JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Je, AI inachukua nafasi za ajira za Wanahabari na ianaathiri uhuru wa Vyombo vya Habari na uandaaji wa taarifa?

Shiriki nasi mjadala huu ili uweze kufahamu kwa undani kuhusu nafasi ya #AI katika Vyombo vya Habari, siku ya Jumanne Aprili 15, 2025, kuanzia Saa 12:00 hadi Saa 2:00 Usiku, kupitia XSpaces ya JamiiForums

Kushiriki bofya https://twitter.com/i/spaces/1eaKbWezOjZGX

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
👍1
DAR: Mdau ndani ya JamiiForums.com anahoji mbona Mamlaka zipo kimya juu ya Barabara ya Mwendokasi ya Kimara hadi Kibaha kutotumika licha ya kuonekana imekamilika?

Anaeleza kuwa kodi za Wananchi zimetumika, makazi ya Watu yalibomolewa kupisha ujenzi huo, hivyo Miundombinu hiyo kama haitumiki inamaanisha hakuna Uwajibikaji

Soma https://jamii.app/BarabaraMwendokasiKutelekezwa

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #ServiceDelivery #Mdau2025
👍3
Kusoma kwa undani habari hizi na mengine yaliyojiri juma lililopita bofya https://jamii.app/YaliyojiriJumaLililopita

#JamiiForums #YaliyojiriJumaLililopita #JFToons
Uhuru wa Wanahabari ni mwanga wa Haki na Ukweli, unaowaangazia Wananchi kuelewa kinachoendelea katika Jamii yao, Serikali, na Dunia kwa ujumla

Tukilinda Uhuru wa Vyombo vya Habari, tunalinda Haki yetu ya kujua na kuelewa ukweli.

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa mamlaka husika kushughulikia changamoto na kero zinazojitokeza kutokana na ujenzi wa barabara katika Mtaa wa Mindu, Kata ya Upanga Magharibi ikiwemo kusimama kwa shughuli za Kijamii

Anadai mbali na hali hiyo, pia Wananchi wanalazimika kulipia maegesho ya magari sehemu ambazo awali walikuwa hawalipii, na kwamba wanapolipa hawapewi risiti, hali ambayo anaamini zoezi hilo la kuziba njia yote lilifanywa kimkakati ili kuwanufaisha Watu wachache

Soma https://jamii.app/UjenziBarabaraUpanga

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #ServiceDelivery #Mdau2025
👍1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Serikali imesema imefanya utafiti wa kina Nchi nzima kuhusu Saratani na imebaini upande wa Kanda ya Ziwa Saratani zinazoongoza ni ya Kibofu cha Mkojo, Mji wa Uzazi (Wanawake), Damu, Macho na Figo

Akijibu swali #Bungeni kuwa lini Serikali itatoa majibu ya tafiti za Saratani upande wa Kanda ya Ziwa kubaini visababishi vya Saratani iliyokithiri, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema visababishi vinavyotajwa bado ni nadharia na kwamba utafiti bado unaendelea kubaini vyanzo.

Soma https://jamii.app/SarataniTaarifa

#JamiiForums #Afya #PublicHealth
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
NJOMBE: Diwani wa Kata ya Kitandililo Halmashauri ya Mji Makambako, Imani Fute ametoa wito kwa Viongozi Wazee na waliokaa kwenye nafasi za Uongozi kwa muda mrefu wawapishe Vijana ili nao waoneshe uwezo wao katika Uongozi, kwani wanatosha na wanaweza

Amesema "Tusiende kwenye Mfumo wa baadhi ya Watu wanaofikiri Uongozi ni mali yao mpaka wafe ndio watoke madarakani."

Soma https://jamii.app/DiwaniKitandililo

#JamiiForums #Democracy #Governance #KuelekeaUchaguziMkuu
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akijibu hoja ya Mbunge Joseph Mkundi aliyesema takwimu zinaonesha Wagonjwa wengi wa Saratani waliopo Hospitali ya Ocean Road wanatokea Kanda ya Ziwa, hivyo kushauri Serikali iboreshe Hospitali ya Rufaa ya Bugando Kitengo cha Saratani ili kusaidia mgawanyo wa Huduma, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema dhana hiyo ya utafiti sio sahihi

Dkt. Mollel amesema utafiti unaonesha Wagonjwa wengi waliopo kwenye Ocean Road wanatokea Kanda ya Kaskazini na sio Kanda ya Ziwa kama ambavyo imekuwa ikiaminika

