KAGERA: Mdau wa JamiiForums.com anadai baadhi ya Walimu wa Shule za Msingi zilizopo Wilayani Missenyi, wamekuwa na utaratibu Mwanafunzi akifeli somo au kufanya kosa, anapewa adhabu ya kuleta Vyuma chakavu
Anadai hali hiyo imechangia baadhi ya Wanafunzi kuchukua Vifaa vya ndani na kuvifanya Vyuma chakavu, ambapo pia wanakuwa katika Mazingira hatarishi, wanapotafuta Vyuma hivyo Mtaani
Anaeleza tabia hiyo imeanza kujitokeza katika Shule ya Msingi Mugana A, Katarabuga n.k, akitoa wito kwa Mkurugenzi wa Missenyi kufuatilia kwa ukaribu suala hilo na kuchukua hatua stahiki
Soma https://jamii.app/ShuleMissenyi
#JamiiForums #Accountability #Elimu #Governance #JamiiAfrica

Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Shauri la uhaini linalomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu limeendelea, leo Juni 2, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo limeahirishwa hadi Juni 16, 2025 baada ya upande wa Jamhuri kueleza upelelezi haujakamilika
Hakimu Mkazi Mfawidhi Franko Kiswaga ameagiza Jamhuri kuharakisha na kutoa taarifa za mwenendo wa upelelezi wa kesi hiyo ili shauri lianze kusikilizwa mapema
Akizungumza baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, Wakili anayemtetea Lissu, Dkt. Rugemeleza Nshala amesema Hakimu ametoa onyo kwa Lissu kwa kitendo cha kuzungungumza “No Reforms No Election” wakati tayari Mahakama imeanza
Soma https://jamii.app/KesiLissuJuni
#JamiiForums #Siasa #Democracy #Governance #HumanRights #Kuelekea2025

Ripoti ya CAG ya Mwaka 2023/2024 ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo imeonesha Mapitio ya nyaraka na ziara za Ukaguzi wa miradi zilibaini Shule mpya 35 za msingi zenye thamani ya Tsh. 15,819,500,000 na shule mpya 148 za Sekondari zenye thamani ya Tsh. 109,327,133,843 zilijengwa katika maeneo ambayo hayakupimwa
Ufuatiliaji hafifu wa Maafisa masuuli katika kupata maeneo kwa ajili ya ujenzi wa Shule ulisababisha hali hii, hivyo kuziweka Shule hizo katika hatari ya Migogoro ya Ardhi, kama vile Migogoro ya Umiliki na Mipaka
Machi 2023, Katibu Mkuu wa OR-TAMISEMI aliagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha Shule hizo zinajengwa katika maeneo yaliyopimwa na hati miliki za Viwanja husika zinapatikana ndani ya Miezi Mitatu tangu tarehe ya agizo
Soma zaidi https://jamii.app/ViwanjaShuleVisivyopimwa
#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii #CAGReport25

❤1
DAR: Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) umeingia mkataba wa Miaka 12 na Kampuni binafsi ya usafirishaji ya Emirates National Group (ENG) kutoka Abu Dhabi kuendesha Mradi wa BRT Jijini Dar
Mkataba huo ulisainiwa Mei 30, 2025 ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa DART, Dkt. Athumani Kihamia amesema Emirates National Group itachukua uendeshaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa BRT na kuleta mabasi mapya 177
Imeelezwa Mchakato huo ulianza Mwaka 2017 kupitia mfumo wa ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), lakini ulipata changamoto za kimajadiliano kuhusu viwango vya nauli na mifumo ya usuluhishi
Ikumbukwe Mwaka 2020, Serikali ilitangaza zabuni upya ambapo kampuni 40 ziliwasilisha maombi, ambapo Emirates National Group iliibuka mshindi.
Soma https://jamii.app/EmiratesKusimamiaMwendokasi
#JamiiForums #JamiiAfrica #ServiceDelivery #Transparency

👎1
DODOMA: Barua inayodaiwa kutoka kwa Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa, imeeleza kufungwa kwa shughuli za Kanisa la Ufunuo na Uzima, linalongozwa na Askofu Josephat Gwajima, kwa madai ya kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa Kisiasa na nia ya kuichonganisha Serikali na Wananchi, kwa kuwa vitendo hivyo vinaathari ya kuhatarisha amani na utulivu nchini
Pia, barua hiyo imeliamuru kanisa hilo kusitisha shughuli zake mara moja na imefutiwa usajili wake, ila lina haki ya kukata rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ndani ya siku 21
Jitihada za kumpata Msajili wa Jumuiya za Kiraia kuzungumzia barua hiyo hazijafanikiwa
Soma https://jamii.app/GwajimaKanisaKufungwa
#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #Utawala

