JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
'SYSTEM' ZA CHANJO YA #COVID19 YA PFIZER ZADUKULIWA

> Kwa mujibu wa taarifa, baadhi ya nyaraka kuhusu chanjo ya #Pfizer na #BioNTech zimeingiliwa

> Chanjo hiyo ilionesha uwezo wa kinga kwa asilimia 95 kwa watu 30,000 waliojaribiwa

Soma - https://jamii.app/PfizerCyberAttack
#DigitalSecurity
RAIS MAGUFULI ATEUA NAIBU WAZIRI WA MADINI

- Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Prof. Shukrani E. Manya kuwa Mbunge na vilevile, Naibu Waziri wa Madini

- Uteuzi wake unaanza leo na ataapishwa mchana Ikulu, Dodoma

Soma - https://jamii.app/JPMUteuzi
SERIKALI KUDHIBITI WANAOUZA DAWA BILA KUFUATA TARATIBU

> Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Abel Makubi, amewaagiza Wakaguzi wa Dawa na Watumishi wa Sekta ya #Afya kudhibiti uuzaji na ununuzi holela ya Dawa bila cheti wala maelekezo ya Daktari

Soma - https://jamii.app/MsakoUuzajiDawa
#JFLeo
SHERIA INASEMA NINI KUHUSU UFUJAJI WA MALI YA UMMA

> Kifungu cha 28 - Kosa: Mtumishi wa umma anayefuja mali za umma, au mtumishi katika taasisi binafsi anayefuja mali alizokabidhiwa, au anayebadilisha umiliki na kuwa mali zake.

> Faini isiyozidi Tsh. Milioni 10 au kifungo kisichozidi miaka 7 au vyote kwa pamoja.

> Mahakama yaweza pia kuamuru mali zilizofujwa au kubadilishwa umiliki zirejeshwe kwa mmiliki au mtuhumiwa alipe fidia kama mali hizo hazipatikani

Soma https://jamii.app/MakosaRushwaAdhabu

#KemeaRushwa #JFLeo
JAJI WARIOBA: VIONGOZI WA SIASA WATAFAKARI NAMNA YA KULINDA AMANI

- Amesema ikiwa Viongozi bila kujali itikadi za Vyama vyao watabeba jukumu la kuhubiri amani kama wanavyofanya Viongozi wa Dini, itasaidia kuimarisha Amani na Haki hapa nchini

Soma https://jamii.app/SiasaHakiAmani
#MALAWI: ADHABU KALI KUTOLEWA KWA WANAOFANYA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

- Rais Chakwera ametangaza mipango ya kutoa adhabu kali baada ya vitendo hivyo kuongezeka kutokana na #COVID19

- Maboresho yanaandaliwa kuharakisha mchakato wa kesi hizo

Soma - https://jamii.app/SheriaMalawi
#KENYA: WABUNGE WATAKIWA KUREJESHA FEDHA ZOTE WALIZOJILIPA

- Mahakama Kuu imemuamuru Katibu wa Bunge kurejesha Ksh. bilioni 1.2 kutoka kwenye mishahara ya Wabunge, fedha ambazo walijilipa wenyewe kama posho ya nyumba kinyume na #Katiba ya Nchi

Soma - https://jamii.app/MpsCashPayback
DR CONGO: WABUNGE WAPIGA KURA NA KUMUONDOA SPIKA MADARAKANI

- Hatua hiyo imetajwa kuwa ya ushindi kwa Rais Tshisekedi ktk jaribio la kujitenga na Rais wa zamani wa nchi hiyo

- Spika Jeanine Mabunda ni mshirika wa muda mrefu wa Joseph Kabila

Soma https://jamii.app/SpikaBungeDRC
WHO: GHARAMA KUBWA ZA MATIBABU HUSABABISHA WATU KUWA MASIKINI

- Takriban nusu ya watu Duniani hawana huduma nzuri ya #Afya na kila mwaka watu milioni 100 huwa masikini sana kutokana na kutumia fedha nyingi kupata matibabu

Soma - https://jamii.app/UmasikiniMatibabu

#HealthForAll
MOROCCO NA ISRAEL KUANZISHA MAHUSIANO YA KIDIPLOMASIA

- Mataifa hayo yamekubaliana kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia chini ya mkataba uliofadhiliwa na Marekani

- Morocco inakuwa taifa la 4 la kiarabu kumaliza uhasama na Israel tangu Agosti

Soma https://jamii.app/MoroccoIsrael
SPIKA NDUGAI ATOA WITO KWA WABUNGE WA ACT-WAZALENDO KWENDA KUAPA

