JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UGANDA: Benki ya Dunia imesema Pato la Mwananchi ni dola 850 (takriban Tsh. 1,979,650) kwa mwaka wa fedha 2022 na sio Tsh. 2,433,805 kama Rais Museveni alivyoeleza

> Pia, ukuaji wa Uchumi ni 3.7% ambayo ni chini ya kiwango cha Uchumi wa Kati

Soma - https://jamii.app/UgandaUchumi
😁22πŸ‘5πŸ€”3πŸ‘Ž1
RASMI: TOTTENHAM YAMSAJILI RICHARLISON KUTOKA EVERTON

Imemsajili Mshambuliaji huyo (25) kwa Β£60m (Tsh. 169,800,000,000) na amesaini mkataba wa miaka mitano

Ni mchezaji wa 4 kusajiliwa na Spurs katika dirisha hili baada ya Ivan Perisic, Fraser Forster na Yves Bissouma

#JFSports
πŸ‘11😁1
Rais Samia Suluhu Hassan amesema, "Tanzania hii haiwezi kusonga mbele kama sisi Wananchi na Viongozi wenu tutakuwa legelege kulinda yaliyo yetu"

Katika Tahariri aliyoandika, amesema anatamani kujenga jamii yenye Maridhiano na Maelewano pasipo kujali tofauti za kisiasa, kidini, kikabila na nyinginezo

Soma zaidi - https://jamii.app/TahaririRais
πŸ‘16πŸ‘Ž7
Dkt. Yonah Mwalwisi kutoka TMDA amesema matumizi ya dawa za kuongeza Nguvu za Kiume bila kuzingatia ushauri wa Wataalamu wa Afya yanaweza kuchangia uwepo wa madhara ya Kiharusi, Mshtuko wa Moyo, Kuzimia na hata Kifo

Soma - https://jamii.app/DawaBilaUtalam

#JamiiForums
πŸ‘13
KATAVI: Malalamiko 57 ya Rushwa yalifikishwa TAKUKURU kati ya Januari - Machi 2022. Pia, Malalamiko mengine 4 ambayo hayakuhusisha Rushwa yalipokelewa

Malalamiko mengi yameelekezwa TAMISEMI, Ardhi na Utawala. Unadhani ni kwasababu gani?

Soma https://jamii.app/RushwaKatavi

#KemeaRushwa
πŸ‘5πŸ€”2🀬1
SERIKALI YASITISHA FOMU YA KUNUNULIA DAWA NJE YA HOSPITALI

Serikali imesitisha matumizi ya Fomu ya 2C katika Hospitali za Umma zinazotumia Bima ya Afya

Fomu hiyo inamwezesha mgonjwa kununua dawa nje ya hospitali kwa kutumia bima

Soma > https://jamii.app/FomuYa2C

#JamiiForums
πŸ€”6πŸ‘4
UTAFITI: Wanasayansi nchini China, wamegundua Virusi vya #Zika na #Dengue huwaachia waathirika harufu inayotajwa kuvutia mbu, ambao huwauma na kubeba Virusi na kupeleka kwa mtu mwingine

> Hii imetoa jibu la sababu za magonjwa hayo kuenea kwa kasi

Soma - https://jamii.app/DengueNaZika

#JamiiForums
πŸ‘7😁3πŸ€”2
MUHIMBILI: UPASUAJI WA PACHA UMEFANYIKA KWA MAFANIKIO

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imetangaza upasuaji wa kutenganisha Watoto waliokuwa wameungana umefanyika kwa mafanikio

> Watoto Rehema na Neema walikuwa wameungana Kifuani

Soma https://jamii.app/WatotoPacha

#JamiiForums
πŸ‘24πŸ‘15
WAKILI AJITOA KESI YA JOHN PIMA

Wakili Valentine Nyalu amejitoa kuwawakilisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dkt. John Pima na wenzake watatu katika kesi ya Uhujumu Uchumi

> Wakili huyo hajataja sababu ya kujitoa

Soma - https://jamii.app/KesiJohnPima

#JamiiForums
πŸ‘17😁3
ARSENAL KUMREJESHA JACK WILSHERE

Arsenal inazungumza na Jack Wilshere (30) kuhusu kumpa nafasi ya ukocha wa timu yao ya vijana U23 na U18

Wilshere kwa sasa hana timu, pia wanazungumza na Per Mertesacker kuhusu nafasi hiyo