❤3👍1👎1
DAR: Baada ya kusambaa kwa Barua mitandaoni iliyodaiwa kuwa imetoka kwa Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa ikihusu kufungia shughuli za Kanisa la Ufunuo na Uzima, Kiongozi wa Kanisa hilo, Askofu Josephat Gwajima, amesema kuna Mtu amefika Kanisani hapo kwa lengo la kuleta barua jioni ya leo Juni 2, 2025
Amesema “Nikiwa kwenye ibada Wasaidizi wangu wamesema kuna Mtu alifika akasema ameagizwa kuleta barua, hawakuipokea, kitambulisho na taarifa zake tunazo, amesema atarudi kesho, tunamsubiri.”
Ameongeza “Hapa nipo na Maaskofu na Viongozi wengi wa Dini, wote wanahoji kuhusu hiyo barua iliyosambaa Mtandaoni ambayo nilieleza kuwa siyo ya kweli, kwa kuwa sikuwa nimepokea barua yoyote na ilizua taharuki kwamba Kanisa letu limefungiwa.”
Awali, barua hiyo ambayo hakuna Mamlaka iliyojitokeza kuizungumzia, ilieleza Kanisa hilo limefungiwa kwa maelezo ya kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa Kisiasa na nia ya kuichonganisha Serikali na Wananchi
Soma https://jamii.app/GwajimaUpdates
#JFMatukio #JamiiForums

#BUNGENI: Mbunge wa Iramba Mashariki, Francis Mtinga, akichangia Mjadala wa #Bajeti ya Wizara ya Afya leo Juni 2, 2025
Soma https://jamii.app/VochaBimaYaAfya
#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii #JFAfya

❤3
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Jeshi la Polisi linadaiwa kuzingira Kanisa la “Ufufuo na Uzima” lenye Makao yake makuu Wilayani Ubungo Jijini Dar Es Salaam, linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM
Taarifa zinadai kuwa Askari hao wakiwa na magari zaidi ya matatu, wakivalia kiraia na wengine sare za Jeshi la Polisi wamezingira kanisa hilo na wengine wakiendelea kuwahoji baadhi ya waumini wa Kanisa hilo waliokutwa katika eneo hilo la Kanisa wakiendelea na shughuli mbalimbali
Haya yanajiri saa chache baada ya uwepo wa taarifa za serikali kulifutia usajili Kanisa hilo, siku moja tangu Kiongozi huyo kutangaza msimamo wake wa kuendelea kukemea na kupambana na vitendo vya utekaji na kupotezwa kwa watanzania
Soma https://jamii.app/PolisiKanisani
#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #Utawala #KuelekeaUchaguzi2025

10,000 inaonekana kuwa kubwa na yenye thamani, lakini inapata thamani hiyo kwasababu ya ile 1 ya kwanza. Bila hiyo, kinachobaki ni 0000 ambazo haina maana yoyote
Vivyo hivyo katika Maisha, Afya ni msingi wa kila kitu. Ukiwa na Afya njema, unaweza kufanya kazi, kutafuta pesa na kufurahia Mafanikio yako
Huku ukiendelea na harakati za Maisha, usisahau kuweka kipaumbele kwenye Afya yako kwa kula vizuri, kufanya mazoezi, kupumzika vya kutosha na kuchunguza afya yako mara kwa mara.
#JamiiAfrica #JamiiForums #Maisha #AmkaNaJF #GoodMorning

Tuambie Mdau, Kikosi chako kitakuwa na Wachezaji gani?
Mjadala zaidi https://jamii.app/SwaliFirst11
#JamiiForums #JamiiAfrica #Sports #Entertainment

DAR: Mdau wa JamiiForums.com anasema kuna Askari zaidi ya 30 kwenye eneo la Kanisa la “Ufufuo na Uzima” linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, huku wakiwa na silaha pamoja na Magari ya Polisi
Anasema licha ya hali hiyo, Waumini wa Kanisa hilo hawajaondoka ila wamekaa chini, ng'ambo ya Barabara toka Polisi walivyozingira Kanisa hilo Usiku wa jana, Juni 2, 2025
Haya yanajiri baada ya uwepo wa taarifa ya Serikali kutoka kwa Msajili wa Jumuiya za Kiraia kulifutia usajili Kanisa hilo, Siku moja tangu Kiongozi huyo kutangaza msimamo wake wa kuendelea Kukemea na Kupambana na Vitendo vya Utekaji na kupotea kwa Watanzania
Soma https://jamii.app/KanisaniGwajimaJuni3
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio #Governance #SocialJustice

❤2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa, akizungumza baada ya wasilisho la Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, Mei 26, 2025, alisema Serikali inaenda kufanya uchambuzi vizuri kuhusu taasisi na Watu wanaofanya Huduma za Kidini bila kujisajili
Soma https://jamii.app/TaasisiDiniKuchambuliwa
#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance #KuelekeaUchaguzi2025

DAR: Akizungumza na Wasafi FM kwa njia ya Simu, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Jumanne Muliro amesema Jeshi la Polisi linawashikilia Watu kadhaa kutoka Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Ubungo, kutokana na kile alichoeleza walikuwa wakizuia Jeshi hilo kutekeleza majukumu yake
Amesema "Wakati tukielekeza nini cha kufanya, kuna baadhi ya Watu walifanya mambo ya kutoelewa, ilibidi tuwachukue na tunaendelea kuzungumza nao kujua kweli walikuwa hawaelewi au walikuwa wanakataa tu ili kusababisha fujo."
Ameongeza “Sisi jukumu letu ni kuona tunaitekeleza Sheria, kama (Askofu Josephat Gwajima) akitaka shughuli ziendelee kufanyika basi afuate utaratibu wa Kisheria ikiwa ni pamoja na kukata rufaa kwa mamlaka za Kisheria zilizowekwa."
Soma https://jamii.app/MuliroKanisaGwajima
#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji