DAR: Jamhuri imeweka mapingamizi matatu kutaka Kesi ya Marejeo iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa CHADEMA - Taifa, Tundu Lissu kwenye Mahakama Kuu kutupiliwa mbali
Kwa sasa kesi hiyo inaendelea kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambapo Mawakili wa Lissu wanawasilisha hoja baada ya upande wa Jamhuri nao kuwasilisha hoja za mapingamizi yaliyowekwa.
Katika kesi hii, Lissu anaomba Mahakama irejee uamuzi wa awali wa Hakimu anayeendesha kesi ya Uchochezi inayomkabili katika Mahakama Kisutu, ambaye alikubali maombi ya upande wa Jamhuri kusikiliza ushahidi wa “mashahidi wa siri”
Soma https://jamii.app/LissuJuni27
#JamiiForums #Accountability #Democracy #JamiiAfrica

❤2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Rais Samia Suluhu Hassan amepongeza kazi inayofanywa na Jeshi la Polisi kwa kueleza kuwa linafanya kazi kubwa katika kuzuia uhalifu.
Amesema hayo wakati akihutubia Bunge, leo Juni 27, 2025
Soma https://jamii.app/BungeKuvunjwaJuni25
#JamiiForums #Siasa #Governance

❤1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akihutubia Bunge la 12, Mkutano wa 19, Kikao cha 55, leo Juni 27, 2025, Rais Samia ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuongeza jitihada za kukomesha matukio ya Watu kupotea
Soma https://jamii.app/WatuKupotea
#JamiiForums #Siasa #Governance
Soma https://jamii.app/WatuKupotea
#JamiiForums #Siasa #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Rais Samia Suluhu amesema baada ya kuingia Madarakani alikuja na Falsafa ya 4R, ambayo iliifanya Serikali kuunda Tume ya Maridhiano ambayo ilitoa mapendekezo ya muda mrefu na mfupi katika kuboresha masuala mbalimbali
Ameeleza kati ya mapendekezo ni kuondoa zuio la Vyama vya Siasa kutokufanya mikutano ya hadhara na hivyo kuviwezesha Vyama hivyo kufanya shughuli zao kwa Uhuru
Soma https://jamii.app/BungeKuvunjwaJuni25
#JamiiForums #Siasa #Governance #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Ameeleza kati ya mapendekezo ni kuondoa zuio la Vyama vya Siasa kutokufanya mikutano ya hadhara na hivyo kuviwezesha Vyama hivyo kufanya shughuli zao kwa Uhuru
Soma https://jamii.app/BungeKuvunjwaJuni25
#JamiiForums #Siasa #Governance #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Rais Samia amesema pendekezo la Tume ya Maridhiano kuhusu mchakato wa Katiba Mpya lipo kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Mwaka 2025/2030, na mchakato utafanyika ndani ya kipindi hicho
Soma https://jamii.app/BungeKuvunjwaJuni25
#JamiiForums #Siasa #Governance #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Soma https://jamii.app/BungeKuvunjwaJuni25
#JamiiForums #Siasa #Governance #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
❤1👍1
Unapokuwa na ratiba katika shughuli zako iwe ya Wiki, Mwezi, Miezi au Mwaka inaweza kusaidia kurahisisha baadhi ya mambo yako na pia kukuwezesha kufanya majukumu mengi kwa mpangilio mzuri
#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJamiiAfrica #GoodMorning #Maisha

Jackson Kabalo na Joseph Mrindoko maarufu kwa jina la 'Wachokonozi' wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kusomewa makosa mawili, jana Juni 27, 2025
Wamesomewa mashtaka ya kuchapisha taarifa za uongo kinyume na Kifungu Namba 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao na kutoa maudhui Mtandaoni bila ya kuwa na leseni kinyume na Kifungu Namba 116(3)(b) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta
Wawili hao wanaosimamiwa na Wakili Ally Mhyellah na Simon Mbwambo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), walipatiwa dhamana, na kesi hiyo itatajwa tena kwaajili ya usikilizwaji wa hoja za awali Julai 21, 2025
Soma https://jamii.app/WachokonoziDhamana
#JamiiForums #JFMatukio #DigitalRights #CivilRights #JamiiAfrica

MOROGORO: Mdau aliyejitambulisha ni Mkazi wa Kijiji cha Lungongole kilichopo Halmashauri ya Mji wa Ifakara, anadai Barabara ya Kilosa kuelekea Kijiji cha Kilama “Mwiche Road” ina hali mbaya kutokana na kuharibika
Anaeleza Barabara hiyo ambayo inatumiwa na Wakulima wanaokwenda na kurudi shambani ni njia kuu ya Wakazi wanaoishi upande huo wa Milimani wakati wanapotaka kuelekea Kilosa Road
Anadai maeneo mengine ya Barabara yamekuwa na makorongo makubwa kiasi kwamba Watumiaji imewabidi kuunda njia mbadala katika mashamba ya Watu, anatoa wito TARURA kumalizia kazi waliyoianza
Soma https://jamii.app/Lungongole
#JamiiForums #Accountability #JamiiAfrica #Uwajibikaji

❤1🔥1
Kupitia Jukwa la Habari na Hoja Mchanganyiko ndani ya JamiiForums.com, Mdau ameandika “Kuna Mtu alienda kufanya marekebisho ya cheti cha zamani kwenda kipya, akaambiwa anatakiwa kulipa Tsh. 30,000 wakati Namba ya Malipo ni Tsh. 7,000.”
Mdau anaeleza kuwa amefanya kazi Iringa, RITA Kilolo Huduma zao ni nzuri, anashindwa kuelewa nini shida ya RITA Misungwi! Hivyo anatoa wito Mamlaka kufuatilia ili kujua shida ilipo na kuondoa changamoto hiyo
Soma https://jamii.app/UtendajiRITA
#JamiiForums #Accountability #Governance

