JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
GATTUSO KOCHA MPYA WA VALENCIA

Kiungo wa zamani wa AC Milan, Gennaro Gattuso ametangazwa kuwa kocha wa Valencia

Raia huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 44 amesaini mkataba wa miaka miwili

Soma > https://jamii.app/GattusoValencia

#JamiiForums #JFSports
👍13
RAIS SAMIA: Serikali imetenga Tsh. Bilioni 20 kuboresha kilimo cha mashamba makubwa Nchini ili kuzalisha mafuta ya kula na kufikia kiwango cha kuuza mafuta nje ya nchi

> Tutapanda Alizeti na Michikichi kwa mbegu za kisasa

Soma - https://jamii.app/SamiaKagera

#JamiiForums
👍13😁9👎6
SRI LANKA: Takriban Wahandisi 900 wa Bodi ya Umeme ya Ceylon inayomilikiwa na Serikali waligoma na kusababisha uhaba wa umeme

> Wahandisi hao wanadai kuondolewa kwa vikwazo vya Ushindani wa Zabuni kwa Miradi ya Nishati Mbadala

Soma - https://jamii.app/MgomoWaWahandisi

#JamiiForums
👍6👎2
RAIS SAMIA: MSIWABAMBIKIE WANANCHI BILI ZA MAJI

Akiwa ziarani Kagera amesema "Wananchi walipe jinsi wanavyotumia, msiwabambikie Bili kufidia gharama za uendeshaji"

Ameelekeza Wizara ya Maji kutoa Mkopo wa Tsh. Milioni 500 kwa Mamlaka za Maji Wilayani Missenyi

Soma - https://jamii.app/SamiaKagera
👍17
DR CONGO YAISHUTUMU RWANDA KUTUMA VIKOSI VYAKE KINYEMELA

Jeshi limedai Wanajeshi 500 wametumwa eneo la Tshanzu Jimbo la Kivu Kaskazini linalopakana na Rwanda na kukaliwa na Waasi wa M23

Rwanda imekanusha tuhuma hizo ikisema hazina mashiko

Soma - https://jamii.app/MgogoroDRC

#JFLeo
👍12😁1
DAR: ADAIWA KUMUUA MPENZI WAKE KISHA KUJIUA

Bunaza Manyanda anadaiwa kumuua Mpenzi wake, Happiness Zakaria kwa kitu chenye ncha kali tumboni kisha naye kujiua kwa kunywa pombe, dawa ya kuua wadudu ya DUDU CRON na vidonge vya Flagyl

Soma > https://jamii.app/MauajiTemeke

#JamiiForums
😢6👍5👎31😁1
KADIRIA MLO KWA KUTUMIA MIKONO YAKO

Ukubwa wa Ngumi; Vyakula vya nafaka na mizizi. Pia kipimo kama hicho kinatakiwa kitumike katika Matunda

Viganja vya Mikono; Mbogamboga zijae kwenye mikono yote

Ukubwa wa Kiganja; Vyakula vya jamii ya kunde na vyenye asili ya Wanyama

Soma - https://jamii.app/AfyaYaChakula
👍13👏1
PUTIN: NCHI ZA MAGHARIBI HAZIWEZI KUKATAA NISHATI YETU SIKU ZOTE

Rais Vladimir Putin amedai Kampuni za Nishati ya Mafuta na Gesi zinaendelea kuchimba visima kwani zinajua Biashara itakuwepo

Faida ya Nishati Nchini Urusi imepanda licha ya vikwazo

Soma - https://jamii.app/RussiaOilGas
👏20😁8👍3🤯1
JamiiForums inatangaza nafasi 10 za Wasimamizi wa Maudhui (Content Managers)

MAJUKUMU: Kusimamia Maudhui ya JamiiForums.com na kuhakikisha Wanachama wanazingatia Miongozo wanaposhiriki Mijadala mbalimbali

Je, unadhani unafaa? Tuma Maombi yako kupitia vacancies @ jamiiforums.com kabla ya Juni 16, 2022

Kwa taarifa zaidi - https://jamii.app/NafasiKaziJF
👍6
AJALI YAUA TAKRIBAN WATU 18: Watu wapatao 18 wamefariki dunia baada ya basi dogo (Coaster) kugongana na lori la mizigo Mkoani Iringa

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ACP Allan Bukumbi amethibitisha ajali kutokea leo Juni 10, 2022

Soma - https://jamii.app/AjaliIringa

#JFLeo
😢27👍6👎2😱1
AFRIKA KUSINI: Rais Ramaphosa amemsimamisha kazi Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Ufisadi kwa shutuma za upendeleo wa kisiasa

