JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com anadai Barabara ya Musoma - Mwanza imekuwa ikitengenezwa mara kwa mara lakini hata miezi miwili haiishi inafumuka, ina matuta kuliko Barabara za Changarawe wakati ni barabara kubwa (cross country road)

Anadai kipande cha Nyanguge - Lugeye kilifumuka hata kabla ya mwezi mmoja kumalizika, kilichofuata wakaanza kuweka viraka

Anatoa wito Mamlaka husika kusimamia ubora kwa kuwa hali inavyoendelea wanaoumia ni wengi na madhara kwa Watu na Vyombo vya Usafiri yanaongezeka

Soma https://jamii.app/MusomaMwanza

#Accountability #JamiiForums
👍2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
ARUSHA: Mchungaji wa Kanisa la Huduma ya Kristo lililopo Mtaa wa FFU, Kata ya Murieti, Steven Jacob Gumbo (35) ambaye iliripotiwa ametekwa na ‘Watu Wasiojulikana’ Mei 16, 2025 amezungumza na Wanahabri na kueleza kuwa Watu waliomchukua walijitambulisha kuwa ni Askari Polisi na wanamhitaji kwa ajili ya mahojiano

Amesema Watu hao walimchukua kwa nguvu huku wakimpiga, akapelekwa sehemu ambayo hakuifahamu na kuingizwa kwenye chumba kisha kuanza kumshambulia

Ameongeza “Naomba nisiongee mengi, sababu ya kutekwa ni ishu za Mtandao. Walichukua maelezo, wakanipeleka porini West Kilimanjaro, wakachukua simu yangu na kunitaka nifute video zangu zote, wakazungumza vitu ambavyo siwezi kuvisema kwa sasa kisha wakanitelekeza hapo.”

Soma https://jamii.app/MchungajiJacob

#JamiiForums #JFMatukio #HumanRights
Mtumiaji wa JamiiForums.com ame'share' picha zikionesha hali halisi ya Barabara ya Mbezi Makabe (Kwa Pesapesa) na changamoto ya usafiri wanayokutana nayo Watumiaji wa Barabara hiyo hasa msimu huu wa Mvua, akitoa wito kwa Mamlaka husika na Viongozi wa eneo hilo kushughulikia uboreshaji wa barabara hiyo

Zaidi https://jamii.app/MakabeKwaPesapesa

#JamiiForums #JamiiAfrica #Uwajibikaji #Accountability #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii #Governance
Nchi ya Denmark inatajwa mara nyingi kuwa kinara kwenye Nchi zenye kiwango kidogo cha Ufisadi kutokana na Uhuru mkubwa wa Vyombo vya Habari, Uwazi na Upatikanaji wa Taarifa kuhusu Matumizi ya Fedha za Umma, Viwango vikubwa vya Uadilifu kwa Maafisa wa Umma na Mfumo huru wa Mahakama

Raia wa Denmark huweka sehemu kubwa ya Mapato yao binafsi kwenye Kodi, wakiwa na Imani kuwa Rasilimali hizo zitatumika kwa manufaa ya wote.

#Democracy #JamiiForums #JamiiAfrica #TheNordics
👍2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa #CHADEMA Kanda ya Magharibi, Wakili Dickson Lucas Matata amesema Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya Kisheria ya kumuwezesha kubatilisha uteuzi wa Viongozi wa Chama cha Siasa

Amesema kwamba suala hilo siyo sehemu ya majukumu yake na kuwa kauli ya kuingilia na kuchukua maamuzi haizingatii misingi ya Sheria na haina dhamira njema kwa Chama

Pia, amehoji Mbatia alipoondolewa kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi alichukua uamuzi upi ili kulinda nafasi halali ambayo alikuwa nayo

Soma https://jamii.app/WakiliMatata

#JamiiForums #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
CAF: Mchezo wa Fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) umekamilika kwa #Simba ya Tanzania kupoteza magoli 2-0 ikiwa ugenini dhidi ya #RSBerkane ya Morocco

