JamiiForums
โœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TETESI: LIVERPOOL YAANZA MAZUNGUMZO KUMSAJILI NUNEZ

Inadaiwa Liverpool inamtaka Mshambuliaji Darwin Nunez kutoka Benfica ili kuziba pengo la Sadio Mane

Ipo tayari kuvunja rekodi yake ya usajili ktk usajili huo unaoweza kufika Paundi Milioni 85 (Tsh. 245,650,000,000)

#JFSports
๐Ÿ‘5๐Ÿ‘1๐Ÿคฎ1
FARAGHA MTANDAONI: Utakuwa salama kwa kufanya yafuatayo;

> Tumia Nywila (Password) imara
> Ruhusu uthibitisho wa njia mbili (Two factor Authentication)
> Huisha (Update) Apps mara kwa mara
> Usitumie Wi-Fi usiyoijua

Soma - https://jamii.app/FaraghaMtandaoni

#DataPrivacy #DigitalSecurity
๐Ÿ‘12๐Ÿ˜1
JUNI 08: SIKU YA BAHARI DUNIANI

Siku hii huadhimishwa ili kuwakumbusha watu umuhimu wa bahari

Tunaweza kutunza bahari kwa kupunguza au kuacha matumizi ya bidhaa za plastiki na kushiriki kusafisha fukwe za bahari

Soma zaidi - https://jamii.app/SikuYaBahariDuniani

#WorldOceansDay
๐Ÿ‘10๐Ÿ˜2
TETESI: CHELSEA YAMTAKA MARTINEZ KAMA LUKAKU ATAREJEA INTER

Romelu Lukaku ameendelea kushinikiza kutaka kuondoka Chelsea na kurejea Inter Milan

Inadaiwa Chelsea inaangalia uwezekano wa kumpata Lautaro Martinez, Milan Skriniar au Alessandro Bastoni kama sehemu ya dili

#JFSports
๐Ÿ‘8๐Ÿ‘4๐Ÿ‘Ž2๐Ÿค”2
#UKRAINE: Idara ya Ujasusi ya Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imesema Urusi imekabidhi miili 210 ya wapiganaji

Imeelezwa kuwa, wengi walifariki wakati wa mapigano walipokuwa wakilinda Mji wa #Mariupol. Mchakato wa kupokea miili unaendelea

Soma - https://jamii.app/Miili210Ukraine
๐Ÿ‘10๐Ÿ˜ข3โค1๐Ÿ”ฅ1๐Ÿ’ฉ1
ADAIWA KUBAKA MTOTO ILI AIJARIBU DAWA YA MGANGA

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema tukio hilo limetokea Juni 7, 2022

Amesema hilo ni jambo la ovyo, aibu, ajabu, kusikitisha, kufedhehesha na halivumiliki

Soma - https://jamii.app/SamiaZiarani

#JamiiForums #HumanRights
๐Ÿ‘Ž13๐Ÿคฏ3โค1๐Ÿ‘1๐Ÿคฌ1
KAMATI YA BUNGE: KITENGO CHA KUDHIBITI FEDHA HARAMU KIMEELEMEWA

Upungufu wa watumishi wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu umetajwa kuwa kikwazo, ikielezwa 90% ni watumishi wa kuazima

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti yashauri mamlaka kamili iundwe

Soma - https://jamii.app/KudhibitiFedha
๐Ÿ‘7๐Ÿ˜1
UGANDA: Tafiti za Umoja wa Mataifa zimebaini kuwa zaidi ya Watu 500,000 ambao ni sawa na 40% ya Wakazi ktk eneo la Karamoja wanakabiliwa na hatari kubwa ya njaa

> Eneo hilo lina kiwango kikubwa cha utapiamlo hasa kwa Watoto chini ya miaka 5

Soma - https://jamii.app/NjaaUganda
๐Ÿ‘3๐Ÿค”3๐Ÿ˜ฑ1
KENYA: TIKTOK YASHUTUMIWA KWA UCHOCHEZI

Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Mtandao wa #Tiktok umeshutumiwa kwa uchochezi Nchini humo kwa kutodhibiti video zilizokuwa na matamshi ya chuki na habari potofu za kisiasa, kinyume na sera yake

Soma - https://jamii.app/TiktokKenya

#KenyaElections
๐Ÿ‘10๐Ÿ˜1
KUFUZU #AFCON2023: TANZANIA 0-2 ALGERIA

#TaifaStars imepoteza mchezo huo dhidi ya #Algeria ikiwa nyumbani katika dimba la Mkapa

Algeria sasa inaongoza Kundi F ikiwa na alama 6, Niger ina alama 2, Tanzania alama 1 na Uganda alama 1

Soma > https://jamii.app/TZ0Algeria2

#JFSports
๐Ÿ‘18๐Ÿ‘Ž7๐Ÿคฌ2โค1
MDAU: Kabla ya kuacha kazi kuna mambo unatakiwa kujiuliza, mfano: Sababu ni ya msingi? Ni muda sahihi? Una chanzo kingine cha kipato?