> Aidha, Juni 8, 2022, Mkhwebane alisema amepokea malalamiko dhidi ya Ramaphosa ya kukiuka maadili ya kiutendaji

Soma - https://jamii.app/UfisadiAfrikaKusini
👍4😁2🤯2
Hukumu ya kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Lengai Ole Sabaya na wenzake inatarajiwa kutolewa leo Juni 10, 2022 ktk Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha

> Pia, watuhumiwa hao wana kesi nyingine ya Uhujumu Uchumi ktk Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi

Soma - https://jamii.app/HukumuOleSabaya
👍7👏2
Baraza Kuu la UN limeichagua Msumbiji pamoja na Ecuador, Japan, Malta na Uswisi kuwa Mwanachama asiye wa Kudumu wa Baraza la Usalama la UN kwa miaka miwili kuanzia Januari 2023

> India, Ireland, Kenya, Mexico na Norway zimemaliza muda wao

Soma - https://jamii.app/MsumbijiUNSC
👍18👏2🤩1
WAZIRI MKUU: HAKUNA MAPAMBANO YA WAFUGAJI NA ASKARI LOLIONDO

Akiwa Bungeni, amekanusha tetesi za mapigano kati ya Askari na Wafugaji huko Loliondo zilizosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii

Amesema "Tulipokuwa tunapitisha magari kuelekea msituni, Viongozi wa Kijiji cha karibu ndio waliorekodi video ya kutaka ionekane kuna tatizo Loliondo, ndio maana katika video huyo huoni kama kuna askari yeyote anatishiwa mshale"

Soma - https://jamii.app/MajaliwaMgogoroLoliondo

#JamiiForums
👍16👎6👏1
WAZIRI MKUU: ILI KUPUNGUZA IDADI YA WATU, WENGINE TUTAWAHAMISHIA HANDENI

Amesema kutokana na ongezeko la Watu Loliondo, Serikali imefanya vikao na Wananchi na kujadiliana ni kwa namna gani watapunguza idadi ya Watu, Mifugo na Ujenzi Holela

Ambao wataridhia watahamishiwa Handeni, Tanga na hadi kufikia Juni 9, 2022, Kaya 263 zenye Watu 1497 zilijiandikisha kuwa tayari kuhama

Soma - https://jamii.app/MajaliwaMgogoroLoliondo
👍8👏5😢2
WAZIRI MKUU: HATUTAWAONEA AIBU WACHONGANISHI

Akitoa taarifa kuhusiana na mgogoro kati ya Wananchi wa Loliondo na Serikali, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa kuna Taasisi zilizosajiliwa na Serikali kufanya shughuli za uhifadhi lakini katika hili kazi yao imekua ni upotoshaji na uchonganishi

Soma - https://jamii.app/MajaliwaMgogoroLoliondo
👍8👏2
TETESI: MAN. UTD YAANGALIA UWEZEKANO WA KUMSAJILI CHAMBERLAIN

Inadaiwa Manchester United inataka kumsajili Alex Oxlade-Chamberlain (28) anayedaiwa kutaka kuondoka Liverpool

Timu hiyo inahitaji Viungo wapya baada ya kuondoka kwa Paul Pogba, Juan Mata na Nemanja Matic

#JFSports
👍9👎4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Ishi kwa ajili yako, usiwaige wengine!
👍26🤩1
SABAYA NA WENZAKE WAACHIWA HURU

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewaachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake sita waliokuwa wanakabiliwa na Kesi ya Uhujumu Uchumi. Imesema ushahidi uliotolewa na Mashahidi wa upande wa Jamhuri ulikuwa na utata

Sabaya, Sylvester Nyegu, John Aweyo na Nathan Msuya watabaki Mahabusu kutokana na Kesi nyingine waliyonayo

Soma - https://jamii.app/KesiSabayaLeo

#JamiiForums
💩23😁14👍13👎11
Inaelezwa kuwa, Angel's Trumpet ni hatari kwa Binadamu na Wanyama, na umakini unahitajika ikiwa Mmea huo utapandwa nyumbani. Inashauriwa kuwa katika maeneo ambayo si rahisi kufikiwa na Watoto

Sehemu zote za Mmea huo zina sumu na ikiwa imekuathiri, baadhi ya dalili zake ni kutapika, ugumu kupumua, homa na hali ya kuchanganyikiwa

#JamiiForums #JFMaarifa
🤔10👍4😢4🔥3