Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kiongozi wa Chama cha #ACTWazalendo, Dorothy Jonas Semu, amesema Chama chao kimetangaza kupigania maboresho ya Mfumo wa Uchaguzi hadi dakika ya mwisho na kuwa Chaguzi tatu zilizopita zimewaonesha sura halisi ya adui yao kuwa sio CCM tu bali Vyombo vya Dola
Ameongeza “Tupaze Sauti zetu hadi Uchaguzi Mkuu 2025 uwe huru, wa haki na wa kuaminika. Madai yetu sita yawe ndio wimbo wetu kuanzia saa hadi Oktoba.”
Soma https://jamii.app/ACTMei5
#UchaguziMkuu2025 #Uchaguzi2025 #Democracy #Siasa

❤1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
TANGA: Mdau anadai kivuko kinachounganisha Pangani na Bweni kimekuwa na hitilafu za mara kwa mara na kimegeuka kero kwa Watumiaji kutokana na kukwama mara kadhaa kwenye Maji
Anadai athari zinazojitokeza ni hofu kwa Watumiaji, kutishia soko la Watalii akitoa mfano maeneo kama Pwani ya Ushongo yenye Hoteli na nyumba binafsi za kulaza wageni yameathiriwa na usafiri huo kwa kuwa Daraja linalojengwa bado haijaruhusiwa kutumika muda wote
Anadai athari nyingine ni usambazaji wa Bidhaa pamoja na shughuli nyingine za kiuchumi kukwama. Anatoa wito kwa Mamlaka husika kuchukua hatua kwa kuwa athari zinazojitokeza ni kubwa
Soma https://jamii.app/KivukoPangani
#ServiceDelivery #JamiiForums #HudumaZaKijamii #JFMdau2025 #JamiiAfrica

👍4
Hatuwezi kurudisha Muda nyuma na hatuwezi kubadili yaliyopita, lakini matendo yetu ya leo yanaweza kuamua kile ambacho kesho yetu itakibeba
#JamiiAfrica #JamiiForums #AmkaNaJF #GoodMorning

👍2❤1
Mchezo wa #Yanga dhidi ya #Simba wa Raundi ya Pili ya Ligi Kuu Bara 2024/25 ambao uliahirishwa, sasa umepangwa kuchezwa Jumapili Juni 15, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa
Ikumbukwe, Yanga imetangaza kuwa haitashiriki mchezo huo na tayari iliwasilisha malalamiko yao kwa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), lakini shauri lao likakwama, wakatakiwa kurejea katika Mamlaka za Nchini, jambo ambalo wamesema hawawezi na hawatacheza Mchezo huo
Mdau, unadhani Yanga watashikilia msimamo wao au ‘mbungi’ itapigwa?
Soma https://jamii.app/DerbyJune15
#JFSports #JamiiForums #KariakooDerby

🤣2
DAR: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kimetoa taarifa kuwa baadhi ya akaunti zao rasmi za Mitandao ya Kijamii zimedukuliwa
Taarifa imeeleza ”Tunaarifu kuwa akaunti zetu za X (zamani Twitter) - ChademaTZ na YouTube - Chadema Media zimeingiliwa na Wadukuzi, taarifa rasmi za CHADEMA zinapatikana kupitia akaunti ya muda ya X: @ChademaTZ2”
Imeongeza “Tunaendelea kuchukua hatua za kiusalama na Kisheria kurejesha udhibiti, kwa sasa, tunaomba wafuasi wawe makini na kupuuza taarifa zinazochapishwa kwenye akaunti zilizodukuliwa hadi tutakapotoa taarifa rasmi ya kurejesha udhibiti.”
Soma https://jamii.app/CHADEMAKudukuliwa
#JamiiForums #Accountability #JFDigital #Kuelekea2025

👍1
DODOMA: Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imetoa wito kwa Jeshi la Polisi kutekeleza wajibu wake wa kulinda Usalama wa Raia na Mali zao na liendelee kuwasaka na kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika na kujeruhiwa kwa Padri Charles Kitima, waliomteka Faluka Nyagali (Mdude)
Pia, imetoa wito kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, awatake Viongozi wa Vyama vya Siasa kuzingatia matakwa ya Katiba na Sheria katika shughuli zao, pia Serikali iendelee kukaa na Wadau wa Demokrasia katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazojitokeza
Soma https://jamii.app/TamkoLaTHBUB
#Uwajibikaji #Accountability #JamiiForums

DAR: Shauri la Kwanza la Uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA – Taifa, Tundu Lissu limeahirishwa mpaka Mei 19, 2025, huku Mahakama ikiutaka upande wa Jamhuri uharakishe upelelezi
Ikumbukwe kuwa wakati mshtakiwa akifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na kusomewa shtaka la uhaini kwenye kesi ya kwanza, upande wa mashtaka ulieleza kwamba bado upelelezi wa kosa hilo ulikuwa bado haujakamilika.
Mchakato wa kesi hiyo unaendelea leo Mei 6, 2025 kwa njia ya Mtandao. Mwanasiasa huyo anakabiliwa na tuhuma mbili ambazo ni Uhaini na Kutoa Taarifa za Uongo
Soma https://jamii.app/LissuUpdatesMei6
#JamiiForums #Siasa #Democracy #Kuelekea2025

