JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Uchambuzi wa Bajeti kutoka Chama cha ACT - Wazalendo umesema kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 Serikali imepanga kutumia Trilioni 56.49, ambapo Mgawanyo wa matumizi ni trilioni 38.99 kwa ajili ya Mishahara, Posho, Magari na Misafara ya Viongozi, Mabango ya Kumsifu Rais, Chai na Deni la Serikali (69.04%)

Wakati Miradi ya Barabara, Mikopo ya Wanafunzi, ujenzi wa vituo vya Afya, Shule, Dawa, Maji, Pembejeo za Kilimo, imetengewa Trilioni 17.49 (30.96%), ikimaanisha katika kila Tsh. 1,000, Tsh. 700 inaenda kwenye Mishahara, Chai, Deni na Posho huku Tsh. 300 tu ndio inaenda kuhudumia Wananchi

ACT imesema Mgawanyo wa Bajeti uliopelekwa kwenye matumizi ya Maendeleo ya Wananchi ni kiwango kidogo zaidi na itategemea zaidi Fedha za nje au Mikopo.

Soma zaidi Uchambuzi huu https://jamii.app/UchambuziBajetiACTWazalendo

#JamiiForums #Uwajibikaji #JamiiAfrica #Accountability #BajetiKuu2025
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete amesema licha ya Vyama ya Siasa kuwa na kaulimbiu zake lakini itakapofika Siku ya kupiga kura, Akili za kuambiwa changanya na zako

Ameyasema hayo leo Juni 21, 2025 katika ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Sheria JNICC

Soma https://jamii.app/KikweteAkiliKura

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #UchaguziMkuu2025 #KuelekeaUchaguzi2025
DAR: Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura amesema moja ya changamoto inayosumbua Sekta ya Habari ni suala la Upotoshaji wa Taarifa unaofanyika kwa makusudi ama kwa kutofahamu

Amesema hali hiyo imetokana na maendeleo ya Teknolojia ambayo yanatengeneza fursa kwa usambaaji wa Taarifa Potoshi, ambapo ameeleza hoja za kukabiliana na changamoto hizo ni sehemu ya Mada zitakazojadiliwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Mabaraza ya Habari Afrika (Julai 14 - 17, 2025)

Aidha, ameongeza kuwa Mkutano huo utajadili mijadala ya kitalaamu kuhusu changamoto zinazoathiri Tasnia ya Habari na namna Mabaraza ya Habari kote Duniani yanavyokabiliana na changamoto hizo

Soma https://jamii.app/MabarazaYaHabari

#JamiiForums #JamiiAfrica #FactChecking #HakikiTaarifa #VisitJamiiCheck
1
DAR: Akizungumzia umuhimu wa kuwa na Watu wanaohusika Uhakiki wa Taarifa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura amesema “Uwepo wa Wadau kama #JamiiAfrica unahitajika kutumika kusaidia kutoa elimu ya Uhakiki wa Taarifa kama ambavyo wamekuwa wakifanya (kupitia #JamiiCheck).”

Ameongeza “Tunahitaji Wadau aina hiyo waongezeke kusaidia kukabiliana na Taarifa Potoshi hasa wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, kwani kupotosha Sera, Ilani au Taarifa za Watu wakati huu tunapoelekea katika kampeni kunaweza kuwa na madhara makubwa.”

Amesema hayo wakati akizungumzia ujio wa Mkutano wa Kimataifa wa Mabaraza ya Habari Afrika (Julai 14-17, 2025) unaoandaliwa na MCT kwa kushirikiana na Mtandao wa Mabaraza Huru ya Habari Afrika (NIMCA), Umoja wa Mabaraza ya Habari ya Afrika Mashariki (EAPC) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Soma https://jamii.app/MCTFactChecking

#JamiiForums #JamiiAfrica #FactChecking #HakikiTaarifa #VisitJamiiCheck
DAR: Imeelezwa kuwa nguvu kubwa ya Kiuchumi ya Kampuni na Taasisi za Kidigitali imechangia kuvinyonya Kiuchumi Vyombo vya Habari vinavyotambulika kama "Traditional Media" (ikiwemo Magazeti, Vituo vya Runinga na Redio) kwa kuwa vimeshindwa kuendana na kasi ya ukuaji wa Soko la Digitali

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura amesema kutokana na hali hiyo Vyombo vya Habari hivyo vinatakiwa kujengewa uwezo na Wadau ili viweze kushindana na Vyombo vya Habari vya Mtandaoni

Amesema kuwa hali hiyo imesababisha Uchumi wa TV, Redio na Magazeti kudorora kiasi kwamba hata taarifa zenye maslahi kwa Umma nazo zimekuwa changamoto kufanyika katika ubora unaotakiwa ikiwemo Habari za Uchunguzi

