JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Rushwa ni adui mkubwa wa Maendeleo. Kila shilingi inayotolewa kama Rushwa inaongeza pengo la Huduma bora kwa Mwananchi, inadhoofisha Uchumi, na kuharibu Imani ya Wananchi

Tuchague Uadilifu, tusimamie Haki, na tuchague Maendeleo ya kweli

#JamiiForums #JamiiAfrica #UraiaWenyeUelewa #CivicEducation #RestlessDevelopment
Unaweza kuwa na kipaji, lakini kuna tabia zinaweza kukurudisha nyuma kama vile uvivu, uzembe au kutokuishi kwa mipango

Kipaji pekee hakitoshi, ili uwe na mafanikio achana na tabia hatarishi

#JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF #GoodMorning #Maisha
DAR: Kiongozi wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania (Kanisa la Ufufuo na Uzima), Askofu Josephat Gwajima, kupitia ukurasa wake wa Instagram Jana Juni 21, 2025, alisema alimtembelea na kumjulia hali Padri Kitima

Aliandika “Leo Tarehe 21 Juni 2025 nimepata nafasi ya kumtembelea na kumjulia hali Padre Dr Charles Kitima, Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).”

Askofu Gwajima ambaye mara ya mwisho alionekana akizungumza hadharani Juni 2, 2025 aliongeza “Namshukuru Mungu afya yake imeendelea kuimarika.”

Soma https://jamii.app/GwajimaNaKitima

#JamiiForums #JFMatukio
3
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa majeshi ya Marekani yamefanikiwa kushambulia vituo Vitatu vya Nyuklia vya Iran vilivyopo Fordow, Natanz na Isfahan, huku akiwaonya Iran kutolipiza kisasi

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amepongeza hatua hiyo ya Marekani akiiita “uamuzi wa kishujaa” na kusema kuwa Israel na Marekani waliratibu hatua hizo kwa pamoja.

Aidha, Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Abbas Araghchi amelaani vikali mashambulizi hayo na kusema ni kitendo cha uhuni, akidai yatakuwa na madhara ya kudumu

Soma https://jamii.app/TrumpShambuliziIran

#JamiiAfrica #JamiiForums #Diplomasia
ARUSHA: Jeshi la Polisi limesema linawashikilia Vijana wawili wanaojulikana kwa jina la Wachokonozi ambao ni Joseph Mrindoko (37) na Jackson Kabalo (32) kwa tuhuma za matumizi mabaya ya Mtandao, ambao awali taarifa zilizosambaa Mtandaoni zilidaiwa wamechukuliwa na Watu Wasiojulikana waliokuwa na silaha

Taarifa ya Polisi ya Juni 21, 2025 imesema Watuhumiwa hao walikamatwa na Jeshi la Polisi mnamo Juni 20, 2025

Aidha, katika taarifa hiyo Jeshi la Polisi limeonya watumiaji wa Mitandao ya Kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hawana uhakika nazo zinazoleta taharuki katika Jamii, hasa zile za kuzusha kuwa Watuhumiwa wamekamatwa na Watu Wasiojulikana jambo ambalo sio la kweli.

Soma https://jamii.app/WachokonozMatumizMtandao

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #FreedomofSpeech
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Baadhi ya Waumini wa Kanisa la Kanisa la 'Glory of Christ Tanzania' (Kanisa la Ufufuo na Uzima), wameamriwa kutawanyika wakati walipokuwa wakifanya maombi pembezoni mwa Barabara maeneo ya karibu na kanisa hilo lililopo Ubungo

Soma https://jamii.app/WauminiJuni22

#JamiiForums #JFMatukio
2
DAR: Chama cha #ACTWazalendo kimesema Serikali imetenga Tsh. Trilioni 1 kwaajili ya Uchaguzi Mkuu, ambapo tayari Tsh. Bilioni 741.5 zimetumika na Tsh. Bilioni 378.2 zimeelekezwa kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa 2025

ACT imesema “Tunasisitiza fedha hizo ni mali ya Wananchi wa #Tanzania si mali ya #CCM wala Chama chochote cha Siasa, zinapaswa kutumika kuimarisha haki na Demokrasia, si kuharibu mchakato wa Uchaguzi kwa upendeleo au udhalimu wa Kisiasa.”

Taarifa ya ACT imeeleza “Tunakumbusha kuwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019, zaidi ya Tsh. Bilioni 254.82 zilitumika, badala ya kuleta haki, zilishuhudiwa kuwezesha uporaji wa #Demokrasia. Hali hiyo ya kuvunjwa kwa misingi ya haki bado inaendelea hadi sasa.”

Soma https://jamii.app/ACTTamkoJuni

#JamiiForums #Democracy #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
MICHEZO: Timu ya #Yanga imeshinda Magoli 5-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC na hivyo kuendelea kubaki kileleni katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufikisha Pointi 79, nafasi ya pili inashikwa na #Simba ambayo imefikisha alama 78 baada ya kuifunga Kagera Sugar Goli 1-0

Kutokana na matokeo hayo bingwa wa ligi hiyo msimu huu anatarajiwa kujulikana wiki ijayo Jumatano Juni 25, 2025 ambapo Yanga itaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Mkapa ukiwa ni mchezo wa mwisho kabisa wa Ligi Kuu Msimu wa 2024/25

Soma https://jamii.app/LigiKuuMatokeo

#JFSports #JFLigiKuu25 #JamiiForums
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MWANZA: Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Lugata Wilayani Sengerema, wameandamana kupinga hatua za viongozi wa Chama hicho ngazi ya Kata kuzuia ujenzi wa Ofisi ya chama hicho, baada ya Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo, kuahidi kuijenga ofisi hiyo kwa gharama zake

Wanachama hao wamesema kuwa wao kama wanachama wa #CCM wanahaki ya kupata msaada kutoka kwa Mbunge wao ambaye amejitolea kujenga ofisi, lakini kuna vikwazo kutoka kwa viongozi wa Chama hicho ngazi ya Kata na kuomba mamlaka husika kuingilia kati Suala hilo

Soma https://jamii.app/ShigongoAkataliwaKujengaOfisi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #ServiceDelivery
2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wakili Addo November kutoka Chama cha Wanasheria wa Serikali amesema “CHADEMA wakija wakitaka kushiriki Uchaguzi nafasi wanayo 'as long as' hatujafikia hatua ya kuanza mchakato wa uchaguzi"

Alisema hayo katika Kongamano la Sheria lililofanyika Juni 21, 2025, alipokuwa akijibu swali la mmoja wa wadau aliyeuliza iwapo CHADEMA bado watakuwa na nafasi ya kushiriki katika Uchaguzi kama wakiamua

Soma https://jamii.app/CHADEMAKanuniUchaguzi

#JamiiAfrica #JamiiForums #KuelekeaUchaguzi2025
2
Kusoma kwa undani habari hizi na nyingine zilizojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
1