JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Kufuatia makubaliano yanayoendelea kati ya #CHAUMMA na makada waliotoka #CHADEMA, Hashim Rungwe anaendelea kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Makamu wake (Bara) anakuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kati, Devotha Minja

Aidha, nafasi ya Katibu Mkuu amepewa Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu Bara amepewa Benson Kigaila, upande wa Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu amekuwa Mohamed Masoud

Mgawanyo huo umekuja baada ya waliokuwa Viongozi wa #CHAUMMA kujiuzulu nafasi zao leo Mei 19, 2025 akiwemo aliyekuwa Katibu Mkuu, Mohammed Masoud Rashid, Naibu Katibu Mkuu Bara, Rahman Rungwe na Makamu Mwenyekiti Bara, Kayungo Mohammed

Zaidi https://jamii.app/G55WalambaVyeo

#JamiiForums #KuelekeaUchaguzi2025 #Governance
1
DODOMA: Rais Samia amesema kutokujitokeza kujiandikisha au kuhuisha taarifa zako katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ni sawa na Mtu kukataa Haki yake ya Kikatiba kwa hiari, jambo ambalo siyo Uzalendo

Akiyasema hayo Mei 17, 2025 ameeleza "Kutokujitokeza kujiandikisha ni kukataa mwenyewe Haki yako ya Kikatiba na unapokataa Haki ya Kikatiba jiulize je, wewe ni Mzalendo? Mzalendo wa aina gani ambaye Katiba imekupa fursa nenda kajiandikishe, piga kura, weka Kiongozi unayehisi atakuja kukuhudumia, wewe unaikataa, ukiikataa wenzio wataenda kuweka wanayemtaka na utakosa fursa ya kushawishi wengine kuweka yule mnayemtaka, kwahiyo unakuwa wewe wa kubabaisha tu na kulalamika."

Soma https://jamii.app/SamiaKajiandikishe

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #Democracy #UchaguziMkuu2025 #TanzaniaElection2025
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais Samia amesema "Nimeona Clip kadhaa za kunisema, mara nina ubaguzi na nini! Ninalofanya ni kulinda Nchi yangu na ndiyo wajibu wangu niliopewa. Kwa hiyo hatutatoa nafasi kwa kiumbe yeyote kutuvuruga awe ndani ama anayetoka nje."

Ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001, Mei 19, 2025

Soma https://jamii.app/ClipMnanisema

#JamiiForums #Kuelekea2025 #Governance
👍3
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Rais Samia ameelekeza Mamlaka mbalimbali ikiwemo za Usalama na Wizara ziwe zinatoa majibu, ufafanuzi au kuelezea hoja zinazotolewa dhidi ya Nchi au Serikali, ili Jamii iwe na uelewa sahihi wa yanayoendelea

Ametoa maelekezo hayo wakati wa Uzinduzi wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001, Mei 19, 2025 katika Ukumbi wa JNICC

Soma https://jamii.app/WanaharakatiKudhibitiwa

#JamiiForums #Kuelekea2025 #Diplomasia #Accountability
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KUMBUKIZI: Mwenyekiti wa #CHAUMMA, Hashim Spunda Rungwe alisema haya Aprili 20, 2024, akiwa katika kipindi cha Medani za Siasa kinachoendeshwa na Chief Odemba

Zaidi https://jamii.app/HelaZaCCM

#JamiiForums #Governance #Accountability #KuelekeaUchagua2025 #JFKumbukizi
1👍1
Mwandishi wa Andiko la Shindano la Stories of Change 2021 anasema kuna wizi unaofanywa na Taasisi za Fedha kupitia mikopo inayoitwa Top Up, hii ni Mikopo ambayo Mkopaji anakuwa na Deni lingine analoendelea kulipa, anapewa mkopo mwingine juu ya ule mkopo wa awali

Anadai mpaka sasa hakuna Sera wala Sheria yoyote inayomlazimisha Mwajiri kuboresha maslahi ya Mtumishi wake, bali kilichopo ni kama hiari kwa Mwajiri jambo linalosababisha Watumishi wengi kukimbizana na Mikopo ya hapa na pale inayowaongezea ugumu wa Maisha

Unakubaliana na hoja ya Mdau huyu?

Soma zaidi https://jamii.app/MikopoWatumishiSOC1

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #SOC2021
👍1
Vipi Mdau, na wewe ni mpenzi wa Paa ndefu au huwa unazingatia nini kwenye Ujenzi wa Paa la Nyumba?

