JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Leo Mei 31, 2025, JamiiAfrica inashiriki kwenye Majadiliano yanayogusia Upatikanaji wa Mtandao kwa Wote pamoja na AI na Teknolojia zinazoibuka, kwa kusisitiza jukumu muhimu la upatikanaji wa Intaneti katika kuvunja Unyanyapaa unaozunguka matatizo ya Afya ya akili na kujenga jamii zenye uthabiti na usaidizi wa kweli

Wadau watajadili unyanyapaa unaohusiana na Afya ya Akili na kutoa Elimu kwa washiriki kuhusu asili yake ikiwa ni pamoja na mitazamo ya kitabibu, kiroho na kisaikolojia.

Teknolojia kama vile Akili Mnemba (AI) inaweza kutumika kuongeza uelewa, kutoa msaada wa mapema na kujenga mifumo rafiki ya Kidijitali inayosaidia Watu wanaokumbwa na changamoto za Afya ya Akili bila kuhukumiwa

Kufuatilia bofya https://jamii.app/SikuYaMwishoIGF

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
Imeelezwa #Tanzania imepiga hatua katika ujenzi wa Miundombinu ya TEHAMA, ikiwa ni pamoja na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano wenye urefu wa Kilomita 13,820 (NICTBB) unaounganisha Mikoa na Wilaya zote, pamoja na kuunganisha Nchi za #Kenya, #Uganda, Rwanda, #Burundi, Zambia, #Malawi, na Msumbiji, ambapo sasa inajiandaa kuunganisha DR Congo kupitia Ziwa Tanganyika

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ambayo imesema Tanzania ni miongoni mwa Nchi zinazoongoza katika Ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuwa na Mtandao mkubwa wa nyaya za nyuzi za Mawasiliano (Fiber optic)

Hayo yameelezwa katika ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la 14 la Utawala wa Mtandao Afrika (AfIGF 2025), Mei 30, 2025, unaoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC)

Soma https://jamii.app/AfIGF2025Day2

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
2
Akizungumza katika Mkutano wa Jukwaa la 14 la Utawala wa Mtandao Afrika, Seneta wa Kenya amesema mara nyingine Watawala au Mamlaka hazina hisia, hawajui changamoto au hali halisi ya Kijinsia, na wanapobuni Sera au zana, mara nyingi ni mzigo unaobebwa na Wanawake

Ameongeza kuwa Idara za Kijinsia zinapaswa kuwa bora zaidi, zinapaswa kuelewa kuwa hazipaswi kutengwa kama idara za pembeni, bali ni Wataalamu wa Sekta mbalimbali wanaopaswa kutoa mwongozo kwa Wizara ya Afya, Wizara ya Maji, Wizara ya Kilimo, n.k.

Ameongeza kwa kusema “Kila Nchi inakuwa na muundo wake wa kukabiliana na changamoto za mambo ya Kijinsia, katika Dunia ya Kiditali, nafikiri kuna mambo yanatakiwa kufanyiwa zaidi”

Zaidi https://jamii.app/AfIGF2025Day2

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
1
Seneta wa Kenya, Catherine Mumma amesema suala la jinsia katika mifumo limekuwa likibaki nyuma, kwa sababu ukiangalia mgawanyo wa masuala mbalimbali kama miundombinu, ushirikishwaji wa Wanawake nakadhalika utagundua kuwa Wanawake bado hawajajumuishwa ipasavyo.

Amesema kuwa Wanawake wanabaki nyuma katika jamii zetu iwe ni katika masomo na hata sasa katika ushiriki wa Teknolojia ya Kidijitali, au Uchumi na biashara za Kidijitali na hata katika tasnia wanazoendesha na kumiliki

Amesema kwa mtazamo wake jambo jema kufanya mazungumzo kuhusu Wanawake kwa sababu yanaweza kuwa na msaada katika kubadilisha Jamii kama yataungizwa kwenye mifumo na kufanyiwa kazi

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
1
Akizungumza katika Mkutano wa Jukwaa la 14 la Utawala wa Mtandao, Dkt Sabra Hussein kutoka Tanzania AI Community amesema “Unakuta Wanawake wa Vijijini labda Mkoani Kilimanjaro, wanatumia programu za Simu kujua wanapoweza kupata msaada lakini wanakutana na changamoto kwasababu vifaa vingi vya AI vipo kwa Kiingereza na hazijabadilishwa kuendana na Mazingira wa kienyeji.”

