JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
JUNI 30: SIKU YA MITANDAO YA KIJAMII

Mitandao ya Kijamii imesaidia upatikanaji wa Taarifa na kutoa fursa kwa sauti za Wananchi kusikika

Mitandao ina nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko

Je, unatumiaje nafasi yako Mitandaoni?

Soma zaidi - https://jamii.app/SMDay2022

#SocialMediaDay
👍9👏4
ETHIOPIA: Watetezi wa Haki za Binadamu wametoa wito wa kuachiwa kwa Watu takriban 9,000 wanaozuiliwa ktk eneo la Kaskazini Mashariki la #Afar tokea Desemba 2021

> Serikali imesema wanazuiliwa kwa Usalama wao, na ili kuruhusu Uchunguzi

Soma - https://jamii.app/HumanRightsTigray
🤔3👍2😁1
MWANZA: Bweni la Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Bwiru limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Juni 30, 2022 na kuunguza Vitanda, Magodoro, Nguo na Vifaa vya Shule

> Uongozi wa Mkoa utaratibu sehemu ya kulala na vifaa vya Wanafunzi walioathirika

Soma - https://jamii.app/ShuleYaBwiru
😢7👎2
LIBYA: Miili ya Watu 20 imekutwa katika Jangwa ambapo Wataalamu wa Afya wanaamini wahusika walipoteza maisha kutokana na kiu

> Miili hiyo ilikuwa Kilomita 320 kutoka Mji wa Kufra, na Kilomita 120 kutoka Mpaka wa Chad

Soma - https://jamii.app/MiiliJangwani

#JamiiForums
😢4👍3👎1
Ili kujilinda unapotumia Mitandao mbalimbali ya Kijamii, inashauriwa;

- Kuwa Makini na Taarifa zako binafsi: Taarifa hizo zinaweza kutumiwa vibaya

- Epuka kuweka kila kitu Mitandaoni: Angalia 'Privacy Settings' kujua namna unaweza kujiongezea usalama

- Nenosiri (Password) Imara: Epuka kutumia tarehe za kuzaliwa

Soma - https://jamii.app/SMDay2022

#DataPrivacy #SocialMediaDay
👍9
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
TEMEKE: Malalamiko 75 yalipokelewa TAKUKURU kati ya Januari - Machi 2022. Kati ya Malalamiko hayo, 49 yalihusu Rushwa na 26 hayakuhusiana na Rushwa

Wewe ni Mkazi wa Temeke, Dar es Salaam? Umewahi kuombwa Rushwa ulipohitaji Huduma katika Idara fulani?

Soma https://jamii.app/RushwaTemeke

#KemeaRushwa
👍5
BUNGENI: Waziri wa TAMISEMI ametoa ufafanuzi wa Wanafunzi kubadili kutoka Vyuo kuelekea Kidato cha Tano akisema wanapaswa kuripoti ktk Vyuo walivyopangwa na kusubiri taratibu nyingine

> Amesema wanatakiwa kukaa Vyuoni humo kwa wiki 2

Soma - https://jamii.app/UhamishoWanafunzi
👎5👍4
BUNGENI: Serikali imepiga marufuku michango holela katika Shule za Umma ngazi ya Msingi na Sekondari na kuagiza fomu za kujiunga na Shule zieleze hivyo

> Pia, imesema fomu hizo zihakikiwe na Katibu Tawala na Maafisa Elimu wa Mkoa husika

Soma - https://jamii.app/MichangoShuleni

#JamiiForums
🤔6👍2
MDAU: Tufichue Wauzaji wa #DawaZaKulevya, ni Wanajamii wenzetu na tunaishi nao. Tusiwatenge Waathirika, tuwapeleke kwenye Vituo vya Kuwasaidia ili wasirudie matumizi ya Dawa hizo haramu

> Je, umewahi kumsaidia Mwathirika wa Dawa za Kulevya?

