JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anasema licha ya umuhimu wa ujenzi wa Miradi ya Barabara, kujengwa kwa wakati mmoja kumechangia foleni ambayo imekuwa ni usumbufu kwa Watu wengi, akishauri ilitakiwa kuwe na mpango mbadala wa kupunguza au kukwepa changamoto hiyo, katika Jiji ambalo lina purukushani nyingi

Anatoa mfano maeneo ambayo yana changamoto ya foleni kubwa kutokana na ujenzi ni Barabara ya Tegeta - Mwenge, Mwenge - Morocco, Morocco - Posta, Posta Kisutu - Mnazi Mmoja, Ubungo - Mwenge, Kimara - Ubungo, Buguru – Kariakoo, TAZARA - Gongo la Mboto n.k

Mdau anadai sehemu ya kutumia nusu saa au dakika 45 kwa gari sasa hivi inaweza kutumika Dakika 120 hadi 180, anaamini Mamlaka husika zilitakiwa kuwa na mbinu mbadala kabla ya kufanya utekelezaji wa hicho kinachoendelea ambacho kina muhimu pia

Soma https://jamii.app/UjenziBarabaraDar

#JamiiForums
3
Dar: Kesi ya jinai namba CC 32444/24 inayomkabili Saleh Ayoub (39), Mwalimu wa Shule ya Msingi Green Acres iliyopo Mbezi Africana, imeendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni.

Saleh Ayoub anatuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wa Kiume mwenye umri wa Miaka 11, ambapo shauri hilo lilitajwa tena Mahakamani Mei 27, 2025, lakini liliahirishwa hadi Juni 19, 2025 kwaajili ya Mshtakiwa kuanza kujitetea.

Awali, kesi hiyo ilipangwa kuendelea Mei 21, 2025, lakini ilishindikana kusikilizwa katika hatua hiyo, baada ya Wakili wa Mshtakiwa kutoonekana Mahakamani.

Upande wa Jamhuri tayari umefunga ushahidi wake kwa kuwasilisha mashahidi Wanne kati ya 6 waliopangwa na kielelezo kimoja.

Shauri hilo lilifikishwa Mahakamani Novemba 12, 2024, baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuchapisha hoja iliyosomeka: “Walimu wa Shule ya Green Acres (Dar) wanaotuhumiwa kulawiti na kuwadhalilisha Wanafunzi, wanalindwa na nani?”

Soma https://jamii.app/KesiMwendelezo

#JFMatukio #JamiiForums #HumanRights #Accountability
3
UPDATES: Jana, Mei 31, 2025, Mdau wa JamiiForums.com alidokeza kuwa tovuti ya Bunge ilikuwa ikionesha Mbunge wa Kinondoni, Tarimba Gulam Abbas alitumia Miaka Miwili (2010 na 2011) kusoma na kuhitimu Shahada (Degree) na Shahada ya Uzamili (Master's Degree) katika Chuo Kikuu cha Dar (UDSM), leo Juni 1, 2025 tovuti hiyo imehariri baadhi ya taarifa

Tovuti ya Bunge imeondoa taarifa za awali za Tarimba kusoma UDSM badala yake sasa inaonyesha alipata Shahada ya Sheria (LLB) katika Chuo Kikuu cha Tumaini (2007 – 2010)

Hata hivyo, taarifa nyingine zilizozua gumzo mtandaoni hazijabadilika, ikiwemo Stashahada aliyoipata Mwaka 1981 katika Chuo cha “Tanzania of Journalism”, pia taarifa za kusoma Diploma nchini Benin (mwaka usiojulikana)

Soma https://jamii.app/TarimbaUpdates

#JamiiForums #Kuelekea2025 #Democracy #Accountability
1
#JFKumbukizi: Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles Kimei alinukuliwa na Gazeti la Mwananchi, Machi 2018, akieleza kuwa kuanzishwa kwa Tawi la Benki hiyo Wilayani Chato haikuwa kutokana na kujiridhisha kwa Menejimenti, bali shinikizo la Rais John Magufuli kuanzia alipokuwa Waziri

Dkt. Kimei alieleza aliwatuma Wasaidizi wake kwenda Chato kujiridhisha na majibu yakawa Uchumi wa Chato haukushawishi kufungua tawi la benki hiyo, lakini Magufuli aligoma na akamwambia “Vijana wako hawajui kufanya utafiti. Nitafanya utafiti wangu.”