DAR: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekubaliana na hoja za upande wa utetezi na sasa shauri linalomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA Taifa, Tundu Lissu halitaendeshwa kwa njia ya Mtandao badala yake Lissu atafikishwa Mahakamani hapo
Uamuzi huo umetolewa wakati wa mchakato wa kuendesha kesi hiyo kwa njia ya Mtandao, leo Mei 6, 2025 ambapo Mahakama ilikuwa inatoa maamuzi ya mapingamizi yaliyowekwa na Mawakili wa Lissu wakiongozwa na Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala
Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu Godfrey Mhini kwenye shauri la kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni likiwa ni shauri la 2 linalomkabili Lissu
Soma https://jamii.app/LissuKufikishwaMahakamani

Mdau wa JamiiForums.com anasema anaipenda Kazi yake lakini hajui atumie mbinu gani kumwambia Mwajiri wake ukweli kuhusu tabia inayomkera ya kumgombeza mbele za Wateja
Hebu mpe Mdau ushauri wa kutatua changamoto hiyo
Mjadala zaidi https://jamii.app/BosiUkweliTabia
#JamiiForums #JamiiAfrica #Maisha #JFChitChats #JFStories

DAR: Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), Mei 5, 2025 kilizindua ripoti ya hali ya Haki za Binadamu Nchini kwa Mwaka 2024 ambapo kuanzia Januari 2015 hadi Februari 2025, LHRC imerekodi jumla ya matukio 100 ya utekaji na kupotea kwa watu kwa njia isiyofahamika
Ripoti hiyo inaeleza Takriban theluthi mbili ya matukio hayo (64) yaliripotiwa Mwaka 2022 (31) na 2024 matukio 33. Hakukuwa na tukio lolote lililoripotiwa Mwaka 2019 na 2020. Zaidi ya theluthi moja ya matukio hayo (35%) yaliripotiwa katika Mkoa wa Dar es Salaam, ukifuatiwa na Mkoa wa Arusha (26%)
Mratibu wa Utafiti, Wakili Fundikila Wazambi amesema ripoti hiyo inaonesha wimbi la Watu kukamatwa na kutiwa kizuizini bila kufuata Sheria, ambapo matukio zaidi ya 600 ya Watu kukamatwa na kutiwa kizuizini yaliripotwa kwa Mwaka 2024
Soma https://jamii.app/LHRCReport2024
#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #CivilRights #HakiZaBinadamu

ZANZIBAR: Chama cha #ACTWazalendo kimesema kinawasilisha malalamiko rasmi dhidi ya kauli na agizo la Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi-Unguja, Idrisa Kitwana Mustafa aliyoitoa Aprili 24, 2025 ya kuwataka Watumishi wa Umma wanaoishi Mkoani hapo kumkabidhi nakala za Vitambulisho vyao vya Kupigia Kura
Msemaji wa Ofisi - Kamati ya Wasemaji wa Kisekta - Zanzibar, Hamad Mussa Yussuf amesema “Kauli hiyo inaelekeza matumizi mabaya ya madaraka kwa nia ya kuwatisha na kuwavunjia heshima Watumishi wa Umma, hivyo kuondosha dhana ya msingi wa Utawala Bora na dalili za kuingilia Uchaguzi Mkuu wa 2025.”
ACT imetoa wito kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Kukemea hadharani kauli hiyo, Kufanya uchunguzi huru na wa haraka na kutoa mapendekezo ya hatua stahiki, Kumtangaza RC Idrisa kuwa amekiuka misingi ya Utawala Bora na Haki za Binadamu, hivyo hastahili kuendelea kushika nafasi ya Uongozi wa Umma.
Soma https://jamii.app/ACTDhidiYaRC
#JamiiForums #Accountability #Siasa #Kuelekea2025 #UchaguziMkuu205

DAR: Wakili Peter Kibatala ambaye ni mmoja wa Mawakili wanaomtetea Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu ametoa wito kwa Wananchi watakaohudhuria kesi inayomkabili mteja wao katika Mahakama ya Kisutu, kuwa na utulivu ili wasije kufanya tukio ambalo linaweza kutumika kuwa kisingizio cha kuharibu mwenendo wa kesi
Awali kesi hiyo iliendeshwa kwa njia ya Mtandao lakini leo Mei 6, 2025 Mahakama imeruhusu Umma kuhudhiria kesi hiyo itakayotajwa tena Mei 19, 2025 katika Mahakama ya Wazi
Zaidi https://jamii.app/KibatalaMei6
#JFMatukio #JamiiForums #Democracy

👍2