Shiriki Mjadala huu zaidi https://jamii.app/NyumbaBatiRefu

#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #JFChitChats #JFStories
👍1
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limesema kuwa Ripoti ya Mkaguzi imeonesha maboresho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa hayawezi kukamilika kwa wakati kwa ajili ya kuandaa Mchezo wa Marudiano wa Fainali ya Kombe la Shirikisho uliopangwa kufanyika Mei 25, 2025

Taarifa ya CAF imeeleza kuwa (Kama ilivyotangaza awali) mchezo huo wa #Simba dhidi ya #RSBerkane unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar

Taarifa hiyo imeeleza kuwa #CAF itaendelea kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Serikali ya Tanzania na Wadau wote kuhakikisha Uwanja wa Mkapa na viwanja vyote vinakuwa tayari kwa Mashindano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) na kukidhi Kanuni na Viwango vya CAF yanayotarajiwa kuanza Agosti 2, 2025

Soma https://jamii.app/CAFMkapaStadium

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSports
👍21
USALAMA MTANDAONI: Jeshi la Polisi limetoa tamko kuhusu taarifa zilizosambazwa kupitia Akaunti za Jeshi la Polisi kwenye Mtandao wa X na kusema taarifa hizo ni za uongo, upotoshaji na zisizo na maadili

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema kuwa taarifa hizo si za kweli na wanaendelea kufuatilia wahalifu waliotengeneza na kusambaza taarifa hizo ili wakamatwe.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa aliyehusika na utengenezaji na utoaji wa taarifa hizo na yeyote yule ambaye ataendelea kuzisambaza

Soma https://jamii.app/TaarifaPotofuPolisiX

#JamiiForums #Misinformation #Accountability #DigitalSecurity
Taarifa ya Wizara ya Afya imesema vipimo vimeonesha hakuna kirusi kipya kinachoweza kusambaa kwa haraka na kusababisha mlipuko aina ya Pandemiki. Ugonjwa wa #UVIKO19, umeendelea kuwepo kwa kiwango cha chini kama yalivyo Magonjwa mengine ya mfumo wa njia ya hewa

Aidha, Wizara imesema hali ya kuongezeka na kupungua kwa Ugonjwa wa UVIKO-19 imekuwepo kila Mwaka tangu kutangazwa kwa Ugonjwa huu Mwaka 2020, kwa kipindi hiki ongezeko linaonekana zaidi katika Mkoa wa Dar es Salaam

Pia, kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Nchi, hususan katika Mikoa ya Pwani, kumekuwa na ongezeko la hatari ya kuenea kwa Magonjwa yanayoenezwa na Mbu, kama vile Homa ya Dengue, Malaria, na Magonjwa mengine ya aina hiyo.

Soma zaidi https://jamii.app/OngezekoUvikoMbu

#JamiiForums #JamiiAfrica #PublicHealth #Afya
👍2
Mwanachama wa JamiiForums.com anasema Nchi nyingi ambazo zilitafuta Amani bila kuzingatia Haki za Binadamu zilishindwa kwasababu Amani waliyoipata ilikuwa ya muda mfupi na isiyo na maana.

Tembelea Mjadala huu https://jamii.app/HakiAmani

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #Democracy
MICHEZO: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com, Mei 13, 2025 kuwasilisha malalamiko kwa mamlaka husika kuchukua hatua dhidi ya tukio la Viongozi wa Simba Queens kuwashambulia Waamuzi baada ya mchezo dhidi ya Mashujaa Queens, Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfungia Meneja wa Simba Queens, Selemani Makanya kwa Miezi 6 na kulipa faini ya Tsh. Milioni 1.5

Mchezo huo wa Mei 12, 2025 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo uliomalizika kwa sare ya 2-2, baadhi ya Viongozi wa Benchi la Ufundi la Simba Queens walianzisha vurugu na kuwavamia Waamuzi, wakipinga baadhi ya maamuzi yaliyotolewa uwanjani

Pia, Kocha Msaidizi wa Simba Queens, Mussa Mgosi amefungiwa mechi tatu na kutakiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 1.5 kwa kuzingatia Kanuni ya 46(2) (1) ya Ligi za Wanawake.

Soma https://jamii.app/SimbaQueensAfungiwa

#JamiiForums #JFMichezo #JFSports #Accountability
1👍1