JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dkt. Fredrick Shoo amesema amekuwa akiumizwa na madai ya baadhi ya Watu ambao kwa sababu zao binafsi wamekuwa wakidai msaada wa Rais Samia Suluhu kwa Taasisi za Dini ni sehemu ya hongo

Askofu Shoo amesema hayo Julai 03, 2025 wakati wa Mkutano Mkuu wa 32 wa CCT ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko alikuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Rais Samia

Amesema “Ni kumsingizia vitu ambavyo hajadhamiria kwenye moyo wake, kwamba hii sasa ni #Rushwa, mwambie Mama avumilie na aendelee kusapoti kazi za Taasisi za Dini pale anapoona inafaa.”

Zaidi Soma https://jamii.app/AskofuShoo

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio #Governance
1
ARUSHA: Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamerudisha ‘zawadi’ ikiwemo mchele, mahindi, sukari, unga, sabuni na chumvi walizodai kupewa na Diwani wa Kata ya Mbureni, Faraja Maliaki ambaye pia ni mtiania wa Nafasi ya Udiwani katika Uchaguzi Mkuu 2025

Wamerudisha vitu hivyo kwenye Ofisi ya Kata ya CCM wakidai awali walirudisha zawadi hizo nyumbani kwa Diwani lakini alikataa kufungua geti

Alipoulizwa Katibu wa CCM Kata ya Ambureni, Josiah Mollel amesema hawakupokea vyakula hivyo kwa kuwa Chama hakikumtuma mhusika kutoa misaada hiyo

Faraja Maliaki alipoulizwa amesema hizo ni njama za Kisiasa zilizopangwa na Wapinzani wake kumchafulia jina na kuwa misaada aliyowahi kutoa ilihusiana na taasisi yake ya Faraja Foundation ambayo ilitolewa Mwaka 2024

Soma pia https://jamii.app/RushwaUdiwani

#JamiiForums #Rushwa #Uwajibikaji #Accountability #Kuelekea2025
1👏1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila amewataka Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Mitaa na Viongozi wengine kusimamia haki na kutokuwa na upendeleo wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu

Akizungumza Julai 4, 2025 katika kikao kazi kilichofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee, amesema ni wajibu wa Viongozi hao kulinda uhuru na haki ya wapiga kura, akieleza kuwa msingi wa #Demokrasia ni kuhakikisha kila raia anapiga kura kwa uhuru na haki

Ameongeza kuwa muitikio wa Wapiga Kura ni kiashiria cha uchaguzi huru na wa haki, na kuwataka Viongozi hao kushirikiana kwa karibu na Jamii ili kuimarisha imani ya Wananchi katika mchakato wa Kidemokrasia

Soma pia: https://jamii.app/ChalamilaKuhusuUchaguzi

#JamiiAfrica #Jamiiforums #Democracy #Accountability
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Sheikh Mohammed Abdallah Mawinda amesema Nchi inaongozwa na Sheria na haitakiwi kufanya masihara ya kuchezea amani

Amesema hayo leo Julai 5, 2025, katika uzinduzi wa Kanisa la Arise and Shine linaloongozwa na Boniface Mwamposa, lililopo Kawe

Soma https://jamii.app/MwindaTaifaNaAmani

#JamiiAfrica #Jamiiforums #Democracy #JFMatukio
Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imewaagiza Waandishi wote wa Habari waliotangaza kugombea katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kusitisha mara moja shughuli zao za kihabari ili kuepuka mgongano wa kimaslahi na kulinda usawa kwa wagombea wote.

Bodi hiyo inayoongozwa na Mwanahabari mkongwe, Tido Mhando imesema mgombea yeyote anayeendelea kushiriki katika shughuli za kihabari kipindi hiki cha Uchaguzi, anakiuka Kanuni ya 12(g) ya Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa. 

