JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Baadhi ya yaliyojadiliwa katika Mjadala na Wataalamu kuhusu Saratani kwa Watoto uliofanyika kupitia Clubhouse ya JamiiForums

#JFAfya
DAR: Maila Majula (29) Mkazi wa Makongo Juu, anashikiliwa na Polisi kwa kudanganya kuibiwa Gari aina ya Toyota IST

Uchunguzi ulibaini alipewa Tsh. Milioni 10 na Kaka yake ili akaziweke Benki ila alizitumia na kuamua kutengeneza tukio hilo

Soma - https://jamii.app/AjifanyaPolisi

#JFMatukio
KESI YA MBOWE: UPANDE WA MASHTAKA WAFUNGA USHAHIDI

Wakili wa Serikali, Robert Kidando amesema "Baada ya Ushahidi wa Shahidi wa 13 tunaialika Mahakama ione Washtakiwa wote 4 wana Kesi ya kujibu hivyo hatua nyingine kwa ajili ya kujitetea ifuate"

Soma - https://jamii.app/MboweKesiUshahidi

#JFSiasa
NAPE: HAKUNA WIZI KWENYE 'BUNDLE' ZA SIMU

Amesema, "Malalamiko kwamba kuna 'Bundle' zinatumika bila Mtumiaji kuzitumia yamekuwepo. Uchambuzi umefanyika na Matokeo yanaonesha hakuna wizi uliotokea, isipokuwa kuna tatizo la matumizi ya simu za kisasa"

Soma - https://jamii.app/WiziBandoSimu

#DigitalRights
SERIKALI YASEMA MSIMAMO KUHUSU 'EPA' UKO PALEPALE

Serikali imekanusha suala la kusaini Economic Partnership Agreement 'EPA'

> EPA ni makubaliano yatakayoruhusu nchi za Ulaya kuingiza bidhaa ktk nchi zinazoendelea bila kutozwa kodi

Soma https://jamii.app/TanzaniaEPA
#JFUchumi
TABORA: Jeshi la Polisi limekamata Watu 9 ambao wametajwa kuhusika na tuhuma za Mauaji na mauziano ya viungo vya Binadamu

Huwachoma Watu na kitu chenye ncha kali Shingoni na kukinga Damu ambayo hununuliwa kwa Tsh. 600,000 kwa chupa.

Soma - https://jamii.app/SehemuZaSiri

#HumanRights #JFMatukio
RIPOTI: UCHAFU HUSABABISHA TAKRIBAN VIFO MILIONI 9 KILA MWAKA

Ripoti ya UN imesema uchafuzi husababisha vifo vingi Duniani kuliko hata vitokanavyo na COVID-19

Uchafuzi umetajwa kusababisha ukiukwaji wa Haki ya kuishi katika Mazingira safi

Soma - https://jamii.app/PollutionDeaths

#JFAfya
UTAFITI: WAENDA KWA MIGUU HUKWEPA MADARAJA KUTOKANA NA UREFU

Wanaovuka Barabara hukwepa kutumia Madaraja kutokana na urefu wa Madaraja, hofu ya Wizi na Uporaji

Hali hiyo ni changamoto kwani 30% ya Ajali zinazotokea zinahusisha watembea kwa Miguu

Soma - https://jamii.app/MadarajaYaJuu
KENYA: MWANAFUNZI MBARONI KWA KUMTUMIA MUME PICHA ZA FARAGHA ZA MKEWE

Stephen Kamande anakabiliwa na Mashtaka ya kutuma picha za utupu zinazodaiwa kuchukuliwa akiwa faragha na Mke wa Mtu

Pia anashtakiwa kwa kumsumbua Mwanamke huyo na kumtishia kifo

Soma https://jamii.app/StudPicsKE

#DataPrivacy #DataProtection
Rais wa #Algeria, Abdelmadjid Tebboune amesema Serikali itaanza kuwalipa Vijana wasio na Ajira kila Mwezi dinari 13,000 (Tsh. 230,000) kuanzia Machi 2022

Pia, Vijana hao watanufaika na Bima ya Afya na kuondolewa Kodi kwenye baadhi ya Bidhaa

Soma - https://jamii.app/UnemploymentBenefits

#Governance
👍1
MOROGORO: MTOTO AUAWA KWA MAPANGA NA BINAMU YAKE

Faidhati Ibrahim (13) ameuawa kwa kukatwa na mapanga na Kaka yake ambaye ni Binamu aitwaye Shomari Malima

Ugomvi kati ya Mama wa Marehemu na Mama wa Mtuhumiwa umetajwa kuwa sababu

Soma - https://jamii.app/MtotoMauaji

#JFMatukio
MAGONJWA YA AFYA YA AKILI YANATIBIKA NA KUEPUKIKA, TUVUNJE UKIMYA

Mdau anasema Jamii inapaswa kuwaonyesha Upendo wenye Matatizo ya Afya ya Akili na kutowatenga. Pia, kuwepo utaratibu wa kuwasaidia katika mahitaji yao ya msingi ikiwemo kuwapeleka kupata huduma

Soma - https://jamii.app/AfyaAkiliSOC

#StoriesOfChange #JFAfya
SARATANI: Takwimu za Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC) na Shirika la Afya (WHO) Mwaka 2020 zinaeleza ongezeko la Visa vipya vya Saratani linakadiriwa kufikia Milioni 19.3, huku Vifo vikiwa Milioni 10

Ulimwenguni kote, inakadiriwa Visa vipya Milioni 28.4 vya Saratani vinaweza kutokea hadi kufikia Mwaka 2040, huku ongezeko kubwa likiwa katika Ukanda wa Nchi zinazoendelea

#JamiiForums #Cancer #JFData
TANZANIA KUFANYA MAKUBALIANO YA KUTENGENEZA NDEGE NDOGO

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema kipo ktk hatua za mwisho za majadiliano na Kampuni ya #Skyleader inayotengeneza Ndege ndogo ili ifanye Uwekezaji wa Ndege hizo Nchini Tanzania

Soma - https://jamii.app/Ultralight
#COVID19: Shirika la Afya (WHO) limesema Maambukizi vya Corona yamepungua kwa 19% Wiki iliyopita. Visa vipya Milioni 16 na Vifo 75,000 viliripotiwa kuanzia Februari 7 - 13, 2022

Virusi aina ya Alpha, Beta na #Delta vinaendelea kupungua

Soma - https://jamii.app/WHOCovid

#UVIKO3
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema baadhi ya Watanzania walijifanya Wagonjwa wa COVID-19 na kwenda kutibiwa #India lakini walikuwa wakibeba #DawaZaKulevya

Watumishi wa Afya wametakiwa kuwa makini wanapotoa vibali

Soma - https://jamii.app/CoronaDawaZaKulevya

#JFMatukio