JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kulalamika kuwa eneo la Bonyokwa Jijini Dar es Salaam lina kero ya kutopata Huduma ya Maji kwa takriban Wiki 5, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Albert Chalamila amesema maelekezo yametolewa kwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (#DAWASA) kuhakikisha wakazi wa eneo hilo wanapata huduma ya uhakika ya maji

Akizungumza na JamiiForums, Chalamila amesema “Kweli kuna shida, nimefuatilia, nashukuru kuwa tayari Rais Samia Hassan Suluhu ameshaelekeza DAWASA waongeze nguvu ya kifedha ili Bonyokwa yote iwe na maji kwa Saa 24 na kazi tayari imeanza. Asanteni sana, msinifiche kitu endeleeni kuwa Mabalozi.”

Soma https://jamii.app/MajiBonyokwa

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #SocialJustice #Accountability #ServiceDelivery #JFSC
👍123
DAR: Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (#TAKUKURU) Mkoa wa Ilala, Sosthenes Kibwengo amesema Ukaguzi wa Mradi wa ujenzi wa Vyoo vya Umma Jijini Dar es Salaam wenye thamani ya Tsh. Bilioni 3.27 ulibaini kasoro kadhaa ikiwemo kuchelewa kukamilika kwa mradi huo kinyume na mkataba

Akisoma Ripoti ya Utendaji kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba, 2023, amesema kasoro za Mradi huo unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar (#DAWASA) zimeendelea kurekebishwa na Mkandarasi amekatwa Tsh. 327,476,502.60 kama faini ya kuchelewesha kazi

Soma https://jamii.app/RipotiYaTAKUKURU

#KemeaRushwa #PCCBReport23 #JFUwajibikaji #Governance #JamiiForums
👍6
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anasema, eneo la Mbezi Louis, Mtaa wa Mshikamano hakuna huduma ya Maji kwa takriban Mwezi mmoja. Mara chache huwa yanatoka Usiku sana na yanayotoka ni machafu

Anasema Serikali ya Mtaa haitoi taarifa yoyote, #DAWASA nao wapo kimya. Anaiomba Mamlaka husika itatue changamoto hiyo au kama kuna Matengenezo ya Mabomba basi taarifa itolewe

JamiiForums imezungumza na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Baraka Mwaijande ambaye amesema “Kweli changamto hiyo ipo kutokana na changamoto ya Umeme. Nawasiliana na DAWASA ambao wanafanya kazi kwa kule Ruvu ili Huduma ipatikane.”

Soma https://jamii.app/MajiMshikamanoDar

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery
👍2
DAR ES SALAAM: Mdau wa JamiiForums.com anadai kutoondolewa kwa changamoto ya Huduma ya Maji maeneo ya Malamba Mawili kunamfanya aamini tetesi kuwa inawezekana kuna wahusika kwenye Mamlaka wanafanya makusudi ili wanufaike kwa kuuza Maji katika Magari binafsi

Anadai uhaba wa Maji unawafanya baadhi ya Wananchi kutumia Maji ya chumvi yaliyochimbwa kwenye Visima ambavyo vingine si rasmi na hivyo kuwa hatarini kupata changamoto za kiafya kwa kuwa maeneo mengi wanayochota Maji hayana usalama

Anatoa wito kwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, kuiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (#DAWASA) kutatua kero hiyo akidai wamesharipoti mara kadhaa kwenye Ofisi husika pasipo kupata utatuzi

Soma https://jamii.app/MlambaMawili

#JFHuduma #JFUwajibikaji #JamiiForums #Governance #CivilRights
👍43👏1
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema changamoto ya Maji katika maeneo ya Malamba Mawili, Kata ya Msigani inatokana na kuzungukwa na vilima vikali, hivyo kukosa Maji kunapokuwa na msukumo mdogo

DAWASA imeeleza maeneo hayo yanahudumiwa kupitia mtambo wa Maji wa Ruvu Juu na Wakazi wa hapo wanapata huduma siku ya Jumanne, Alhamis na Jumapili

Ufafanuzi huo umetolewa baada ya Mdau wa JamiiForums.com kulalamikia kero ya kukosa huduma ya Maji kwa zaidi ya miezi miwili katika baadhi ya maeneo

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa #DAWASA, Everlasting Lyaro juhudi zinazofanyika ili kuongeza msukumo wa Maji kwa kulaza bomba lenye kipenyo cha Inchi 8 kwa urefu wa Kilometa 3.5 na kuwa utelezaji umefikia 48%