Soma https://jamii.app/SarataniUtafitiMpya

#JamiiForums #Afya #PublicHealth
Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani 2025, usikose kushiriki mjadala muhimu kuhusu nafasi ya Teknolojia ya Akili Mnemba (AI) katika mabadiliko ya tasnia ya habari, ambapo tutajadili fursa, changamoto na mustakabali wa Uandishi Huru wa Habari

Ni Jumanne hii, Aprili 15, 2025, Saa 12 Jioni hadi 2 usiku, kupitia Xspaces ya JamiiForums

Kujiunga bofya https://twitter.com/i/spaces/1eaKbWezOjZGX

#JamiiForums #WPFD2025 #AIForMedia #AIandMedia #PressFreedom #Democracy
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Manyoni, Kapteni John Chiligati, amesema kuna tabia za Rushwa zinaendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi, akitoa wito wa kukomesha tabia hizo

Amesema "Embu Mwaka huu tujitahidi kabisa, kabisa hasa ndani ya CCM. Hawa watoa #Rushwa wanaotaka kununua Uongozi, Uongozi unakuwa kama bidhaa, kama ni mnada, mwenye hela nyingi ndio anapata, aibu kwa Chama chetu, aibu kabisa."

Soma https://jamii.app/UongoziMnada

#JamiiForums #Uwajibikaji #Governance #Demokrasia #KemeaRushwa
Ni kwa namna gani matumizi ya AI katika Sekta ya Habari yanaweza kuhakiki usahihi ukweli wa taarifa na kugundua Habari za uongo?

Kufahamu haya na mengine, usikose kujiunga nasi katika Mjadala maalum na Wataalamu, Jumanne hii kuanzia Saa 12 jioni hadi 2 usiku, kupitia Xspaces ya JamiiForums

Kujiunga bofya https://twitter.com/i/spaces/1eaKbWezOjZGX

#WorldPressFreedomDay #WPFD2025 #PressFreedom #MediaAndAI #AIForMedia
DODOMA: Uamuzi huo umetolewa na jopo la Majaji Winfrida Korosso, Sam Rumanyika na Abdul-Hakim Ameir Issa, walipokubali rufaa iliyokatwa na Kamishna Mkuu wa TRA dhidi ya Vodacom, ambayo ilipinga uamuzi wa awali wa Bodi ya Rufaa ya Kodi pamoja na Baraza la Rufaa ya Kodi

Awali, Bodi na Baraza la Rufaa ya Kodi waliamua kuwa wajibu wa kulipa Kodi ya zuio unatokea wakati riba inalipwa, na si wakati mpokeaji wa riba anapopata haki ya kupokea malipo hayo. Hivyo, waliona kuwa Vodacom haikustahili kutozwa riba kwani ililipa na kuwasilisha kodi hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 82(1) na 84(1) cha Sheria ya Kodi ya Mapato

Hata hivyo, Mahakama ya Rufani imebatilisha maamuzi hayo na kusisitiza kuwa riba hiyo inapaswa kulipwa kutokana na Ucheleweshaji wa ulipaji wa kodi ya zuio

Soma https://jamii.app/VodacomNaTRA

#JamiiForums #Accountability
MAREKANI: Serikali kupitia Tume ya Biashara imeishtaki Kampuni ya #Meta, ikidai ununuzi wa Mitandao ya Kijamii ya #Instagram na #WhatsApp ulikuwa na nia ya kuondoa Ushindani katika Sekta ya Mitandao ya Kijamii

Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa leo Aprili 14, 2025, Washington DC inatarajiwa kuchukua Wiki kadhaa, huku Mwanzilishi wa Meta, Mark Zuckerberg, pamoja na aliyekuwa Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Sheryl Sandberg wakitarajiwa kutoa ushahidi

Imeelezwa, ingawa FTC iliidhinisha manunuzi ya Mitandao hiyo, imeendelea kufuatilia athari zake kwa ushindani wa soko na kama itashinda kesi hiyo, Meta inaweza kulazimika kuuza Instagram na WhatsApp

Meta si Kampuni pekee ya Teknolojia inayochunguzwa kwa tuhuma za ukiritimba. Google pia inakabiliwa na uwezekano wa kulazimishwa kuuza kivinjari (Browser) chake cha #Chrome ili kuvunja utawala wake katika soko la Utafutaji mtandaoni (Online Search)

Soma https://jamii.app/MetaKuuzaIgNaWhatsApp

#JamiiForums #EmbracingTechnology #DigitalWorld