JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Jeshi la Polisi linadaiwa kuzuia kufanyika kwa Mkutano wa #CHADEMA na Waandishi wa Habari uliokuwa ufanyike leo Juni 17, 2025 katika Ukumbi wa Seashells Millennium Hotel, kwa maelezo kwamba Chama hicho kimezuiwa na Mahakama kufanya shughuli za Kisiasa

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia amesema wakati wakijiandaa kwa Mkutano huo, walifika Watu waliojitambulisha kuwa ni Maafisa wa Polisi na kuzuia usifanyike

Alipoulizwa kuhusu zuio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema “Wanalalamika nini? Basi tunafuatilia wasichokijua na ambacho wanakilalamikia.”

Soma https://jamii.app/CDMBanPolisiDar

#JamiiForums #JamiiAfrica #Siasa #Democracy #UchaguziMkuu2025
1
DODOMA: Kampuni za madini za Geita Gold Mine (GGM), Shanta na Buckreef Gold zimeingia mikataba na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya utekelezaji wa Sheria ya Madini, inayozitaka kampuni binafsi za uchimbaji madini kuiuzia BoT dhahabu inayozalishwa na kampuni hizo kwa kiwango kisichopungua Asilimia 20

Mikataba hiyo imesainiwa na Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba mbele ya Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, Juni 16, 2025

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema mikataba hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini, kinachowataka wachimbaji wa Madini kutenga 20% ya uzalishaji wao kwaajili ya kuiuza katika masoko ya ndani ikiwemo kuiuzia BoT, ambayo imepewa haki ya kwanza Kisheria ya ununuzi wa Dhahabu.

Ameongeza ‘‘Hadi leo BoT imenunua Tani 5 za dhahabu sawa na Dola za Marekani Milioni 554 na kupitiliza malengo yake ya kununua Dhahabu ya Dola za Marekani Milioni 350."

Soma https://jamii.app/BOTKuuziwaDhahabu

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uchumi
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ametoa onyo kwa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina pamoja na Wanasiasa wengine wa Mkoa wa Simiyu, kuacha kutumia zao la Pamba kama mtaji wa Kisiasa

Bashe amesema Mpina aliwahi kumdanganya Hayati Rais Magufuli kuhusu Bei ya Zao la Pamba Duniani na kusababisha Wakulima kupata hasara, kwa kuuza Pamba kwa Tsh. 500

Soma https://jamii.app/BasheMpinaKuuaKitalu

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #JamiiAfrica #Siasa #Transparency
2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amemwambia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Jimbo lake bado linamdai na kwamba maeneo mengine yanayodai hayamdai, fedha zao zihamishiwe Kisesa

Ameyasema hayo leo Juni 17, 2025 wakati wa mkutano wa hadhara Wilayani Meatu, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Rais Samia Mkoani humo.

Soma https://jamii.app/SamiKisesaTunakudai

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Rais Samia Suluhu akiwa ziarani Mkoani Simiyu, amesema Mbunge wa Kisesa (Luhaga Mpina) 'amerukaruka' kwenye kutaja Mambo yaliyofanyika Jimboni kwake, huku akieleza amelidharau Jimbo lake kwa kusema "Kisesa iko kama Mwanamke aliyesuka Nywele"

Soma https://jamii.app/SamiaMpinaKisesa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #UchaguziMkuu2025 #KuelekeaUchaguzi2025
DAR: Kesi ya Marejeo iliyopo Mahakama Kuu Dar es Salaam iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa CHADEMA-Taifa, Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri ambayo ilipangwa kutajwa leo Juni 17, 2025 imeahirishwa hadi Juni 27, 2025.

Shauri hilo lilipangwa kusikilizwa kwa njia ya Mtandao mbele ya Jaji Mkwizu, lakini Mahakama imeagiza kuwa litakapotajwa tena Juni 27, Lissu anatakiwa kufikishwa Mahakamani

Katika shauri hilo Lissu anaoimba Mahakama kufanya marejeo ya mwenendo wa Kesi ya tuhuma za 'kutoa taarifa za uongo Mtandaoni', ambayo inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi Muhini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Soma https://jamii.app/KesiMarejeoLissu

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Rais Samia Suluhu amesema Vijana wanne wamepoteza maisha kwa ajali ya gari wakiwa njiani kuelekea katika mkutano uliofanyika leo, Juni 17, 2025, ambapo kabla ya mkutano huo Rais alitembelea majeruhi wa ajali hiyo, waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya Meatu

Awali, Jeshi la Polisi Mkoa lilitoa taarifa kuwa Watu wanne wamepoteza maisha na wengine 15 wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea Kijiji cha Mwamishari, Kata ya Mwamishari, Meatu ikihusisha gari aina ya Scania lililobeba Wananchi waliokuwa wanatoka kwenye Zoezi la Chanjo ya Mifugo na Utambuzi, jana Juni 16, 2025 Usiku

Soma https://jamii.app/AjaliSimiyuJuni16

#JFMatukio #JamiiForums #Misinformation #Disinformation
3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Emilian J. Duzu (21) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya Gerald P. Said (22), Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu katika Chuo hicho, tukio ambalo limetokea Alfajiri ya Juni 14, 2025

Polisi imeeleza tukio lilitokea katika maeneo ya Klabu ya Muziki ya Mbeya Pazuri, ikidaiwa Emilian alimjeruhi Gerald kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali tumboni, akakimbizwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya lakini alifariki Saa 7:00 Mchana

