JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DODOMA: Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Kuu imetengua uamuzi wote wa Mkutano Mkuu wa NCCR-Mageuzi wa Septemba 24, 2022 uliopindua Uongozi wa Mbatia na kukubaliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa

Mahakama imesema Mkutano Mkuu wa NCCR Mageuzi wa Septemba 24, 2022 haukumpatia Haki ya msingi (Natural Justice) Mbatia ya kusikilizwa, hivyo ulikiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba ya Chama cha NCCR-Mageuzi na Sheria za Vyama vya Siasa

Aidha, Mahakama imetengua maamuzi yote yaliyofanywa na Mkutano huo ya kumuondolea Mbatia Uanachama na Uenyekiti huku ikikitaka Chama hicho kulipa gharama zote za kesi

Zaidi https://jamii.app/MbatiaAshinda

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Democracy #Kuelekea2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KATAVI: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) imebaini Mabati yenye thamani ya Tsh. Milioni 220 yaliyonunuliwa kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Katavi na Sekondari Rungwa kuwa yapo chini ya kiwango

Kaimu Mkuu wa #TAKUKURU Mkoa, Daud Lyamongo akitoa taarifa ya Ufuatiliaji wa Utelelezaji wa Miradi ya Maendelo ya Robo Mwaka, leo Mei 28, 2025 amesema Taasisi hiyo ilikagua Miradi miwili ya Elimu yenye thamani ya Tsh. Bilioni 4.3 na kubaini kasoro

Lyamongo ameongeza kuwa walibaini Mzabuni alilipwa Tsh. 220,023,980 na Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kabla ya Mabati kufika eneo la ujenzi kinyume na utaratibu

Soma https://jamii.app/TAKUKURUKatavi

#JamiiForums #Accountability #Governance #JamiiAfrica
DAR: Goli pekee la Steven Mukwala katika dakika ya 42 limeipa Simba ushindi wa Goli 1-0 dhidi ya Singida Black Stars kwenye Uwanja wa KMC Complex

Ushindi huo unaifanya #Simba kufikisha alama 72 ikiwa nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara ikiwa nyuma ya #Yanga yenye pointi 73, timu zote zikiwa zimecheza Michezo 27

Singida imebaki katika nafasi ya nne ikiwa na alama 53 katika Michezo 28

Soma https://jamii.app/SimbaSingidaMei28

#JamiiForums #JFSports #JFLigiKuu25
👍2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, amesema maoni yaliyotolewa na baadhi ya Wabunge wakati wa mjadala wa Bajeti za Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Maendeleo ya Jamii hayawakilishi msimamo rasmi wa Bunge hilo

Kauli hiyo inagusa baadhi ya kauli zilizotolewa kuhusu Wanaharakati kutoka Kenya na Uganda ambao waliingia Nchini kufuatilia kesi dhidi ya Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, Tundu Lissu ambapo baadhi ya Wabunge waliooneshwa kukerwa ujio wa Wanaharakati hao

Soma https://jamii.app/MaelezoYaSpika

#JamiiForums #Siasa #Diplomacy #Kuelekea2025 #Democracy #JamiiAfrica
👍2
KENYA: Rais #WilliamRuto ameomba radhi kwa Nchi jirani za Uganda na Tanzania, endapo kuna migogoro au sintofahamu ambazo hazijatatuliwa na zinaweza kudhoofisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Nchi hizo

Akizungumza katika Hafla ya Kitaifa ya Maombi, Rais Ruto amesisitiza kuwa #Kenya ipo katika safari ya 'kufufuka' na kujijenga upya na kuhimiza Wakenya kubadili mtazamo na kuwa na roho ya upatanisho na mshikamano, akieleza Serikali yake inalenga kuunganisha Taifa na kulijenga kwa pamoja

Amesema "Nawaomba tuache lawama na badala yake tujenge Madaraja ya maridhiano na umoja yatakayoiinua Nchi yetu kuwa bora zaidi,”

Soma https://jamii.app/RutoAombaRadhi

#JamiiAfrica #JamiiForums #Accountability #UtawalaBora #Diplomacy
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ZANZIBAR: Jeshi la Polisi limesema linafanya uchunguzi kuhusu kifo cha Sheikh Jabir Haidar Jabir Mkazi wa Fuoni ambaye Mwili wake uliokotwa eneo la Kizimbani Bumbwisudi Mkoa wa Mjini Magharibi ukiwa hauna jeraha wala hakukuwa na dalili za vurugu

