JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KENYA: Vijana kadhaa leo Juni 3, 2025 wamevamia na kuchoma moto Kituo cha Polisi cha Mawego kilichopo Rachuonyo Mashariki, Kaunti ya Homa Bay, eneo ambalo Mwanaharakati Albert Ojwang alishikiliwa kabla ya kupigwa na kusababisha kifo chake

Awali, waombolezaji walitakiwa kuaga mwili wa Ojwang katika Shule ya Msingi ya Nyawango, lakini ratiba ilibadilika baada ya Vijana kuzuia msafara wa Jeneza la marehemu na kulazimisha mwili huo upelekwe katika Kituo cha Polisi cha Mawego

Walipofika kituoni vijana hao waliondoa vizuizi vilivyowekwa na Polisi kisha kuchoma kituo hicho kama ishara ya kupinga mauaji ya Ojwang’

Zaidi bofya https://jamii.app/kituochapolisi

#JamiiAfrica #Accountability #HumanRights #Governance #KenyanPolitics
1👍1
Maisha ni kama mchezo kwa sababu kila uamuzi tunaochukua ni kama hatua moja mbele

Hatuna uwezo wa kurudi nyuma kubadilisha tuliyofanya zamani (makosa au mafanikio), lakini tunayo nafasi na uwezo wa kuhakikisha hatua au uamuzi wetu unaofuata unakuwa bora zaidi na unaleta matokeo mazuri.

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
DODOMA: Jeshi la Polisi Mkoanii Geita linawashikilia Ferdinand Antony, Afisa Mtendaji Kijiji cha Liyobahika pamoja na Hussein Ally kwa tuhuma za mauaji ya Enock Mhangwa. Tukio hilo lilitokea Juni 26, 2025 ambapo Watuhumiwa walimshambulia kijana huyo kwa kipigo mpaka kufariki Dunia

Aidha, Watuhumiwa wengine akiwemo Mtendaji wa Kijiji cha Uyovu na mgambo wawili wanaendelea kutafutwa baada ya kukimbia

Video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo JamiiForums.com ilionesha kijana huyo akipigwa fimbo akiwa amefungwa kamba akituhumiwa kuwa mwizi

Zaidi bofya https://jamii.app/MauajiEnock

#JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #HumanRights #Governance #JamiiForums
1
Filamu ya "Squid Game" msimu wa 3 iliyotoka Juni 27, 2025 ni miongoni mwa filamu zinazohusisha michezo hatarishi.

Baadhi ya wadau wamedai kuwa wasingetoboa katika mchezo wa "Hide and Seek" katika filamu hiyo maarufu kama (Kombolela)

Mdau, umeitazama Squid Game 3? Ni mchezo gani unaona kabisa usingetoka salama?

Mjadala zaidi https://jamii.app/squidgame3

#JamiiAfrica #Jamiiforums #JFBurudani #JFEntertainment
🔥21
DAR: Baada ya Mdau kushauri Hospitali ya Amana kuboresha huduma ikiwemo ya "Ambulance", akidai kuna gari mbili na Dereva mmoja, hivyo kasi kuwa ndogo ya kubeba Wagonjwa huku akiongeza kuwa baadhi ya Wauguzi wajirekebishe katika kauli zao wakati wa huduma, Uongozi wa Hospitali umetoa majibu

Kuhusu Mgonjwa kusubiri gari kuanzia Jioni hadi Saa Saba Usiku, Juni 23, 2025, Amana imeeleza “Kulikuwa na Wagonjwa sita wa rufaa, wawili walipelekwa Muhimbili – Mloganzila, wanne walipelekwa Muhimbili Upanga, mgonjwa wa mwisho alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya Saa Saba Usiku”

Taarifa ya Hospitali imeeleza “Amana ina Ambulance mbili, lakini kutokana Serikali kufanya maboresho ya huduma za Afya, idadi ya Wagonjwa wanaopewa Rufaa kutoka Amana imepungua na muda mwingine kuweka dereva mmoja kwa zamu za usiku, na hata siku hiyo ya Juni 23, 2025 alipangwa dereva mmoja