Soma https://jamii.app/AmuuaMwanafunziClub

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio
2
Vijana tusibaki kuwa watazamaji wa kinachoendelea kwenye jamii yetu, tujifunze haki na wajibu wetu, tujue sheria na sera zinazotugusa na tushiriki kikamilifu kwenye maamuzi yanayojenga mustakabali wetu

Kila mmoja wetu ana nafasi ya kuwa sehemu ya mabadiliko tunayoyataka, kwa kufanya maamuzi sahihi

Tuchukue hatua kwa kufuatilia taarifa kwa makini, kuhoji kwa hoja, na kutoa maoni yanayojenga. Tuwajibike sasa kwa mabadiliko na maendeleo tunayoyataka katika Jamii zetu

#JamiiAfrica #JamiiForums #RestlessDevelopment #RaiaWajibika #CivicEducation #SautiYaRaia #UraiaWenyeUelewa
KENYA: Polisi wa kutuliza ghasia wamempiga Risasi Kijana mmoja aliyekuwa kwenye #Maandamano ya kudai haki kwenye kifo cha Mwanaharakati Albert Ojwang, ambaye Uchunguzi na Mahojiano ya Polisi vilimebaini alifariki kwa kupigwa na Wafungwa kwa amri ya Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS) na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (DIG)

Video inayosambaa Mtandaoni inawaonesha Askari wawili wa kutuliza ghasia wakimfuata Kijana muuza Barakoa, kumpiga na kitako cha Bunduki, kisha kuongea nae kidogo kabla ya Polisi mmoja wao kumnyooshea bunduki na kumfyatulia Risasi, kisha kuondoka

Imeelezwa, Polisi aliyehusika katika tukio hilo tayari anashikiliwa, baada ya Inspekta Jenerali wa Huduma ya Polisi ya Taifa (NPS) kuagiza kukamatwa mara moja na kufikishwa Mahakamani

Soma https://jamii.app/KifoRaiaProtestOjwang

#Democracy #HumanRights #JamiiAfrica #JamiiForums #PoliceBrutarity
1
DIPLOMASIA: Siku kadhaa baada ya Rais wa Marekani, #DonaldTrump kuwaonya raia wa #Iran waliopo Mji wa Tehran kuhama, kwa kile alichoeleza kutakuwa na mashambulizi yanayoweza kufanyika katika eneo hilo, amedai Marekani ina udhibiti wa anga la Iran

Kupitia Mtandao wa Truth Social, Trump ameandika “Marekani sasa inadhibiti kikamilifu anga la Iran. Iran ilikuwa na vifaa vizuri vya kufuatilia anga na ulinzi wa kutosha na vingi lakini haviwezi kulinganishwa na ‘vitu’ vilivyotengenezwa na Wamarekani. Hakuna anayefanya vizuri zaidi ya Marekani.“

Ameongeza “Tunajua kwa uhakika kabisa alipojificha huyo anayeitwa ‘Kiongozi Mkuu’ (akimaanisha Ayatollah Ali Khamenei). Ni mlengwa rahisi, lakini yuko salama pale alipo hatutamwondoa (kumuua!), angalau si kwa sasa. Hatutakubali makombora yaelekezwe kwa raia au kwa Wanajeshi wa Marekani. Subira yetu inaanza kuisha. Asanteni kwa kulipa hili uzito!”

Soma https://jamii.app/MarekaniKumilikiAngaIran

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio
2
Usikimbilie kufanya mengi bila ubora, fanya kwa kiasi lakini kwa kiwango cha juu na ubora zaidi

Katika maisha au kazi mafanikio si idadi, bali ubora ndio huleta matokeo ya kweli

#JamiiAfrica #JamiiForums #Maisha #GoodMorning #AmkaNaJF
1
Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa mamlaka husika kushughulikia kero ya mazingira duni ya vyoo vya Stendi Kuu ya Mkanaledi ya Mtwara, akidai hali hiyo inahatarisha #Afya za Watumiaji na wanavyovizunguka

Soma https://jamii.app/VyooVichafuMkanaledi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #JFMdau2025
1
Kupitia Televisheni ya Taifa ya Iran, Wananchi wamehimizwa kuondoa programu ya #WhatsApp kwenye Simu zao, ikidaiwa (bila ushahidi wowote wa moja kwa moja) kuwa programu hiyo inakusanya taarifa za Watumiaji na kuzipeleka kwa #Israel

Katika taarifa yake, Kampuni ya #Meta ambayo inamiliki WhatsApp imesema “Tunasikitishwa na ripoti hizi za uongo ambazo huenda zikatumiwa kama kisingizio cha kuzuiwa kwa Huduma zetu wakati Watu wanazihitaji zaidi.”

Serikali ya #Iran imekuwa ikizuia upatikanaji wa Mitandao mbalimbali ya Kijamii kwa Miaka mingi, lakini Watu wengi nchini humo hutumia mbinu za kukwepa vizuizi hivyo kama #proxies na Mitandao Binafsi ya Intaneti (VPNs) ili kuendelea kupata Huduma

Mwaka 2022, Iran ilipiga marufuku WhatsApp na Google Play wakati wa Maandamano makubwa ya kupinga Serikali yaliyotokana na kifo cha Mwanamke aliyekuwa ameshikiliwa na Polisi wa Maadili wa Nchi hiyo. Marufuku hiyo iliondolewa mwishoni mwa Mwaka 2024

Soma https://jamii.app/IranVSWhatsApp

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance
1