JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SERIKALI KUINUA #UTALII KANDA YA KUSINI

- Serikali imewekeza zaidi ya Bilioni 365 kuinua Sekta hiyo

- Kaya 27,450 ktk Vijiji 61 vinavyozunguka mradi huo vitanufaika, na utawekwa utaratibu wa kuboresha shughuli za kujipatia kipato

Soma - https://jamii.app/UtaliiKandaKusini
UJERUMANI YAIPA TANZANIA TSH. BILIONI 56 KUSAIDIA UHIFADHI NCHI

Waziri wa Maliasili na #Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amesema miradi inayofadhiliwa ina umuhimu mkubwa katika Uhifadhi

> Mradi utadumu kwa miaka 3, utaanza baada ya bajeti kupitishwa

Soma https://jamii.app/UhifadhiNchi
MKURUGENZI WA HOTEL ASSOCIATION OF TANZANIA AOMBA MSAMAHA WA KODI

Katika mjadala unaoangazia madhara ya #COVID19 kwa sekta ya #Utalii, Mkurugenzi wa HAT, Kennedy Edward ameiomba serikali kutoa msamaha wa kodi na kipindi cha neema ili kuinua sekta

Amesema wafanyabiashara kwa kipindi cha COVID-19 wanafikiria namna ya kustahimili na kupita katika kipindi hiki badala ya kufikiria kupanua biashara

Aidha ametaka washirikishwe kwenye mabadiliko ya sheria na kanuni ili kuhakikisha mawazo yanakuwa katika mstari mnyoofu

#JamiiForums
DKT. NDUMBARO: HAKUNA UTHIBITISHO PEMBE ZA FARU ZINAONGEZA NGUVU ZA KIUME

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro, amesema Faru ambao ni kivutio kikubwa cha #Utalii Tanzania huwindwa kwa imani potofu na kuitaka Jamii kuwalinda

Soma > https://jamii.app/FaruNguvu
#JFLeo
ATHARI ZA #COVID19: UCHUMI WA KENYA WASHUKA. WAGENI WAPUNGUA KWA 71.5%

Ukuaji wa #Uchumi umeshuka kwa 0.3% mwaka 2020 huku mfumuko wa bei ukipanda hadi 5.4% kutokana na kudumaa kwa usambazaji wa bidhaa

Pato la Taifa kutoka sekta ya #Utalii limepungua kwa 43.9% huku idadi ya wageni Hotelini ikipungua kwa 58.0% hadi Watu Milioni 3.8

Soma - https://jamii.app/UchumiCoronaKE
#UVIKO3
UTALII: NUSU YA SIMBA DUNIANI WANAPATIKANA TANZANIA

Rais wa Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa (SCI), Sven Lindqueast ameipongeza #Tanzania kwa juhudi za utunzaji Wanyamapori

Tanzania inakusudia kukomesha Ujangili kwa 90% ifikapo 2025

Soma - https://jamii.app/SimbaTz

#Utalii
WAZIRI MKUU: HUWEZI KUZUNGUMZIA UTALII BILA KUWATAJA WAMAASAI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hauwezi kuzungumzia Utalii wa #Tanzania bila kutaja Wamaasai na suala la wao kuishi na Wanyamapori Hifadhi ya Ngorongoro linavutia

Soma - https://jamii.app/WamaasaiNgorongoro

#Utalii #JFLeo #Governance
Mwaka 2019/20 CAG alionesha uwepo kwa viashiria vya #Rushwa, Udanganyifu na Ubadhirifu katika usimamizi wa matumizi ya kawaida

Matumizi ya Tsh. Bilioni 34.99 katika Mfuko wa Maendeleo ya #Utalii yalitumika pasipokuwa na nyaraka zilizoidhinishwa

#JamiiForums #Accountability #WAJIBU #JFUwajibikaji
Moto katika Hifadhi ya Mlima #Kilimanjaro umeteketeza Kilomita za mraba 34.2 za Uoto wa Asili wenye Mimea aina ya Erica sp.

Pia, umeharibu Mandhari ya Ukanda wa juu, umesababisha taharuki na kuteketeza Viumbe ambao uwezo wao wa kutembea ni mdogo

Soma https://jamii.app/MotoMlimani

#Utalii
😒3πŸ‘1πŸ€”1😱1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIMBA KUITWA BOB JR. SERIKALI YASEMA AKIITWA MASANJA HAKUNA ATAKAYEMJUA

Imeelezwa majina maarufu yanapotumika katika #Utalii mfano kwa Wanyama kama Simba aliyeitwa #BobJunior na mwanaye #Rihanna ni sehemu ya kujitangaza kimataifa

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema β€œTunapotumia majina maarufu tunaitangazia Dunia na si #Tanzania pekee, tukimpa jina la Masanja hakuna atakayemjua.”

Soma https://jamii.app/MajinaYaUtalii

#Tourism #Governance
😁8πŸ‘6πŸ‘2
AFRIKA KUSINI: Pendekezo la kumlipa #TrevorNoah Randi Milioni 33 (takriban Tsh. Bilioni 4.2) kwa Video ya Dakika 5 ya kuitangaza #SouthAfrica kama Kivutio cha Kitalii, limesababisha mpasuko baada ya baadhi ya Wabunge na Wananchi kupinga kwa kudai kuwa Nchi hiyo inapitia Mgogoro mkubwa wa kifedha kwa wakati huu

Waziri wa Utalii, Patricia de Lille amesema kuwa Mcheshaji na Mtangazaji huyo atalipwa na Baraza la Biashara la Utalii Nchini humo na sio kwa kupitia Fedha za Umma

Hata hivyo, Wadau wengine wameunga mkono pendekezo hilo wakisema ushawishi wa Nyota huyo unaweza kukuza Utalii wa Afrika Kusini

Soma https://jamii.app/UtaliiSA

#JamiiForums #SATourism #Utalii #Tourism #Governance #Democracy
πŸ‘3πŸ‘2
NJOMBE: Mdau wa JamiiForums.com anadai hapo awali Mtalii mmoja alilipa Tsh. 30,000 kulala kwa usiku mmoja katika majengo yaliyojengwa kwa fedha za Serikali katika Hifadhi ya Mpanga Kipengere, lakini Mwekezaji aliyepo sasa anatoza Tsh. 150,000 kwa Mtu ndani ya Usiku mmoja, jambo ambalo linalalamikiwa na wengi

Anasema huo ni mfano wa baadhi ya mambo kadhaa ambayo hayapo sawa, hivyo akitoa wito kwa mamlaka husika itoke hadharani kuelezea kwa uwazi aina ya uwekezaji, ili kuona kama una faida kwa Taifa au unafaidisha Watu wachache

Pia, anaeleza kuwa kuzidisha gharama inaweza kupunguza kasi ya #Utalii hasa wa ndani, akidai kuwa Serikali imepunguza kiingilio ili kuongeza Wageni lakini wanaoingia hifadhini ndani ya β€˜bandas’ wameongezewa malipo kwa asilimia kubwa

Soma https://jamii.app/MpangaKipengere

#JamiiForums #Accountability #Governance #Transparency