JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
#JFKUMBUKIZI: Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, Seleman Bungara (Bwege) kupitia #CUF akizungumzia thamani ya Maisha ya Mtu

Mjadala https://jamii.app/BwegeKuuaWatu

#JamiiForums #HumanRights #HakiZaBinadamu
👍3🥰1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#KENYA: Jeshi la Polisi limefika katika Jengo la Ubalozi wa Tanzania Jijini #Nairobi, leo Mei 22, 2025 ikiwa ni hatua ya tahadhari kufuatia taarifa za Maandamano yaliyopangwa na Wanaharakati wanaoshinikiza kuachiwa huru kwa Mwanaharakati maarufu #BonifaceMwangi

Wanaharakati hao wanaandamana kwa Amani wakitaka Serikali ya #Tanzania kutoa maelezo kuhusu sababu ya kushikiliwa kwa Mwangi ambaye walikuja Tanzania kufuatilia kesi inayomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu, Mei 19, 2025.

Soma https://jamii.app/PolisiUbaloziTZKE

#JamiiForums #JamiiAfrica #Diplomacy
👍1👏1
KENYA: Kituo cha Runinga cha NTV kimeeleza kuwa Mwanaharakati Boniface Mwangi amerejeshwa Kenya baada ya Siku kadhaa za kushikiliwa Jijini Dar es Salaam ambapo alikwenda fuatilia kesi inayomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu

NTV imeripoti kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora, Musalia Mudavadi amesema Mwangi aliachiliwa Asubuhi ya leo Mei 22, 2025 bila kutoa taarifa zaidi

Aidha, NTV imesema Familia ya Mwangi imethibitisha Ndugu yao alisafirishwa kwa Gari na kutelekezwa kwenye Mpaka kati ya Tanzania na Kenya eneo la Ukunda ambapo kwasasa wamempeleka Hospitali kwaajili ya kuangalia Afya yake.

Soma https://jamii.app/MwangiFreedUkunda

#JamiiForums #JamiiAfrica #Diplomacy #HumanRights
😁1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka kushughulikia kero ya mtaro uliopo ya Mtaa wa Karatu (Mbezi Beach) kwa umesababisha changamoto kwa Watumiaji wa barabara hiyo

Soma https://jamii.app/KeroMtaaKaratu

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #JFMdau2025
👍1
Handaki la Lærdal nchini #Norway ndilo handaki refu zaidi la barabarani Duniani ambalo inauunganisha Miji ya Lærdal na Aurland

Ujenzi wake ulianza Mwaka 1995 na kuanza kutumika rasmi Mwaka 2000.

#JamiiForums #JamiiAfrica #NordicWeek #Tourism #LærdalTunnel
#MALEZI: Mdau wa JamiiForums.com anasema alipomaliza Darasa la saba alipewa kazi ya kupanda miti kwenye shamba la Ekari moja alilonunua Baba yake mpaka muda wa kwenda Kidato cha 1 ulipofika

Pia, alipomaliza Kidato cha 4 alikabidhiwa Shamba la Vitunguu kuanzia kuandaa Shamba hadi kuvuna kipindi cha likizo ya kusubiri Kidato cha 5

Mafunzo yote hayo aliyopitishwa na Wazazi wake anasema yamemjengea Kujiamini na kuw na Ujuzi wa kufanya vizuri kwenye Ajira aliyojiajiri na kuweza kuwasimamia aliowaajiri.

Soma zaidi https://jamii.app/MtotoKufanikiwaMalezi

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #LifeLessons #Parenting
1
MWANZA: Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) imesema Meli ya New MV Victoria inatarajiwa kuanza safari zake rasmi leo Alhamisi Mei 22, 2025 ikitokea Bandari ya Mwanza Kaskazini kuelekea Bandari ya Bukoba kupitia Bandari ya Kemondo

Itakuwa mara ya kwanza meli hiyo kufanya safari baada ya kusimamisha huduma kwa miezi miwili ambapo TASHICO imewataka abiria kufika bandarini Saa 1:30 Jioni au kabla ya muda huo kwa kuwa meli inatarajiwa kuanza safari Saa 3:00 Usiku

Ikumbukwe Machi 10, 2025, Mdau wa JamiiForums.com alihoji ukimya wa Mamlaka kuhusu meli hiyo kusitisha huduma, TASHICO ikajitokeza na kueleza ipo katika matengenezo ya mwezi mmoja, baadaye ikaeleza maboresho yanaenda.

