JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI YAIDHINISHA MATUMIZI YA DHARURA YA CHANJO YA PFIZER

- Mamlaka ya Chakula na Dawa (FDA) imeidhinisha matumizi ya dharura ya Chanjo hiyo dhidi ya #CoronaVirus

- Rais Trump amedai chanjo za kwanza zitatolewa chini ya saa 24 zijazo

Soma - https://jamii.app/PfizerUS
VODACOM FOUNDATION WAPAMBANA KURUDISHIWA USAJILI WAO

> Sept. 11, 2019 BRELA walifuta kampuni zote zenye ukomo wa ahadi, Vodacom Foundation ikiwa mojawapo

> Vodacom wameomba kurejeshewa usajili ili wamalizane na watendaji na wahisani wao

Soma https://jamii.app/VodacomFoundation
KENYA: MAADHIMISHO YA 57 YA #JAMHURIDAY KUHUDHURIWA NA WATU 5,000

- Kutokana na #COVID19, maadhimisho hayo yatahudhuriwa na watu wachache tofauti na miaka ya nyuma

- #Kenya inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo mdororo wa uchumi na madeni

Soma - https://jamii.app/JamhuriKE
RAIS MAGUFULI AAGIZA WATUMISHI WA TMAA WAPUNGUZIWE MISHAHARA

> Amemtaka Katibu Mkuu Kiongozi kuwapunguzia mishahara Watumishi waliokuwa Wakala wa Ukaguzi wa Madini na kuhamishiwa Wizara ya Madini, kwa kuwa kazi waliyoifanya TMAA ilikuwa ya hovyo

Soma https://jamii.app/MaguMishaharaTMAA
ETHIOPIA YAANZA KUWAREJESHA WAKIMBIZI WALIOKIMBIA MAPIGANO #TIGRAY

> Wakimbizi 96,000, wengi wao wakiwa raia wa #Eritrea walitajwa kwenye ripoti ya UN kuwa hatarini kutokana na mapigano yaliyotokea kati ya Vikosi vya Serikali na Waasi wa TPLF

Soma https://jamii.app/WakimbiziTigray
MAREKANI: MAHAKAMA KUU YAKATAA KUBATILISHA MATOKEO YA UCHAGUZI

- Mahakama Kuu ya Nchi hiyo imekataa kubatilisha matokeo ktk Majimbo 4 licha ya Rais Trump kushinikiza suala hilo

- Rais Mteule, Joe Biden alitangazwa mshindi wa Majimbo hayo

Soma - https://jamii.app/SupremeCourtTrump
MOSHI: AFISA UGAVI MBARONI KWA KUTAPELI WATUMISHI WA SERIKALI

- Dominic Mpombe amewashawishi kutoa Tsh. milioni 4.3 kama kiingilio kujiunga na Kampuni ya Q-NET huku walengwa wakiwa ni Walimu, Manesi, Madaktari, Wastaafu na Wafanyabiashara

Angalia - https://youtu.be/iTPW09JE1bY
#JFLeo
CHANJO BILIONI 1 ZA #COVID19 KUTOLEWA KWA NCHI ZENYE UCHUMI WA KATI NA CHINI

- Mkurugenzi Shirika la #Afya Duniani (WHO), Tedros Ghebreyesus amesema, wanakabiliwa na pengo la dola bilioni 4.3 ili kusambaza chanjo kwa Nchi zenye uhitaji mkubwa

Soma https://jamii.app/CoronaUchumiKati
WAZIRI AAGIZA TAASISI ZINAZODAIWA NA TANESCO KUKATIWA UMEME

- Dkt. Kalemani ameiagiza TANESCO kuzikatia umeme Taasisi za Umma zinazodaiwa zaidi ya Bilioni 182

- Alitaka Shirika la Umeme kukata nishati hiyo akisema lazima mapato yaongezeke

Soma - https://jamii.app/TaasisiUmeme
MASWA: WANAFUNZI 68 WAPATA UJAUZITO NDANI YA MIEZI 11

- Taarifa ya Dawati la Jinsia Wilayani humo inasema, Wanafunzi wa Shule ya Msingi ni 3 na Sekondari ni 65

- Pia, Jamii imeendelea kuficha matukio haya na kutotoa ushahidi kwa baadhi ya kesi

