JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mjadala wa "Demokrasia Yetu, Viongozi wetu: Changamoto za Uchaguzi Mkuu" upo hewani muda huu

Shiriki kuimarisha Demokrasia yetu kwa kusikiliza, kuuliza maswali na kutoa maoni na mapendekezo

Kushiriki, bofya: https://jamii.app/MjadalaUchaguziJAN30

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaDemokrasia #Demokrasia #Governance #Accountability
Akizungumza katika mjadala wa "Demokrasia Yetu, Viongozi wetu: Changamoto za Uchaguzi Mkuu", Mwenyekiti wa CHADEMA Dodoma, Aisha Madoga amesema Changamoto mama ya Uchaguzi ni usimamizi wenyewe wa Uchaguzi, hapo ndipo changamoto zote zinapoanzia

Amesema ngazi ya Majimbo msimamizi ni Mkurugenzi ambaye ni mteule wa Rais na Kada wa CCM, wanaomsaidia ni Watendaji wa Kata, hao ndio wanaosimamia taratibu zote kuanzia ngazi za awali kunakuwa hakuna uhalali

Amesema “Kada wa Chama anakuwa na jukumu la kusimamia Uchaguzi, huyo ndiye ambaye anapaswa kumsimamia Mgombea wa Chama cha Upinzani, ni vigumu Kutenda haki. Hivyo hivyo ipo kwa Watendaji wa chini ambao nao asilimia 80 wanakuwa ni makada wa Chama Tawala ”

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaDemokrasia #Demokrasia #Governance #Accountability
Mwenyekiti wa CHADEMA Dodoma, Aisha Madoga, amechangia mjadala kwa kusema “Mawakala wa Uchaguzi nao wanakuwa wanadhibitiwa na Watendaji ambao wanasimamia Uchaguzi, hiyo haiwezi kufanya kuwe na matokeo ya Haki”

Ameongeza kuwa Kanuni za Uchaguzi zinaeleza Tume ya Uchaguzi yenyewe ndio inatakiwa kuamua wapi pa kuweka Kituo cha Kupiga Kura, hiyo imesababisha waweke vituo katika Mazingira ambayo yanakuwa magumu kwa Wakala kuweza kufanya Kazi

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaDemokrasia #Demokrasia #Governance #Accountability
👍1
Akizungumza katika mjadala wa "Demokrasia Yetu, Viongozi wetu: Changamoto za Uchaguzi Mkuu", Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara (ACT), Mwanaisha Mndeme, amesema ameshiriki katika chaguzi na kuona jinsi hali ilivyo ngumu kwa Vyama vya upinzani ikiwemo matumizi ya nguvu ya Jeshi la Polisi

Anasema Kifungu cha Uchaguzi 40 (5) kimekuwa kikitumiwa vibaya na kinapaswa kubadilishwa kutokana na wasimamizi kutokutambulisha mawakala, wengine walichelewa kupata utambulisho na Wasimamizi wengine kudai hawajapewa maelekezo ya kuwatambua mawakala

Amesema “Changamoto nyingine ni ‘enguaengua ya Wagombea’, kwa makosa madogo madogo bila kuzingatia Katiba na hali hiyo imetokea katika Chaguzi zilizopita na imekuwa ikiathiri kwa kiasi kikubwa Vyama vya Upinzani”

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaDemokrasia #Demokrasia #Governance #Accountability
Akizungumza katika mjadala wa "Demokrasia Yetu, Viongozi wetu: Changamoto za Uchaguzi Mkuu" Msemaji wa CHAUMA, Eugene Kabendera, amesema “Tanzania iliamua kuingia katika Mfumo wa Vyama Vingi ili kuwapa Wananchi Mamlaka ya kuamua Viongozi inaowataka lakini kwa mwenendo unavyokwenda Nchini tunapoka Mamlaka ya Wananchi kuamua”