Upo katika tasnia gani? Utafanya nini? Vipi kuhusu stahiki au haki zako?

Soma zaidi - https://jamii.app/KuachaKazi

#JamiiForums
๐Ÿ‘12
RASHFORD AKATAA OFA YA KWENDA SPURS

Mshambuliaji Marcus Rashford wa Manchester United anataka kubaki kupigania namba chini ya kocha mpya, Erik ten Hag

Rashford (24) amesalia na mwaka mmoja tu katika mkataba wake

Soma > https://jamii.app/RashfordUtd

#JamiiForums #JFSports
๐Ÿ‘12๐Ÿ‘1
EU YARIDHIA SIMU ZOTE KUTUMIA USB-C

Uamuzi huo uliotajwa kuwa pigo kwa Kampuni ya Apple utaanza kutekelezwa Mwaka 2024

Imeelezwa kuwa, Kanuni hiyo inalenga kupunguzia wateja usumbufu wa kutumia Chaja tofauti na kudhibiti uchafu wa kielektroniki

Soma - https://jamii.app/EUPhoneCharge
๐Ÿ‘28๐Ÿ‘Ž3๐Ÿ˜3๐Ÿ‘2๐Ÿ˜ฑ1
UTAFITI: DAWA YA DOSTARLIMAB YALETA AHUENI KWA WAGONJWA WA SARATANI

Kwa mujibu wa Utafiti uliochapishwa na "The New England Journal of Medicine", Wagonjwa 12 waliotumia Dawa ya Majaribio ya Dostarlimab kwa kipindi cha miezi 6 walionekana kupata nafuu

Japokuwa jaribio hilo limeonesha matokeo chanya, Wanasayansi wametahadharisha kuhusu kuhitimisha moja kwa moja kuwa Wagonjwa hao wamepona

Soma - https://jamii.app/UtafitiSarataniDawa
๐Ÿ‘7๐Ÿ‘1
CHADEMA: Tutaandika barua rasmi kuwataka Viongozi (akiwemo Lissu na Lema) waliokimbia kwa sababu za kiusalama warudi Nchini kwa kuwa usalama kwa sasa upo

> Chama hicho kimesema suala la Usalama lilikuwa moja ya ajenda za Maridhiano

Soma - https://jamii.app/UsalamaUpo

#JamiiForums
๐Ÿ‘31โค3๐Ÿฅฐ3๐Ÿ˜1
UCHAGUZI KENYA: SERIKALI YASEMA MITANDAO HAITAZUIWA

Waziri wa Mambo ya Ndani, Fred Matiangโ€™i amesema Serikali haitoingilia upatikanaji wa Mitandao ya Kijamii kabla, wakati wa na baada ya Uchaguzi Mkuu kwani #Kenya ni Nchi ya Kidemokrasia

Asema, "Hakuna kiasi cha matusi kitakachotufanya tujihusishe na vitendo kama hivyo"

Soma - https://jamii.app/SociaMediaKE

#KenyaElections #DigitalRights
๐Ÿ‘14๐Ÿ”ฅ2๐Ÿ˜1
MUSEVENI: TUMEINGIA UCHUMI WA KATI

Amesema licha ya migogoro, Pato la Taifa la mwaka kwa mtu mmoja limefika Tsh. 2,437,180 sawa na Dola za Marekani 1,046 na wamevuka kiwango cha hadhi ya kati ambacho ni Tsh.2,399,900 sawa na Dola za Marekani 1,030

Soma - https://jamii.app/UgandaUchumiWaKati
๐Ÿ˜17๐Ÿ‘11๐Ÿ‘1
NIGERIA: APC YAMPITISHA BOLA TINUBU KUGOMBEA URAIS

Chama tawala kimemchagua kuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Februari 2023. Amepitishwa kwa Kura 1,271

Atashindana na Kiongozi wa upinzani, Atiku Abubakar kumrithi Rais Muhammadu Buhari

Soma - https://jamii.app/Nigeria2023Elections
๐Ÿ‘5๐Ÿ˜3
WANAJESHI WATATU WA TANZANIA WAJERUHIWA DR CONGO

Inaripotiwa kuwa, Wanajeshi hao wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa wamejeruhiwa katika mapigano dhidi ya waasi wa M23

Tanzania ina Wanajeshi zaidi ya 800 miongoni mwa vikosi vya UN Nchini humo

Soma - https://jamii.app/WanajeshiWaTzDRC
๐Ÿ‘6๐Ÿ˜ฑ4๐Ÿ˜ข4๐Ÿ‘Ž1
SRI LANKA: Kaka wa Rais Gotabaya Rajapaksa ametangaza kujiuzulu Ubunge akisema kuanzia sasa hataki kujihusisha na shughuli zozote za Serikali

Basil Rajapaksa ambaye amewahi kuhudumu kama Waziri wa Fedha anakuwa ndugu wa pili wa Rais kujiuzulu

Soma - https://jamii.app/KakaRaisUbunge
๐Ÿ‘5๐Ÿ”ฅ2