Mwili huo uliokotwa Usiku wa kuamkia Mei 28, 2025 ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa, Richard Mchomvu, amesema umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya uchunguzi zaidi

Amesema Marehemu alikuwa anaishi na Kijana aliyekuwa akimsaidia na Mei 27, 2025 Saa 12 Jioni Sheikh alitembelewa na Vijana kadhaa ambapo aliondoka nao Saa 2:30 Usiku na baadaye akapatikana akiwa amefariki

Soma https://jamii.app/SheikhJabirHaidar

#JamiiForums #HumanRights #JamiiAfrica
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MAREKANI: Msanii wa Kenya, Bien-Aime Baraza "Bien" akihojiwa katika Kipindi cha Breakfast Club Power amezungumzia mambo yanayoendelea katika Nchi yake akitaja uwepo wa matukio ya Utekaji, Upinzani kuminywa na nafasi ya Vijana katika kuiwajibisha Serikali

Amesema kumekuwa na Uhuru wa Kujieleza lakini hakuna Uhuru baada ya Kujieleza na kwamba ana Imani kubwa kwa Vijana wa sasa kuliko Viongozi lakini pamoja na hayo bado anajivunia kuishi Kenya kwa kuwa ni Nchi nzuri na ina mambo mengi mazuri

Soma https://jamii.app/BienInterview

#JamiiForums #Governance #JamiiAfrica #Democracy #Entertainment #FreedomOfSpeech
1
Katika Mkutano Mkuu wa 14 wa Afrika wa Jukwaa la Utawala wa Mtandao (AfIGF) leo Mei 29, 2025, JamiiAfrica inashiriki kwenye Mjadala unaohusu 'Nani Anaongoza? Mashindano ya Uzingatiaji wa Haki za Kidigitali kati ya Nchi 27 za Afrika"

Wadau wa Mjadala huu watajadili mwenendo na matokeo ya Ripoti ya Haki za Kidigitali na Ujumuishaji Barani Afrika (LONDA) ya Paradigm Initiative, pamoja na namna Watetezi wa Haki za Kidigitali wanaweza kupima kiwango cha uzingatiaji wa Nchi za Afrika kwenye Tamko la Tume ya Afrika kuhusu Kanuni za Uhuru wa Kujieleza na Upatikanaji wa Taarifa.

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
Kuanzia leo Mei 29 hadi 31, 2025, JamiiAfrica inashiriki katika Mkutano wa 14 wa Afrika wa Utawala wa Mtandao (AfIGF2025) unaofanyika Dar es Salaam katika Ukumbi wa JNICC.

Mkutano huu unawakutanisha wadau mbalimbali kutoka Serikalini, Sekta binafsi, Asasi za Kiraia na Vijana ili kujadili kwa pamoja mustakabali wa Maendeleo ya Kidigitali Barani Afrika

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
3
Mkutano wa Jukwaa la Utawala wa Mtandaoni Afrika umeanza leo, Mei 29, 2025 ambapo JamiiAfrica itashiriki majadiliano kuhusu "Kuimarisha Uadilifu wa taarifa Mtandaoni", kuanzia Saa 3 hadi 4 asubuhi, katika chumba cha Bagamoyo

Majadiliano haya yanalenga kujadili changamoto za upotoshaji wa taarifa, mbinu za kujenga Mifumo ya taarifa iliyo thabiti na kuhamasisha ushirikiano wa Kimkakati kati ya wadau wote muhimu

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mbunge Halima Mdee ameeleza kuwa tuhuma dhidi ya Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu, kuhusu uhaini anashindwa kuzungumzia kwa kuwa anaamini kama ni kauli pekee za Kisiasa ndio zinahusika kwenye makosa ya Uhaini basi Wanasiasa wengi watakuwa matatizoni

Amesema hayo alipohojiwa na Kituo cha BBC ambapo ameeleza hafurahishwi na mgawanyiko unaoendelea ndani ya CHADEMA, kuhusu Kauli ya ‘No Reforms No Election’ amesema hana cha kuzungumza kwa kuwa hakuwa mshiriki wa mchakato wa Sera hiyo

Soma https://jamii.app/MdeeInterview

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Tabani Moyo kutoka The Media Institute of Southern Africa (MISA) amesema mbali na kuwa sehemu ya mnyororo wa Wahakiki wa Taarifa (Tact-Checkers), wameweka pia Msisitizo wa 'Kudemokrasisha' zoezi la Uhakiki wa Taarifa, kwa kuwajumuisha Wanahabari Wananchi (Citizen Journalists) na kuwapatia Mafunzo ya Kuchambua na Kuhakiki Taarifa kabla ya Uchaguzi.