Soma > https://jamii.app/WilshereArsenal

#JamiiForums #JFSports
πŸ‘11πŸ‘2
LIBYA: RAIA WAANDAMANA, WADAIWA KUCHOMA SEHEMU YA JENGO LA BUNGE

Kumekuwa na Maandamano katika Miji mbalimbali Nchini humo kupinga ukatikaji umeme, ongezeko la bei na mkwamo wa kisiasa

#Libya imewahi kuwa na viwango bora vya maisha Afrika

Soma - https://jamii.app/2LibyaProtests
😒11πŸ‘8πŸ‘3πŸ”₯2
MDAU: GESI YA JOKOFU HAITAKIWI KUISHA

Mfumo wa gesi unazunguka katika duara, ikivuja ndipo inapoisha, hivyo fundi anatakiwa kuziba, kuondoa hewa ya kawaida kisha kujaza gesi

> Mdau anasema mafundi wengi hawana uelewa wa mchakato huo

Soma zaidi - https://jamii.app/ElimuYaJokofu
πŸ‘19πŸ‘5
DAR: Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amemuombea dua Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aoe mke wa pili

> Anaamini hiyo itamuongezea Waziri Mkuu utulivu zaidi katika mizunguko yake

Soma - https://jamii.app/MajaliwaAombewa
πŸ‘16🀬8πŸ‘Ž5😁5
MAGEREZA KUANZA KUWALIPA WAFUNGWA

Kamishna Jenerali wa Magereza amesema "Tumeanzisha vitenga uchumi vingi kila gereza Tanzania. Tunakoenda tutaanza kuwalipa, hii itasaidia pindi wanapotoka wanakuwa na kiasi cha kuanzia maisha"

Soma - https://jamii.app/MagerezaKulipa
πŸ‘24πŸ”₯8πŸ‘6
UCHAGUZI KENYA: Naibu Rais, William Ruto anayewania Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 2022 amesema endapo atashinda, ataunda Tume kuchunguza Sera na baadhi ya vitendo vilivyofanywa na Rais Uhuru Kenyatta

Soma - https://jamii.app/RutoKenyatta

#KenyaElections
πŸ‘9😁8πŸ”₯1
RUMANDE KWA TUHUMA ZA KUMLAWITI MLEMAVU WA AKILI

Said Hassan Mabrouk β€œSaid King” wa Chake Chake yupo rumande akituhumiwa kumlawiti mlemavu wa akili Mei 10, 2022

Mwathirika ametoa ushahidi Mahakamani akieleza ilivyotokea

Soma - https://jamii.app/TuhumaUlawiti

#HumanRights
🀯10πŸ‘Ž4
COVID-19 YAONGEZEKA KWA 30% UINGEREZA

Takwimu zimeonesha kuwa ongezeko hilo ni ndani ya wiki moja iliyopita na Watu milioni 3 wakiambukizwa

> Uingereza iliondoa masharti ya kujilinda na Corona ikiwemo kuvaa barakoa kwa lazima

Soma - https://jamii.app/UKCovid19
πŸ‘Ž6πŸ‘1
YANGA BINGWA WA ASFC

Yanga imetwaa ubingwa huo baada ya kuifunga Coastal Union kwa penati 4-1

Timu hizo zilimaliza dakika 120 zikiwa zimefungana goli 3-3 katika fainali iliyochezwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha

Soma > https://jamii.app/YangaBingwaFA

#JamiiForums
πŸ‘24πŸ‘Ž8πŸ”₯5πŸ‘4
RONALDO AOMBA KUONDOKA MAN UTD, MASHABIKI WASEMA β€˜MUACHENI AENDE ZAKE’

Cristiano Ronaldo ameomba kuondoka Manchester United, inadaiwa sababu ni timu hiyo kutofuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutofanya usajili mzuri

Baadhi ya mashabiki wa United mitandaoni wamenukuliwa wakisema β€˜muacheni aende’

Soma https://jamii.app/RonaldoOut

#JamiiForums
πŸ‘30😁8πŸ‘Ž3πŸ‘3
ARGENTINA: WAZIRI WA UCHUMI AJIUZULU

Martin GuzmΓ‘n amejiuzulu wakati mdororo wa Kiuchumi ukiendelea kushika kasi Nchini humo

#Argentina inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo Mfumuko wa Bei na kupanda kwa bei za Chakula na Nishati

Soma - https://jamii.app/WaziriUchumiArg
πŸ‘7πŸ‘Ž2