JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Dkt. Wilbroad Slaa ameshindwa kufikishwa Mahakamani kwasababu iliyoelezwa na upande wa Jamhuri kuwa ni uwepo wa changamoto ya usafiri ambapo Gari ambalo lingetakiwa kuwaleta washtakiwa katika Mahakama hiyo limepata hitilafu ya kiufundi

Kesi hiyo imeendelea kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ikiwa ni siku moja baada Mahakama Kuu kuagiza shauri la Dkt. Slaa lirejeshwe Mahakama ya Kisutu kwaajili ya kushughulikiwa kwa dhamana yake ambayo amekuwa akiikosa tangu alipofikishwa Mahakamani Januari 10, 2025 kusomewa shtaka la kusambaza taarifa za uongo kupitia Mtandao wa X

Soma https://jamii.app/SlaaGariUfundi

#JamiiForums #Governance #CivilRights
👍1
Mshiriki wa Shindano la 'Stories of Change' Mwaka 2022 aliandika manyanyaso mengi yanayotokea kwenye Ndoa siku hizi yanafanyika chini ya kivuli cha “Uvumilivu katika Ndoa”

Kupitia andiko lake alisema ifike wakati Jamii ielewe kuwa, “NDOA SIO PAHALA PA MANYANYASO!”. Inapobidi kuvunjika kwa ustawi wa Wanandoa wenyewe na wanaowazunguka, ni vema zaidi hilo likafanyika kwa Amani kabisa, ili kuepusha madhara ambayo tumekuwa tukiyashuhudia kila Siku

Unakubaliana na hoja zake?

Soma zaidi Andiko hili https://jamii.app/NdoaIsininyanyase

#JamiiForums #HumanRights #SOC2022 #GBV #JFWomen
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wakili Peter Madeleka amezungumzia kitendo cha Mwanasiasa, Dkt. Wilbroad Slaa kutofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Jeshi la Magereza kusema limeshindwa kumfikisha mshtakiwa huyo Mahakamani kwa kuwa kuna changamoto ya magari

Hatua hiyo imekuja siku moja baada Mahakama Kuu Tanzania, Masijala Kuu Dar es Salaam kuagiza shauri linalomhusu Dkt. Slaa lirejeshwe Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaajili ya kushughulikiwa kwa dhamana yake.

Soma https://jamii.app/SlaaKutofikaMahakamani

#JamiiForums #Governance #CivilRights
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wakili Peter Madeleka akizungumza na Wanahabari amegusia utendaji wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) pamoja na kumtaja Steven Wasira ambaye ni Makamu Mwenyekiti Bara (CCM)

Amesema hayo leo Januari 31, 2025 wakati akizungumzia mwendelezo wa Shauri la jinai Namba 993 ya Mwaka 2025 lililofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Mwanasiasa Dkt. Wilbroad Slaa

Soma https://jamii.app/SlaaKutofikaMahakamani

#JamiiForums #Governance #CivilRights
😁1
SINGIDA: Mdau ametoa wito kwa mamlaka husika kushughulikia matengenezo na maboresho ya barabara iliyopo Mtaa wa Ginery karibu na Shule ya Singida Sekondari, kwani wakazi wa eneo hilo wanapitia changamoto ya usafiri na Magari ya Wanafunzi (school bus) kushindwa kupita

Soma https://jamii.app/SingidaBarabaraHaipitiki

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #JFMdau2025
Hebu tuambie, Ukipewa nafasi ya kujua jambo 1 tu kuhusu Maisha yako utatamani kujua nini?

Fuatilia zaidi Mjadala huu ndani ya JamiiForums.com kupitia Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko au bofya https://jamii.app/Jambo1Maishani

#JamiiForums #JFChitChats #Maisha #LifeLessons
1
Mdau, unawezaje kuhifadhi Soksi na kuzipata kwa uharaka unapozihitaji au mambo ni yaleyale?

Tembelea Jukwaa la Urembo, Mitindo na Utanashati (Lifestyle) ndani ya JamiiForums.com au bofya https://jamii.app/KuhifadhiSoksi kuchangia mada

#JamiiForums #JFStories #JFChitChats #LifeStyle
👍2
DAR: Japokuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilitarajia kutoa uamuzi leo, Januari 31,2025 kwenye shitaka linalomkabili Dkt. Wilbroad Slaa, ikiwa ni baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuagiza shauri la Dkt. Slaa lirejeshwe Kisutu kwaajili ya kushughulikiwa kwa dhamana yake, uamuzi umeshindwa kutolewa