Soma https://jamii.app/CRDBKumbukizi

#JFKumbukizi #JamiiForums
3👍1😁1
Pyramids ya Misri imekuwa Bingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika (#CAFChampionsLeague) 2024/25 kwa kuifunga #MamelodiSundowns ya Afrika Kusini Magoli 2-1 katika Fainali ya pili, hivyo kubeba taji kwa jumla ya Magoli 3-2 kwa kuwa Fainali ya kwanza, matokeo yalikuwa sare ya 1-1

Pyramids imepata Magoli yake kupitia kwa #FistonMayele dakika ya 23 na Ahmed Samy (56), wakati Mamelodi ilifunga kupitia kwa Iqraam Rayners (75), Mchezo ukichezwa kwenye Uwanja wa 30 June Jijini #Cairo

Soma https://jamii.app/PyramidsWinner

#JFSports #JFCAFCL25 #JamiiForums
DAR: Mahakama ya Tanzania imesema Shauri la Jinai Namba 8606/2025 na Namba 8607/2025 kati ya Jamhuri na Tundu Lissu, ambayo yamepangwa kutajwa na kusikilizwa Juni 2, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mwenendo wote utarushwa mubashara (live) na pia Mshtakiwa atafikishwa Mahakamani

Taarifa ya Mahakama imeeleza, lengo ni kuwawezesha Wananchi kufuatilia bila kuwa na ulazima wa kufika Mahakamani, pia ni Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania kuimarisha uwazi, uwajibikaji na matumizi ya teknolojia katika huduma ya utoaji haki

Taarifa imeeleza Mahakama ya Wazi Kisutu ni ndogo, inachukua Watu 80, hivyo imekubalika watakaoingia ni Mawakili wa Serikali na Watu wengine (10), Mawakili Utetezi na Watu wengine (60) na Waandishi wa Habari (10)

Soma https://jamii.app/LissuJune2

#JFMatukio #JamiiForums #Governance #Democracy
3
Kusoma kwa undani habari hizi na mengine yaliyojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons #AmkaNaJF
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu alivyowasili ndani ya Mahakama ya Kisutu kwaajili ya kuanzia kusikiliza kesi zinazomkabili, leo Juni 2, 2025

Mahakama ya Tanzania ilitoa taarifa kuwa mwenendo wote wa kesi hiyo utarushwa mubashara (live) ili kuwawezesha Wananchi kufuatilia, bila kuwa na ulazima wa kufika Mahakamani kutokana na udogo wa Mahakama ya Kisutu

Zaidi https://jamii.app/KesiLissuJuni

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights #Kuelekea2025
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#DEMOKRASIA: Viongozi mbalimbali na baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wamejitokeza Mahakamani Kisutu kusikiliza kesi ya Lissu leo Juni 2, 2025

Soma https://jamii.app/KesiLissuJuni

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights #Kuelekea2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamezuiliwa kuingia ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia kesi ya Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, Tundu Antiphas Lissu

Soma https://jamii.app/PolisiVirunguCHADEMA

#JamiiForums #Siasa #JamiiAfrica #Democracy #Governance #HumanRights #UchaguziMkuu2025
😢1
DAR: Imeelezwa Mawakili 30 kati ya 120 wanaomtetea Tundu Lissu wapo Mahakama уа Hakimu Mkazi Kisutu kwaajili ya kusikiza kesi zinazomkabili Mteja wao leo Juni 2, 2025, wakiwemo Dkt. Rugemeleza Nshala na Wakili Peter Kibatala

Zaidi https://jamii.app/KesiLissuJuni

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights #Kuelekea2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
SIMIYU: Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina, akizungumza na Wananchi wa Mwandu Itinje, Juni 1, 2025, alisema “Hatuwezi kuwa Viongozi wa kuongea mapambio tu wakati Fedha za Wananchi zinaliwa”

Video Credit: Habari Digital

Soma https://jamii.app/MpinaVigelegeleWezi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #UchaguziMkuu2025