JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TAKRIBAN WATU 4,000,000 WAKABILIWA NA UHABA WA CHAKULA NCHINI KENYA

Idadi hii inatajwa kuongezeka kutoka zaidi ya watu 3,000,000 mwaka jana

> Aidha, zaidi ya Watoto 900,000 walio chini ya umri wa miaka mitano wamegundulika kuwa na utapiamlo

Soma - https://jamii.app/NjaaKenya
πŸ‘6πŸ‘Ž1
JELA MAISHA KWA KUMLAWITI MTOTO WA DADA YAKE

Ramadhan Musa Chewa (34), Mkazi wa Iringa amehukumiwa kwa kosa la kumuingilia kinyume na maumbile Mtoto wa kike wa dada yake mwenye umri wa miaka 12

> Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Aprili 4, 2020

Soma - https://jamii.app/JelaKwaKulawiti
πŸ‘6πŸ‘1
MDAU: USINUNUE VITU VYA THAMANI KWENYE NYUMBA YA KUPANGA

Anashangazwa na wanaokimbilia kununua mali za gharama kubwa ilihali bado wanapanga. Anashauri kuwa na mahitaji muhimu, huku kipato kingine kikielekezwa kwenye kiwanja ili ujenge

Unakubaliana na mtazamo wake kuwa kujenga ni ishara ya mafanikio katika maisha? Nini maoni yako?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/VituNyumbani
πŸ‘40πŸ‘4
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Tunawatakia wote weekend njema!
πŸ‘15❀7
UKRAINE: Wanasayansi wanasema mvua katika Mji wa #Mariupol inaweza kusababisha mlipuko wa Kipindupindu

Meya wa Mji huo, Vadym Boichenko amesema maji ktk baadhi ya visima ni machafu, na ikiwa Mlipuko utatokea maelfu ya watu wanaweza kupoteza maisha

Soma > https://jamii.app/KipindupinduUkraine
πŸ‘10😒3
MAREKANI: CHINA INAZIDI KUTUMIA MABAVU NA FUJO

Waziri wa Ulinzi, Lloyd Austin amesema Marekani itasimama na Washirika wake, ikiwemo Taiwan

Uhusiano kati ya China na Marekani umekuwa tete miezi ya hivi karibuni, kutokana na mivutano kwenye masuala kadhaa yakiwemo Taiwan na Haki za Binadamu

Soma - https://jamii.app/ChinaUsTaiwan
πŸ‘14πŸ”₯3
MAREKANI: KANUNI YA WASAFIRI WA KIMATAIFA KUPIMA COVID-19 YAONDOLEWA

Kanuni ya upimaji kwa Wasafiri wa Anga wanaoingia kutoka nje ya Nchi itaondolewa kuanzia Juni 12, 2022

Mashirika ya Ndege na wadau wengine wamekuwa wakishinikiza iondolewe

Soma - https://jamii.app/USTestsCOVID
πŸ‘15
MONGELLA: ASKARI AMEUAWA LOLIONDO

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema tukio hilo limetokea Alasiri ya Juni 10, 2022, baada ya askari huyo kuchomwa mshale

> Amesema imetokea baada ya Waziri Mkuu kuhutubia Bunge

Soma - https://jamii.app/MgogoroLoliondo

#JamiiForums
πŸ‘22πŸ€”4😁1
Unafahamu hapa ni wapi?
πŸ‘14
Kamanda Jumanne Muliro amesema kutokana na mwendelezo wa matukio ya kikatili inawezekana kuna tatizo kubwa zaidi katika jamii kuliko inavyofikiriwa

> Je, unadhani nini kifanyike ili kupunguza matukio ya ukatili katika jamii zetu?

