JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Serikali ya #Tanzania imekanusha madai yaliyotolewa na Wanaharakati wa #Kenya na #Uganda, Boniface Mwangi na Agather Atuhaire kuhusu kufanyiwa Unyanyasaji wa kingono, baada ya kushikiliwa Nchini walipokuja kusikiliza kesi dhidi ya Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu

Akizungumza kwenye mahojiano ya Simu na DW Swahili, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema "Hii Nchi ina Heshima zake, inaheshimiwa na kila Mtu na Watu wote wanaifahamu Tanzania. Wao si Watu wa kwanza kuja Tanzania, kama wanakwenda kuzalisha tuhuma zao za uongo, wacha waendelee kufanya hivyo lakini Tanzania haiko hivyo."

Soma https://jamii.app/MsingwaMwangiAgather

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #Governance

Video credit: DW Swahili
2
ARUSHA: Mdau wa JamiiForums.com anadai Wasimamizi wa Soko la NMC - Samunge wamekuwa na Mfumo mbaya wa Ukusanyaji Ushuru, kitu kinachosababisha baadhi ya Wafanyabiashara kunyanyaswa kwa maneno mabaya ya kashfa, na wengine kunyang'anywa bidhaa zao pale wanaposhindwa kulipa Ushuru kwa Siku husika

Ameshauri Halmashauri itengeneze Mfumo wa malipo ili kurahisisha zoezi, ikiwezekana kila Mfanyabiashara awe na Namba yake ya kumbukumbu ya malipo

Pia, ameshauri Halmashauri ifuatililie Utendaji kazi wa Wakusanya Ushuru ili kuwabaini wanaonyanyasa Wafanyabiashara.

Soma https://jamii.app/SamungeUshuruSoko

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #Accountability #Uwajibikaji
DAR: Mgogoro wa Ardhi unaoendelea katika eneo la Mbopo, Wilaya ya Kinondoni umeibua malalamiko kutoka kwa Wakazi na Wamiliki wa Viwanja wanaodai kunyimwa Haki zao, huku wakiomba Serikali kuchunguza utendaji wa Shirika la Maendeleo la Dar (DDC), linalosimamia zoezi la upimaji na uuzaji wa Ardhi katika eneo hilo.

Wananchi wanadai DDC imekuwa ikivamia maeneo ya Watu na kuyapima upya kwa upendeleo, maeneo yanafinywa na kugawiwa kwa wengine bila ridhaa ya wamiliki halali. Kipande kinachobaki huuzwa kwa Watu wengine, mara nyingi kwa ushawishi wa Kifedha au Urafiki wa karibu.

Baada ya kufika Mbopo kusikiliza malalamiko hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule ameahidi kufanya ziara maalum katika eneo hilo ili kujionea hali halisi. Hata hivyo, alieleza DDC haikuweza kushiriki mkutano huo kutokana na dharura ya kikazi, lakini aliwahakikishia Wananchi kuwa watahusishwa katika Ukaguzi ujao

Soma https://jamii.app/DDCViwanjaMbopo

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #Accountability #Uwajibikaji
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
IRINGA: Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Festo Kiswaga ametangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Isimani Mkoani Iringa katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, ameweka hadharani mpango wake huo wakati alipozungumza na Waandishi wa Habari, jana Juni 3, 2025

Soma https://jamii.app/LukuviTutamstaafisha

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #KuelekeaUchaguzi2025
2
#HISTORIA: Kuna Bustani katikati ya Barabara za Samora, India, Aggrey na Mosque Jijini Dar es Salaam, ambapo ndani yake kuna Kaburi ambalo halina jina, tarehe wala maelezo yoyote kuhusu aliyezikwa hapo

Kaburi hilo linadaiwa kuwa la Sharif Abdul Shakur Salim L’attasi, aliyekuwa Diwani wa Kijiji cha Mzizima, na Imamu wa Msikiti uliokuwa jirani na hapo, ambaye alifariki Mwaka 1862 kabla ya Sultani Majid kuhamishia Makao Makuu ya Sultanate kutoka Zanzibar hadi Pwani ya Tanganyika

Inaelezwa Wajerumani walipofika Tanganyika walipata upinzani kutoka Jumuiya ya Waislam na wenyeji kuhusu kuvunjwa kwa Msikiti huo. Baadae walikubaliana kuuhamisha Msikiti huo na kujengwa Kitumbini ila Kaburi la Sharif libaki hapohapo kama ukumbusho kwa walioleta Uislam Dar es Salaam.

Soma Historia hii zaidi https://jamii.app/HistoriaKaburiDar

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFHistoria
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Viti Maalum, Riziki Said Lulila akichangia Hotuba ya Wizara ya Fedha, leo Juni 4, 2025, ametaka fedha zinazoingia nchini zikaguliwe na zichunguzwe kwa kina kwani zinaweza kuingia kwenye michakato ambayo siyo iliyolengwa

Soma https://jamii.app/PesaZichunguzweNje

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #Accountability #KuelekeaUchaguzi2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Mbunge wa Jimbo la Mbogwe (Geita), Nicodemas Maganga, ameishauri Serikali kutumia njia aliyoiita ni rahisi ya kuwabaini Watakatishaji Fedha, ikiwa ni pamoja na pale Mtu anapoonekana anafanya Maendeleo lazima Serikali ijue anajishughulisha na nini

Nicodemas amesema "Fedha haramu zipo, unajuaje zipo? Unaweza ukamuona Mtu anajenga ghorofa lakini hajulikani anafanya Biashara gani."