Soma https://jamii.app/MajiMalambaMawili

#JFUwajibikaji #JamiiForums #ServiceDelivery
👍5
Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano #DAWASA, Everlasting Lyaro amesema Visima vya maji vinavyojengwa katika eneo la Msumi, vinachimbwa Kwenda chini hadi kwenye matabaka ya maji safi na yenye ubora, tofauti na visima vya Wakazi wa eneo hilo vilivyopo sasa vyenye Mita 80 hadi 100 ambavyo viko katika miamba yenye maji ya chumvi nyingi
-
Ameongeza kuwa visima hivyo vitatoa huduma katika mitaa ya Msumi A, B na C na vitawanufaisha wakazi zaidi ya 144,000

Soma https://jamii.app/MsumiMaji

#JFMatukio #JFHuduma #JFUwajibikaji
2👍2
DAR: Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Kiula Kingu, ametakiwa kupisha nafasi hiyo huku Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji, Shaban Mkwanywe akisimamishwa kazi kutokana na uzembe na kuwakosesha Maji Wananchi

Imeelezwa, Katibu Mkuu wa Maji alifanya ziara ya kushtukiza na kubaini Miundombinu Chakavu, Upotevu wa Maji, Watendaji wa #DAWASA wa ngazi za chini kutopewa stahiki zao hali iliyosabisha kufanya kazi bila hamasa na hata kuwajibu vibaya Wateja

Akitoa maelekezo ya hatua hizo, Waziri wa Maji, Juma Aweso amesema “Mwanzoni tulikuwa tunasema vyanzo vya Maji vimekauka, Umeme hakuna lakini leo niambieni kwanini hatuna maji kwenye matenki? Kwanini Wananchi wanateseka?" Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni Wadau wa JamiiForums.com walilalamikia huduma za Mamlaka hiyo.

Soma https://jamii.app/DAWASAPangua

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #SocialJustice #Accountability
👏1
DAR: Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemsimamisha Kazi Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) - Kinyerezi, Burton Mwalupaso kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ikiwemo kutojua Takwimu za mahitaji ya Maji ya eneo hilo pamoja na malalamiko mengi ya Wananchi

Waziri Aweso amechukua hatua hiyo wakati akizungumza na wakazi wa Tabata Kinyerezi na kumhoji Meneja kuhusu mahitaji ya Maji na Uzalishaji katika Kata ya Kinyerezi ambapo alitoa majibu yanayotofautiana huku akishindwa kueleza amepataje takwimu anazotoa

Ziara ya Waziri Aweso inafanyika katika maeneo yanayohudumiwa na #DAWASA ambayo mara kadhaa yamekuwa yakilalamikiwa na Wadau wa JamiiForums.com juu ya huduma mbovu za Maji

Soma https://jamii.app/AwesoTabata

#JamiiForums #Governance #JFHuduma #SocialJustice #Accountability
👍81😁1
UWAJIBIKAJI: Waziri wa Maji, Juma Aweso amesema amebaini uzembe na hujuma za makusudi kutoka kwa baadhi ya Watendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) kwa kutotekeleza majukumu yao na kuzoea kero na malalamiko ya Wananchi

Waziri Aweso amesema hayo akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya Maji Jijini Dar es Salaam na Mkoani Pwani ambapo inaelezwa kuwa alikutana na Malalamiko ya Wananchi kuhusu Watendaji na Huduma zisizoridhisha

Aidha, ziara hiyo imesababisha kuondolewa kwa baadhi ya Watendaji wa #DAWASA akiwemo aliyekuwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na nafasi hiyo kuchukuliwa na Mhandisi Mkama Bwire aliyekuwa Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)

Soma https://jamii.app/AwesoUzembe

#JamiiForums #JFHuduma #Governance #Accountability #ServiceDelivery
👍6
PWANI: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (#DAWASA) - Kibaha kurejesha huduma ya Maji kwa Wakazi wa Tankini, Muheza na maeneo ya jirani na hayo, akidai hawana huduma hiyo kwa wiki moja licha ya Mamlaka kuwaambia changamoto zilizokuwepo zimeshatatuliwa

Soma https://jamii.app/KibahaMaji

#JFHuduma #JamiiForums #Accountability #CivilRights
👍4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameitaka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (#DAWASA) kuja na mkakati wa kudhibiti wizi wa Mita za Maji baada ya kuelezwa kuwa kuna matukio mengi ya wizi wa Mita hizo

Akitoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya kukagua Mradi wa Maji maeneo ya Malamba Mawili, RC Chalamila amesema, Wezi wa Mita wapo Mtaani na hawatakiwi kuchekewa, hivyo DAWASA ishirikiane na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kutokomeza tabia hiyo

Awali, kwa nyakati tofauti Februari, 2023, Juni na Julai 2024, Wadau wa JamiiForums.com walidai licha ya kuripoti uwepo wa matukio ya wizi wa Mita za Maji ikiwemo katika maeneo ya Mbezi Luis na Mbweni Teta hakukuwa na hatua zilizochukuliwa na Mamlaka

Soma https://jamii.app/WiziMitaZaMaji

#ServiceDelivery #JFUwajibikaji #Governance #JamiiForums
👍31
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR ES SALAAM: Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amezitaka Mamlaka za Maji Nchini kuacha kutoa maji Usiku kwa kuwa hakuna sababu ya kufanya hivyo kutokana na uwepo wa Maji na Umeme

Akizungumza wakati wa kuzindua rasmi Kampeni ya "Mtaa kwa Mtaa" ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (#DAWASA), amesema kunapotokea changamoto taarifa itolewe na Kitengo cha Mawasiliano ili kuondoa manung’uniko ya Wananchi

Aidha, ameelekeza elimu itolewe kwa Wananchi kusoma Mita zao za Maji ili kuepusha msuguano unaoweza kutokea wakati wanapotumia ujumbe wa kiwango cha maji waliyotumia

Soma https://jamii.app/AwesoMaelekezo

#JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery #Accountability
👍3
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anasema, maeneo ya Masaki na Mtongani (Skanska), hakuna huduma ya Maji kwa takriban Wiki 1 sasa

Anasema Serikali ya Mtaa haitoi taarifa yoyote, #DAWASA nao wapo kimya

Anatoa wito kwa Mamlaka itatue changamoto hiyo, pia kama kuna Matengenezo ya mifumo au mitambo basi taarifa itolewe kwa Wateja ili wajipange mapema

Soma https://jamii.app/HakunaMajiDar

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery #JFHuduma
👍1
DAR: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kueleza hakuna Maji kwenye Vyoo vya Stendi ya Mabasi ya Magufuli kwa siku mbili, Meneja wa kituo, Isihaka Waziri amesema huduma imerejea lakini waliishiwa Maji ya akiba baada Huduma ya DAWASA kukatika bila wao kupewa taarifa

Wakati huohuo, Afisa Habari wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Joina Nzali amesema “Tulikuwa na mpango wa kuchimba Visima lakini Watalaam wakasema Maji yatakayopatikana (Stendi) hayafai kutumika kwa matumizi ya Binadamu, hivyo tunafikiria kuchimba visima na kuvuna Maji ya mvua.”

Ameongeza “Kisima kilichopo (Stendi) kinaweza kutumika kwa Saa 72 au Saa 48 (wakati wa abiria wengi), #DAWASA wangetoa taarifa mapema tungetafuta njia mbadala changamoto iliyotokea ni kwa kuwa hakukuwa na taarifa, tungejaza maji kwenye ‘matenki’, yapo 11 yale ya Lita 10,000.”

Soma https://jamii.app/MajiStendiMagufuli

#JFHuduma #ServiceDelivery #Accountability #JamiiForums
DAR: Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mkama Bwire amesema eneo la Kariakoo lina changamoto ya Mfumo wa Majitaka kutokana na Miundombinu iliyopo kuelemewa na kushindwa kuendana na uhitaji uliopo sasa

Amesema #DAWASA wapo katika hatua za mwisho za mazungumzo na Mkandarasi ili kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa ambao utaleta suluhu katika maeneo ya katikati ya Jiji hususani Kariakoo na Buguruni. Pia, kufikia Januari 2025, Mkandarasi atakuwa ameanza utekelezaji wa mradi

Hivi karibuni Mdau wa JamiiForums.com aliitaja Mitaa yenye tatizo la Majitaka kusambaa ikiwemo Pemba na Nyamwezi ambapo kuna Wafanyabiashara wanapanga Matunda na Bidhaa nyingine chini

