JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau wa JamiiForums.com ameanzisha Mjadala akisema tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, ni muhimu kutafakari kwa makini iwapo Viongozi tuliowachagua waliwakilisha maslahi yetu kikamilifu

Mdau, Mbunge wako ni nani, na juhudi zake Jimboni kwako zimetimiza matarajio yako? Unampa alama ngapi kati ya 10 kulingana na utendaji wake?

Mjadala https://jamii.app/RateYourMP

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #ServiceDelivery #Governance #KuelekeaUchaguzi2025
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KILIMANJARO: Mbunge wa Jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe amekutana na Walimu Shule za Msingi na Sekondari Wilayani hapo kuwashukuru kwa ushirikiano na ametoa Tsh. Milioni 2 yakununua matofali ya kujenga Ofisi za Chama cha Waalimu Hai

Kikao hicho kilifanyika Juni 21, 2025, Mjini Bomang'ombe

Soma https://jamii.app/MbungeWaHai

Video: Bananafm Tz

#Siasa #Accountability #JamiiForums #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, John Mnyika amesema kitendo cha Jaji Hamidu Mwanga, aliyepangwa kusikiliza kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa #CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohamed na wenzake Wawili dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chama hicho, kutotokea Mahakamani ni mwendelezo wa kutotenda Haki

Mnyika ameeleza kuwa tayari wameshaandika barua ya kuonesha kutokuwa na Imani na Jaji huyo na kutaka ajiondoe na shauri hilo apangiwe Jaji mwingine

Katika kesi hiyo Said na wenzake wanadai CHADEMA imekuwa ikiitenga #Zanzibar katika masuala mbalimbali, ikiwemo mgawanyo wa Rasilimali Fedha

Soma https://jamii.app/JajiKesiYaCHADEMA

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Governance #Siasa
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwanachama wa #ACTWazalendo, Wakili Peter Madeleka, amesema kitendo cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kuzuia Uchaguzi Mkuu 2025 kwa ya kudai “reforms” kipindi hiki ni kosa la Jinai

Amesema hayo wakati akihojiwa na Wasafi TV ambapo ameongeza kuwa ana uhakika wa kushinda Ubunge katika Uchaguzi wa 2025 kwa kuwa licha ya changamoto zilizopo bado nafasi ipo kwa Vyama vya Siasa

Madeleka ambaye aliwahi kuwa Askari wa Jeshi la Polisi kabla ya kujipambanua kuwa Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, alijiunga na ACT, Mei 2025

Soma https://jamii.app/MadelekaKauli

#JamiiForums #Kuelekea2025 #Democracy #UchaguziMkuu2025
Kujiheshimu si tu kuhusu namna unavyowatendea wengine, bali zaidi ni namna unavyojitendea mwenyewe. Kujitunza ni tendo la upendo wa ndani, ishara ya kwamba unatambua thamani yako na unathamini maisha yako katika ukamilifu wake

Unapojitunza, unatangaza kuwa nafsi yako ina thamani. Unapojithamini, unawaonesha wengine jinsi ya kukuheshimu. Unapokuwa na amani ndani yako, una uwezo wa kuwapa wengine toleo bora la ‘wewe’ na si kilichobaki.

Jitunze, Jiheshimu, Jipende!

#GoodMorning #JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF #Maisha #Selflove
2🙏2
Juni 16 - 17, 2025, JamiiAfrica iliendesha mafunzo maalum kuhusu Akili Unde katika Uandishi wa Habari (AI in Journalism) yaliyolenga kukuza Uelewa na Ujuzi wa Teknolojia katika Taaluma ya Habari

Mafunzo hayo yalilenga kuendana na Mabadiliko ya Dunia na Teknolojia ya Habari ambapo Wanafunzi walijifunza na kujadiliana masuala anuai kuhusu AI ikiwemo matumizi, faida na changamoto zinazotokana na Teknolojia hiyo hususan suala la Upotoshaji wa Taarifa

Mafunzo haya yaliyohusisha Wakufunzi na Wanafunzi wa Shahada ya Uandishi wa Habari pamoja na Uhusiano wa Umma yalitoa fursa ya kujua namna teknolojia inavyobadilika mara kwa mara na namna ya kukabiliana na taarifa zisizo sahihi zinazozalishwa na AI.

