JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Ripoti mpya ya Shirika la Muungano wa Mawasiliano Duniani (ITU) inasema Watu Bilioni 2.9 bado hawatumii kabisa Mitandao, na Mamilioni wanakumbwa na changamoto ya gharama na ubora wa Intaneti wa hali ya chini

Gharama ya Huduma za Mitandao na vifaa vya kidigitali bado ni changamoto kwa Nchi zenye Uchumi wa Chini na Kati

Soma - https://jamii.app/ReportITU

#DigitalRights
πŸ‘13😒2
SIKU YA CHAKULA SALAMA DUNIANI

Chakula salama ni miongoni mwa vichocheo muhimu vya Afya njema. Vyakula visivyo salama ni chanzo cha magonjwa mengi

Kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha usalama wa Chakula katika hatua zote za mnyororo wa thamani, kuanzia kinapozalishwa hadi kinapofika kwa mlaji wa mwisho

Soma - https://jamii.app/FoodSafety

#WorldFoodSafetyDay
πŸ‘7πŸ”₯3
Somalia inakabiliwa ukame mbaya zaidi kushuhudiwa ndani ya miaka 40, huku bei ya chakula ktk Soko la Dunia ikizidi kuwa juu

> Ripoti za FAO, WFP na UNICEF zinasema kuwa, karibu nusu ya Watu ktk Taifa hilo wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula

Soma - https://jamii.app/NjaaSomalia
πŸ‘4πŸ€”3😒2
MOSHI: Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake 4 imeahirishwa hadi Juni 20, 2022

Mawakili wa Sabaya wameomba Mahakama kuharakisha upande wa Jamhuri ukamilishe ushahidi ili mteja wao akatibiwe

Soma - https://jamii.app/SabayaJuni7
πŸ‘8😁5πŸ€”2πŸ‘Ž1🀬1
WIZARA YA FEDHA YAOMBA KUIDHINISHIWA TRILIONI 14.94

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba ameomba Bunge kuidhinisha Bajeti hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2022/23

Amesema miongoni mwa changamoto katika Wizara hiyo ni Mfumuko wa Bei katika Soko la ndani na kasi ndogo ya ukuaji wa Pato la Taifa kutokana na athari za COVID-19 na vita kati ya Urusi na Ukraine

Soma - https://jamii.app/BajetiWizaraFedha
πŸ‘Ž10πŸ€”8πŸ‘3😁1
BALOZI WA URUSI ASUSIA KIKAO CHA UN

Vassily Nebenzia ametoka nje ya Kikao cha Baraza la Usalama la UN baada ya Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel kuishutumu Moscow kwa kusababisha janga la Chakula duniani kutokana na vita inayoendelea Nchini Ukraine

Soma - https://jamii.app/RussiaUNAmb
πŸ‘16πŸ‘Ž2😁2
JamiiForums inatangaza nafasi 10 za Wasimamizi wa Maudhui (Content Managers)

Je, unadhani unafaa? Tuma Maombi yako kupitia vacancies @ jamiiforums.com kabla ya Juni 16, 2022.

Kwa maelezo zaidi, soma - https://jamii.app/NafasiKaziJF
πŸ‘3πŸŽ‰2
KIFAHAMU KIWANJA CHA NDEGE KITAKACHOHUDUMIA ABIRIA WENGI DUNIANI

Kiwanja cha Ndege cha Istanbul kitaweza kuhudumia abiria milioni 200 kwa mwaka

Kitakuwa na maduka yatakayochukua eneo la Mita za Mraba 55,000, pamoja na Bustani na Ufukwe

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/IstanbulAirport
πŸ‘11πŸ‘1
MALI: Utawala wa Kijeshi umeahidi kurejeshwa kwa Utawala wa Kiraia ifikapo 2024 baada ya kuandamwa na vikwazo toka Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS)

> Kiongozi wa Jeshi alichukua Urais mnamo mwezi Mei, 2021

Soma - https://jamii.app/UtawalaMali

#JamiiForums
πŸ‘7πŸ‘3
MADHARA YA β€˜ENERGY DRINKS’

Vinywaji vya kuongeza nguvu β€˜Energy Drinks’ vinachangamsha mwili na akili lakini vinaweza kusababisha Shambulio la Moyo, Uraibu na Kisukari

> Inashauriwa kusoma maelekezo kabla ya kutumia

Soma - https://jamii.app/VinywajiVyaNguvu

#FoodSecurity #JFAfya
πŸ‘20😒3πŸ‘Ž2πŸ‘2😁2πŸ”₯1😱1
Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema Tanzania ni salama na haina tishio lolote la usalama hivyo Viongozi wa CHADEMA waliopo nje ya Nchi warejee ili watumie fursa zilizopo