Amesema Uchaguzi kwa sasa umekuwa kama vita, hali hiyo inasababisha Wananchi kuwa na hofu na tunapoelekea, itafikia hatua Wananchi watakuwa hawana Mamlaka ya kuamua, tutachekwa na Dunia

Ameongeza kuwa hakuna Sheria inayosema Viongozi au vyombo vya dola vinaweza kuingilia lakini ndivyo ilivyotokea katika Chaguzi zilizopita na Viongozi wetu wasiwakatishe tamaa Vijana, hali ikiendelea hivyo ipo siku wanaweza kuamua kupita njia nyingine

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaDemokrasia #Demokrasia #Governance #Accountability
Akizungumza katika mjadala wa "Demokrasia Yetu, Viongozi wetu: Changamoto za Uchaguzi Mkuu", Mkurugenzi wa CUF, Mohamed Ngulangwa, amesema mijadala mingi inaendeshwa kuhusiana na Uchaguzi lakini ili tuweze kuwa na Uchaguzi Huru na Haki ni vyema kukawa na mabadiliko ya Katiba pamoja na kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi inayotenda Haki na sio ambayo inabadilishwa jina lakini utendaji unakuwa ni uleule

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaDemokrasia #Demokrasia #Governance #Accountability
👍1
Akizungumza katika mjadala wa "Demokrasia Yetu, Viongozi wetu: Changamoto za Uchaguzi Mkuu", Obadia Ndanga (Mdau), amesema Taasisi nyingi zipo chini ya Serikali, ingekuwa zipo huru na zinazojitegemea ingechangia kuwa na Uchaguzi wa haki na huru

Ameongeza “Jambo lingine la muhimu ni kuwa Vyama vinatakiwa kuwa na umakini katika kuchagua aina ya Watu ambao wanaenda kuwa Mawakala wao, baadhi yao wakirubuniwa kidogo tu wanaacha kile kilichowafanya wawe hapo”

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaDemokrasia #Demokrasia #Governance #Accountability
Akichangia katika mjadala wa "Demokrasia Yetu, Viongozi wetu: Changamoto za Uchaguzi Mkuu", Dedan Kapongo (Mdau), amesema “Katiba imeeleza wazi nini kinatakiwa kufanyika kuweza kupiga kura na vitu ambavyo vinazuia ni kutokuwa raia, changamoto ya akili, kosa la Jinai na kutokuwa na Kitambulisho cha kupiga Kura. Sababu nyingine zinazotumiwa ni kutoweka uwanja sawa wa Uchaguzi, Katiba imekemea matendo kama hayo”

Ameongeza kuwa inapotokea makosa madogo kama vile kukosea umri kama inajulikana umri wake umekidhi vigezo vya kupiga kura haitakiwi kuwa sababu ya kumzuia Mtu kupiga au kupigiwa kura

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaDemokrasia #Demokrasia #Governance #Accountability
Akichangia katika mjadala wa "Demokrasia Yetu, Viongozi wetu: Changamoto za Uchaguzi Mkuu" Mwenyekiti wa CHADEMA Dodoma, Aisha Madoga, amesema “Political Will" (nia ya kisiasa) ni moja ya kitu muhimu kwa kuwa kama wahusika hawajaamua hata kama Sheria zikiwemo hazitasaidia

Ameongeza kuwa kuna wakati Wananchi wenyewe wanaweza kuamua kufanya maamuzi ya kuwalazimisha Wanasiasa au Serikali kuwa na nia ya mabadiliko ya Kisiasa

Amesema “Sisi Viongozi au Wanasiasa hata kama tukiamua kusimama wenyewe bado haitasaidia lakini Wananchi wakiamua wao wenyewe itakuwa na nguvu na mabadiliko yataonekana “

