JamiiForums
βœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#BUNGENI: Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amependekeza Uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu uweke mwongozo wa Nambari au Kitambulisho cha Taifa (NIDA) kuwa lazima kwa Waombaji wote ili kuimarisha Mfumo wa ukusanyaji Madeni, na uendelevu wa utoaji Mikopo

Ukaguzi wa CAG ulibaini Bodi ina deni la Mikopo ya Wanafunzi lililoiva la Tsh. Trilioni 2.10 hadi Juni 2023 na imekusanya Tsh. Trilioni 1.29 (62%) tangu Mwaka 2006/07, ikimaanisha Tsh. Trilioni 0.81 haijakusanywa.

Soma https://jamii.app/NIDAMikopoElimu

#JamiiForums #ServiceDelivery #HakiElimu #Governance
πŸ‘8
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#BUNGENI: Mbunge Mohammed Said Issa amesema baada ya mabadiliko ya Tume ya Uchaguzi kuwa Tume Huru ya Uchaguzi kufanyika, kuna ulazima wa Tume hiyo kuundwa na isiwe mabadiliko ya jina pekee

Pia, amesema mabadiliko hayo ya Tume hayajafanyika #Zanzibar kwa maana kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (#ZEC) sio huru, hivyo haitakiwi kusimamia Uchaguzi

Soma https://jamii.app/MradiWaSGR

#Democracy #Siasa #JamiiForums #JFUwajibikaji #Governance
πŸ‘4
Jambo mojawapo ambalo Mdau amelitaja ni Mzazi kumpa Mtoto wake Hela licha ya kuwa Mtu mzima anayejitegemea

Unadhani kipi kingine hufanyika kama Upendeleo tu kwa Mtu?

#JamiiForums #Maisha #JFChitChat
πŸ‘8
Denzel Hayes Washington (69) ni Muigizaji, Mtayarishaji na Muongozaji wa Filamu za #Hollywood, alitoa ujumbe huu alipowahutubia Wahitimu katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania Nchini Marekani
-
#JFQuotes #AmkaNaJF #GoodMorning #JFNukuu #LeaderShip #JamiiForums
πŸ‘8
#BUNGENI: Serikali imesema tathmini ya athari ya Miundombinu ya Barabara imefanyika Nchini na kubaini hadi Aprili 14, 2024 inahitajika Tsh. Bilioni 500 ili kurejesha Barabara na Madaraja katika hali yake ya kawaida kwenye maeneo yaliyoathiriwa na Mvua za El-nino

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, amesema β€œWakati wa Bunge la Februari (2024) tulifanya tathmini ya uharibifu wa Miundombinu na hasara ilikuwa ni Tsh. Bilioni 200, lakini mpaka Aprili 14 #Miundombinu mingi imeharibika na ili tuweze kuirudisha tunahitaji Tsh. Bilioni 500."

Soma https://jamii.app/UjenziBarabara

#JFHuduma #Accountability #Governance #JamiiForums #ServiceDelivery
πŸ‘2😁1
Baadhi ya mijadala inayoendelea kwenye Jukwaa la Ujenzi na Makazi ndani ya JamiiForums.com

1. Wadau mbalimbali wametoa ushauri kama vile Kufunika Paa ili Milango isinyeshewe, kupiga 'vanish' na kutumia 'Water Repellent' kwa mdau aliyeomba ushauri kuhusu tatizo la Milango ya Mbao kuvimba kipindi cha mvua.

Kuufikia mjadala huu bofya https://jamii.app/MilangoKutokufunga

2. Moja ya njia ambazo Wadau wamependekeza ni kutafuta Ndugu Unayemwamini umlipe ili asimamie 'site' yako kupepuka kuibiwa na Mafundi kipindi cha Ujenzi

Kufahamu njia nyingine bofya https://jamii.app/MbinuKuzuiaUpigaji

3. Mdau anauliza "Nifanyeje kuzuia msingi wa nyumba yangu usiingie maji?"

Kumshauri mdau huyu bofya https://jamii.app/MsingiMaji
πŸ‘3
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
#UGANDA: Wabunge Wanawake wameomba kufunguliwa saluni ya urembo Bungeni ili kuhamasisha ushiriki wao. Hivi karibuni Bunge lilifungua sehemu ya kufanya Mazoezi (gym) lakini Wabunge hao wakasema Mazoezi hayo yanaacha Nywele zao zikiwa zimeharibika hivyo kusababisha kutohudhuria Mazoezi.

