JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kikosi cha Urusi kimefanya mashambulizi makubwa Nchini Ukraine na kusababisha uharibifu katika ghala la silaha ambazo taifa hilo ilizipata kutoka kwa Marekani na Nchi za Ulaya

> Mashambulizi yamefanyika katika Mji wa Ternopil

Soma - https://jamii.app/KomboraUkraine

#JamiiForums
👍22😢12👏5🔥2😁2
IMF KUIKOPESHA TANZANIA TSH. 2,400,000,000,000

Mkopo huo ambao ni kupitia Kitengo cha Mikopo ya Dharura unalenga kuendeleza Uchumi wa Nchi uliodumazwa na Janga la #COVID19

> Pia, unakusudiwa kuboresha mazingira ya Biashara na Ushindani

Soma - https://jamii.app/TanzaniaYakopaIMF

#JamiiForums
👎24👍13😁3
AFRIKA KUSINI: Idadi ya waliofariki kutokana na Mafuriko na Maporomoko ya Ardhi yaliyosababishwa na mvua ya Aprili 2022 imefikia 461 huku Watu 87 wakiwa hawajulikani walipo

> Nyumba 27,000 na Watu 85,280 waliathiriwa na mvua hizo

Soma - https://jamii.app/87PeopleAreMissingInDurban
👍6👎4
Bajeti ya Serikali inatakiwa kumsaidia Mfanyabiashara kujua namna ya kufanya biashara baada ya kuona mabadiliko ya Kodi, Tozo na Ushuru

Pia, inatakiwa kumsaidia Mwananchi kujua vipaumbele vya Serikali na namna ya kutumia fursa hizo

Juni 14, 2022 Waziri wa Fedha na Mipango atasoma Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2022/23. Je, unafahamu umuhimu gani wa Bajeti ya Serikali?

Soma - https://jamii.app/Bajeti2023

#Bajeti2023
👍9
JamiiForums inatangaza nafasi 10 za Wasimamizi wa Maudhui (Content Managers)

MAJUKUMU: Kusimamia Maudhui ya JamiiForums.com na kuhakikisha Wanachama wanazingatia Miongozo wanaposhiriki Mijadala mbalimbali

Je, unadhani unafaa? Tuma Maombi yako kupitia vacancies @ jamiiforums.com kabla ya Juni 16, 2022.

Kwa taarifa zaidi - https://jamii.app/NafasiKaziJF
👍7
RAIS SAMIA: BIASHARA ZIFANYWE NA SEKTA BINAFSI

Amesema tangu achukue madaraka, Sera imekuwa ni kuacha Serikali iongoze na Sekta Binafsi ifanye Biashara

Amesisitiza, "Namaanisha nikisema hakuna Biashara zaidi kwa Serikali, sisi tunatengeneza mazingira rafiki kwa ajili ya Sekta Binafsi kukua"

Soma - https://jamii.app/RaisBiashara
👏12👍6
Naibu Spika wa Bunge amesema ktk Mjadala wa Bajeti Kuu, Mbunge hataruhusiwa kutoa taarifa na atakayekaidi ataadhibiwa chini ya kifungu 84 au 85 cha Kanuni za Bunge

> Amesema kuna baadhi ya Wabunge hutumia kutoa taarifa ili kupoteza muda

Soma - https://jamii.app/WabungeWakemewa

#JFSiasa
👍7
RAIS SAMIA: Kuna Nchi zinakuja kuvua kwenye eneo la Tanzania na hatuwezi kuwafukuza kwa sababu hatuna vifaa

> Hili ni eneo lingine ambalo Tanzania na Oman zinaweza kushirikiana kwa pamoja. Pia, uwepo kwa Vyombo vya Usafirishaji wa Majini ili kusafirisha Wanyama walio hai na bidhaa mbalimbali kwenda Oman utaboresha biashara kati ya Tanzania na Oman

Soma - https://jamii.app/BiasharaOmanTz
👎15👍9
WANAOIKOSOA KODI YA HUDUMA ZA KIDIGITALI WANA HOJA GANI?

1) Digital Service Tax (DST) inatajwa kuathiri Wajasiriamali na uwepo wake umeonekana kuwa kikwazo

2) Kodi hii huongeza Mapato kidogo kuliko inavyotabiriwa

3) Inaweza kuwagusa Watumiaji katika Nchi husika

#DigitalServiceTax #DigitalRights
👍1🤔1
KODI YA HUDUMA ZA KIDIGITALI INAMUATHIRI VIPI MWANANCHI?

