JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Mbunge wa Jimbo la #Simanjiro Mkoani #Manyara, Christopher Ole Sendeka amenusurika baada ya Watu ambao bado hawajafahamika kushambulia gari lake kwa risasi akiwa safarini katika Kijiji cha Ngabolo Wilayani #Kiteto, jana Machi 29, 2024

Akizungumzia tukio hilo Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime amesema “Jeshi la Polisi limepokea taarifa hiyo, Ole Sendeka na Dereva wake wote hawajapata madhara, uchunguzi umeanza baada ya kupokea taarifa.”

Ameongeza “Timu ya Wataalam wa Matukio yaliyohusisha matumizi ya risasi kutoka Makao Makuu #Dodoma imetumwa kwenda kushirikiana na Timu ya Manyara kubaini Wahusika na madhumuni yao au kusudio lao, baada ya uchunguzi taarifa kamili itatolewa.”

Soma https://jamii.app/OleSendeka

#JFMatukio #JamiiForums
👍82🤔1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Utachukua hatua gani ukigundua Cheti chako cha Ndoa ni feki?

Nchini Zimbabwe, ndoa kadhaa hivi karibuni zimeonekana kuwa batili kutokana na kunukuu Sheria za zamani kwenye Vyeti

#JamiiForums
👍3😁2
Shirika la Kimataifa la kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limeitaka #Somalia kutoruhusu marekebisho ya #Katiba ambayo yanalenga kupunguza umri wa Utu uzima kwa madai hali hiyo itadhoofisha Haki za Watoto

Mabadiliko yaliyopendekezwa ambayo yatajadiliwa #Bungeni leo, Machi 30, 2024 yanapendekeza Umri wa Utu Uzima wa Miaka 15 na Miaka 18 kama Umri wa kuwajibika Kisheria

Human Rights Watch imesema mabadiliko yaliyopendekezwa yatawaweka Wasichana katika hatari kubwa ya Ndoa za Utotoni, ambazo huathiri Afya zao, haswa Afya ya Uzazi, upatikanaji wa Elimu, na Ulinzi wao dhidi ya Unyanyasaji

Soma https://jamii.app/SomanChildAge

#JamiiForums #HumanRights #InvestInWomen #ChildProtection #HakiWatoto
👍81
Siku ya Kimataifa ya Kutozalisha Taka inalenga kuongeza uelewa wa Mipango ya Kitaifa, ya Kikanda, na ya Mitaa katika kufikia Maendeleo Endelevu

Mipango hii inaweza kuchochea usimamizi mzuri wa taka, pia kupunguza na kuzuia uzalishaji wa taka ili kuondoa Uchafuzi wa Hali ya Hewa.

Soma https://jamii.app/ZeroWasteDay24

#InternationalDayOfZeroWaste #WastePollution #BeatWastePollution
👍2
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imehimiza katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kutenda mema na kudumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi

Serikali imesisitiza kuhusu ustaarabu wa Wazanzibari kuvumiliana kidini kama msingi wa mshikamano miongoni mwa Wananchi huku ikilaani vitendo vya unyanyasaji vinavyoendelea kufanyika sehemu mbalimbali Zanzibar, na kusema kadhia hiyo ni kinyume na misingi ya kuvumiliana katika imani za kidini

Aidha, imewahimiza Wananchi kujizuia kwa namna yoyote ile kuingilia uhuru wa mtu binafsi katika kuabudu na kuongeza kuwa hatua yoyote yenye kuhatarisha Umoja, Amani na Mshikamano haitavumiliwa

Soma https://jamii.app/SMZYalaaniUnyanyasaji

#JamiiForums #Governance
👍41👏1
TANGA: Watumishi Watano wa Kituo cha Afya cha #Mikanjuni, wamesimamishwa kazi baada ya tukio la kumuongezea damu Mgonjwa ambaye hakuhitaji huduma hiyo na kusababisha kifo chake

Akielezea tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, James Kaji amesema Marehemu alifanyiwa upasuaji na kufanikiwa kupata Mtoto wa Kike wa kilo 3.4 na hakuwa na changamoto yeyote

Inaelezwa kuwa kwenye Wodi aliyokuwa amelazwa Marehemu, kulikuwa na mgonjwa ambaye alihitaji kuwekewa damu na damu yake ilikuwa tayari imeandaliwa. Muuguzii aliyekuwa zamu alimuwekea Marehemu damu ambayo hakustahili kupewa na hakuwa na uhitaji huo, iliyomsababishia mzio mkali uliosababisha kifo chake