Soma https://jamii.app/AmanaHospitali

#JamiiForums #JamiiAfrica #ServiceDelivery #Accountability
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Katani Ahmed Katani amesema "Upige picha kwenye barabara za Doha-Qatar, halafu upite barabara za Tandahimba na uweke kwenye mtandao huwezi kuona tofauti"

Ameyasema hayo Julai 3, 2025 katika mahojiano kwenye kipindi cha Wasafi cha 'One on One'

Watu wa Tandahimba, tuambieni hali ikoje?

Soma https://jamii.app/Tandahimbakamadoha

#JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #ServiceDelivery #Governance #JamiiForums #KuelekeaUchaguzi2025
1🤣1
DAR: Rais wa Shirikisho la Soka la Tanzania (#TFF), Wallace Karia amesalia kuwa Mgombea pekee wa nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Agosti 16, 2025 baada ya Wagombea wengine kukosa vigezo kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyoeleza amepita kwenye mchujo wa awali

Wagombea wengine wa nafasi hiyo Ally Mayay Tembele, Mbette Mshindo Msolla, Mustapha Salumu Himba na Shija Richard Shija wamekosa vigezo huku Ally Thabit Mbingo hakufika katika usaili

Nafasi ya Kamati ya Utendaji ya TFF wamepita Wagombea 10 kati ya 17 ambao walifika kwenye usaili wa awali, hivyo Kamati ya Uchaguzi inasubiri kupokea Rufaa za Wagombea watakaokata rufaa ambayo inatakiwa kukatwa ndani ndani ya siku 6

Soma https://jamii.app/kariamgombeaurais

#JamiiForums #JFSports #JamiiAfrica
1
MAREKANI: Chama cha Democratic kimemteua Zohran Mamdani, mwenye asili ya Uganda na India, kuwa mgombea katika kinyang’anyiro cha Umeya wa Jiji la New York baada ya kushinda mchujo wa ndani wa chama hicho uliofanyika Juni 25, 2025.

Mamdani amezaliwa Uganda, na anatoka katika familia yenye asili ya Kihindi. Baba yake, Mahmood Mamdani, ni profesa maarufu katika Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani, huku mama yake, Mira Nair akiwa ni mtayarishaji wa filamu kimataifa.

Aliwasili Marekani akiwa na umri wa miaka 7 na alipata uraia mwaka 2018. Iwapo atachaguliwa kwenye Uchaguzi utakaofanyika Novemba 4 2025, Mamdani atakuwa Meya wa kwanza Muislamu wa jiji hilo na pia Meya wa kwanza nchini Marekani mwenye asili ya Kihindi na Uganda

Soma pia: https://jamii.app/mamdanimeya

#JamiiAfrica #Democracy #Governance #JamiiForums
1
Wakati mwingine picha, video au maneno yanayodhalilisha dini, kabila, jinsia au Watu fulani husambazwa kwa mzaha, lakini kwa Mtu anayelengwa, si mzaha, ni tusi, ni kejeli, ni maumivu

Chuki huanza kwa utani, huishia kwa madhara makubwa. Inaweza kuchochea fujo, kuchafua sifa ya Mtu, au hata kumweka hatarini

Ni wajibu wetu kama Vijana kuhoji kila tunachotaka kusambaza

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #KauliZaChuki #StopHateSpeech #DigitalPeace #NoToHateSpeech #ResponsiblePosting #JamiiYenyeUelewa
Sio lazima kila mtu akubaliane na wewe

Wengine hawaoni mambo kama unavyoyaona, na hiyo haimaanishi wako sahihi au wamekosea, ni mtazamo tu tofauti.