Wachezaji waliosababisha kilio kwa Simba ni Mamasou Camara dakika ya 8 na Oussama Lamlaoui dakika ya 14

Kutokana na matokeo hayo sasa kila kitu kinaelekezwa katika mchezo wa pili ambao bado kuna utata kama utacheza kwenye Uwanja wa Mkapa (Dar es Salaam) au New Amaan Complex (Zanzibar)

Je, unadhani Simba inaweza kupindua matokeo au ndio imeisha hiyo?

Soma https://jamii.app/BerkaneSimba

#JamiiForums #CAFCC #JFCAF25
🔥1
Kujisamehe na kusamehe wengine ni hatua muhimu ya kujikomboa kutoka katika maumivu ya zamani

Kujisamehe ni kujipa nafasi ya kukua na kujifunza, bila kujihukumu milele, huku kusamehe wengine kukituondolea mzigo wa chuki na machungu

Msamaha hauhalalishi makosa, bali huleta uhuru wa ndani na kutupa amani ya kweli. Kuanzia leo tujifunze kusema "Nimesamehe na najisamehe pia"

Jumapili Njema!

#GoodMorning #AmkaNaJF #Maisha #LifeLessons #Lifelessons
Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima ametoa wito kwa Wananchi kutochana karatasi ambazo zina orodha ya Wapigakura katika vituo kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuathiri zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Soma https://jamii.app/INECYaonya

#JamiiForums #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
MICHEZO: Timu ambazo zimeshinda Kombe la Shirikisho Africa (CAF Confederation Cup) mara moja ni: FAR Rabat, Hearts of Oak, Stade Malien, FUS Rabat, MAS Fez, AC Léopards, Al Ahly na USM Alger.

Zilizobeba Kombe hilo zaidi ya mara moja ni: CS Sfaxien (3), RS Berkane (2), Étoile du Sahel (2), TP Mazembe (2), Zamalek (2) na Raja CA (2)

Soma https://jamii.app/CAFWinners

#JFSports #JamiiForums #JFCAF25 #CAFCC
🤣1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwanasiasa na Waziri wa zamani wa Sheria wa Kenya, Martha Karua amedai kuzuiwa kuingia nchini Tanzania akiwa na Watetezi wengine wa Haki za Binadamu na Mawakili wenzake, Lynn Ngugi na Gloria Kimani

Karua ameposti na kueleza akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Pasipoti yake ilichukuliwa, akazuiwa kwa Saa moja bila maelezo yoyote na kwamba walikuwa wanasubiri kurejeshwa walipotoka

Amesema yeye na wenzake walialikwa na Jumuiya ya Wanasheria Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria wa Kenya pamoja na Chama cha Wanasheria wa Uganda

Soma https://jamii.app/KaruaDeported

#JamiiForums #Diplomacy #JFMatukio
👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kiongozi Mkuu Mstaafu wa Chama cha #ACTWazalendo, Zitto Kabwe amesema amefunguliwa kesi na Harbinder Singh Seth akidaiwa kumkashifu mtu huyo na kumvunjia heshima mbele ya jamii wakati Zitto alipozungumzia sakata linalohusu Kampuni ya Ufuaji Umeme ya IPTL

Zitto ambaye amesema anashutumiwa akidaiwa kutoa kauli ya kukashifu na kumchafua Sethi kupitia ukurasa wake wa X, amesema “Nipo tayari kwa kesi, nitaweka ukweli wote wazi na mwisho kufukia kabisa huu mzoga unaoitwa Sakata la IPTL.”

Ameongeza “Ninampongeza sana (Sethi) na kumshukuru kwa ujasiri wake wa kunishtaki kwasababu kesi hii itatoa fursa ya kumaliza jambo hili lililoweka wingu kwa muda mrefu sana katika Taifa letu."