Soma pia https://jamii.app/KatazoBodiYaIthibati

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
MAREKANI: Timu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa imetinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA (#FIFACWC) 2025 baada ya kuibuka na ushindi wa Magoli 2-0 dhidi ya #BayernMunich ya Ujerumani katika mchezo wa Robo Fainali

PSG imeungana na Chelsea ya England na Fluminense ya Brazil katika Nusu Fainali, hivyo inasubiri mshindi kati ya #RealMadrid na #BorussiaDortmund ili kukamilisha orodha ya timu nne

Soma Zaidi https://jamii.app/FIFAClub

#JamiiForums #JFSports #JamiiAfrica #FIFACWC
Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeagiza waandishi wote wanaoendelea kufanya kazi kwenye Vyombo vya Habari vya uchapisho na kielektroniki bila kusajiliwa na Bodi hiyo wanatakiwa kuacha mara moja shughuli zao hadi pale watakapokamilisha usajili kupitia mfumo wa TAI HABARI. 

Bodi imeeleza kufanyakazi bila kujisajili ni kuvunja Kifungu cha 19 cha Sheria ya Huduma za Habari, kinachokataza mtu yeyote kufanya kazi za kihabari bila kibali rasmi.

Aidha, Bodi hiyo imesema inaendelea kufuatilia kwa makini mwenendo wa Waandishi wote nchini na kwamba haitasita kuwachukulia hatua wote watakaokiuka miongozo hiyo

Soma https://jamii.app/KatazoBodiYaIthibati

#JamiiAfrica #Jamiiforums #Democracy #Kuelekea2025
2
Usiruhusu hofu ikuzuie kufanya kile unachokiamini. Maisha ni safari ya mara moja tu, hakuna kurudia

Chukua hatua, fuata ndoto zako, na uende ukijua hujayaacha mambo muhimu nyuma yako

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
4
DAR: Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi maeneo ya Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church (Ufufuo na Uzima) lililopo Ubungo - Kibo, leo Jumapili Julai 6, 2025 ambapo Askari wapo hadi katika maeneo ya Kanisa la Kilutheri la Africa Mashariki (KKAM)

Ulinzi huo umeimarishwa ikiwa ni siku moja tangu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne alipotoa onyo kwa Waumini ambao wana mpango wa kujikusanya na kuingia barabarani mara baada ya ibada kutoka katika Kanisa la KKAM

Ikumbukwe Jumapili iliyopita baadhi ya Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima ambalo limefungiwa na Serikali walishiriki Ibada katika Kanisa la KKAM, baada ya ibada waliingia katika mvutano na Askari kutokana na kuingia Barabarani wakiwa na mabango wakipinga Kanisa lao kufungiwa

Soma zaidi https://jamii.app/UlinziKibo

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #Governance #Democracy #HumanRights
DAR: Nyota wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Ally Samatta amefiwa na Baba yake mzazi, Mzee Ally Samatta ambaye amefikwa na umauti leo Julai 6, 2025 akiwa nyumbani kwake Mbagala. Taarifa za msiba huo zimethibitishwa na mtoto wake, Mohamed Samatta.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na ndugu wa familia Mzee Samatta alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya.

Soma zaidi https://jamii.app/SamattaMzazi

#JamiiForums #JFMatukio #JFSports
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
TABORA: Akizungumza mbele ya Viongozi wa Serikali, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha amedai kuna Wagombea wa Kisiasa wamekuwa wakijaribu Kumshawishi kwa Fedha ili waweze kushinda katika kura za maoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, akimtolea mfano mmoja bila kumtaja jina

Chacha pia alikumbusha kuwa Rais Samia ameshatoa maelekezo kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (#TAKUKURU) kuhakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi ya yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya #Rushwa wakati wa Uchaguzi

Zaidi bofya https://jamii.app/SiasaTabora

#JamiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025 #Accountability #ElectionInformation2025
4👏1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
TANGA: Mwanasiasa Rashid Kilua ambaye ni mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Bumbuli aliingia katika hali ya mvutano na baadhi ya Watu mara baada ya kuchukua fomu ya Ubunge katika Ofisi za Wilaya, tukio hilo lilitokea Juni 28, 2025

Watu hao walimzuia kupiga picha na kufanya mahojiano mara baada ya kuchukua fomu, mvutano huo ulidumu kwa dakika kadhaa kabla ya kila Mtu kuondoka eneo la tukio kutokana na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokuwepo eneo hilo kuingilia