Soma https://jamii.app/Mimba68Maswa
#JFLeo
TANAPA KUANZA KUWEKA 'CABLE CAR' MLIMA KILIMANJARO

- Cable Car itaanzia karibu na Geti la Machame la kupandia Mlima #Kilimanjaro na kuishia Uwanda wa Shira

- Itakuwa na Urefu wa mita 3,700 kati ya 5,895 za Mlima na haitafika kwenye Kilele

Soma - https://jamii.app/CarCableKilimanjaro
#JFLeo
#ETHIOPIA YAAGIZA MAAFISA WA JUU ZAIDI YA 40 KUKAMATWA

- Polisi nchini humo wametoa hati ya kukamatwa kwa zaidi ya Maafisa 40 wakiwemo waliotumikia Jeshi zamani, wakihusishwa na mapigano ya #Tigray

- Wanatuhumiwa kwa uhaini na utekaji nyara

Soma - https://jamii.app/ArrestWarrantsTigray
#JFLeo
MAREKANI: CHANJO YA #COVID19 KUANZA KUTOLEWA KESHO

- Mamlaka zimesema Chanjo dhidi ya #CoronaVirus toka Pfizer na BioNTech itaanza kutolewa kwa Wananchi

- Hadi kesho vituo vya kutolea chanjo 145 vitakuwa vimepokea shehena ya kwanza

Soma - https://jamii.app/USCovidVaccine
WAZIRI MKUU WA ESWATINI(ZAMANI SWAZILAND) AFARIKI KWA COVID-19

> Ambrose Dlamini(52) amefariki dunia akiendelea na matibabu nchini Afrika Kusini

> Alipata maambukizi ya #CoronaVirus katikati mwa mwezi Novemba lakini hakuwa na dalili yoyote

Soma https://jamii.app/EswatiniPMDies

#JFLeo
MAREKANI YATEKELEZA ADHABU NYINGINE YA KIFO, WATATU KUUAWA JANUARI

> Brandon Bernard aliuawa Alhamisi na Alfred Bourgeois siku ya Ijumaa

> Hukumu zote zikitekelezwa Trump atakuwa ameua watu wengi ndani ya karne moja ya historia ya Urais Merekani

Soma https://jamii.app/DeathPenaltUSA
UJERUMANI KUFUNGA MADUKA NA SHULE ILI KUDHIBITI CORONA

- Shule zote zitafungwa Desemba 16, 2020 hadi Januari 10, 2021 na Waajiri watatakiwa kusitisha shughuli zao au kufanyia kazi Nyumbani

- Idadi ya maambukizi imefikia 1,320,716

Soma - https://jamii.app/SchoolsShopsBan
WATOTO NJITI: WITO KWA SERIKALI NA WADAU KWA AJILI YA KUBORESHA HUDUMA YA AFYA

- Wajawazito wahudhurie Kliniki kabla na baada ya kujifungua, wajifungulie ktk vituo vya kutolea huduma

- Mtoto mchanga apatiwe huduma ya Afya stahiki.

https://jamii.app/WitoWatotoNjiti

#PreMatureBabie
UNICEF: WATU BILIONI 1.8 WANATEGEMEA VITUO VYA AFYA VISIVYO NA MAJI

> Ripoti ya UNICEF imesema, ukosefu wa Maji na Sabuni huwaweka wagonjwa ktk hatari ya kupata #COVID19

> Hali ni mbaya nchi zinazoendelea ambapo Kituo 1 kati ya 2 hukosa maji

Soma https://jamii.app/HealthCentresWASH
IRAN YAMNYONGA MWANAHABARI KWA KUHAMASISHA MAANDAMANO 2017

- #Iran imetekeleza adhabu ya kifo dhidi ya Mwandishi wa Habari, Ruhollah Zam, kutokana na kazi zake za mtandaoni zilizohamasisha maandamano ya kuipinga Serikali mwaka 2017

Soma - https://jamii.app/RuhollahExecution
IBM: WADUKUZI WANAILENGA CHANJO YA #COVID19

- Watafiti wanasema, 'Phishing Emails' zimekuwa zikitumwa kwa Mashirika yanayosambaza chanjo tangu Septemba 2020

- Maeneo lengwa ni Ujerumani, Italia, Korea Kusini, Ulaya, Czech na Taiwan

Soma https://jamii.app/CoronaCyberAttacks
#DigitalSecurity