Soma https://jamii.app/MajiKariakoo

#PublicHealth #JFHuduma #Accountability #JamiiForums
👍3
DAR: Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar (DAWASA), Everlasting Lyaro amesema #DAWASA inatoa wito kwa Wananchi kuacha kutupa taka ngumu kwenye Miundombinu ya Majitaka ili kuitunza

Ametoa wito huo wakati akifafanua uamuzi wa maboresho wa Miundombinu ya Soko la Ilala iliyokuwa ikivujisha Maji Taka kama ilivyoelezewa na Mdau wa JamiiForums.com

Soma https://jamii.app/MajiTakaIlala

#JamiiForums #SeriviceDelivery #Accountability #Governance
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MOROGORO: Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa #DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire amesema Bwawa la Kidunda likikamilika Juni 2026 litasaidia kuufanya Mto Ruvu ambao ni tegemeo kwa chanzo cha maji katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kutokauka na hivyo kusaidia kuondoa kero ya kukosekana kwa huduma hiyo

Amesema “Wakati wa kiangazi mikoa hiyo imekuwa na uhaba wa maji kwa kuwa 87% ya maji yanayozalishwa (Pwani na Dar) yanategemea Mto Ruvu, hivyo Bwawa hilo ambalo likikamilika litahifadhi Lita Bilioni 190 pia litakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme Megawati 20.”

Ikumbukwe kwa nyakati tofauti, Wadau wa JamiiForums.com wamelalamika kukosa huduma ya maji kwa muda mrefu maeneo tofauti ya Dar na Pwani, baadhi yao wakisai wanapata kwa mgawo na wengine wakisema hawana huduma kwa zaidi ya mwaka

Soma https://jamii.app/BwawLaKidunda

Video Credits: Daily News Digital

#JFHuduma #JamiiForums
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau ndani ya JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kushughulikia kero ya chemba kutiririsha Maji taka yenye harufu katika baadhi ya Mitaa ya Kariakoo tangu Machi 2025

Amedai hali hiyo imekuwa changamoto ya kuzua hofu kwa Wakazi wa eneo hilo hasa kipindi hiki cha Mvua kwani Watu wapo hatarini kupata Magonjwa kutokana na chemba hizo kuwa karibu na Makazi na Biashara

Aidha, amedai kuna Maafisa wa #DAWASA walifika kuangalia hali hiyo siku kadhaa nyuma, hakukuwa na utatuzi uliofanyika na sasa hali inaendelea kuwa mbaya zaidi, Maji ni mengi na yanatoa harufu

Soma https://jamii.app/MajiTakaKeroKariakoo

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #Mdau2025
👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anadai Wakazi wa Mtaa wa Makamba, Mbezi Msakuzi wana uhaba wa Huduma ya Maji katika Mtaa wa Makamba kutokana na Mradi kutokamilika kwa maelezo Mhandisi amesitisha uchimbaji mtaro kwa "sababu binafsi"

Mdau anadai baadhi ya Wananchi walikataa maelekezo hayo ya Mhandisi, hivyo mtaalam huyo akasimamisha zoezi kisha Wachimbaji waliokuwa wanaendelea na kazi wakahamishiwa upande mwingine wa Mtaa na Wananchi walipohoji wakajibiwa Mtaa wao "una Watu wachache"

Malalamiko hayo yamewasilishwa kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (#DAWASA), ambayo imeahidi kutoa majibu kuhusu hoja hiyo ya Mdau

Soma https://jamii.app/MajiShidaMsakuzi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #ServiceDelivery #Uwajibikaji #Mdau2025
DAR: Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amesema tathmini iliyofanyika imebaini eneo la Kawe linalolalamikiwa na baadhi ya Wananchi wa Kawe kuwa barabara imezibwa kutokana na ujenzi wa Kanisa la Arise and Shine, sio sahihi

DC amesema licha ya Wananchi kutumia barabara hiyo muda mrefu, haipo rasmi kwenye ramani, ameelekeza busara itumike kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na uongozi wa Kanisa la Mwamposa waangalie uwezekano wa kuweka njia kwa ajili ya Wananchi na kuruhusu Watoto kutumia baadhi ya maeneo kwa michezo

Kuhusu madai ya miundombinu ya maji kuharibiwa, Mhandisi Erasto Mwakilulele wa #DAWASA Kawe amesema wameanza kazi ya kuboresha miundombinu ili huduma ya maji irejee haraka kwa Wananchi

Soma https://jamii.app/KaweUjenzi

#JamiiForums #Accountability #CovilRights #Governance #JFMatukio
🔥1