#JamiiForums #BungeLaUganda
πŸ‘2😁1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Mdau wa JamiiForums.com anasema Uongozi wa Soko la Ndizi la Mabibo unapaswa kuwajibika kwa kufumbia Macho kero ya muda mrefu ya Uchafu wa Mazingira utokanao na Ubovu wa Miundombinu hasa kipindi cha Mvua

Anahoji kama Soko linatengeneza Mapato, kwanini Mamlaka haziwajibiki kuweka Miundombinu rafiki au wanangojea Magonjwa ya mlipuko yatokee ndio washikane Uchawi?

Soma https://jamii.app/MabiboSokoniUchafu

#JamiiForums #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability #Uwajibikaji #Governance
πŸ‘3❀1
Mdau wa JamiiForums.com anadai tangu kutokea mvutano baina ya Serikali na Hospitali binafsi kwenye Huduma za Bima ya Taifa ya NHIF kuna utaratibu umeibuka wa kunyimwa baadhi ya Dawa kwa maelezo kuwa hazipatikani kwenye Kitita kipya

Je, kuna Mfumo wowote unaomsaidia Mwanachama kuthibitisha kile anachoambiwa?

Shiriki Mjadala zaidi https://jamii.app/UkweliDawaNHIF

#JamiiForums #PublicHealth  #AfyaBora2024 #Afya
πŸ‘4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#DODOMA: Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu amesema asilimia kubwa ya Mgambo Nchini wamekuwa wakiwanyanyasa Wafanyabiashara Wadogo (Machinga) bila kujali wanafanya biashara katika mazingira halali

Awali, Mbunge Jesca Msambatavangu aliuliza lini Serikali itatekeleza ahadi ya Rais ya Mwaka 2022 kuwasaidia Machinga wa Iringa Mjini kiasi cha Tsh. Milioni 700 ili kuboresha mazingira yao? ambapo Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis amejibu kuwa ahadi hiyo itatekelezwa

Soma https://jamii.app/BungeniAprili16

#JFUwajibikaji #JamiiForums #Governance
πŸ‘6
#AFYA: Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba Tanzania (TMDA) imesitisha toleo Na. 329304 la Dawa ya kikohozi ya Benylin ya Watoto inayotengenezwa na Kampuni ya Johnson & Johnson, kama hatua ya tahadhari baada ya Mamlaka za #Nigeria kusema Vipimo vimeonesha kuwepo na kiwango kikubwa cha Sumu katika Dawa hiyo

Kulingana na Shirika la Habari la Reuters, Nchi nyingine zilizositisha utumiaji wa Dawa hiyo ni #Rwanda, Zimbabwe, Nigeria, #Kenya na Afrika Kusini.

Reuters imesema Vipimo vya Maabara vilionesha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha Kemikali ya Diethylene glycol, ambayo imehusishwa na vifo vya watoto kadhaa Nchini #Gambia, Uzbekistan na Cameroon tangu Mwaka 2022.

Soma https://jamii.app/SitishaDawaKikohozi

#JamiiForums #Governance #PublicHealth
πŸ‘5
#RipotiYaCAG: Kwa mujibu wa Ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka 2022/23 ulibaini Ucheleweshaji wa Fedha kutoka Serikalini ulisababisha madeni kwenye Mashirika 99 ya Umma yaliyofikia Tsh. Trilioni 3.49

Sababu nyingine za madeni ni pamoja na changamoto za Mtiririko wa Fedha na Kutofanya vizuri kwa Mashirika ya Kibiashara hali inayochangia kushusha hadhi ya Mashirika pamoja na Wazabuni kukataa kutoa Huduma

