JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DRC: Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepiga marufuku Vyombo vya Habari Nchini humo kuripoti shughuli zote za aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo, Joseph Kabila, pamoja na kuwahoji Wanachama wa Chama chake cha Siasa

Agizo hili linakuja wakati kukiwa na Mivutano mikali ya Kisiasa kati ya Kabila na Serikali ya Rais Félix Tshisekedi, ambapo Mamlaka ya kusimamia Vyombo vya Habari nchini DRC (CSAC) imesema Chombo chochote kitakachokiuka marufuku hiyo kitakabiliwa na adhabu, ikiwemo kufungiwa

Mamlaka Nchini humo inaripotiwa kuongeza juhudi za kumfungulia mashtaka Kabila kwa tuhuma za Uhaini na madai ya kuwa na mafungamano na kundi la Waasi la M23, ambalo limekuwa likipambana na jeshi la Serikali, Mashariki mwa Nchi japokuwa Kabila amekanusha madai hayo

Soma https://jamii.app/BanReportingKabila

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #PressFreedom #Democracy
3
DAR: Mdau ndani ya JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kushughulikia changamoto ya udondokaji wa mabati katika ghorofa lililopo Mtaa wa Nyamwezi na Mkunguni, kwani yanawajeruhi wapita njia na Wafanyabiashara wa eneo hilo

Soma https://jamii.app/MabatiKudondokaKariakoo

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #ServiceDelivery #Mdau2025
1
TANZIA: Rais wa zamani wa #Zambia, Edgar Chagwa Lungu, ameaga Dunia akiwa na Umri wa Miaka 68, ambapo Chama chake cha Patriotic Front (PF) kimesema alikuwa akipatiwa Matibabu maalum Afrika Kusini kwa Ugonjwa ambao haukuwekwa wazi

Lungu aliongoza Taifa la Zambia kwa kipindi cha Miaka sita, kuanzia Mwaka 2015 hadi 2021. Alichukua Madaraka baada ya kifo cha Mtangulizi wake, Michael Sata. Alishinda Uchaguzi mdogo wa Rais Januari 2015 na kisha akachaguliwa tena kwa muhula kamili Mwezi Agosti 2016.

Soma https://jamii.app/EdgarLunguDies

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais Samia Suluhu Hassan amesema “Utumishi wa dini ni kusaidia Jamii, siyo kama wale wengine wanaojifanya ni Watumishi wa Mungu lakini ni Watumishi wa Shetani.”

Amesema hayo leo Juni 5, 2025, katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Watoto wenye mahitaji Maalum cha Bagamoyo Diaconic Lutheran Centre, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee

Soma https://jamii.app/UtumishiWaDini

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance
6
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando, amesema Askofu Josephat Gwajima ajitokeze kutoka alipojificha aelezee umma ni nini kilichotokea, huku akihoji kama hana makosa ni kwanini anawaogopa Polisi?

Soma https://jamii.app/MsandoSakataGwajima

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
UWAJIBIKAJI: Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, amesema "Deni letu kwa mwaka lilikuwa linaongezeka kwa 5% tu, sasa hivi deni letu la Taifa kwa mwaka linaongezeka 18%. Hiki ni kiwango kikubwa sana cha ongezeko la deni la Taifa. Inaonyesha tunakopa kupita kiasi, sio kwamba tunakopa kwa kutekeleza miradi."

Ameyasema hayo katika Viwanja vya Bunge, leo Juni 5, 2025

Soma https://jamii.app/DeniTaifaKukua

#JamiiForums #JamiiAfrica #Transparency #Accountability #Uwajibikaji
👍21
Badala ya kuyaogopa matatizo, tuyatazame kama nafasi za kujifunza na kubadilisha mambo kuwa bora

Changamoto si mwisho wa safari, zinaweza kutufundisha na kutuongoza kufanya mambo kwa njia mpya au bora zaidi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #AmkaNaJF #GoodMorning
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mchungaji Anthony Lusekelo (Mzee wa Upako) ametoa wito kwa Serikali kuacha kufungia Makanisa sababu Kanisa ni Taasisi, Waumini hawana kosa, hivyo itumie Hekima kwa kuchukua hatua kwa wanayemtaka huku ikiwaacha Waumini wakiendelea na Ibada kwenye eneo lao