Soma - https://jamii.app/MatukioYaUkatili
πŸ‘22πŸ”₯2
MAREKANI: Kesi ya kudaiwa kumbaka Kathryn Mayorga iliyokuwa ikimkabili nyota wa Manchester United, Cristiano Ronaldo imefutwa baada ya Jaji Jennifer Dorsey kusema nyaraka za ushahidi zilipatikana isivyo halali

Soma - https://jamii.app/CR7Mahakamani

#JamiiForums
πŸ‘26😁9🀬2πŸ”₯1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Vitendo vya Rushwa, Urasimu na Ubadhirifu vinarudisha nyuma maendeleo ya Wananchi na Taifa kwa ujumla, na wote tunawajibika kuvikemea

#JamiiForums #KemeaRushwa
πŸ‘11
MBEYA: Mwili wa Padre Michael Samson wa Shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers') aliyetoweka Ijumaa Juni 10, 2022 umekotwa kando ya Mto Meta jijini humo

> Mashuhuda wamesema mwili huo ulikuwa umefungwa kwenye blanketi

Soma - https://jamii.app/PadreAfarikiMbeya

#JFMatukio
😒14πŸ‘Ž5πŸ‘4😁1
ILO: UMASIKINI UNACHANGIA TATIZO LA AJIRA KWA WATOTO

Bila kuwepo Mikakati, Shirika la Kazi Duniani (ILO) linakadiria idadi ya Watoto wanaotumikishwa inaweza kuongezeka kwa Milioni 8.9 ifikapo mwisho wa 2022

Juni 12 ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ajira kwa Watoto. Japokuwa hatua kubwa zimepigwa kupunguza tatizo hili, bado Watoto Milioni 160 Duniani wapo katika Ajira

Soma - https://jamii.app/ILOWatoto

#EndChildLabour
πŸ‘10😁2πŸ€”2
DAR: Zheng Lingyao (Me) anatafutwa kwa tuhuma za kumuua Fu Nannan (Me) na kumjeruhi Nie Mnqin (Ke) wote ni raia wa China

> Tukio lililotokea jana Juni 11, 2022, chanzo kikitajwa kuwa ni mgogoro wa kimapenzi

Soma - https://jamii.app/MauajiYaWachina

#JamiiForums
😒15πŸ‘4πŸ‘Ž2😱2
TUNISIA: Polisi wanadaiwa kumshikilia Mwanahabari, Salah Atiyah kwa kudai kwamba, Rais Kais Saied alilitaka Jeshi kufunga Makao Makuu ya Chama cha Wafanyakazi cha UGTT na kuwafunga Viongozi wa Upinzani kifungo cha nyumbani

Soma - https://jamii.app/PressFreedomTunisia
πŸ‘5πŸ‘Ž1
β€œKODI YA HUDUMA ZA KIDIGITALI” NI NINI?

Kodi ya Huduma za Kidigitali (Digital Service Tax) hutozwa kwa Kampuni kulingana na Mapato yao kutokana na shughuli zao za Kidigitali katika Nchi husika. Kawaida, hutozwa kwa kampuni za kimataifa

Nchi nyingi zilikubaliana kuahirisha mfumo wa DST mpaka mwaka 2024 wakati Mfumo unakamilishwa. DST ilitajwa kama kikwazo kwenye Biashara ya Kidigitali

#DigitalServiceTax #DigitalRights
πŸ‘5πŸ€”2
KODI YA HUDUMA ZA KIDIGITALI HUTOZWAJE?

Kodi hii hutozwa kwenye Mapato ghafi ya Kampuni bila kujali gharama zilizotumika kuzalisha Mapato hayo

Biashara nyingi zina Mapato yanayotosha kulipa gharama, na mara nyingine gharama zinazidi mapato yanayopatikana

#DigitalServiceTax #DigitalRights
πŸ‘6🀯1
KWANINI TANZANIA IMEFIKIRIA KUTOZA KODI HUDUMA ZA KIDIGITALI?

1) Nchi inahamia digitali hivyo ni muda sahihi kutambulisha kodi hiyo

2) Kuongeza wigo wa kodi badala ya kuendelea kutoza kwenye vyanzo vilivyopo

#DigitalServiceTax #DigitalRights
🀯10πŸ‘9
POCHETTINO KUONDOKA PSG

Kocha Mauricio Pochettino amekubali kusitishwa kwa mkataba wake ndani ya Paris Saint-Germain

> Wanaopewa nafasi ya kurithi mikoba ni Zinedine Zidane, Jose Mourinho na Christophe Galtier

Soma - https://jamii.app/PSGKocha

#JamiiForums
πŸ‘10😁1