Soma https://jamii.app/ZittoKabweMei18

#JamiiForums #JFMatukio
AFYA: Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, katika uchaguzi uliofanyika leo Mei 18, 2025, Geneva-Uswisi

Prof. Janabi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Kanda hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile, aliyefariki dunia Novemba 2024

Wagombea wengine waliowania nafasi hiyo lakini hawakufanikiwa ni pamoja na Prof. Moustafa Mijiyawa kutoka Togo, Dkt. N’Da Konan Michel Yao kutoka Ivory Coast, Dkt. Boureima Hama Sambo wa Niger na Mohamed Lamine Dramé kutoka Guinea

Aidha, Kwa mujibu wa utaratibu wa WHO, Prof. Janabi anatarajiwa kuhudumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha Miaka Mitano, huku akiwa na fursa ya kuchaguliwa tena kwa muhula mwingine mmoja pekee

Soma https://jamii.app/JanabiAshinda

#JamiiForums #JamiiForums #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii #Governance
4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Makamu Mwenyekiti wa #CHADEMA, John Heche amedai aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama, John Mrema ameondoka na Akaunti ya X (Twitter) na YouTube na kudai alikuwa akijinufaisha kwa kuingiza kipato yeye na Msaidizi wake

Akijibu madai hayo, Mrema amesema “Nilikuwa Kiongozi wa Kitengo lakini waliohusika kuposti ni Maafisa wengine, Apolo alisimamia X wakati YouTube ilikuwa chini ya Abdulkarim, binafsi sikuwa hata na ‘password’, nilipotaka kutuma ujumbe, niliandika na kuwakabidhi hao.”

Ameongeza “Nilichosikia, kulikuwa na majaribio mengi ya kuingia kimakosa, akaunti zikafungwa, wao (CHADEMA) hawana password ya email iliyotumika kufungua, pia Abdulkarim ana madai yake, aliwasilisha kwa Heche akaambiwa anadai fedha nyingi, wataangalia namna, so wanajua kilichotokea mimi sihusiki.”

Soma https://jamii.app/MajibuYaJohnMrema

#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili mzunguko wa pili na uwekaji wazi wa Daftari la awali linaendelea katika mikoa 16, linafanyia Mei 16 - 22, 2025

Mikoa husika ni Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na Kusini Pemba

Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amesema Daftari la Wapiga Kura linawekwa wazi katika vituo vya kuandikisha Wapiga Kura vilivyotumika Awamu ya Kwanza, moja kati ya takwa la kufanya hivyo ni kukidhi matakwa ya Kisheria na kutoa fursa ya Watu kukagua kama kuna dosari

Soma https://jamii.app/UboreshajiDaftari

#JamiiForums #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025
Finland inakadiriwa kuwa na Sauna (Bafu la Mvuke) Milioni 3.2 huku likiwa ni Taifa lenye idadi ya Watu zaidi ya Milion 5.5 (Takwimu za Mwaka 2023), hali ambayo inaonesha uwepo wa mabafu hayo sio fasheni au kitu cha gharama kubwa kwa Watu fulani kama ilivyo katika baadhi ya Nchi nyingi, bali kwao ni sehemu ya maisha na sehemu ya tamaduni

Baadhi ya faida za Sauna zinazoaminiwa na Wakazi wa #Finland ni kuwa: Matumizi ya mara kwa mara yanazuia matatizo makubwa ya Kisaikolojia, yanapunguza hatari ya kupata Ugonjwa wa Akili ikiwemo wa Dementia (kupoteza ufahamu)

Pia, inaongeza mabadiliko ya mapigo ya moyo na kuboresha kazi ya moyo, huboresha mzunguko wa damu na kuimarisha ulegevu wa mishipa ya damu. Wanaotumia mara kwa mara huwa na mfumo wa kinga wenye nguvu zaidi

#JamiiAfrica #JamiiForums #NordicWeek
2