Amesema kuwa, Kuna baadhi ya Mifumo ya kuomba Ajira, Mwanamke anapojaribu kutumia programu hizo kutafuta kazi, hazitamtambua kwa usawa na inaweza kumuathiri

Hali hiyo Matokeo yake ni Wanawake kutopata nafasi sawa za Ajira kama Wanaume, na hivyo kuongeza pengo la Kiuchumi na Ajira kati ya Jinsia

Zaidi https://jamii.app/SikuYaMwishoIGF

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
Dorris Magiri (Kijiji Link) amesema “Siku hizi wengi wetu tunaona ni bora kuzungumza na Simu zetu badala ya kuzungumza na Watu. Mtu akiwa na jambo anaamini sana kwenda kuiambia ChatGPT badala ya kumwambia Rafiki yake”

Amesema "tunatakiwa kujiuliza kwamba Je, tunaweza kuiamini AI? Jibu ni kwamba Binadamu tayari anaiamini AI. Nadhani tunatakiwa kurejesha ule Muunganiko wa Kibinadamu, tuzungumze na Watu wetu wa karibu kuhusu yale tunayoyapitia Kihisia"

"Tujenge Mfumo wa kweli wa kusaidia Afya ya Akili kwa kutumia AI kwa Uangalifu, kwa kushirikiana na Watu wenye uzoefu, na tukikumbuka Hekima ya Kiafrika"

Zaidi https://jamii.app/SikuYaMwishoIGF

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
1
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mary Gervas Matogolo (22), amewekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana kufuatia kesi ya Jinai inayomkabili yeye na Wanafunzi wenzake wawili, wakidaiwa kumshambulia mwenzao kwa kumgombania Msanii na Mtangazaji wa Redio, Burton Mwemba maarufu Mwijaku

Mary na wenzake, Ryner Ponci Mkwawili wa Chuo Kikuu Ardhi na Asha Suleiman Juma wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), walisomewa mashtaka 8 yakiwemo kusababisha madhara ya Mwilini, kutishia kuua, kusambaza taarifa za uongo kupitia Mitandao ya Kijamii na Uharibifu wa Mali

Ryner na Asha walitimiza masharti hayo na kuachiwa kwa dhamana, Mary alishindwa kutimiza vigezo na hivyo kupelekwa mahabusu hadi Juni 13, 2025, kesi hiyo itakapotajwa tena

Soma https://jamii.app/MaryDhamana

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #HumanRights #JFWomen #SocialJustice
1
MANYARA: Timu ya Singida Black Stars SC imeingia Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank, kwa kuichapa Simba SC Magoli 3-1, kwenye Uwanja Tanzanite Kwaraa katika Nusu Fainali

Singida imepata Magoli kipitia kwa Emmanuel Keyeke (35, 48) na Jonathan Sowah (17), huku Jean Ahoua akiifungia Simba goli pekee

Hivyo, mchezo wa Fainali unatarajiwa kuwa kati ya Yanga iliyoingia Fainali kwa kuifunga JKT Tanzania Magoli 2-0 dhidi ya Singida

Soma https://jamii.app/NusuFainali

#JFSports #JamiiForums
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Jumanne Muliro amesema Jeshi la Polisi linasubiri Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC), Padri Kitima apate nafuu kiafya kisha ndio watachukua maelezo ya tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa lililotokea Aprili 30, 2025

Akizungumzia tukio hilo lililotokea kwenye makazi na Makao Makuu ya Baraza hilo, Kurasini, Muliro amesema ni jukumu la Kisheria kuhakikisha wanapata maelezo ya Padri Kitima ya Kimaandishi, ili yaende Ofisi ya Mashtaka kwa kuwa Askari Polisi walienda mara kadhaa kumuona lakini wakamkuta akiwa katika mazingira magumu ya kuumwa

Ikumbukwe, Padri Kitima inadaiwa alishambuliwa na kuumizwa kichwani ambapo Jeshi la Polisi lilisema linafanya uchunguzi na tayari linawashikilia Watu Wawili wakihusishwa na tukio hilo

Soma https://jamii.app/MuliroKuhusuKitima

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #HumanRights
3
Mdau wa JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Siasa amehoji kuwa tovuti ya Bunge inaonyesha Wasifu wa Mbunge wa Kinondoni, Tarimba Gulam Abbas kuwa alitumia Miaka Miwili (2010 na 2011) kusoma na kuhitimu masomo katika ngazi ya Shahada (Degree) na Master's Degree katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Anahoji “Hii inawezekanaje, wakati kwa kawaida Shahada pekee si chini ya Miaka mitatu? Ukiachana na hilo hata ngazi nyingine zote amesoma Mwaka mmoja mmoja, ni kwamba tovuti ndio imekosea au ni kweli alisoma hivyo mwaka mmoja mmoja?”

Soma https://jamii.app/MdauTarimba

#JamiiForums #Kuelekea2025 #Democracy
Akichangia katika Mjadala unaongazia jukumu la upatikanaji wa Intaneti katika kuvunja Unyanyapaa unaozunguka matatizo ya Afya ya akili, Ajimah Olaghere amesema “Mimi binafsi naamini katika nguvu ya Watu na suluhisho ninalopendekeza linaanzia kwa Watu wenyewe, kwa sababu hapo ndipo palipo na Upatikanaji halisi wa msaada.”

Ameongeza kwa kusema Elimu ya Afya ya Akili ni muhimu sana. Ingawa ana Elimu ya hali ya juu na uzoefu mkubwa, anajua hana maarifa ya kutosha kuhusu Afya ya Akili.