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha
KENYA: Rais #WilliamRuto amesema hatamuomba yeyote msamaha kwa kitendo cha yeye kujenga Kanisa ndani ya Ikulu, akiongeza kuwa anawashangaa wanaomsema kuhusu ujenzi huo kwani atatumia pesa zake mwenyewe na sio kutoka Serikalini

Ametoa msimamo huo Julai 4, 2025, na kusisitiza kuwa hajajenga Kanisa jipya bali anaboresha alilolikuta lililokuwa limejengwa kwa mabati ambalo haliendani na hadhi ya Ikulu

Zaidi bofya https://jamii.app/KujengaKanisaIkulu

#JamiiAfrica #Accountability #KenyanPolitics #Uwajibikaji
Serikali imetangaza kuanzisha malipo ya bima ya safari kwa raia wa kigeni wanaoingia Tanzania Bara itakayogharimu Dola za Marekani 44 (Tsh. 116,100)

Wizara ya Fedha imeeleza lengo la bima hiyo ni kwa ajili ya matibabu ya dharura kwa wageni wanapokuwa nchini, kupotea kwa mizigo, huduma za uokoaji na kurudishwa kwa mgeni nchini kwake iwapo itatokea dharura

Taarifa ya Wizara imeeleza kuwa utekelezaji utaanza rasmi mara baada ya kanuni husika kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali

Zaidi bofya https://jamii.app/BimaKwaWageni

#JamiiAfrica #Uwajibikaji #ServiceDelivery #JamiiForums
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Kiongozi Mstaafu wa Chama cha #ACTWazalendo, Zitto Kabwe amekemea vitendo vya utekaji na mauaji yanayoendelea nchini, akitolea mfano tukio la Watendaji wa Vijiji Mkoani Geita wanaotuhumiwa kumtesa mpaka kumuua Enock Thomas.

Akizungumza kwenye mkutano wa Oparesheni Majimaji, Wilayani Bariadi, Zitto amesema thamani ya uhai nchini imepotea na ndio maana hata Watendaji wa Vijiji wanapata ujasiri wa kutekeleza vitendo kama hivyo. 

Amesema “Thamani ya uhai katika nchi yetu inapotea. Matendo ya utekaji wa watu kama vile kina Mdude, Soka, Sativa na wengine inawafanya Watu kama Watendaji wa Vijiji kuona nao wanaweza kukamata, kutesa mpaka kuua.” 

Zaidi soma https://jamii.app/ZittoKabweUtekaji

#JamiiAfrica #Jamiiforums #HumanRights #Accountability #Governance
2
Usiishi kwa mazoea au kudhani mambo fulani ni sawa kwa sababu 'watu wengi wanafanya'. Zijue Sheria mapema ili uweze kujilinda wewe na wengine pia

Jifunze kidogo kidogo kwa kujisomea na kusikiliza Vyombo vya Habari na hata kutumia mitandao mbalimbali ya kijamii.

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro amesema anatoa onyo kali kwa Watu ambao wamekuwa wakifanya vurugu, Jumapili kadhaa zilizopita maeneo ya Ubungo Kibo na kwamba wakijaribu tena watajikuta kwenye msuguano wa usimamizi wa Sheria.

Amesema kuna kundi la Watu ambao wamekuwa wakitokea katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM) wakiwa na mabango baada ya ibada na badala ya kutawanyika kama Waumini wengine, wao huanza kupiga kelele na kutaka kuingia barabarani kwa nguvu kwa lengo la kuchochea vurugu.

Soma https://jamii.app/MuliroIbadaKanisani

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #Governance #Democracy #HumanRights
DAR: Azam FC imemtangaza rasmi kocha wa zamani wa Al Hilal ya Sudan, Florent Ibenge, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo kuelekea Msimu wa 2025/2026, akichukua nafasi ya Rachid Taoussi ambaye aliondoka mwishoni mwa msimu uliopita.

Taarifa hiyo inakuja wakati #AzamFC ikijiandaa kuiwakilisha #Tanzania kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF Confederation Cup) msimu ujao

Soma Zaidi https://jamii.app/IbengeKochaAzam

#JamiiForums #JFSports #JamiiAfrica