Zaidi Soma https://jamii.app/CAGMashirika

#JamiiForums #RipotiYaCAG24 #Governance #JFUwajibikaji24 #CAGReport24 #RipotiMashirikaYaUmma #JFDATA
πŸ‘4
#BUNGENI: Serikali imetangaza kurejeshwa kwa utoaji Mikopo ya 10% kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu kuanzia Julai 2024 ambapo Halmashauri 10 zitaanza utoaji kwa majaribio

Halmashauri zitakazofanyiwa majaribio kwa utaratibu wa kukopa kupitia Benki ni Majiji ya Dodoma na Dar es Salaam, Miji ya Newala na Mbulu, Manispaa za Kigoma Ujiji na Songea, Wilaya za Siha, Bumbuli, Nkasi na Itilima

Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, amesema Halmashauri nyingine 174 zitatumia utaratibu utakaoboreshwa ambapo jumla ya Tsh. Bilioni 227.96 zinatarajiwa kutolewa. Awali mikopo hiyo ilisitishwa baada ya Ripoti ya CAG ya 2021/22 kubaini Ubadhirifu katika utoaji na urejeshwaji wake.

Soma https://jamii.app/Asilimia10

#JamiiForums #Governance #Accountability #SocialJustice
πŸ‘5❀1
#BUNGENI: Serikali imepanga kutumia Tsh. Bilioni 190.57 katika ununuzi wa Magari 113 ya Viongozi wa Mikoa na Wilaya, Kuendelea na Ujenzi, Kukarabati na Kukamilisha Miundombinu ya Mikoa 26 ikiwemo majengo ya Utawala, Ikulu Ndogo, Makazi ya Viongozi na Watumshi wa Mikoa, Wilaya na Tarafa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa wa amesema "Shughuli zitakazotekelezwa katika Utawala Bora ni ununuzi wa Magari 9 ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa, Magari 56 ya Wakuu wa Wilaya na 47 ya Wakurugenzi wa Halmashauri”

Soma https://jamii.app/Matumizi2024

#JamiiForums #Governance #JFUwajibikaji24 #KutokaBungeni
πŸ‘Ž6πŸ‘4
#DIPLOMASIA: Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Israel Katz, kupitia Mtandao wa X amesema ametuma barua kwa Nchi 32 na kuzungumza na Mawaziri wengi wa Mambo ya Nje Duniani akitaka vikwazo viwekwe dhidi ya Mradi wa Makombora unaofanywa na Iran

Pia, ametoa wito wa Jeshi la IRGC litangazwe kuwa kikundi cha Kigaidi, amesema "kama njia ya kudhoofisha Iran" na kuongeza "Iran lazima izuiliwe kabla hatujachelewa"

#IsraelKatz amesema anaongoza 'Mashambulizi ya Kidiplomasia' dhidi ya #Iran wakati wakizingatia kujibu Kijeshi shambulio la Makombora na Ndege zisizokuwa na Rubani lililotokea Usiku wa Aprili 13, 2024

Soma https://jamii.app/IsraelVsIranMissiles

#JamiiForums #IsraelVsPlalestine #MiddleEastWar #Diplomacy
πŸ‘5
Moja ya sababu ya Bakteria kuwa Sugu kwenye Dawa za Kuua Vimelea (#Antibiotic) ni matumizi makubwa kupita kiasi, kukatisha Dozi au matumizi mengine yasiyo sahihi ya Dawa hizo

Tafiti mbalimbali zimebaini uuzwaji holela wa Dawa hizo kwenye Maduka ya Dawa za Binadamu, husababisha Watu kuzitumia bila kufanya vipimo vya Afya na hivyo kujitibu pasipo mwongozo

#JamiiForums #PublicHealth #AfyaBora2024 #Afya
πŸ‘3❀1
Mdau wa JamiiForums.com anasema ili kuepuka Ajali za Barabarani wakati huu wa Mvua kubwa ni muhimu kwa Madereva kuzingatia mambo muhimu kama kutodharau maji yanayotembea bila kujali wingi wake na kuhakikisha 'Break Pad' na taa ziko kwenye hali nzuri

Soma https://jamii.app/UsalamaWakatiWaMvua

#JamiiForums #RoadSafety #RoadAccidents
πŸ‘1