Soma https://jamii.app/MPKujengaGhorofa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #Bungeni #MoneyLaundering
Mdau wa JamiiForums.com ametolea mfano, katika Mtaa anaoishi, waliposikia Mwenge utapita kuzindua Kisima cha Maji na Vyumba vya Madarasa, ghafla walishuhudia 'Greda' likisafisha Barabara mchana na usiku, Mafundi wakikesha eneo la Mradi na viongozi wakiwa karibu kusimamia kila hatua

Hilo lilifanya ajiulize: Je, kuna bajeti maalumu inayotolewa kwaajili ya Utekelezaji wa Miradi kwa haraka wakati wa Mwenge? Na kama hakuna, kwanini jitihada kama hizi hazifanyiki wakati wote hata bila Mwenge?

Shiriki Mjadala huu zaidi https://jamii.app/KasiUwajibikajiMwenge

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #JamiiAfrica #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii
1👏1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche, ametangaza Chama hicho kitafungua kesi kupinga uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa, akisema ameenda kinyume na Sheria na #Demokrasia

Ametoa kauli hiyo leo Juni 4, 2025 alipowasilisha maazimio ya Kamati Kuu ya CHADEMA, akisema "Kamati Kuu baada ya kutafakari kwa kina imeamua kwenda Mahakamani kwa vile imeshindwa kuiona nia njema ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika maamuzi yake kuhusu kujaza nafasi zilizo wazi za Viongozi ambao walishachaguliwa."

Kuhusu ruzuku amesema "Tunaenda Mahakamani kwasababu Msajili wa Vyama vya Siasa amechukua jukumu la kuzuia ruzuku ya Chama chetu, sasa Sheria ya Vyama Siasa, kifungu cha 18(6) kinasema Msajili ana uwezo wa kuzuia ruzuku ya Chama kingine chochote cha Siasa kinachopokea ruzuku pale tu ambapo kuna kweli ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Chama hicho."

Soma https://jamii.app/CHADEMAMahakamani

#Democracy #JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa
2
Uongozi si nafasi ya kujitajirisha, bali ni jukumu la kusimamia Haki. Sio kutafuta umaarufu, bali kutumikia Watu kwa Moyo na Utu.

Dunia inahitaji Viongozi wanaotanguliza Haki na Ubinadamu mbele ya maslahi binafsi. Uongozi wa kweli hujengwa juu ya Misingi ya Maadili, si tamaa.

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #AmkaNaJF #GoodMorning
1👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Mbunge wa Jimbo la Kalambo, Sinkamba Josephat Kandege akichangia kwenye uwasilishaji wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya fedha kwa mwaka 2025 - 2026, jana Juni 4, 2025, alilalamikia kuhusu ukubwa wa gharama za makato kwenye miamala ya fedha ya kielektroniki, hivyo kusababisha Wananchi kuepuka kufanya miamala ya aina hiyo

Soma https://jamii.app/MakatoMiamalaMakubwa

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFDigitali #Accountability
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#JFKUMBUKIZI: Ijumaa ya Septemba 7, 1973 yalifanyika Maandamano makubwa ya Wananchi Jijini Dar es Salaam kuunga Mkono Kampeni dhidi ya Mavazi yasiyofaa

Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Rashidi Mfaume Kawawa, Maafisa wa Serikali, Vijana wa TANU na Mashirika mbalimbali walihudhuria kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika mwisho wa Maandamano hayo, katika Makao Makuu ya TANU Mtaa wa Lumumba

CREDIT: ISSA MICHUZI

Soma https://jamii.app/MaandamanoVimini1973

#JamiiForums #JamiiAfrica #Historia
2🤣1
Mwamuzi wa kati, Hery Sasii aliyecheza mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya #Simba dhidi ya Singida Black Stars SC, amefungiwa Miezi 6 kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo huo ambapo Simba ilishinda Goli 1-0 (lililofungwa na Steven Mukwala) baada ya kufanya maamuzi mengi yaliyoashiria kushindwa kutafsiri vema Sheria 17 za Soka

Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu imeeleza kuwa adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42:1(1.1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi

Aidha, Kocha wa Simba, Fadlu Davis ametozwa faini ya Tsh. Milioni 2 kwa kosa la kuishutumu Bodi ya Ligi Kuu wakati akihojiwa na Azam TV, kuwa ina ajenda tofauti kuhusiana na ratiba ya michezo ya klabu hiyo kwenye Ligi Kuu ya NBC

Soma https://jamii.app/RefaKufungiwa

#JFSports #JamiiForums
2
DAR: Katibu Mkuu wa #ACTWazalendo, Ado Shaibu amemtambulisha Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda kuwa amejiunga kuwa Mwanachama wa Chama hicho

Kwa takribani Miaka 20, Sheikh Ponda amekuwa akijipambanua kama Mwanaharakati huru wa kutetea Haki za Binadamu Nchini Tanzania

Soma https://jamii.app/PondaAjiungaACT

#JamiiForums #JFMatukio #Kuelekea2025 #Democracy #UchaguziMkuu
2