JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mdau wa Jukwaa la Biashara, Uchumi na Ujasiriamali ndani ya JamiiForums.com amesema Watu wachache wako tayari kuingia kwenye gharama ya kujifunza kidogo na kuwa na moyo usiokata tamaa ndiyo maana matajiri ni wachache kwa kisingizio cha kauli ya "Sina Mtaji wa Biashara"

Je, unakubaliana na Mdau huyu?

Mjadala zaidi https://jamii.app/MtajiSioMafanikio

#JamiiForums #Lifestyle #Biashara
UGANDA: Kituo cha Utafiti cha Agora kimethibitisha kuwa Mkurugenzi wao, Agather Atuhaire amepatikana katika Mpaka wa Uganda na Tanzania (Mutukula) leo asubuhi Mei 23, 2025 akiwa hai

Taarifa ya Agora kupitia Mtandao wa X imesema kuwa "Tunafarijika kuufahamisha Umma kuwa amepatikana. Alitelekezwa mpakani na Mamlaka ya Tanzania. Maelezo zaidi yatatolewa baadaye leo. Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kila mtu ambaye alisimama kwa mshikamano wakati huu. Juhudi zako zilifanya mabadiliko."

Ikumbukwe kuwa wanaharakati Agather Atuhaire na Boniface Mwangi kutoka Kenya walishikiliwa Jijini Dar es Salaam ambapo walienda fuatilia kesi inayomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, #TunduLissu

Soma https://jamii.app/AgatherAkutwaMpakani

#JamiiForums #JamiiAfrica #Diplomacy #HumanRights
DAR: Makamu Mwenyekiti wa Chama cha #ACTWazalendo, Isihaka Mchinjita amekamatwa na Jeshi la Polisi, leo Mei 23, 2025 baada ya kuingia kwenye Kituo cha Mwendokasi cha Kimara Mwisho kwa lengo la kujionea adha ya usafiri huo

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa ACT, Shangwe Ayo amesema “ACT tumekuwa tukipata malalamiko mara nyingi ya malalamiko ya Usafiri wa Mwendokasi kutoka kwa Wananchi hasa wa Kimara, hivyo Baraza Kivuli la Mawaziri tulikwenda kujionea, kukagua na kufichua madudu yanayoendelea katika huduma hiyo, ndipo Askari Polisi wakafika na kumkamata."

Ameongeza "Amekamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi Kimara, aliongozana na Mlinzi wake na Mwandishi wa Habari, tunafuatilia kujua kinachoendelea, tutatoa taarifa kamili baadaye.”

Zaidi https://jamii.app/MchinjitaAkatwaKimara

#JamiiForums #JamiiAfrica #Governance
👍1
ZANZIBAR: Mdau wa JamiiForums.com anasema Mamlaka zimekuwa zikifungia Watu Nyumba kwasababu ya uchafu katika maeneo ya Kilimahewa na Jang'ombe lakini kwanini Wakazi wa Nyumba za Michenzani zinazoweka Afya za Watu hatarini zimekuwa hazichukuliwi hatua?

Soma https://jamii.app/MajitakaMichenzani

#JamiiForums #Accountability #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Governance
MAREKANI: Serikali ya Rais #DonaldTrump imekizuia Chuo Kikuu cha Harvard kuandikisha Wanafunzi wa Kigeni ambapo inaelezwa imechukua hatua hiyo kwa kuwa #Harvard inaiunga Mkono Palestina pamoja na kushirikiana na Chama cha Kikomunisti cha China

Barua iliyoelekezwa kwa Uongozi wa Chuo hicho inaeleza kuwa Cheti cha Usajili cha Mpango wa Kubadilishana Wageni (Student Exchange Visitor Program – SEVP) cha Chuo hicho kimefutwa rasmi

Chuo cha Harvard kina jumla ya Watu 9,970 katika kundi lake la Taaluma ya Kimataifa na takwimu zinaonesha Wanafunzi wa Kimataifa 6,793 wanachangia 27.2% ya Usajili wake kwa Mwaka wa Masomo wa 2024–2025

Soma https://jamii.app/HarvardBannedOutsiders

#JamiiForums #Governance #Diplomacy #JamiiAfrica
👍1👎1
Mwaka 2021, Denmark ilizindua Shamba kubwa zaidi la Upepo katika eneo la Skandinavia (Scandnavia) linaloitwa "Kriegers Flak." Shamba hili lina uwezo wa kuzalisha Umeme wa kutosha kuhudumia takriban Kaya 600,000 za Denmark

Hata hivyo, Upepo sio Nishati mbadala pekee inayotumiwa Nchini Denmark, nafasi ya kwanza inashikiliwa na Nishati ya Mimea (Bioenergy), ikifuatiwa na Upepo, Jua na Nishati kutoka kwenye Joto la Ardhini (Geothermal).

#JamiiForums #JamiiAfrica #NordicWeek #WindEnergy #RenewableEnergy
1
Jukwaa la 14 la Utawala wa Mitandao Afrika litawakutanisha Wadau mbalimbali wa Teknolojia na Mitandao kujadili ushirikiano wa Kidijitali na upatikanaji wa huduma ya Mtandao kwa wote

Jukwaa hili litafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam kuanzia Mei 29 hadi Mei 31, 2025

#AfIGF2025 #AfricalGF #KuimarishaKidijitaliAfrika #JamiiForums
👍1
Unapochagua eneo moja na kuwekeza Muda, Nguvu na Akili zako zote, unajitengenezea nafasi kubwa ya kuwa Mbobezi wa kile unachokifanya (mastery)

Hii inakuwezesha kufanya kwa ubora zaidi, kukua kwa kasi na hatimaye kufikia mafanikio makubwa, ambayo usingeweza kuyafikia kwasababu kugusagusa kila kitu kwa uchache.

JamiiAfrica inakutakia Mapumziko mema ya mwisho wa Wiki

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #Weekend #GoodMorning #AmkaNaJF #Lifelessons
Mwandishi wa Andiko la Stories of Change 2023 anasema Ajira za kujua zinaweza kuchangia Taasisi za Elimu kuajiri Watu wasio na Uwezo na Ujuzi unaohitaji na kusababisha Wanafunzi kupata Mafunzo kutoka kwa Watu wasiojitosheleza kitaaluma

Vipi Mdau, umeshawahi kuwa mwathirika wa Ajira za kujuana?

Soma Andiko hili kwa undani zaidi https://jamii.app/AjiraKujuanaSOC03

#JamiiForums #JamiiAfrica #SOC2023 #EmploymentCrisis
Mdau wa JamiiForums.com amewashauri Watumishi wa Umma kuwa makini na Mikopo wanayoichukua kwasababu hali ya Maisha ni ngumu, hivyo baadhi ya Taasisi za Kifedha zinatumia huo mwanya kuwahadaa na kuwaingiza mkenge ambapo mwisho wake wengi hujutia

Mjadala zaidi https://jamii.app/MikopoWatumishiUmma

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFStories #JFChitChats
Mdau wa JamiiForums.com anasema wakati mwingine #Biashara kuwa na Mkopo kunatoa kinga kwa mmiliki wa Biashara hiyo

Ametolea Mfano suala la Majanga kama Moto kwenye Biashara, akisema ikiwa Mfanyabiashara ulichukua Mkopo Benki na kununua Hisa, zinaweza kufanyika msaada kwako pale yanapotokea Majanga

Je, unakubaliana na hoja hii?

Soma zaidi https://jamii.app/MikopoBiashara

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uchumi