Kampuni nyingi huona upenyo wa kuweza kupitishwa (na hupitisha) kodi hii kwa Watumiaji wa mwisho

Hii inamuumiza mwananchi wa kawaida bila yeye kujua. Hivi ndivyo ilivyokuwa katika Masoko makubwa kama vile Uingereza na Ufaransa

#DigitalServiceTax #DigitalRights
👍2
MDAU: Kuna tabia ya baadhi ya Walimu wa Shule za Msingi za English Medium kutowaelewesha vizuri Wanafunzi na kuwapa kazi za kufanyia nyumbani ili wakafundishwe na Wazazi au Walezi wao

> Anahoji "Kwanini hawawafundishi ndipo wawape hizo homework?"

Soma - https://jamii.app/TabiaYaWalimu
👍8😁2
MUSEVENI ALAUMU TAWALA ZILIZOPITA KWA UMASIKINI

Amesema Wakoloni na Tawala zilizopita ndio wa kulaumiwa kwa viwango vya juu vya Umasikini katika Taifa hilo

Amedai Wakoloni walitia sumu akili za Wakulima kwa kuwafanya walime mazao waliyotaka

Soma - https://jamii.app/PovertyUG
🤔9👍8👎5😁5👏1🤯1🤩1🤮1
KENYA: JAJI MKUU ATAKA KENYATTA AONDOLEWE MADARAKANI

Jaji amesema Rais Kenyatta alikiuka Katiba baada ya kukataa kuteua Majaji 6 miongoni mwa 40 walioidhinishwa na Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) miaka mitatu iliyopita

Soma - https://jamii.app/KenyaSiasa

#JamiiForums
👍12😁1
PITSO MOSIMANE AACHANA NA AL AHLY

Kocha huyo ameachana rasmi na Klabu ya Al Ahly kwa makubaliano ya pande zote mbili

Ameiandikia Bodi barua akiomba kuondoka baada ya kuwaongoza kupata mafanikio makubwa kwenye michuano mbalimbali

Soma > https://jamii.app/MosimaneResignAlahly

#JFSports
👍16👏1
DST IMEFUTWA NCHI NYINGI, NI KENYA PEKEE IMEIBAKIZA

Kodi ya Huduma za Kidigitali (DST) inatajwa kuwa kandamizi kwa Maendeleo ya Ubunifu, na kwa Vijana wanaotegemea Sekta ya Digitali kujiajiri

Nchi nyingi zilizokuwa na Kodi za namna hii zimeshaziondoa na Nchi pekee iliyobaki ni Kenya. Jitihada za Serikali ya Kenya kuongeza Kodi hii kutoka 1.5% mpaka 3% ziligonga mwamba Bungeni

#DigitalServiceTax #DigitalRights
👍5
BURKINA FASO: WATU 50 WAMEUAWA KTK SHAMBULIZI

Washambuliaji wenye ukaribu na Vikundi vya Al-Qaeda na ISIL (ISIS) ndio waliodaiwa kutekeleza shambulio hilo

> Inadaiwa tangu mwaka 2015 zaidi ya Watu 2,000 wameuawa ktk matukio kama hayo

Soma - https://jamii.app/50KilledBurkinaFaso
👍6😢4😱1
Jeshi la DR Congo limeishutumu Rwanda kwa uvamizi baada ya Waasi wa M23 kuuteka Mji Muhimu wa Bunagana uliopo mpakani mwa Nchi hiyo na Rwanda

> Aidha, Rwanda imekuwa ikikataa kuwasaidia Waasi wa M23 kwa muda mrefu sasa

Soma - https://jamii.app/M23SeizesBunagana

#JamiiForums
👍8😁1
Dkt. Mwigulu Nchemba (Waziri wa Fedha na Mipango): Ukuaji wa Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2021 ulikua kwa 4.9% ikilinganishwa na ukuaji wa 4.8% mwaka 2020

> Ongezeko limetokana na jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo uwekezaji wa kimkakati ktk Miundombinu ya Nishati, Maji, Afya, Elimu

#JamiiForums
👎5👍4😁3
Dkt. Mwigulu Nchemba: Mfumuko wa Bei ulifikia wastani wa 3.8% Aprili 2022 ikilinganishwa na 3.3% Aprili 2021

> Kuongezeka kwa Mfumuko wa Bei kulichangiwa na sababu zilizo nje ya udhibiti wa kibajeti/kisera zikiwemo kuvurugika mnyororo wa uzalishaji na usambazaji bidhaa

#JamiiForums
👍7👎4
DKT. MWIGULU: 2022/23 NGUVU KUBWA ITAELEKEZWA SEKTA ZA UZALISHAJI

Waziri wa Fedha amesema katika kutekeleza Mpango wa 2022/23, msukumo mkubwa utawekwa katika Sekta za Uzalishaji ambazo ni Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Nishati kwani Sekta hizi ndizo zinazochochea uzalishaji na huzalisha ajira zinazowagusa Wananchi wengi"

#JamiiForums
👍52