Soma https://jamii.app/SiasaBumbuli

#JamiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Waumini wa Kanisa la Kilutheri la Afrika Mashariki (KKAM) lililopo Kibo, Ubungo wanaendelea na ibada leo Julai 6, 2025 huku kukiwa na ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi maeneo ya karibu na Kanisa hilo

Soma Zaidi https://jamii.app/UlinziIbada

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #JFMatukio #Governance #Democracy #HumanRights
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi eneo la Kata ya Terati baada ya baadhi ya Wananchi kufunga Barabara ya Mapambazuko mapema leo Julai 6, 2025, wakipinga uteuzi wa Julias Lenina kuwa mgombea wa Udiwani kupitia CCM, wakidai alishindwa kutekeleza majukumu yake katika kipindi cha Miaka mitano iliyopita.

Inaelezwa kuwa Lenina ameteuliwa tena na Kamati ya Siasa ya Kata kuwa miongoni mwa watakaopitishwa kuwania nafasi hiyo.

Zaidi, soma https://jamii.app/WananchiWamkataaMgombea

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Governance #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
1
Kila mmoja ana wajibu wa kulinda amani na heshima mtandaoni.

Ukiona mtu anasambaza chuki au uchochezi, usikae kimya ripoti.

Chagua kueneza upendo na uelewa, si migawanyiko.

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #KauliZaChuki #StopHateSpeech #DigitalPeace #NoToHateSpeech #ResponsiblePosting #JamiiYenyeUelewa
Mdau wa Jukwaa la Elimu ndani ya JamiiForums.com ameanzisha mjadala akitaka kujua kwa zama na nyakati za sasa, Mwanafunzi anapofaulu vizuri Kidato cha Nne, Je ni vyema ajiendeleze kwa kujiunga na masomo Ngazi ya 'Diploma' au elimu ya Kidato cha Tano na Sita?

Unaonaje Mdau, ungekuwa wewe ungemshauri achukue uamuzi upi? 

Zaidi Soma https://jamii.app/DiplomaAuAdvance

#JamiiAfrica #Jamiiforums #Elimu
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
JF KUMBUKIZI: Video hii inamuonesha Msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni Mtangazaji wa Wasafi FM, Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Baba Levo, alipofanya mahojiano na Mchekeshaji Kipotoshi, Agosti 26, 2020 kwenye Kipindi cha BambaLive+

Ikumbukwe kuwa Juni 29, 2025, Baba Levo alichukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia CCM

Soma pia https://jamii.app/BabaLevoMuswada

#JFkumbukizi #JamiiForums #JamiiAfrica #Kuelekea2025 #Siasa
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG), Nyanda Shuli ametoa wito kwa Wananchi wa Tanzania kuendelea kupewa elimu kuhusu #Rushwa na madhara yake ili iwasaidie katika kuchagua Viongozi sahihi katika Uchaguzi Mkuu wa 2025

Alisema hayo Julai 4, 2025 katika mjadala ulioandaliwa na Taasisi ya JamiiAfrica na kuwakutanisha Wadau mbalimbali ambapo alisisitiza kuwa Wananchi wasipotoshwe na taarifa potofu kuhuru Rushwa, watambue ni mbaya na madhara yake ni ya muda mrefu

Ziadi Soma https://jamii.app/NenoKuhusuRushwa

#JamiiForums #Accountability #ElectionInformation2025 #MisDis2025 #Democracy #Siasa
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Peter Madeleka, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani kupitia ACT Wazalendo, amesema endapo chama chake kitaingia madarakani, kila askari atahakikishiwa maisha bora ikiwemo kumiliki ghorofa na gari aina ya Land Cruiser ili kuongeza hamasa ya kuilinda Amani na Usalama wa Wananchi

Alisema hayo Julai 4, 2025 Busega, Mkoani Simiyu kama sehemu ya Sera za chama chake za kuboresha maslahi ya Watumishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama

Zaidi, soma https://jamii.app/MadelekaMaslaiYaAskari

#JamiiAfrica #Jamiiforums #HumanRights #Accountability #Governance
Usikae pembeni ukisubiri taarifa zikutafute, nenda kwenye vikao, sikiliza, uliza maswali na toa mawazo yako

Hapo ndipo unakuwa sehemu ya mabadiliko yanayokuhusu moja kwa moja

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa