JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Maryam Omar Said, Mbunge wa Pandani, Zanzibar, leo Mei 26, 2025 amesema "Tumemuacha Martha Karua anaendelea kuzungumza akiwa Kenya kule, Mheshimiwa Waziri hili lisitokee tena. Anayekuja kwetu tunamalizana naye hapa hapa, anayeingia ndani ya kumi na nane zetu, tumalizane naye hapa, hapa,"

Zaidi https://jamii.app/KaruaKurudishwaMzima

#JamiiForums #JamiiAfrica #SocialJustice #Kuelekea2025 #Governance #Diplomacy
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Leo Mei 26, 2025, Mbunge wa Viti Maalum, Esther Matiko amesema "Udhalilishaji mtandaoni unafanywa na hao watu wa nje tunasema lakini zinasambazwa na kwenye mitandao ya Kitanzania, tuko wapi? Kwa nini tunaruhusu hii? Ni udhalilishaji na unaweza kuona kwamba ni udhalilishaji kwa sababu Mama, yaani Rais wetu ni mwanamke,"

Ameongeza "Mshirikiane, Mambo ya Ndani ya hapa, Idara ya Mawasiliano na kule Kenya, tuwakamate hawa Gen-Z wa kule"

Soma https://jamii.app/GenZWakamatwe

#JamiiAfrica #JamiiForums #Diplomacy #Kuelekea2025 #Accountability #DigitalRights
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Abbas Tarimba amekitaka Chama cha Mapinduzi (CCM) kumchukulia hatua Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima kupitia Kamati ya Maadili ya Chama hicho, kufuatia kauli alizotoa dhidi ya Rais, alipozungumza na Waandishi wa Habari, Mei 24, 2025

Akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2025/2026, leo Mei 26, 2025, Tarimba amesema kauli za Gwajima kuhusu madai ya utekaji ni za kudhalilisha na hazikubaliki

Soma https://jamii.app/TarimbaVsGwajima

#JamiiAfrica #JamiiForums #Kuelekea2025 #Uwajibikaji #SocialJustice
Katika dunia ya leo yenye ushindani mkubwa, hakuna njia ya mkato kuelekea mafanikio ya kweli. Mafanikio si jambo la bahati au muujiza wa ghafla, ni matokeo ya juhudi za kila siku, nidhamu, na kujitoa kwa dhati.

Mafanikio hayawezi kuja bila kutoka 'jasho', lazima tukubali kupitia changamoto, kuamka mapema, kukosa usingizi na mara nyingine hata kushindwa, lakini tusikate tamaa.

Vumilia, endelea kujituma na uamini kuwa jasho lako leo litakuwa faraja yako kesho

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJF #GoodMorning
👍2
MOROGORO: Mdau wa JamiiForums.com anadai baadhi ya Viongozi katika Kata ya Lukobe Kihonda, Mtaa wa Majengo Mapya wamekuwa wakiuza mchanga unaochimbwa kwenye maeneo ya Shule ya Juhudi kisha Fedha zinaenda kwenye Mifuko yao

Anatoa wito kwa Mamlaka za juu kufika kukagua Miundombinu inavyozidi kuharibika na kuchukua hatua, tofauti na hapo Shule hiyo ndio inaweza kuzidi kupoteza mwelekeo

Soma https://jamii.app/MorogoroMazingira

#JamiiForums #Accountability #JamiiAfrica #Uwajibikaji
👍1
#SIASA: Kupitia akaunti rasmi ya #JohnMrema, aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CHADEMA ametangaza kuwa kundi Sogozi la G-55 limekufa rasmi na halipo tena, hivyo pia Usemaji wake kwenye Kundi hilo umekoma.

Amesema kama kuna jambo lolote litakalotumia jina la Kundi hilo, ieleweke kuwa ni Watu watakuwa wanatumia jina hilo kwa maslahi yao binafsi na hawaisemei G-55 ambayo imeshakufa rasmi na haipo tena

Mrema amesema tangazo hilo ni kufuatia taarifa kuwa kuna Watu wamepanga kutumia jina hilo ili kuhadaa Umma, kuwa kundi hilo bado lipo jambo ambalo sio la kweli

Soma https://jamii.app/KifoChaG55

#JamiiAfrica #JamiiForums #Kuelekea2025 #Democracy #Accountability
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
SONGWE: Jeshi la Polisi limesema linamshikilia Mtu mmoja kwa tuhuma za mauaji ya Katekista wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu wa Mtoto Yesu lililopo Tazara - Tunduma, Vincent Mwenda ambaye alifariki Mei 10, 2025 kwa kushambuliwa na kitu chenye ncha kali

Kamanda wa Polisi Mkoa, Augustino Senga amesema wanamshikilia Lameck Mwamlima (29), Fundi Magari ambaye ni Mkazi wa Migombani Tunduma na kuwa uchunguzi wa awali umebaini Mtuhumiwa alimtuhumu Katekista kutembea na mke wake, hivyo kufanya mauaji hayo kama kisasi na kwamba kuna mtuhumiwa mwingine ambaye anatafutwa.

