JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
JF YAENDESHA SEMINA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI NA FARAGHA KWA WABUNGE

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson jana (Juni 27, 2022) alishiriki Semina ya Umuhimu wa Kulinda Taarifa Binafsi na Faragha za Watanzania iliyoendeshwa na Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo katika Ukumbi wa Msekwa, Bungeni Jijini Dodoma

Spika ameipongeza JamiiForums na wadau wake (TLS, LHRC, Twaweza, CIPESA, Paradigm Initiative) na Wadau wengine walioshiriki kuandaa Muswada wa Mfano (Model Bill) unaolenga Kulinda Taarifa Binafsi na Faragha za Wananchi

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaData #DataPrivacy
👍17
Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo akiendesha Semina ya Umuhimu wa Kulinda Taarifa Binafsi na Faragha kwa Wabunge alisisitiza umuhimu wa kuwa na Sheria rafiki na shirikishi itakayolinda Utu wa Mtanzania na kuweka mazingira rafiki kwa Uwekezaji Nchini

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaData #DataPrivacy
👍27🔥3
Umoja wa Mataifa: Zaidi ya Watu milioni 6.2 wamepoteza au kuyakimbia makazi yao ndani ya Ukraine kutokana na vita inayoendelea kati ya Taifa hilo na Urusi

> Pia, Watu milioni 5.26 wakikimbilia nje ya nchi tangu kuanza kwa vita Februari 24, 2022

Soma https://jamii.app/UkraineWakimbizi
👍7👏1😢1
UFILIPINO: SERIKALI YAAMURU TOVUTI YA RAPPLER KUFUNGWA

#Rappler ni miongoni mwa Vyombo vichache vya Habari vinavyokosoa Serikali ya Rais Duterte

Mmiliki wake, Maria Ressa aliyeshinda Tuzo ya Nobel 2021 amesisitiza itaendelea kufanya kazi

Soma https://jamii.app/TovutiRappler

#PressFreedom
👍9
DAR: TMDA imekamata Dawa za Shinikizo la Damu, za Kuongeza Nguvu za Kiume na za Kutoa Ujauzito ambazo hazijasajiliwa na zenye thamani ya Tsh. milioni 294.4 katika Ghala Bubu

> Mmiliki wa ghala hilo atalipa faini isiyopungua Tsh. milioni 85

Soma - https://jamii.app/DawaBilaKibali
😁9👍5
MDAU: NENO 'KUHONGA' LITAFSIRIWE VYEMA LINACHANGANYA NA NENO 'KUHUDUMIA'

Katika Jukwaa la Lugha lililopo JamiiForums.com, Mdau amesema kumlipia mtu kula, mavazi au makazi sio kuhonga ni kuhudumia

> Je, kuhonga na kuhudumia kuna maana tofauti?

Soma - https://jamii.app/KuhongaKuhudumia
👍16😁7👎2
MDAU: Mabasi ya Mikoani kujaza abiria hadi wengine kusimama ni hatari kwa Usalama wa Abiria. Kinachosikitisha ni kuwa kuna "Trafiki" wanajua hili na hawachukui hatua stahiki

> Je, unachukua hatua stahiki unapoona Usalama wa Abiria unahatarishwa?

Soma - https://jamii.app/MabasiYaMikoani
👍17
Kwa mujibu wa Shirika la Muungano wa Mawasiliano Duniani (ITU), inakadiriwa 71% ya Watoto/Vijana kati ya Miaka 15 - 24 wanatumia Intaneti

Mtandao unatoa fursa nzuri ya kujifunza, lakini unakuja na hatari zake. Ni muhimu Wadau kushirikiana ili kuwalinda Watoto na Vijana

Soma - https://jamii.app/ReportITU

#DigitalRights
👍3
SENEGAL: Wahamiaji 14 wamefariki baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kulelekea Ulaya kupitia Visiwa vya Kanari vya Hispania kushika moto karibu na Jimbo la Casamance

