JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: Rais William Ruto amesema Wakenya wote waliokuwa wametoweka katika Mazingira ya kutatanisha wamepatikana wakiwa salama na kurejeshwa kwa Familia zao, akisisitiza Serikali yake imejipanga kikamilifu kuzuia visa vya Utekaji au kutoweka kwa Watu kwa njia zisizoeleweka

Kauli hiyo ameitoa wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari akiwa na Rais wa Finland, Alexander Stubb, anayefanya ziara rasmi ya Siku tatu Nchini Kenya.

Soma zaidi https://jamii.app/RutoUtekajiKE

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accountability #HumanRights #EndAbductions #Uwajibikaji
2
DAR: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kimetoa taarifa kuwa Naibu Katibu Mkuu-Bara, Amani Golugwa amekamatwa na Jeshi la Polisi usiku wa leo Mei 13, 2025 wakati akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere

Taarifa imeeleza kuwa Amani alikuwa asafiri kuelekea Ubeljiji kuwakilisha chama katika Mkutano wa International Democracy Union (IDU) unaotarajiwa kuanza Mei 14, 2025

CHADEMA imeongeza “Tumezungumza na Shirika la Ndege la Turkish Airlines ambalo alikuwa asafiri nalo, wametujuza hajafanikiwa kusafari, pia aliyetutaarifu ameeleza Amani amepigwa sana na Jeshi hilo na simu zake zote hazipatikani.”

Muda mfupi uliopita Akaunti ya CHADEMA imeripoti "Tumetaarifiwa kuwa Amani Golugwa yupo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam."

Soma https://jamii.app/AmaniGolugwa

#JFMatukio #JamiiForums #Democracy #JamiiAfrica
🤔2👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa BAWACHA Mkoa wa Kichama Ilala, Nice Gisunte amedai kuna mpango wa siri kwa wenzao waliojiondoa CHADEMA kufadhiliwa kwa kupewa Tsh. Milioni 100 hadi 200 kwa kila mtiania. Amesema hayo leo Mei 13, 2025 alipokuwa anazungumza na Wanahabari

Soma https://jamii.app/BAWACHATamko

#JamiiForums #Democracy #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu2025 #Siasa
DAR: Jeshi la Polisi Kanda Maalum limekiri kumshikilia Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA-Bara, Amani Golugwa aliyekuwa akijiandaa kuelekea Brussels, Ubelgiji kwa maelezo kuwa kuna taarifa za siri wamezipata amekuwa na mienendo ya kuondoka na kurudi Nchini bila kufuata taratibu za kisheria hapa Nchini

Taarifa ya Polisi imeeleza kuwa uchunguzi wa kina wa taarifa hizo unaendelea kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Usalama na kutoa wito kwa Wananchi kupuuza taarifa za upotoshaji kuhusu hatua za Kisheria zinazochukuliwa

Awali, #CHADEMA ilitoa taarifa kuwa Golugwa amekamatwa na Polisi akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kudai wamejulishwa kuwa amepigwa wakati wa mchakato wa kumkamata

Soma https://jamii.app/PolisiNaGolugwa

#JamiiForums #Democracy #Siasa #Kuelekea2025
👎1
SIASA: Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inadaiwa kutengua uteuzi wa Wajumbe nane wa Sekretarieti na Kamati Kuu ya CHADEMA, waliothibitishwa na Baraza Kuu la Chama hicho, Januari 22, 2025 kwa maelezo akidi haikutimia wakati wakiteuliwa

Viongozi walioteuliwa na Mwenyekiti wao, #TunduLissu ambao Msajili amewaweka kando hadi Baraza Kuu jingine liitishwe ni; Katibu Mkuu (John Mnyika), Amani Golugwa (Naibu Katibu Mkuu - Bara) na Ally Ibrahim Juma (Naibu Katibu Mkuu - Zanzibar)

Wengine ni Wajumbe wa Kamati Kuu; Godbless Lema, Rose Mayemba, Salma Kasanzu, Hafidh Ally Saleh na Dk Rugemeleza Nshala ambaye pia aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA

JamiiForums inaendelea na jitihada za kuitafuta Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kupata ufafanuzi zaidi wa Maamuzi haya

Soma https://jamii.app/MsajiliAtengua

#JamiiForums #Siasa #Kulekea2025 #UchaguziMkuu2025 #Democracy
👍2👎1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Treni inayofanya safari Pugu hadi katikati ya Jiji imepata ajali baada ya behewa kuachia njia maeneo ya Karume, inadaiwa Watu kadhaa wamejeruhiwa

Taarifa zaidi zitafuata

Video Credits: Jamvi Media

Soma https://jamii.app/MabehewaKarume

#JFMatukio #JamiiForums
#MALEZI: Sera ya Uzazi na Malezi nchini Sweden inawapa Wazazi jumla ya Siku 480 za likizo ya Uzazi na Malezi yenye malipo pale Mtoto anapozaliwa au kuasiliwa. Iwapo kuna Wazazi wawili, kila mmoja anapewa Siku 240

Kwa Watoto waliozaliwa mwaka 2016 au baadaye, kila Mzazi ana siku 90 ambazo haziwezi kuhamishiwa kwa Mzazi mwingine kama hazitatumika. Mzazi mmoja (single parent) anapewa Siku zote 480

Wazazi pia wanaweza kuamua kuhamisha hadi Siku 45 za likizo yao kwa Babu, Bibi au Rafiki wa karibu wa Familia, anayewasaidia kulea. Wanaostahili likizo hii ni wanaolea badala ya kufanya Kazi, Kusoma au kutafuta Kazi

#JamiiForums #NordicWeek #ParentHood #LifeStyle
👍1
Mdau wa JamiiForums.com anasema
kama mamlaka husika haziwezi kuchukua hatua za kuhakikisha Taa za Makutano ya Uhuru-Msimbazi (Kariakoo) zinafanya kazi basi Trafiki awepo muda wote, ili kuepusha ajali, magari kukwaruzana na msongamano wa Vyombo vya Moto ambao ni kero kubwa

Zaidi https://jamii.app/TaaHazifanyikazi

#JamiiForums #JamiiAfrica #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii #Governance #Accountability #Uwajibikaji
Kila mafanikio yana safari yake. Usikate tamaa unapokutana na vikwazo; vinafundisha, vinakuimarisha na mwisho vinakuandaa kwa ushindi.

#JamiiForums #JamiiAfrica #AmkaNaJF #GoodMorning
DAR: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kufuatilia malipo ya mitihani ambayo Mwanafunzi hakufanya vizuri (Supplementary Examination), akidai baadhi ya Vyuo vinatoza gharama kubwa kuliko maelekezo ya Serikali

Anadai hiyo inawezekana ikatengenezwa mazingira ya Wanafunzi ‘kufelishwa’ ili Chuo kiingize malipo mengi ya Sup

Pia, anadai mifumo ya uendeshaji taasisi hizo za Elimu ikiwemo usajili wa Wanafunzi, matokeo na utoaji vyeti hakuna utaratibu wa kueleweka na kwamba baadhi ya Vyuo vimeweka namba za mawasiliano katika matangazo na mitandao ya kijamii lakini namba zao hazipokelewi na nyingine hazipatikani

Soma https://jamii.app/VyuoVyaKati

#JamiiForums #Accountability
👍2