- Spika wa Bunge la Tanzania asema, kama kweli waliomba Ubunge kutumikia Raia hawana sababu ya kuendelea kuzurura

- Amewataka watoe taarifa haraka ili wapangiwe kupata kiapo

Soma - https://jamii.app/SpikaWabungeACT
RIPOTI: UTOAJI WA GESI YA UKAA WAPUNGUA 2020

> Utoaji wa Gesi ya Ukaa kutokana na matumizi ya Makaa ya Mawe, Petroli na Gesi Asilia umepungua kwa 7%

> #CoronaVirus imechangia kutokana na kufungwa kwa shughuli nyingi za uzalishaji Duniani

Soma - https://jamii.app/GesiUkaa2020
UGANDA: MGOMBEA MWANAMKE PEKEE WA URAIS ASITISHA KAMPENI SABABU YA UKATA

- Nancy Kalembe amesema hatajiondoa katika mbio za kuwania Urais, na badala yake anajipanga upya

- Uchaguzi Mkuu nchini #Uganda unatarajiwa kufanyika Januari 14, 2021

Soma - https://jamii.app/NancyCampaignsUG
SERIKALI KUINUA #UTALII KANDA YA KUSINI

- Serikali imewekeza zaidi ya Bilioni 365 kuinua Sekta hiyo

- Kaya 27,450 ktk Vijiji 61 vinavyozunguka mradi huo vitanufaika, na utawekwa utaratibu wa kuboresha shughuli za kujipatia kipato

Soma - https://jamii.app/UtaliiKandaKusini
RAIS MAGUFULI: WIZARA YA MADINI INAKOSA WATAALAMU NAFASI ZA JUU

- Katika hafla ya kumuapisha Naibu Waziri, Rais amesema taaluma ya Waziri wa Madini ni Mwalimu

- Ameitaka Wizara kuhusisha Wataalamu ili madini yaliyopo nchini yaanze kutumika

Soma https://jamii.app/JPMWizaraMadini
MINYOO ISIPOTIBIWA HUWEZA KUSABABISHA MATATIZO YA AKILI

> Afisa Lishe Mwandamizi wa TFNC, Dkt. Analace Kamala amesema, Minyoo inapojenga himaya ndani ya mwili wa binadamu huenda kuathiri mifumo mingine ikiwamo ya Hewa, Damu na Fahamu

Soma - https://jamii.app/MinyooTatizoAkili
#Afya
WATOTO NJITI: Takwimu zinaonesha Watoto wachanga 25 kati ya 100 hufa kutokana na matatizo yanayoambatana na kuzaliwa na uzito pungufu

- Inaelezwa kuwa wengi wa wanaofariki ni wale ambao wamezaliwa kabla ya wakati(WatotoNjiti)

Soma > https://jamii.app/WitoWatotoNjiti

#PrematureBabies
KASSIM MAJALIWA: KUAPA KUNAHITAJI NGUVU KIDOGO

> Waziri Mkuu amesema, kitendo cha kuapa sio kitendo rahisi na yaliyotokea juzi (Uapisho wa Francis Ndulane) 'sio ya Lindi'

> Amuambia Rais Magufuli "Tuendelee kumuombea kijana wetu. Naamini bado unaweza ukaangalia angalia"

#JamiiForums
JE, UNAFAHAMU UHURU WA MAHAKAMA UNAMAANISHA NINI?

- Dhana ya uhuru wa mahakama inaitaka mahakama kutekeleza majukumu yake bila woga wala upendeleo. Uhuru wa mahakama unahifadhiwa na kulindwa katika maeneo manne yafuatayo;

i) Kuzuia kuondolewa kwa Jaji au Hakimu ktk ofisi bila ya sababu za msingi na bila ya kufuata taratibu zilizowekwa hata kama kuna sababu za kumuondoa

ii) Kuweka kinga ya kutoshtakiwa kwa Jaji au Hakimu kwa makosa yoyote na maamuzi yake ya kimahakama aliyoyafanya

iii) Kutopunguza au kuondoa mishahara na maslahi ya Jaji au Hakimu

iv) Kutokuwa na vyeo kwenye vyombo vingine vya dola au kushiriki katika shughuli za vyama vya siasa

https://jamii.app/UhuruMahakama

#UhuruWaMahakamaTz
MBWA MWITU NA FARU HATARINI KUPOTEA TANZANIA

- Sensa ya mwaka 1970, walikuwepo Faru 10,000 lakini kufikia 2020 idadi ni 190. Ujangili umechangia kupungua kwao

- Mbwa Mwitu sasa wapo 220 na kupungua kwao kunatokana na shughuli za Binadamu

Soma - https://jamii.app/FaruMbwaMwitu
#Animals