Ameongeza pia wamegundua kwamba, bila Kushirikisha Majukwaa ya Kidijitali katika mjadala kuhusu Kanuni na Mifumo yao, wanakuwa wameacha pengo linaloweza Kuchochea Upotoshaji wa Taarifa

Kufuatilia bofya https://jamii.app/AfIGF2025Day1

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
JamiiAfrica imeshiriki kwenye Mjadala unaohusu Kujenga Utamaduni wa Usalama wa Kidigitali katika Jamii zilizotengwa, kwenye Mkutano Mkuu wa 14 wa Afrika wa Utawala wa Mtandao (AfIGF2025) unaofanyika katika Ukumbi wa JNICC.

Mjadala huu ulijadili zaidi ya uelewa wa kinadharia hadi utekelezaji wa vitendo kuhusu Usalama wa Kimtandao.

Washiriki waliangazia mikakati bunifu, mipango inayoongozwa na Jamii, na zana zinazoweza kutumika kwa vitendo ambazo zimetengenezwa ili kuingiza Usalama wa Kidigitali katika maisha ya kila siku ya jamii zisizohudumiwa ipasavyo.

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
1
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tech and Media Convergency (TMC), Asha Abinallah amesema tukiangalia suala la Uadilifu wa Taarifa kwa ujumla, ni jambo moja lakini hali hubadilika kabisa linapokuja kwenye Uadilifu wa Taarifa zinazohusiana na Uchaguzi

Ameongeza kuwa, Sifa au Vigezo vya kuamua kama taarifa ni Sahihi kwenye muktadha wa kijamii vinaweza kuendana na hali ya kawaida, lakini pindi taarifa hizo zinapohusiana moja kwa moja na Masuala ya Kisiasa, hali hubadilika

Kufuatilia bofya https://jamii.app/AfIGF2025Day1

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
1😁1
Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi anasema “Jukwaa la Utawala wa Intaneti kwa Vijana wa Afrika ni muhimu kwa mazungumzo, ubunifu, na utetezi, linaakisi roho ya kizazi ambacho si tu kinajua kutumia teknolojia, bali pia kina malengo kizazi chenye maono, sauti, na maadili yanayohitajika kuunda mustakabali wa mazingira ya kidijitali ya Afrika.”

Ameongeza “Kuwawezesha Vijana wa Afrika si jukumu la Serikali peke yake, Jukwaa linahitaji ushirikiano wa Serikali, Sekta Binafsi, Taasisi za Elimu ya Juu, na Jamii ya Kiraia. Kwa pamoja, lazima tuhahakikishe Vijana wanapata elimu, miundombinu, maarifa ya kidijitali, na huduma za intaneti zinazoweza kumuduwa.

Soma https://jamii.app/AfIGF2025Day1

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights
1
Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi anasema “Jukwaa la Utawala wa Intaneti kwa Vijana wa Afrika ni muhimu kwa mazungumzo, ubunifu, na utetezi, linaakisi roho ya kizazi ambacho si tu kinajua kutumia teknolojia, bali pia kina malengo kizazi chenye maono, sauti, na maadili yanayohitajika kuunda mustakabali wa mazingira ya kidijitali ya Afrika.”

Ameongeza “Kuwawezesha Vijana wa Afrika si jukumu la Serikali peke yake, Jukwaa linahitaji ushirikiano wa Serikali, Sekta Binafsi, Taasisi za Elimu ya Juu, na Jamii ya Kiraia. Kwa pamoja, lazima tuhahakikishe Vijana wanapata elimu, miundombinu, maarifa ya kidijitali, na huduma za intaneti wanazoweza kuzimudu"

Soma https://jamii.app/AfIGF2025Day1

#JamiiAfrica #AfIGF2025 #UadilifuWaTaarifa #MaendeleoYaKidijitali #HakiZaKidijitali #UsalamaMtandaoni #UpotoshajiWaTaarifa #UtawalaWaMtandao #Uwajibikaji #DigitalRights