Soma https://jamii.app/MvVictoriaReturn

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #ServiceDelivery
PWANI: Mdau wa JamiiForums.com anahoji ni kwa nini Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) halichukui hatua au kukagua uharibifu wa mazingira unaofanywa na Kiwanda cha Pombe kilichopo Misugusugu Kibaha ikiwa Wananchi wameshalalamika mara kadhaa kwa Mamlaka hiyo?

Anadai maji hayo machafu yamekuwa na athari kwa viumbe wanaoishi au kutumia mabwawa madogo yaliyopo jirani

Soma https://jamii.app/MazingiraKibaha

#JamiiForums #ClimateChange #Accountability
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
UCHUMI: Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Akaro amesema "Kwa Mwaka huu fedha za kigeni zilizopo kwenye soko zimeongezeka ukilinganisha na Mwaka uliopita (2024), tulikuwa na Dola Milioni 30 kwa siku, sasa hivi tuna Dola Milioni 70 kwa siku."

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika Semina ya Waandishi wa Habari iliyofanyika Mei 20, 2025 katika ofisi za Benki Kuu, Dar es Salaam

Soma https://jamii.app/MarufukuFedhaKigeniManunuzi

#JamiiForums #JFUchumi
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KAGERA: Baada ya ujenzi wa Daraja la Mto Kanoni kuonekana unasuasua kwa madai ya ujenzi holela kando ya Mto huo, Mkuu wa Mkoa, Fatma Mwassa ameelekeza TANROADS na Manispaa ya Bukoba kufanya vipimo kubaini usahihi wa kingo za Mto huo

Ikumbukwe Januari 6, 2025, Mdau wa JamiiForums.com alieleza ujenzi holela maeneo hayo mfano jengo la 'Night Club & Bar' limejengwa katika eneo la Hifadhi ya Mto Kanoni, akahoji Mamlaka zinatoaje kibali cha ujenzi wakati sehemu hiyo sio salama kwa Watu

Soma https://jamii.app/DarajaMtoKanoni

#JamiiForums #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Kaulimbiu ya Mwaka 2025 ikiwa ni "Kuimarisha Mustakabali wa Kidijitali wa Afrika" mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo Miundombinu ya Umma ya Kidijitali na Utawala wa Taarifa, Usalama Mtandaoni, Uhimilivu na Uaminifu pamoja na Akili Mnemba (AI) na Teknolojia Zinazoibuka katika Jukwaa la 14 la Utawala wa Mtandao Afrika utakaofanyika kuanzia Mei 29 hadi Mei 31, 2025 Jijini Dar es Salaam.

#AfIGF2025 #AfricalGF #KuimarishaKidijitaliAfrika #JamiiForums
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anasema Barabara ya Tabata - Kimanga kutokea Tabata Bima imeharibika sana hasa kutokea Chama mpaka Mawenzi

Anaeleza kuwa Gari nyingi zinaharibika kila Siku na kipindi cha Mvua baadhi ya Daladala zinashusha Abiria au kukatisha ruti kwasababu hakupitiki, hivyo Mamlaka husika iangalie namna ya kurekebisha changamoto hiyo

Soma https://jamii.app/RoadTabataBimaKimanga

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii
1
Kwenye Elimu kidogo umetupa ahueni japo Mazingira ya Shuleni magumu ila kwenye Afya unanikamua haswa, Umeme nako mpaka nimeshindwa kuunganisha Nyumbani, Maji siyaoni. Kwani unafanya Biashara kwamba unahitaji faida? Nakuchangia kwa kila ninachopata kwani unazipeleka wapi mbona sioni matumizi yake

Ila niliambiwa waliopo kwenye ‘System’ wanazifaidi, hivi ni kweli? Maana wakipoteza Mabilioni wanaambiwa walipe faini Milioni, inashangaza.

Hili ni Andiko liliwasilishwa kwenye Shindano la Stories of Change 2023 na unaweza kulisoma zaidi kwa kubofya hapa https://jamii.app/TabasamuTZSOC03

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #Uwajibikaji #SOC2023
👍2