> Waziri ametoa wito huo leo Juni 7, 2022

Soma - https://jamii.app/NchiIpoSalama

#JamiiForums
πŸ‘10πŸ€”6🀯2
TETESI: MONACO YAKUBALI KUMUUZA TCHOUAMENI KWA R. MADRID

- Inadawa usajili wa Kiungo Aurelien Tchouameni (22) utagharimu jumla ya zaidi ya Paundi Milioni 85 (Tsh. 249,405,355,250)

- Klabu za Liverpool, Manchester United na PSG zilikuwa zinamuwania pia mchezaji huyo

#JFSports
πŸ‘14
TETESI: MANCHESTER CITY YATAKA KUMSAJILI SAKA

Inadaiwa Manchester City imeongeza jitihada za kutaka kumsajili nyota wa Arsenal, Bukayo Saka

Man. City inafuatilia kwa karibu mustakabali wa Saka katika Klabu ya Arsenal ambapo amebakiza miaka miwili katika mkataba wake

#JFSports
πŸ‘13
VICTOR WANYAMA ATAJWA KWA WANAOLIPWA VIZURI

Kiungo wa Montreal Impact, Victor Wanyama anaongoza kwa kulipwa vizuri katika timu yake

Analipwa Dola Milioni 3.09 (Tsh. Bilioni 7) kwa mwaka, katika Major League Soccer anashika nafasi ya 14

Soma - https://jamii.app/WanaolipwaZaidi
πŸ‘17
UVIKO-19: MAAMBUKIZI YAONGEZEKA NCHINI

Kuanzia Mei 05 - Juni 03, maambukizi mapya 161 yamerekodiwa ikiwa ni ongezeko la 137%

Visa vimeripotiwa Dar, Arusha, Mwanza, Shinyanga, Mtwara, Dodoma, Mara, Morogoro, Simiyu, Katavi, Kilimanjaro na Mbeya

Soma > https://jamii.app/TaarifaUVIKO
πŸ‘Ž14😁2πŸ”₯1πŸ€”1
URUSI: Bunge limepitisha Miswada miwili inayomaliza Mamlaka ya Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu nchini humo, baada ya kutangaza kuwa itaondoka katika Mahakama hiyo kutokana na #RussiaUkraineWar

Soma - https://jamii.app/UrusiYajiondoaECHR

#JamiiForums
πŸ‘18❀7πŸ‘3😱2
RAIS SAMIA: MAFUTA NI JANGA LA ULIMWENGU, SI LA SERIKALI

Akizungumza na Wananchi wa Bwanga, amesema kwasababu ya Vita inayoendelea Nchini Ukraine, bei ya mafuta imepanda duniani kote

Ameeleza, "Bilioni 100 zimetolewa kufidia bei za mafuta zishuke. Tutaendelea kutoa Ruzuku mpaka duniani kukae sawa. Tutakata Bilioni 100 kila mwezi kwenye matumizi ya Serikali ili kupunguza makali"

Soma - https://jamii.app/RaisMafutaBei
πŸ‘Ž13πŸ‘12πŸ‘1
RUTO: SERIKALI INAMSAIDIA ODINGA KUSHINDA UCHAGUZI

Amelalamikia kile alichosema ni matumizi mabaya ya taarifa na huduma za kijasusi kwa manufaa ya Raila Odinga

Chama cha UDA kimesema hali hiyo inahatarisha Usalama ktk Mchakato wa Uchaguzi Mkuu

Soma - https://jamii.app/RutoGovtRaila
😁12
MDAU: Wafanyabiashara haswa wa vitafunwa wamekuwa wakitumia karatasi zenye CV, Fomu za Mikopo, Fomu za Uanachama, Mitihani na nyinginezo

> Uanikaji huo wa Taarifa Binafsi za Watu ni hatari kwa usalama wa mhusika

Soma - https://jamii.app/UlinziWaDataBinafsi

#DataProtection
πŸ‘13😁2😒2
JamiiForums inatangaza nafasi 10 za Wasimamizi wa Maudhui (Content Managers)

MAJUKUMU: Kusimamia Maudhui ya JamiiForums.com na kuhakikisha Wanachama wanazingatia Miongozo wanaposhiriki Mijadala mbalimbali

Tuma Maombi yako kupitia vacancies @ jamiiforums.com kabla ya Juni 16, 2022

Kwa taarifa zaidi - https://jamii.app/NafasiKaziJF
πŸ‘9πŸ₯°1😁1