JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kusoma kwa undani taarifa hizi na nyingine zilizojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
1
Leo Julai 7, 2025 ni Kilele cha Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama "Sabasaba". Maonesho ambayo hutumika kuonesha shughuli mbalimbali za Kibiashara kutoka ndani na nje ya nchi

Kwa mara ya kwanza Maonesho ya Kibiashara yalifanyika mwaka 1963, yakiandaliwa na Wataalam kutoka Wizara ya Biashara na Vyama vya Ushirika

Ni kitu gani kinakuvutia zaidi kutembelea maonesho haya?

Zaidi soma https://jamii.app/Maonesho77Day2025

#JamiiAfrica #JamiiForums #77Day #SabaSaba2025 #MaoneshoYa77 #JFMatukio
1
Tunaweza kuwa na mitazamo tofauti bila kuwa maadui

Si lazima ukubaliane na kila mtu, lakini unaweza kupinga kwa heshima bila kudhalilisha au kutukana

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #KauliZaChuki #StopHateSpeech #DigitalPeace #NoToHateSpeech #ResponsiblePosting #JamiiYenyeUelewa
Kila Julai 7, ni Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani, iliyopitishwa rasmi Novemba 2021, kupitia Azimio namba 41 C/53 la Umoja wa Mataifa chini ya UNESCO

Siku hii ni rasmi kwa lengo la kutambua mchango wa Kiswahili katika Kukuza Tamaduni mbalimbali, Kujenga Hamasa na Kukuza Mazungumzo ya Kistaarabu Duniani

Haya Mswahili, tuambie maana ya neno 'Fofomoa'?

Zaidi soma https://jamii.app/Maadhimishosikuyakiswahili

#JamiiAfrica #JamiiForums #KiswahiliDay #SikuYaKiswahili #WorldSwahiliDay25 #WSD2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Kiongozi wa #ACTWazalendo, Dorothy Semu akizungumza katika Mkutano wa hadhara, Julai 5, 2025 uliofanyika Sapiwi, Bariadi Vijijini alisema “Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, Majeshi kwenye Uchaguzi wasitumike kukibeba Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi wa Mwaka 2025."

Amedai kuwa Chaguzi za Mwaka 2020 na 2024 ziligubikwa na uwepo wa Kura feki hadi katika Vituo vya Kupiga Kura na kwamba kwa sasa wanakataa na hawataki uwepo wa Kura hizo

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiKutumikaNaCCM

#JamiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025 #Accountability
1
Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Biashara, Uchumi na Ujasiriamali ameanzisha Mjadala akiomba ushauri na mbinu za upatikanaji wa mtaji wa dharura au mbadala kwa wafanyabiashara, wakati biashara imeyumba kifedha.

Mdau huwa unatumia mbinu gani kupata “backup” ya mtaji kila unapokwama?

Zaidi, soma https://jamii.app/BiasharaNaUchumi

#JamiiAfrica #Jamiiforums #Biashara
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) leo Julai 7, 2025 limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) pamoja na Mitihani ya Ualimu iliyofanyika mwezi Mei 2025

Akizungumza na wanahabari Visiwani Zanzibar, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Said Mohammed, amesema kwamba mwaka huu ufaulu wa jumla umeongezeka na kufikia asilimia 99.95, ambapo watahiniwa 125,779 kati ya 125,847 wamefaulu kwa kupata Division 1, 2, 3 na 4 likiwa ni ongezeko la asilimia 0.03 ikilinganishwa na mwaka jana

Aidha, katika taarifa yake, Dkt. Said aliongeza kuwa, kwa mwaka huu hakuna tofauti kubwa ya ufaulu kati ya wanawake na wanaume kwani wanawake waliofaulu kwa kupata Division 1, 2, 3 ni asilimia 99.57 huku wanaume ikiwa asilimia 99.68

Zaidi bofya https://jamii.app/MatokeoNECTA

#JamiiForums #JamiiAfrica #Elimu #MatokeoNecta
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha kimetoa ufafanuzi kuhusu madai yanayomkabili aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mbureni, Faraja Maliaki ambaye hivi karibuni ilisambaa video kwenye mitandao kijamii inayoonesha baadhi ya wanachama wa CCM wakirudisha zawadi alizowapa wakidai kuwa ni rushwa

Akizungumza kwa njia ya simu na Global TV, Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Saipuran Ramsey amesema kwa sasa chama hicho kinafanya uchunguzi kubaini kama tukio hilo ni la kweli na iwapo itathibitika kuwa ni kweli basi vikao hivyo vitaamua ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya diwani huyo

Soma https://jamii.app/DiwaniCCMArusha

#JamiiAfrica #Jamiiforums #Accountability #Kuelekea2025
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Shinyanga: Naibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, Shangwe Ayo amesema kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 hautakuwa tukio la kawaida, bali itakuwa ni mapambano ya kuikomboa Demokrasia ya Tanzania, ambayo kwa mujibu wa chama hicho, imetekwa na Chama cha Mapinduzi (CCM)

Shangwe alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Town School, Kata ya Kambarage, Wilaya ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya chama hicho kuhamasisha Wananchi kulinda Kura

Soma zaidi https://jamii.app/AyoMapambano

#Democracy #JamiiAfrica #Jamiiforums #Accountability #Demokrasia #Governance #Kuelekea2025
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa ACT-Wazalendo, Abdul Nondo amesema kuna mifano hai ya waliojaribu kususa kushiriki uchaguzi lakini hawakupata mageuzi wala mabadiliko, akahoji; "Kwanini tusidhani wanaosusa uchaguzi wanatumika na CCM ili kuipa nafasi ya kupita bila kupingwa?"