Soma https://jamii.app/MauajiSongweUpdates

#JamiiForums #HumanRights #Accountability #JFMatukio
1
Uwajibikaji una nafasi gani katika kuleta maendeleo endelevu? Na wale waliofanikiwa, walifanya nini tofauti?

Usikose kushiriki nasi kwenye mjadala huu muhimu, tukijifunza kutoka kwa mifano halisi na kuchambua hatua zinazoweza kuleta mabadiliko ya kweli katika uongozi na maendeleo ya jamii

Njoo utoe maoni, jifunze na kuwa sehemu ya mjadala wa kujenga Tanzania tunayoitaka, Jumatano hii, Mei 28, 2025, kuanzia Saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku, kupitia #XSpaces ya JamiiForums

Kujiunga bofya https://twitter.com/i/spaces/1eaKbWqZegXGX

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSpaces #TheNordics #NordicWeek #Uwajibikaji #Accountability
SIASA: Mmoja wa waasisi wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Eugene Kabendera ametangaza kujiondoa rasmi katika Chama hicho baada ya kukitumikia kwa Miaka 13, akieleza kuwa Chama hicho kimepoteza dira na kwamba uamuzi wake ni wa kimaadili kwa lengo la kulinda uadilifu wa Kisiasa.

Kabendera, ambaye aliwahi kuwa Msemaji rasmi wa Kwanza wa Chama, Naibu Katibu Mkuu wa Tanzania Bara, na Mwakilishi wa CHAUMMA katika Baraza la Vyama vya Siasa, amesema mwelekeo wa sasa wa Chama hauakisi tena misingi na maono yaliyowasukuma kukianzisha Mwaka 2012.

Aidha, ameeleza kuwa ingawa hatangazi kujiunga na Chama kingine kwa sasa, yuko wazi kuchunguza ushirikiano wa baadaye wa Kisiasa utakaolingana na misingi na maono yake kwa taifa

Soma https://jamii.app/KabenderaCHAUMMA

#JamiiAfrica #JamiiForums #Kuelekea2025 #Governance #Uwajibikaji
👍1
#SIASA: Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mohamed Kawaida kupitia akaunti yake ya Mtandao wa Instagram amesema hawawezi kumkalia kimya Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima na kumtaka wakutane 'site'

Soma https://jamii.app/KawaidaGwajima

#JamiiForums #JamiiAfrica #Democracy #Accountability #Governance #Kuelekea2025
👍1
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Mamlaka zinazohusika na Kituo cha Stendi cha Mbagala Rangi Tatu kutenga fedha kwa ajili ya kufanya uboreshaji hata kama ni ya muda mfupi kwa kuwa hali ilivyo sasa inasababisha kesho kwa Watumiaji

Soma https://jamii.app/StendiYaMbagalaRangiTatu

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Afrika inaendelea kupiga hatua katika teknolojia na matumizi ya mtandao, lakini ili tufike mbali zaidi tunahitaji sera bora, usimamizi wa haki na sauti za wadau wote hasa Vijana, Wanawake, Sekta Binafsi na asasi za kiraia

Jukwaa la Utawala wa Mtandao Afrika (AfIGF2025) litafanyika kuanzia Mei 29 hadi 31 na linalenga kuwaleta pamoja wataalamu wa teknolojia, watunga sera, watoa huduma na watumiaji wa mtandao kwa majadiliano ya kina kuhusu mustakabali wa Kidijitali wa Afrika

Ni jukwaa la kujifunza kutoka kwa wengine, kujenga mitandao ya ushirikiano na kuchangia mawazo yatakayosaidia kujenga Afrika jumuishi zaidi mtandaoni

#AfIGF2025 #AfricalGF #KuimarishaAfrikaKidigitali #JamiiForums #JamiiAfrica
Mwanachama wa #CCM aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basilla Mwanukuzi ametuma ujumbe kwa Rais Samia Suluhu kupitia Ukurasa wake wa Instagram akisema “Uzalendo ni kuweka siri ila uzalendo zaidi ni kutofanya hayo yanayovujishwa ili kutakiwa kubakishwa sirini.”

Ameandika “Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa heshima na taadhima na upendo mkuu kwako, kuvujisha siri ni utovu mkubwa wa maadili, na ni kosa kubwa ila kufanya yanayovujishwa ni ukosefu mkubwa zaidi wa maadili na kosa kubwa zaidi.”

Ameongeza “Kama wanaokosea ni Viongozi na ni Watu, ni Wanadamu wenye mapungufu, vivyo hivyo wanaovujisha nao ni Watumishi na ni Watu, ni binadamu wenye mapungufu na wakati mwingine ukute anafanya ili mkubwa aone apate kuchukua hatua, akijiweka yeye mwenyewe matatizoni.”

Soma https://jamii.app/BasillaMwanukuzi

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
👍21