Soma https://jamii.app/MabarazaYaHabari

#JamiiForums #JamiiAfrica
#PressFreedom #DigitalRights #Accountability
4
Rushwa ni adui mkubwa wa Maendeleo. Kila shilingi inayotolewa kama Rushwa inaongeza pengo la Huduma bora kwa Mwananchi, inadhoofisha Uchumi, na kuharibu Imani ya Wananchi

Tuchague Uadilifu, tusimamie Haki, na tuchague Maendeleo ya kweli

#JamiiForums #JamiiAfrica #UraiaWenyeUelewa #CivicEducation #RestlessDevelopment
Unaweza kuwa na kipaji, lakini kuna tabia zinaweza kukurudisha nyuma kama vile uvivu, uzembe au kutokuishi kwa mipango

Kipaji pekee hakitoshi, ili uwe na mafanikio achana na tabia hatarishi

#JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF #GoodMorning #Maisha
DAR: Kiongozi wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania (Kanisa la Ufufuo na Uzima), Askofu Josephat Gwajima, kupitia ukurasa wake wa Instagram Jana Juni 21, 2025, alisema alimtembelea na kumjulia hali Padri Kitima

Aliandika “Leo Tarehe 21 Juni 2025 nimepata nafasi ya kumtembelea na kumjulia hali Padre Dr Charles Kitima, Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).”

Askofu Gwajima ambaye mara ya mwisho alionekana akizungumza hadharani Juni 2, 2025 aliongeza “Namshukuru Mungu afya yake imeendelea kuimarika.”

Soma https://jamii.app/GwajimaNaKitima

#JamiiForums #JFMatukio
3
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa majeshi ya Marekani yamefanikiwa kushambulia vituo Vitatu vya Nyuklia vya Iran vilivyopo Fordow, Natanz na Isfahan, huku akiwaonya Iran kutolipiza kisasi

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amepongeza hatua hiyo ya Marekani akiiita “uamuzi wa kishujaa” na kusema kuwa Israel na Marekani waliratibu hatua hizo kwa pamoja.

Aidha, Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Abbas Araghchi amelaani vikali mashambulizi hayo na kusema ni kitendo cha uhuni, akidai yatakuwa na madhara ya kudumu

Soma https://jamii.app/TrumpShambuliziIran

#JamiiAfrica #JamiiForums #Diplomasia
ARUSHA: Jeshi la Polisi limesema linawashikilia Vijana wawili wanaojulikana kwa jina la Wachokonozi ambao ni Joseph Mrindoko (37) na Jackson Kabalo (32) kwa tuhuma za matumizi mabaya ya Mtandao, ambao awali taarifa zilizosambaa Mtandaoni zilidaiwa wamechukuliwa na Watu Wasiojulikana waliokuwa na silaha

Taarifa ya Polisi ya Juni 21, 2025 imesema Watuhumiwa hao walikamatwa na Jeshi la Polisi mnamo Juni 20, 2025

Aidha, katika taarifa hiyo Jeshi la Polisi limeonya watumiaji wa Mitandao ya Kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hawana uhakika nazo zinazoleta taharuki katika Jamii, hasa zile za kuzusha kuwa Watuhumiwa wamekamatwa na Watu Wasiojulikana jambo ambalo sio la kweli.

Soma https://jamii.app/WachokonozMatumizMtandao

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #FreedomofSpeech
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Baadhi ya Waumini wa Kanisa la Kanisa la 'Glory of Christ Tanzania' (Kanisa la Ufufuo na Uzima), wameamriwa kutawanyika wakati walipokuwa wakifanya maombi pembezoni mwa Barabara maeneo ya karibu na kanisa hilo lililopo Ubungo

Soma https://jamii.app/WauminiJuni22

#JamiiForums #JFMatukio
2
DAR: Chama cha #ACTWazalendo kimesema Serikali imetenga Tsh. Trilioni 1 kwaajili ya Uchaguzi Mkuu, ambapo tayari Tsh. Bilioni 741.5 zimetumika na Tsh. Bilioni 378.2 zimeelekezwa kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa 2025

ACT imesema “Tunasisitiza fedha hizo ni mali ya Wananchi wa #Tanzania si mali ya #CCM wala Chama chochote cha Siasa, zinapaswa kutumika kuimarisha haki na Demokrasia, si kuharibu mchakato wa Uchaguzi kwa upendeleo au udhalimu wa Kisiasa.”

Taarifa ya ACT imeeleza “Tunakumbusha kuwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019, zaidi ya Tsh. Bilioni 254.82 zilitumika, badala ya kuleta haki, zilishuhudiwa kuwezesha uporaji wa #Demokrasia. Hali hiyo ya kuvunjwa kwa misingi ya haki bado inaendelea hadi sasa.”

Soma https://jamii.app/ACTTamkoJuni

#JamiiForums #Democracy #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025