> Wahamiaji hao ni raia wa Guinea, Nigeria, Gambia na Senegal

Soma - https://jamii.app/14MigrantsDie

#JamiiForums
👍3🤔3😢2
RAILA ODINGA: NITAKUBALI KUSHINDWA

Akimjibu Mshindani wake Mkuu, William Ruto aliyetaka aseme wazi kuwa atakubali matokeo ya kushindwa, Odinga anayegombea nafasi ya Urais kwa mara ya 5 amesema atafanya hivyo na kumpongeza Mshindi

Soma - https://jamii.app/OdingaMatokeo

#KenyaElections
👍18
MDAU: Ukiingia Stendi za Nanenane (Dodoma), Magufuli (Dar) na Msamvu (Morogoro) huwa unatozwa hela mlangoni ambayo ni ya gharama za uendeshaji na unapotaka kutumia Huduma ya Choo unatakiwa kulipa

> Ni kwanini ulipie choo wakati umelipa kiingilio?

Soma - https://jamii.app/TozoZaStendi
👍28🤔6😁1
Ili kuweza kuona fursa hizi na nyingine nyingi za Ajira, tembelea > https://jamii.app/NafasiAjira

#JamiiForums
👍7
ZIMBABWE: Serikali imetangaza mipango wa kutumia Dola ya Marekani kuwa fedha rasmi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, sababu ikiwa ni mfumuko wa bei

> Mfumuko wa Bei umefikia 192% ambapo Wafanyakazi wametaka walipwe kwa fedha za kigeni

Soma - https://jamii.app/ZimbabweEconomy
👍12
HALI YA RUSHWA SINGIDA: Katika Taarifa 100 yaliyopokelewa na Mamlaka kati ya Januari - Machi 2022; 73 zilihusu vitendo vya Rushwa na 27 hazikuhusu Rushwa

TAMISEMI imepokea Malalamiko mengi zaidi (41). Changamoto kubwa katika eneo hili ni nini? Hatua zinazochukuliwa zinasaidia?

Soma - https://jamii.app/TaarifaSingida

#KemeaRushwa
👏4👍1
UTEUZI: Rais Samia amemteua Meja Jenerali Jacob John Mkunda kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF)

Pia, amempandisha cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni Jenerali na kumteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania

Soma - https://jamii.app/UteuziCDF
👍23👏4😁1
GHANA: Raia wamekusanyika katika Mji wa Accra kwa siku ya pili ya maandamano kupinga kuongezeka kwa mfumuko wa bei na kudorora kwa uchumi

> Mfumuko wa bei unadaiwa kufika 27.6% kwa mwezi Mei

Soma - https://jamii.app/MaandamanoGhana
👍7👎2
MAREKANI: Mwanamuziki #RKelly amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa unyanyasaji wa kingono kwa wanawake na mabinti wadogo

> Aidha, amepatikana na hatia za kulazimisha, kushawishi na usafirishaji wa kingono wa binti wa chini ya miaka 18

Soma > https://jamii.app/RKellySentence
👎6👍5
PUTIN: URUSI ITAJIBU VIKOSI VYA NATO VIKIPELEKWA FINLAND NA SWEDEN

Amesema Nchi yake haina shida #Sweden na #Finland kujiunga NATO, lakini Mataifa hayo lazima yaelewe hakukuwa na tishio awali, lakini hivi sasa mivutano kati yao inaweza kutokea

Soma > https://jamii.app/NATOUrusi
👍22👎3
MACAU: Mamlaka zinapambana kudhibiti mlipuko mkubwa wa #COVID19. Wakazi wote wametakiwa kukaa nyumbani mara nyingi iwezekanavyo

Maeneo mengi ya Mji huo ikiwemo Baa na Saluni yamefungwa ili kukabiliana maambukizi, na watu 7,000 wapo Karantini

Soma - https://jamii.app/COVIDMacau
👍5👏1
MEXICO: Mwandishi wa Habari, Antonio de la Cruz (47) ameuawa kwa kushambuliwa na risasi nje ya nyumba yake huku binti yake akijeruhiwa vibaya huko Ciudad Victoria

> Anakuwa Mwandishi wa Habari wa 12 kuuawa Nchini humo kwa mwaka 2022

Soma - https://jamii.app/ReporterKilled

#JamiiForums
👎7👍3😢3