Nondo aliyasema hayo Julai 6, 2025, akihutubia katika Jimbo la Shinyanga Mjini katika kampeni ya kuhamasisha Wananchi kulinda Kura

Zaidi bofya https://jamii.app/NondoKususaUchaguzi

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Democracy #Demokrasia #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
2
KENYA: Zaidi ya Watu 10 wameripotiwa kuuawa huku wengine 29 wakijeruhiwa katika maandamano ya kuadhimisha Siku ya Sabasaba, hiyo imetokea wakati wa makabiliano kati ya Polisi na Waandamanaji maeneo mbalimbali ambapo pia kuna visa vya utekaji (2) na Watu 37 wamekamatwa, kukiwa na hali ya taharuki katika Kaunti 17.

Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya Kenya (KNCHR) imelaani ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliojitokeza, ikiwemo matumizi makubwa ya nguvu na ukamataji kiholela. Maandamano hayo yameathiri shughuli za kawaida katika maeneo kadhaa

Soma Zaidi https://jamii.app/WatanoSabasaba

#JamiiAfrica #Accountability #KenyanPolitics #Governance #HumanRights
1
Opportunity Alert: Consultant for Media Monitoring and Analysis

JamiiAfrica, through the “Empowering Journalists for Informed Communities (2025–2027)” funded by the European Union and jointly implemented with IMS and UTPC, is seeking a consultant to monitor the media landscape on mis-/disinformation, hate speech and online gender-based violence (OGBV) and to produce high-quality quarterly reports.

Key Deliverables
• Assist the team in the design of a monitoring framework
• Analysis of complex quantitative and qualitative data
• Identify key narratives and trends in mis-/disinformation, hate speech, and OGBV
• Timely submission of high-quality and reader-friendly quarterly reports
• End of Activity Report explaining the procedure and all lessons learned

Submit Your Proposal with cover letter, previous experience, CV and/or company portfolio and consultancy budget Breakdown by 9th July 2025.

For more info visit https://jamii.app/ConsultantMediaAnalysis

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFOpportunities
1
Mara nyingi tunavyowahukumu wengine huonesha zaidi kuhusu mitazamo, hofu au mapungufu yetu sisi wenyewe kuliko makosa yao

Badala ya kukimbilia kutoa hukumu, jaribu kuelewa kwanza

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
Akiandika ndani ya JamiiForums.com, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amesema amefikishiwa visa na malalamiko kadhaa vya ukatili kuhusu Watoto wa "maboss" kuwanyanyasa kingono Wasaidizi wa kazi za nyumbani

Ameandika "Lengo la kushirikisha Mwanajamii ni ufahamu kuwa haya nayo yapo na huenda huko kwako pia yapo ila yanafichwa kwa uoga au kumlinda Mtoto wa boss. Hivyo, chunguza chukua hatua a.k.a FAHAMU, ELIMIKA, CHUKUA HATUA."

Aidha, ameongeza kuwa "Wengine nao wanasema, kuna Wasaidizi wa Kazi wananyanyasa Watoto wa maboss, nao tupate taarifa pia."

Zaidi soma https://jamii.app/WatotoBossKunyanyasa

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #Uwajibikaji #Accountability #Maisha
1👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) Bara, John Heche, akihojiwa na ST Bongo TV, Julai 7, 2025 amesema madai ya kwamba chama hicho kimejifungia kushiriki Uchaguzi na hakiwezi tena kusaini Sheria ya Maadili ya Uchaguzi si ya kweli kwa kuwa Sheria haipo hivyo

Ikumbukwe, Aprili 12, 2025, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (#INEC) iliwasainisha Vyama vya Siasa Kanuni za Maadili ya Uchaguzi ambapo Mkurugenzi wa Uchaguzi wa #INEC, Ramadhani Kailima alisema chama ambacho hakitasaini maadili hayo hakitaruhusiwa kushiriki kwenye Uchaguzi wa 2025

Zaidi soma https://jamii.app/HecheMahojiano

#JamiiForums #Accountability #ElectionInformation2025 #MisDis2025 #Democracy #Siasa
2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche akizungumza Julai 7, 2025 kupitia ST Bongo TV amesema “CHADEMA ipo tayari kushiriki Uchaguzi kama mabadiliko ya kimsingi yanayoridhisha yatafanyika”

Ameongeza kuwa bado msimamo wa Chama hicho kuhusu Mabadiliko upo pale pale ili wote waende kwenye Uchaguzi ambao ni Huru na Haki

Soma https://jamii.app/ChademaUchaguziMkuu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Democracy #Demokrasia #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025