#JamiiAfrica #JamiiForums #AIJournalism #FactChecking
1
Mshiriki wa Shindano la Stories of Change 2024 amependekeza mambo kadhaa kwa Shirika la Posta ili kuboresha Huduma hasa kwa njia ya Mtandao

Anasema ingawa Shirika la Posta limejitahidi kukabiliana na Maendeleo ya Kiteknolojia kwa kiwango fulani, bado kuna changamoto kama vile kutokuwa na Miundombinu ya Kidijitali ya kutosha, ufinyu wa Upatikanaji wa Huduma za Posta katika maeneo ya Vijijini na Ushindani kutoka kwa watoa Huduma wa Kampuni binafsi.

Soma https://jamii.app/PostaHudumaMtandao

#JamiiForums #ServiceDelivery #JamiiAfrica #HudumaZaKijamii
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Familia ya Flavian Methew Nyandikuu (85) Mkazi wa Mwenge Mlalakuwa, Mtaa wa Nyendikuu imedai Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa ‘imewapora’ Viwanja viwili ambavyo wamevimiliki kihalali kwa Miaka 40 na kudai Viwanja hivyo vimekabidhiwa kwa Watu wengine kinyume cha utaratibu

Msemaji wa Familia, Fortunatus Buyobe amesema “Ni Viwanja Namba 2107 na 2120 vipo Kilongawima, Mbezi Beach, ilikuwa sehemu ya shamba baadaye vikapimwa, miaka kadhaa nyuma kuna Wavamizi walijitokeza, kesi ikaenda Mahakamani, Mzee Nyandikuu akashinda na nyaraka halali zipo.”

Akifafanua kuhusu mgogoro huo, Wakili Barnaba Luguwa amesema “Nimepitia nyaraka za hukumu zimeonesha viwanja vinamilikiwa kihalali na Mzee Nyandikuu.”

Akihojiwa na ITV kuhusu madai hayo, Kamishna wa Ardhi Mkoa, Shukran Kyando amesema “Sisi hatujawahi kummilikisha mlalamikaji hiyo ardhi wala hatujawahi kumpa ofa, ardhi ile ilipimwa Mwaka 2000.”

Soma https://jamii.app/FamiliaYaNyandikuu

#JFMatukio #JamiiForums #Accountability #CivilRights
Wadau mbalimbali wa JamiiForums.com wameanzisha mijadala tofauti kuhusu tabia ya Wabunge kutelekeza Majimbo yao na kusubiri hadi Miezi michache kabla ya uchaguzi ndio wanarudi kumalizia miradi na ‘vi zawadi vya hapa na pale’ ili kuwahadaa wapiga kura

Mdau mmoja amesema kama maendeleo anayoyaona sasa yangekuwa yanafanyika kwa utaratibu tangu mwaka wa kwanza wa uongozi, jamii ingekuwa mbali sana

Mdau mwingine amesema Wananchi wanapaswa kujifunza na kutambua tofauti kati ya maendeleo ya kweli na propaganda za kisiasa. Kwa wale wanaotaka kuendelea kuongoza, wajue kuwa Wananchi wa sasa si kama wale wa zamani, macho na masikio yao yako wazi

Mdau, vipi ‘hekaheka’ za jimboni kwako?

Soma https://jamii.app/WabungeMlikuwaWapi

#JamiiAfrica #JamiiForums #KuelekeaUchaguzi2025 #Governance #Accountability #Uwajibikaji #ServiceDelivery
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax amesema Veterani waliopigana Vita ya Kagera ambao walikuwa hawapati Pensheni wataanza kulipwa Julai 2025 na si Julai 2026 kama alivyoeleza Bungeni, Juni 23, 2025 (Bunge la 12 Mkutano wa 19 na Kikao cha 51)

Ikumbukwe Juni 13, 2024, akiwa Bungeni, Waziri Tax aliliambia Bunge “Maveterani wote waliopigana Vita ya Kagera wameshalipwa na hakuna anayedai.”

Aidha, Septemba 2, 2024, Mdau wa JamiiForums.com aliandika “Natoa ushuhuda Mzee wangu ni mmoja kati ya ambao hawajapata kifuta chasho cha kupigana Vita ya Kagera”, pia Desemba 19, 2024, Mdau mwingine aliandika "CPL NGUSSA GULINJA 692 DET sijalipwa malipo yangu ya Vita ya Kagera, kila nikifuatilia naambiwa hakuna anayedai”.

Soma https://jamii.app/MalipoVitaKagera

#JamiiForums #Governance #Uwajibikaji #CivilRights