❤3👍1
DAR: Baraza la Sanaa la Taifa (#BASATA) limefuta Leseni ya kuendesha Shindano la Miss Tanzania kwa Kampuni ya The Look Company Limited kwa kueleza imeshindwa kutekeleza maagizo halali ya Baraza licha ya kupewa maelekezo kupitia barua Aprili 15, 2025 na Mei 9, 2025
BASATA imesema kibali chao cha kufanya kazi hakijahuishwa kwa zaidi ya Miezi sita, kukaidi agizo la Baraza kwa kutowasilisha nyaraka muhimu kama nakala ya Cheti/Leseni ya kushiriki Shindano la Dunia, kushindwa kuandaa Shindano la Miss Tanzania kwa Mwaka 2023/2024 na kutowakilisha kwenye “Miss World 2024/2025”
Kampuni hiyo inasimamiwa na Basilla Mwanakuzi (Mshindi wa Taji la Miss Tanzania 1998) ambaye pia ni Mwanasiasa. Hivi karibuni (Mei 2025) kupitia ukurasa wake wa Instagram alitoa kauli kadhaa akikosoa baadhi ya maamuzi na Utendaji wa Chama chake cha CCM
Soma https://jamii.app/MissTZKufutwa
#Entertainment #JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, akizungumza na Wanachama wa CCM, amesema "Lazima tuambiane ukweli, Sisi Viongozi huku Meza kuu, na ninyi Viongozi huko, kwasababu sote tunakwenda kwenye maamuzi. Tutende Haki, tuwatendee Haki Watu, ukitenda Moyo wako utajisikia faraja sana."
Soma https://jamii.app/MakamuHemed
#Democracy #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025 #Kuelekea2025 #Siasa #JamiiForums

ZANZIBAR: Chama cha #ACTWazalendo kimetoa taarifa kuwa Juni 26, 2025, Vijana wanne Wafanyabiashara wa Darajani walitekwa na Askari wa Mamlaka ya Mji Mkongwe, wakafungiwa katika chumba kichafu, wakapigwa na baadaye usiku wakatupwa maeneo ya Chukwani Buyu
ACT imeeleza tukio hilo la kinyama ni miongoni mwa matukio ambayo hujirudia kila kukicha kwa Vijana wa Kizanzibari na kwamba wanalichukuliwa tukio hilo kwa mshituko mkubwa
Taarifa ya ACT imedai kutokana mfululizo wa matukio hayo inapendekeza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji Mkongwe ajiuzulu kupisha uchunguzi, iundwe Kamati kuchunguza matukio ya utekaji na mauaji Zanzibar. Pia, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iweke hadharani ripoti za uchunguzi
Soma https://jamii.app/ACTTamkoJuni28
#HumanRights #JamiiAfrica #JamiiForums #Democracy

DAR: Makamu Mwenyekiti wa #CHADEMA – Bara, John Heche ametoa wito kwa Mahakama kutumia Vyumba vikubwa wakati wa kesi ambayo Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Tundu Lissu, ameifungua katika Mahakama Kuu akiiomba Mahakama kufanya marejeo ya kesi ya uchochezi inayomkabili katika Mahakama ya Kisutu
Heche ameyasema hayo alipozungumza na Wanahabari, Juni 27, 2025 baada ya Mahakama hiyo kuamua kuwa uamuzi wa mapingamizi ya Jamhuri utatolewa Julai 11, 2025
Soma https://jamii.app/HecheMahakamaKuu
#Democracy #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025 #Kuelekea2025 #Siasa #JamiiForums
Heche ameyasema hayo alipozungumza na Wanahabari, Juni 27, 2025 baada ya Mahakama hiyo kuamua kuwa uamuzi wa mapingamizi ya Jamhuri utatolewa Julai 11, 2025
Soma https://jamii.app/HecheMahakamaKuu
#Democracy #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025 #Kuelekea2025 #Siasa #JamiiForums
❤1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ZANZIBAR: Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, ametoa wito kwa Viongozi kuwa makini na aina ya Watu wanaoomba Uongozi na kutowapa nafasi ambao wanalenga kuwanunua
Soma https://jamii.app/NukuuZaHemed
#Democracy #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025 #Kuelekea2025 #Siasa #JamiiForums
Soma https://jamii.app/NukuuZaHemed
#Democracy #JamiiAfrica #UchaguziMkuu2025 #Kuelekea2025 #Siasa #JamiiForums
❤2
Elimu si tu kwa Ajira, bali inapaswa kuwafundisha Wanafunzi Maisha ya kuwajibika kama Raia.
Shule na Vyuo havipaswi kufundisha maarifa ya kazi pekee, bali pia kusaidia Wanafunzi kuwa Watu wenye Uwajibikaji, Uadilifu, na Heshima kwa Jamii.
#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #RestlessDevelopment #CivicEducation #UraiaWenyeUelewa

Ujumbe huu uliandikwa na Isaac Asimov, ambaye alikuwa raia wa Marekani, Mwandishi na Profesa aliyefundisha katika Chuo Kikuu cha Boston
Alizaliwa Mwaka 1920 na kufariki Mwaka 1992 akiwa na umri wa Miaka 72
#Governance #JamiiForums #Accountability #Transparency #JFNukuu #JFQuote #Quotes #JamiiAfrica

❤3🔥2👍1