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaDemokrasia #Demokrasia #Governance #Accountability
Akichangia katika mjadala wa "Demokrasia Yetu, Viongozi wetu: Changamoto za Uchaguzi Mkuu", Owek Dozi (Mdau- Kenya), amesema Uchaguzi umekuwa ukipata changamoto katika Nchi nyingi za Afrika kutokana na Serikali kuingilia michakato kuanzia mwanzo hadi kuelekea katika Uchaguzi

Amesema Tanzania inaweza kujifunza kujiamini kutokana na kile ambacho kimekuwa kikitokea katika Uchaguzi wa Kenya

Ameongeza kuwa “Hatutakiwi kuchagua Viongozi ambao wapo na tamaa binafsi, huku Kenya kama kuna kitu mbaya hatuwezi kunyamaza, tunazungumza ili Dunia ijue”

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaDemokrasia #Demokrasia #Governance #Accountability
Akichangia katika mjadala wa "Demokrasia Yetu, Viongozi wetu: Changamoto za Uchaguzi Mkuu" Mwenyekiti wa CHADEMA- Dodoma, Aisha Madoga amesema “Uchaguzi wa Serikali za Mtaa ulikuwa wa ovyo kuliko Chaguzi nyingine zote, kulikuwa na uibaji wa Kura kwa njia rahisi. Kuna marekebisho makubwa yanatakiwa kufanyika kuboresha Mfumo mzima wa Uchaguzi”

Ameongeza kwa kusema “Kuna Watu bado wana matumaini na Serikali iliyopo Madarakani, wapo wenye matumaini hadi Asilimia 50 na wengine Asilimia 100 lakini mimi nina matumaini Asilimia 0 kwa haya yanayoendelea sasa”

Amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa Wananchi kutambua wajibu wao na kwa ufupi tunauhitaji Umma kuliko wakati mwingine wowote

#JamiiForums #UchaguziMkuu25 #MaoniYaDemokrasia #Demokrasia #Governance #Accountability
1👍1
Maisha yako yana nguvu zaidi unapojifunza kuishi kwa sasa badala ya kung’ang’ania yaliyopita au kuahirisha furaha yako kwa kesho isiyo na uhakika

Kila siku ni fursa mpya ya kujenga, kujifunza na kustawi. Usiruhusu jana ikufunge au kesho ikupotezee leo

#JamiiForums #AmkaNaJF #Maisha #LifeStyle #LifeTips #MorningQuote
DAR: Mdau wa JamiiForums.com aliyejitambulisha Mfanyakazi kutoka Kampuni ya China Tanzania Security (CT), ambayo inahusika na usimamizi wa Miundombinu katika Vituo vya Mabasi ya Mwendokasi (DART), amedai Wafanyakazi takriban 200 hawajalipwa Mishahara kwa Miezi 3 pamoja na kutokupewa Mikataba ya Kazi

Afisa Utawala wa Kampuni hiyo, Pascal Temba amezungumza na JamiiForums na kusema "Suala la Mishahara ambayo wanadai ni ya miezi miwili na siyo mitatu na hiyo inatokana na changamoto ambayo tunapitia ambayo inaweza kutokea katika ofisi yoyote ile"

Amesema "Suala hilo kwanza halijawahi kutokea huko nyuma na kuhusu Mikataba siyo kweli kuwa hawana mikataba, yote iliyopo ni Mikataba ya maandishi"

Soma https://jamii.app/DARTWalinziMshahara

#JamiiForums #JFMdau2025
TABORA: Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuwasilisha kero ya kukosekana kwa vifungashio vya dawa katika Hospitali ya Rufaa ya Tabora (Kitete) Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo amesema changamoto hiyo itatatuliwa

Dkt. Joachim Joctan Eyembe amesema kuwa, hilo ni suala dogo ambalo sio rahisi kutambua kwa urahisi na wakati mwingine inawezekana vifungashio vimeisha kwa muda ambao mdau alienda kuchukua dawa, lakini litafanyiwa kazi haraka

Soma https://jamii.app/VifungashioDawaHakuna

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #ServiceDelivery #JFMdau2025
👍1