Soma - https://jamii.app/FightAgainstDrugs

#JamiiForums
👍1
RAIS SAMIA KUMPANGIA MABEYO MAJUKUMU MAPYA

Akizungumza baada ya kumuapisha Jacob John Mkunda kuwa CDF, Rais Samia ameahidi kumpangia majukumu mengine aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Venance Mabeyo akisema amefanya kazi kwa uadilifu mkubwa

Soma - https://jamii.app/SamiaAkiapisha
👍21👏2
NIGERIA: Abba Haruna (21) anashikiliwa na Polisi kwa kudanganya Waumini atawajengea majengo mapya kupitia Taasisi ya Kigeni na kusababisha Waumini hao kuvunja Misikiti 14

> Abba alichukua mabati, madirisha na milango iliyoondolewa Misikitini

Soma - https://jamii.app/UtapeliNigeria
👍13😁8
UTEUZI: Rais Samia amemteua Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Mstaafu Jenerali Venance Salvatory Mabeyo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA)

Uteuzi wake umeanza leo (Juni 30, 2022)

Soma - https://jamii.app/UteuziMabeyo
👍33👎31👏1😁1
BAKWATA: Sikukuu ya Eid El-Adh’haa inatarajiwa kuwa Jumapili Julai 10, 2022 ambapo sherehe za kitaifa zitafanyika Dar es Salaam

> Swala ya Eid itaswaliwa Msikiti wa Mfalme Mohamed VI, Kinondoni ikifuatiwa na Baraza la Eid

Soma https://jamii.app/EidElAdhhaa

#JamiiForums
👍11😁4
Mahakama Kuu ya Dar inatarajia kutoa uamuzi wa maombi ya Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee na wenzake 18 Julai 6, 2022

> Wabunge hao wameomba kibali cha Mahakama ili kuwasilisha mapitio ya kimahakama wakipinga kuvuliwa uanachama wa CHADEMA

Soma - https://jamii.app/MaombiYaMdee

#JamiiForums
👎6🔥4🤬2👍1👏1
MAHAKAMA YATAKA WAINGEREZA WASINYONGWE URUSI

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu (ECHR) imeitaka Urusi kuzuia kunyongwa kwa Waingereza wawili waliokuwa katika Jeshi la Ukraine

Waingereza hao walikuwa sehemu ya Jeshi la Ukraine

Soma > https://jamii.app/WanajeshiWaUK
👍3👎3🤔3👏1
TUNISIA: Rasimu ya Katiba Mpya iliyopendekezwa na Wanakamati walioteuliwa na Rais Kais Saed, inatajwa kumpa Rais Mamlaka ya maamuzi ya mwisho juu ya Serikali, Bunge na Mahakama

> Rasimu hiyo inatarajiwa kupigiwa Kura ya Maoni Mwezi Agosti

Soma - https://jamii.app/KatibTunisia
🤮4👍1👎1
KOREA KASKAZINI: Serikali imedai, #COVID19 ilianza Nchini humo baada ya Watu kugusa "Vitu vya ajabu" (Alien Things)

> Uchunguzi uliwabaini Watu wawili waliopata maambukizi baada ya kushika vifaa visivyojulikana karibu na Mpaka wa Korea Kusini

Soma - https://jamii.app/CoronaVirusNK
👍13
SUDAN: Polisi wanadaiwa kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na risasi za moto Waandamanaji waliodaiwa kufunga barabara ili kushinikiza ukomo wa Utawala wa Kijeshi

> Huduma za Intaneti na Simu zilikatizwa ili kuzuia uhamasishaji mtandaoni

Soma - https://jamii.app/InternetblockageInSudan
👍7
DAR: Hospitali ya Taifa ya Muhimbili inatarajiwa kuwafanyia upasuaji wa kuwatenganisha Watoto Pacha walioungana Kifuani, leo Julai Mosi, 2022

> Upasuaji huo unakadiriwa kutumia saa 7 na utakuwa chini ya Wataalamu wa Afya 31

Soma - https://jamii.app/PachaWalioungana
👍11🙏3
MDAU: BIASHARA ZINAZOFUNGULIWA NA WATU HAWA LAZIMA ZIFE

- Waliopata Pesa Ghafla: Mara nyingi hawana mpango wa kuanzisha Biashara ila hushawishiwa

- Waliochoka Kuajiriwa: Wanaona kufungua Biashara na kujiajiri ni kitu kirahisi

Ni kweli mara nyingi Biashara zilizofunguliwa katika Mazingira haya hufa?

Mjadala > https://jamii.app/MdauBiashara
👎10👏2