Soma https://jamii.app/MzeeUpakoGwajima

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #Governance
Mwandishi wa Andiko la Stories of Change 2023, anasema kwa kile ambacho kinaendelea kwenye Tasnia ya Filamu #Tanzania, Maisha ya Mwanadamu ya kila Siku sio kuhusu Mahaba na Usaliti, kuna vitu vingi ambavyo vinahitaji kuoneshwa ili Watu wapate kuwajibika na kuvifanyia Kazi

Anasema, kwa mfano ukitazama Filamu ya #Odama alituonesha Asili ya Mtanzania kuanzia Mavazi, matumizi ya Majina ya Asilia, Mfalme Garagarauka Adumba, Mtabiri Tambitambi, Msisi wa Msisiri, Kantala n.k.

Soma zaidi Andiko https://jamii.app/FilamuUtamaduniSOC23

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #Arts #SOC2023
1👎1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina ameyasema hayo katika Viwanja vya Bunge Juni 5, 2025

Soma https://jamii.app/DeniTaifaKukua

#JamiiForums #JamiiAfrica #Transparency #Accountability #Uwajibikaji
Hebu tuambie Mdau, ikitolewa ofa ya kupata Milioni 10 sasa hivi kwa kigezo cha Usafi wa Miguu na Kucha zako, hela unapata au ndio mpaka majaaliwa?😂😂

Mjadala https://jamii.app/WkeTukumbukeMiguu

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFChitChats #JFStories #Beauty
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anadai Wakazi wa Mtaa wa Makamba, Mbezi Msakuzi wana uhaba wa Huduma ya Maji katika Mtaa wa Makamba kutokana na Mradi kutokamilika kwa maelezo Mhandisi amesitisha uchimbaji mtaro kwa "sababu binafsi"

Mdau anadai baadhi ya Wananchi walikataa maelekezo hayo ya Mhandisi, hivyo mtaalam huyo akasimamisha zoezi kisha Wachimbaji waliokuwa wanaendelea na kazi wakahamishiwa upande mwingine wa Mtaa na Wananchi walipohoji wakajibiwa Mtaa wao "una Watu wachache"

Malalamiko hayo yamewasilishwa kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (#DAWASA), ambayo imeahidi kutoa majibu kuhusu hoja hiyo ya Mdau

Soma https://jamii.app/MajiShidaMsakuzi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #ServiceDelivery #Uwajibikaji #Mdau2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mwanasiasa James Mbatia, amesema hakukuwa na haja ya Jeshi la Polisi kutumika kwenda kuzingira Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, kwa kuwa walitakiwa kumuita badala ya kutumia nguvu

Amesema hayo Juni 05, 2025 alipozungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam.

Soma https://jamii.app/GwajimaMitutuMbatia

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance
3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Baada ya kutoonekana kwa zaidi ya Mwezi mmoja tangu Aprili 22, 2025, imebainika Dkt. Hashimu Titho Kilosa, aliyekuwa Mwanafunzi katika Chuo cha Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS) na Mtumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini (Mtwara), alifariki na tayari mwili wake ulizikwa

Baba Mzazi wa Daktari huyo akizungumza na The Chanzo, mzee Titho Kilosa amesema Aprili 24, 2025, Polisi waliuokota mwili wa mwanaye maeneo ya Coco Beach, wakatoa taarifa lakini wao (familia) wakachelewa kuiona, zilipopita Wiki 2 mwili huo ukazikwa

Ikumbukwe, Jeshi la Polisi halikuweka wazi chanzo cha kifo hicho na lilisema uchunguzi unaendelea

Soma https://jamii.app/HashimTithoKilosa

#JFMatukio #HumanRights #JamiiAfrica #JamiiForums
3
Na wewe ulikuwa unawaona Ndugu zako wa Dar wabinafsi au wewe ndiye Ndugu uliye Dar unayeonekana mbinafsi?😂😂😂

Shiriki kwenye Mjadala https://jamii.app/LawamaNduguDar

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFStories #JFChitChats #Maisha
4