JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.42K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Mdau wa JamiiForums, Mkazi wa Mtaa wa Zavala - Kwambiki, Kata ya Buyuni Chanika, anasema wanapitia Changamoto ya Umeme kukatika katika kila Siku kwenye baadhi ya Nyumba, ambapo anadai walielezwa Mita zao ambazo namba za mwanzo ni '40', zinashindwa kuhimili Umeme unapokuwa mdogo

Anahoji, TANESCO wanawasaidiaje kuhusu hili na kwanini waliwawekea Mita hizo ikiwa wanajua Umeme wa eneo lao Mita zinazostahimili ni zile zinazoanza na 30?

Soma https://jamii.app/KukatikaUmemeKwambiki

#JamiiForums #ServiceDelivery #HudumaZaKijamii
CAF: Safari ya Timu ya #Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika 2024/25 imefikia tamati kwa kuishia Hatua ya Makundi baada ya kulazimishwa matokeo ya 0-0 dhidi ya #MCAlger ya Algeria kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar

Matokeo hayo yanaifanya Yanga ishike nafasi ya tatu katika Kundi A nyuma ya Al Hilal ya Sudan yenye alama 10 ikifuatiwa na MC Alger yenye alama 9, hivyo timu hizo mbili za juu zimefuzu kucheza Robo Fainali

Timu ya #TPMzembe ambayo imeshika mkia licha ya kushinda magoli 4-0 dhidi ya Al Hilal katika mchezo wa mwisho, ina pointi 5 ikiwa imeshinda mchezo mmoja

Soma https://jamii.app/YangaMCAlge

#JFSports #JamiiForums #JFCAF25
Mafanikio huanza kwa hatua ndogo. Sio lazima kufanya mambo yote kwa wakati mmoja

Kugawa kazi zako kutakusaidia kufanya jambo moja kwa wakati, kwa uweledi na umakini zaidi

#AmkaNaJF #LifeLessons #JamiiForums #Maisha #Goodmorning #LifeTips #MorningQuote
👍1👏1
ENGLAND: Mshambuliaji Erling Haaland (24) amesaini mkataba mpya ambao utamwezesha kubaki katika Klabu ya Manchester City hadi Mwaka 2034, ambapo atalipwa Pauni 500,000 kwa wiki kutoka Pauni 375,000 kwa wiki alizokuwa akilipwa katika mkataba uliopita

Soma https://jamii.app/HaalandContract

#JFSports #JFDATA #JamiiForums
1
TABORA: JamiiForums imewasiliana na Waziri wa Ulinzi wa Chuo Polytechnic College, Mtiba Chacha kuhusu uwepo wa kundi la Vijana wanaokaba na kupora Watu ambapo amesema “Ni kweli hiyo changamoto ipo na tumesharipoti mara kadhaa kwa Jeshi la Polisi lakini hatua zimekuwa hazichukuliwi na Vijana hao wanaendelea kufanya yao na kibaya zaidi wameanza hadi kuingia Chuoni nyakati za usiku."

Ameongeza "Tunaomba Mamlaka zinazohusika zitusaidie kwani hali siyo nzuri na hii inaweza kuathiri mwenendo wa Masomo na kuwafanya Wanafunzi na Wananchi kwa jumla kuishi kwa hofu.”

Soma https://jamii.app/VibakaPolytechnic

#JamiiForums #Accountability #Accountability
👍1
DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuwajibika katika zoezi la uzoaji taka katika Soko lililopo maeneo ya Tegeta Kwa Ndevu kwani zinarundikwa muda mrefu barabarani bila kuzolewa

Aidha, amesema ijengee miundombinu rafiki katika eneo hilo kwani imekuwa chanzo cha kusababisha uwepo wa foleni wakati magari ya taka yanaposimama kupakia uchafu huo uliopo eneo la barabara

Soma https://jamii.app/JchafuSokoTegeta

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #ServiceDelivery
2
ENGLAND: Baada ya timu yao kufungwa Magoli 2-0 dhidi ya #Fulham ikiwa ni mchezo wao wa 7 mfululizo kupoteza katika #PremierLeague, mashabiki wa Leicester City wamemgeukia Kocha wao, Ruud van Nistelrooy na kumwambia “Hujui unachokifanya”

Mashabiki hao waliimba katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa King Power Stadium ikiwa ni mara yao ya kwanza kumshambulia Van Nistelrooy ambaye alijiunga na timu hiyo Novemba 29, 2024

Aidha, mashabiki ambao baadhi yao waliondoka Uwanjani dakika ya 68 mchezo dhidi ya Fulham, walimjia juu Mkurugenzi wa Soka wa Leicester, Jon Rudkin wakiamini ameshindwa kuiongoza timu hiyo

Soma https://jamii.app/RuudVan

#JFSports #JFEPL25 #JamiiForums
SINGIDA: Baada ya Mdau wa JamiiForums kutoa wito kwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania- OUT) kuboresha mazingira ya Chuo hicho kwani ni mabovu na kukishushia hadhi, Chuo hicho kimeahidi kufanyia kazi ushauri huo

Soma https://jamii.app/ChuoHuriaSingidaKuboreshwa

#JamiiForums #Accountability #Governance #JFUwajibikaji
1