Kwa mujibu wa Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki, uamuzi huo umekwama baada ya Jamhuri kukata Rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa hivyo wanafungwa mikono katika uamuzi mpaka majibu ya rufaa hiyo yatakapotolewa

Aidha, kufuatia uamuzi huo baada ya mabishano ya Kisheria, Wakili upande wa Mshtakiwa, Peter Madeleka ameeleza kuwa yeye na timu ya mawakili wengine wa utetezi hawajaridhishwa na maamuzi hayo kwani uwepo wa rufaa bado hauzuii haki zingine za msingi za mshatakiwa kama kupatiwa dhamana

Soma https://jamii.app/MahakamaKisutuRufaaSlaa

#JamiiForums #Governance #CivilRights
👍3
Mdau wa JamiiForums, hongera kwa kuanza Mwezi Mpya wa Februari 2025

Tunafurahi kuendelea kuwa nawe katika safari hii ya kujifunza na kubadilishana maarifa. Katika Mwezi huu, mbali na maudhui mbalimbali utakayopata, tutakuletea pia Kampeni maalum zinazogusa masuala muhimu katika Jamii

Tunakukaribisha kushiriki nasi katika mijadala yenye tija, kujifunza, na kusambaza maarifa kwa wengine ili wote tufaidike

Endelea kutufuatilia na kuwa sehemu ya mabadiliko chanya katika Jamii yako

#JamiiForums #JFCampaigns
Haki za kiraia ni uhakikisho wa fursa sawa za Kijamii na Ulinzi chini ya sheria, bila kujali Rangi, Dini, au Sifa nyingine za kibinafsi

Mifano ya Haki za Kiraia ni pamoja na: Haki ya kupiga kura, kufikishwa Mahakamani, kupata Huduma za Serikali, Haki ya kupata Elimu ya Umma, na Haki ya kutumia Miundombinu ya Umma

Haki za kiraia ni sehemu muhimu ya #Demokrasia. Mfano: pale ambapo Watu wananyimwa fursa ya kushiriki matukio ya Kisiasa, wananyimwa Haki zao za Kiraia

Soma zaidi https://jamii.app/CivilRightsCampg

#JamiiForums #HakiZaKiraia #CivilRights #HumanRights
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MANYARA: Mwanakijiji wa Njoro akimueleza Mkuu wa Mkoa huo, Queen Sendiga, namna Mwenyekiti wa Mtaa wake pamoja na Askari Polisi walivyochukua Vitu vya Nyumbani kwake ikiwemo Godoro, Kochi na TV kwa kushindwa kumuwekea Mumewe dhamana aliyekamatwa kwa kuuza Simu (Tsh. 190,000) iliyobainika kuwa ya Wizi

Soma https://jamii.app/MkitiPolisiMjamzito

#JamiiForums #HakiZaKiraia #CivilRights #HumanRights #JFMatukio
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
JamiiForums imeboresha mwonekano kwenye Kurasa za Mitandao ya Kijamii ili kukupa Mwonekano wa Kisasa na rahisi kwenye kuthibitisha Maudhui yake

Mwonekano huu mpya utakupa nafasi ya kushiriki Mijadala mbalimbali inayoendelea kwenye Jukwaa letu pendwa la JamiiForums.com na zaidi ya yote utaweza kuhakiki uhalali wa maudhui hayo kwa kufuata Maelekezo yanayotolewa kwenye Video hii

Asante na endelea kufuatilia akaunti zetu kwa maudhui bora zaidi

#JamiiForums #GraphicsUpdate
👍1
KATAVI: Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi, Dkt. Thadeus Makwanda ametoa ufafanuzi kuhusu hoja ya Mwanachama wa JamiiForums.com aliyeeleza kuwa Hospitali ya Wilaya ya Mlele haina Mhasibu hali ambayo inaweza kusababisha upotevu wa Fedha

Amesema Utaratibu wa sasa hakuna Fedha ambayo Mtumishi anakaa nayo, kila kiasi kinachoingizwa kwa maana ya kufanyika malipo kinapelekwa Benki, hakuna Mtu anayekaa na Fedha mkononi."

Ameongeza ““Unajua tuna Wakaguzi wa Nje, wanakuja kutukagua kila mwaka hawawezi kukubali fedha zikae mkononi, pia, kuanzia mwezi huu wa pili, katika vituo vyote tumefunga mfumo ambao utamwezesha mlipaji kutumia Namba ya Malipo, hivyo fedha itaenda Serikalini moja kwa moja.”

Soma https://jamii.app/MhasibuHospMlele

#JamiiForums #Accountability #Uwajibikaji #JFMdau2025