Aidha, amependekeza Mfumo wa "daraja" (bridge framework), ambao unasisitiza kuhusisha Jamii kwa karibu kwenda kwenye Asili, kuelewa jamii na Tamaduni zao na kujenga Madaraja ya mawasiliano na Msaada.

Zaidi https://jamii.app/SikuYaMwishoIGF

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
1
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa ‘Ligue 1’, Paris Saint-Germain (#PSG) wameonesha huu ni mwaka wao, kwa kubeba taji la #UEFAChampionsLeague (Ligi ya Mabingwa Ulaya), pia kushusha kipigo Kizito kwa #InterMilan ya Italia, Magoli 5-0

PSG inayonolewa na Kocha Luis Enrique, imebeba taji hilo kwa magoli ya Achraf Hakimi (12), Désiré Doué (20, 63), Khvicha Kvaratskhelia (73) na Senny Mayulu (86)

Huo unakuwa ubingwa wa kwanza kwa timu ya Ufaransa katika michuano hiyo

Soma https://jamii.app/UEFAFinal25

#JFSports #JamiiForums
🔥1
Akizungumza katika Siku ya Mwisho ya Mkutano wa Jukwaa la Utawala wa Intaneti Afrika, jana Mei 31, 2025, Daktari John Weilsh alisema tunaweza kutumia Mitandao ya Kijamii, sababu ya uwezo wake wa kuunganisha Watu kupitia intaneti, si tu katika Jamii za Nyumbani bali muhimu zaidi Kimataifa

Alisema eneo mojawapo lenye uwezekano mkubwa wa mafanikio ni kuhimiza ushirikiano kati ya Wataalamu wa tiba hapa Tanzania au Kenya, na Watafiti katika Nchi nyingine wanaojaribu sio tu kushughulikia matatizo ya Afya ya Akili kwa kutumia Teknolojia tulizonazo sasa, bali pia kufikiria Teknolojia za baadaye zitakazokuwa na ufanisi zaidi kupitia mbinu za Akili Mnemba (AI)

Aliongeza "Naamini katika kuunganisha maarifa yetu ya pamoja na ya kipekee ili kujenga jamii ya pamoja ya wataalamu wa Sayansi ya Neva (Neuroscience) na Akili (Neuropsychiatry), kwaajili ya kushughulikia changamoto za Afya ya Akili zinazoathiri jamii katika Mataifa mbalimbali"

Zaidi https://jamii.app/SikuYaMwishoIGF

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #DigitalRights
1
Leo hii, tunaishi katika dunia ambayo si kila mmoja anapata haki au fursa sawa. Wapo wanaokumbwa na changamoto kwasababu ya jinsia, ulemavu, hali ya kiuchumi au mazingira waliyozaliwa. Wanaweza wasiwe na jukwaa la kujisemea, lakini wewe unalo. Wanaweza wasisikike, lakini wewe unasikika.

Sauti yako inaweza kuwa faraja, kinga, au dira kwa mwingine. Tuchague kuwa watu wanaojali. Tuchague kuungana kwa ajili ya haki, utu na usawa. Kwasababu, kuijenga jamii salama na yenye haki, ni jukumu letu sote

#JamiiForums #JamiiAfrica #SocialJustice #Demokrasia #Uwajibikaji
RUVUMA: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mmalaka husika kurekebisha mazingira ya Vyoo vya Shule ya Msingi Miembeni, iliyo Kata ya Msamala, Manispaa ya Songea

Amedai hali ya uchafu wa Vyoo hivyo, inaweza kusababisha mlipuko wa Magonjwa, hivyo kuhatarisha afya za Walimu na Wanafunzi wa Shule hiyo

Soma https://jamii.app/ShuleYaMiembeni

#JamiiForums #PublicHealth #Afya #ServiceDelivery #Accountability #Uwajibikaji
2
Mwongoza Mjadala ulioangazia jukumu la upatikanaji wa Intaneti katika kuvunja Unyanyapaa unaozunguka matatizo ya Afya ya akili, Mary Uduma amesema Kwa upande wa Sera, hatupaswi kuwaangalia Watu walio kwenye Changamoto za Kiakili kama Wahalifu. Tunahitaji sera zinazoweka Watu kwenye Huduma na si kuwaweka Gerezani au kuwafungia.

Amesema "Tunahitaji Haki inayoponya (Restorative Justice), ambayo ni sehemu ya Utamaduni wetu wa Kiafrika, kushirikiana kama Jamii, Kusamehe, na Kuponya.”

Ameongeza "Elimu ya Afya ya Akili ni muhimu. Wengi wetu, hata walioelimika, hatujui Changamoto ya Afya ya Akili inavyoonekana. Tunahitaji kufundishwa jinsi ya kutambua, kupokea, na kuwahudumia wanaopitia. Na haya yote yanaanza na kusikiliza hadithi kama ya Doris, kujifunza kutoka kwenye uzoefu wa kweli.

Zaidi https://jamii.app/SikuYaMwishoIGF

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #MaendeleoYaKidijitali #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights