jipendekeze kwa watu au Kampuni fulani kwani 'kuwa chawa' kwenye vitu vya msingi si vibaya

Soma https://jamii.app/ConnectionTz

#StoriesOfChange #JFMdau
#AFCON2021: SENEGAL YAINGIA FAINALI

- #TeamSenegal imeingia fainali kwa kuifunga #TeamBurkinaFaso goli 3-1 ndani ya dakika 90

- Senegal itacheza fainali na mshindi wa mechi ya kesho kati ya #TeamCameroon na #TeamEgypt

- Burkina Faso itashindania nafasi ya 3 na timu itakayofungwa kesho

#JFSports
#COVID19: Kampuni ya #BioNTech pamoja na mshirika wake #Pfizer, wameomba kibali cha dharura Marekani, cha matumizi ya Chanjo ya Corona kwa Watoto chini ya miaka 5

Wakipata Kibali itakuwa Chanjo ya 1 kutumika kwa Watoto kuanzia Miezi sita

Soma - https://jamii.app/BioNtechInfants

#UVIKO3 #JFAfya
ARUSHA: Mlinzi wa Shule ya Winnings Spirit iliyopo Terati, Issa Dinaiah (57) amechinjwa. Waliotekeleza mauaji hayo wamechukua kichwa chake

Mwili wa Mlinzi huyo uligundulika Februari 2, 2022. Chanzo na waliofanya tukio hilo hawajajulikana

Soma - https://jamii.app/MlinziAuawa

#JFMatukio
TBS: KUWEKA BIDHAA ZA VYAKULA JUANI KUNAHARIBU UBORA

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa tahadhari kwa Wafanyabiashara wa bidhaa za Chakula ikiwemo Mafuta ya Kula kuweka Juani ili Wateja wazione

Yasema ktk uchunguzi wamebaini hali hiyo inaweza kuhatarisha Afya ya Walaji kwa kuharibu ubora wa bidhaa hata kama haijafikisha muda wake wa matumizi kuisha (Expire date)

Soma - https://jamii.app/VyakulaJuani

#JFAfya
KENYA: MWANAFUNZI AJERUHIWA KWA KULA CHAPATI 5 BADALA YA 1

Caleb anayesoma Darasa la 7 anadaiwa kupigwa na Walimu ambao pia waliamuru Wanafunzi wenzie wampige

Hawezi kusimama, ana vidonda vya Moto Mgongoni na Figo yake 1 imeharibika

Soma https://jamii.app/CalebChapatiKE

#UkatiliWatoto
UNICEF: WATOTO WALIO MAENEO YENYE MIZOZO WALINDWE

Shirika la Kuhudumia Watoto limelaani mauaji yaliyotokea DR Congo hivi karibuni ambapo Watoto wapatao 15 waliuawa

Wengine takriban 30 walijeruhiwa baada ya Waasi kuvamia Kambi ya Wakimbizi

Soma - https://jamii.app/IturiWatoto

#HakiMtoto
ARUSHA: ANAYETUHUMIWA KUMUUA MLINZI NA KUONDOKA NA KICHWA APATIKANA

Raymond Mollel amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumchinja Mlinzi mwenzake na kuondoka na kichwa

Amekiri kuhusika na mauaji na kuonesha alipoficha kichwa cha mwenzake

Soma - https://jamii.app/MauajiYaArusha

#JFMatukio
Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kimesema Mawakili 65 wamefariki dunia kwa #COVID19 tangu kutangazwa kisa cha kwanza cha Ugonjwa huo Machi 16, 2020

Serikali imechukua hatua kadhaa kudhibiti maambukizi ikiwemo kutoa chanjo bila malipo

Soma - https://jamii.app/Mawakili65Corona

#UVIKO3
UCHAGUZI WA KUMPATA NAIBU SPIKA KUFANYIKA FEBRUARI 11, 2022

Kila Chama chenye Uwakilishi Bungeni kinachokusudia kushiriki, kinashauriwa kuanza mchakato wa kumpata Mgombea miongoni mwa Wabunge wake

Jina la Mgombea linapaswa kuwasilishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi kabla ya Saa 10:00 Jioni, Februari 10

Soma - https://jamii.app/NSpikaFeb11

#Bungeni #Democracy
#AFGHANISTAN: WASICHANA KURUHUSIWA KUHUDHURIA MASOMO CHUONI

Wanafunzi wa Kike wataruhusiwa kuhudhuria Masomo endapo watatenganishwa na wa kiume na mtaala utafuata kanuni za Kiislamu

Wanafunzi wa kiume watahudhuria masomo Asubuhi na wa Kike mchana

Soma - https://jamii.app/GirlsUnivTaliban

#ChildRights #JFElimu
DAR: Kesi inayomkabili aliyekuwa RC wa Dar, Paul Makonda imeahirishwa hadi Februari 8 baada ya Makonda kutofika Mahakamani

> Kesi ilifunguliwa na Saed Kubenea, ilitakiwa kusomwa kwa mara ya kwanza leo, Februari 3 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni

Soma https://jamii.app/MakondaKesi

#JFSiasa
UJERUMANI: KADINALI AOMBA KANISA KATOLIKI KURUHUSU NDOA KWA MAPADRI

Askofu Reinhard Marx amekitaja kigezo cha Useja kuwa hatari lakini hawezi kukihusisha moja kwa moja na Kashfa za Unyanyasaji wa Kijinsia zinazotikisa Kanisa hilo Duniani

Soma - https://jamii.app/NdoaMapadri
#JFLeo
TACAIDS: 40% YA VIJANA HAWAJUI HALI ZAO ZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

Imeelezwa, Wasichana wanapata maambukizi kwa kasi mara tatu zaidi ya Wavulana

Ndoa za kulazimishwa zimetajwa miongoni mwa sababu zinazopelekea Wasichana kupata maambukizi zaidi

Soma - https://jamii.app/MaambukiziWasichana

#JFAfya
Waziri wa Ujenzi, Prof. Mbarawa amesema Fedha zilizojenga Daraja la Tanzanite ni za Mkopo kutoka Korea Kusini na zitalipwa na Serikali, hivyo Watanzania hawatalipa kulitumia

Daraja la Kigamboni linalipiwa kwasababu lilijengwa na Fedha za NSSF

Soma - https://jamii.app/DarajaTanzanite

#JFSiasa
Mshiriki wa #StoriesOfChange amesema Wanawake hupoteza fedha kufanya sherehe zisizo za lazima huku wengine wakitunga sherehe ili kutunzwa na wanakikundi

> Ameshauri "Msisubiri Rais aje awawezeshe wakati mtaji mdogo mlionao mnautumia vibaya"

Soma https://jamii.app/ShereheUmasikini

#JFMdau