Watumishi waliosimamishwa kazi ni Wauguzi Fadhila Ally Hozza, Restitua Kasendo Deusdedit, na Muya Ally Mohamed, pamoja na Madaktari Andrew Eliasikia Kidee na Hamis Mohamed Msami

Soma https://jamii.app/MjamzitoDamuUchunguzi

#JamiiForums #Accountability
👍132
Mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya #Yanga na #MamelodiSundowns umemalizika kwa matokeo ya 0-0 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam

Licha ya Wageni kumiliki mpira muda mwingi, Yanga ndio waliofanya mashambulizi mengi ya hatari ikiwemo kupiga mashuti manne yaliyolenga goli huku Wapinzani wakipiga mawili

Mchezo wa marudio utachezwa Aprili 5, 2024 Nchini Afrika Kusini kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria na mshindi atafuzu kucheza Nusu Fainali

Hii ni mara ya tatu timu hizo kukutana katika michuano hiyo, zilikutana Mei 13, 2001 (Mamelodi Sundowns 3-2 Yanga) na kurudiana Mei 26, 2001 (Yanga 3-3 Mamelodi Sundowns)

Soma https://jamii.app/YangaMamelodi

#JFSports #CAFCL #JamiiForums
👍8
PAUL MAKONDA ATEULIWA KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

Rais Samia Suluhu Hassan amemtua aliyekuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha

Makonda anayechukua nafasi ya John Vianney Mongella, amewahi pia kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni

https://jamii.app/MakondaRCArusha
👍7
NDALICHAKO AONDOLEWA UWAZIRI, NDEJEMBI ACHUKUA NAFASI HIYO

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Deogratius John Ndejembi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akichukua nafasi ya Prof. Joyce Lazaro Ndalichako

Kabla ya Uteuzi, Ndejembi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Soma https://jamii.app/UteuziNdalichakoWatenguliwa
👍3
MAKALLA ATOLEWA MWANZA, KUPANGIWA KAZI NYINGINE

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mohamed Mtanda kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akichukua nafasi ya Amos Gabriel Makalla

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus imesema Makalla atapangiwa kazi nyingine

Soma https://jamii.app/MakallaAtolewaMWZ

#JFSiasa #Governance
👍52
Jumapili hii ya Pasaka ikupe msukumo na tumaini jipya, furaha na mafanikio katika yote unayoyafanya

Heri ya Sikukuu ya Pasaka

#HappyEaster #JamiiForums
13🙏7🎉3
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) hufanya ukaguzi wa matumizi ya Fedha za Umma ili kuthibitisha matumizi yamefanywa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni husika na kuna uwazi katika matumizi ya fedha hizo

Ufuatiliaji wa uwasilishwaji wa ripoti hizi ni muhimu kwa Wananchi ili kuhakikisha kuna Uwajibikaji na wote waliohusika kwenye Ufisadi na ubadhirifu wa fedha za Umma wanachukuliwa hatua stahiki

Je, huwa unafatilia uwasilishwaji wa ripoti hii?

Kwa mjadala zaidi https://jamii.app/Ripoti_CAG

#JamiiForums #Accpuntability #Uwajibikaji #UtawalaBora #Governance #JFToons
👍51
Kwenye Maisha kuna vitu, mienendo au matendo ya Mtu yanayoweza kuwa ya kero kwa mwingine, iwe ni kwa kujua au kwa kutojua. Kwako Mdau, kitu gani hakikufurahishi au ni kero kwako kinafanywa na Mtu wako wa karibu?

Soma https://jamii.app/TabiaYaMtu

#Maisha #LifeStyle #JamiiForums
2
Chama cha #ACTWazalendo kimelitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha, linawakamata na kuwafikisha katika Vyombo vya Sheria Waliohusika na kifo cha Katibu wa chama hicho katika Jimbo la Chaani, Ali Bakari Ali ikidaiwa kabla ya mauti alitekwa, alishambuliwa na kutupwa na Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi

Taarifa ya ACT imeeleza Ali alifariki Usiku wa kuamkia Machi 29, 2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazimmoja kutokana na Majeraha ambapo chama hicho kinaeleza uhalifu wa kutekwa, kupigwa na kuumizwa unatia shaka hali ya usalama wa Watu na Mali

ACT imeeleza huo ni muendelezo wa vitendo vya uhalifu na ukatili katika Mji wa Zanzibar na viunga vyake, pia vinaashiria uwepo wa vikundi vya kihalifu ambavyo vinajiimarisha bila Jeshi la Polisi kuvidhibiti

Soma https://jamii.app/TamkoLaACT

#JFMatukio #CivilRights #HumanRights #Governance #Accountability #JamiiForums
👍93