JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MALEZI: UDHALILISHAJI WA MTOTO KWA NJIA YA MANENO

Udhalilishaji kwa njia ya maneno unatokea pale ambapo Mzazi/Mlezi au Mtu aliye karibu na Mtoto anapotumia maneno yenye kumuumiza Mtoto Kihisia

Baadhi ya maneno ni; Kumkemea au kumkaripia mbele ya hadhara ya Watu au Familia/Ndugu. Kumuita Mtoto majina mabaya (Matusi) na majina mengine ikiwemo majina ya Wanyama

Soma - https://jamii.app/AbuseWordsChild
#Malezi #ChildViolence
Novemba 29, 2021, Taasisi ya WAJIBU ilizindua kitabu kiitwacho "Principles of Public Sector Auditing - The Case of SAI Tanzania" Jijini Dar es Salaam
-
Kitabu hicho kilizinduliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emanuel Tutuba kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba
-
Kitabu hicho kimeandikwa na CAG mstaafu na Mkurugenzi Mtendaji wa WAJIBU, CPA. Ludovick Utouh.

#JamiiForums #JFUwajibikaji
Taarifa binafsi ni taarifa zozote zinazohusiana na Mtu na ambazo zinaweza kumtambulisha Mmiliki wa taarifa hizo

Hizi ni taarifa ambazo Mtu anapaswa kuwa makini katika Matumizi yake ili kuepuka uwezekano wa kutumika vibaya

#JamiiForums #PersonalDataProtection
HOJA: JE, UMEWAHI KUFANYIWA 'BULLYING' KWENYE MAISHA YAKO?

'Bullying' ni aina ya Unyanyasaji unaofanywa hasa na Watoto na unaweza kujidhihirisha kwa kusukumwa ovyo, kupigwa, kuitwa majina yasiyofaa, matusi au vitisho. Hali hii huweza kumuathiri Mtoto Kisaikolojia na Kihisia

Je, umewahi kufanyiwa 'Bullying' kutokana na maumbile au mwonekano wako? Uliathirikia kwa namna gani na umewezaje kupambana na athari hizo?

Mjadala - https://jamii.app/AthariBullying

#Bullying
DKT. GWAJIMA: VIONGOZI WASIOCHANJA WAACHIE NGAZI

Waziri wa Afya atoa wito huo akisema Viongozi hao hawatetei msimamo wa Serikali kwani hata Rais amechanja

Asema hawawezi kuwa na hamasa ya kusimamia kampeni ya uchanjaji dhidi ya #COVID19

Soma - https://jamii.app/ViongoziChanjo

#UVIKO3
MAREKANI: TRUMP AIOMBA MAHAKAMA KUZUIA BUNGE KUPATA TAARIFA ZAKE

Rais wa zamani wa Marekani ameiomba Mahakama ya Rufaa kuzuia Wabunge wanaochunguza ghasia za Januari 6 katika jengo la Bunge kupata taarifa za mazungumzo yake ya wakati huo

Soma - https://jamii.app/TrumpDataBunge
#JFLeo
Desemba 1 kila Mwaka ni Siku ya UKIMWI Duniani ambao uligundulika kwa mara ya kwanza Mwaka 1988. Takwimu mbalimbali zinaonesha Vijana ndio kundi linaloathirika zaidi

Kaulimbiu ya Mwaka 2021 inasema, "Komesha ukosefu wa usawa. Komesha UKIMWI. Komesha Magonjwa ya milipuko"

Umoja wa Mataifa unalenga kukomesha janga hili ifikapo 2030

#WorldAIDSDay2021 #JamiiForums
ZIMBABWE: WASAFIRI WA KIMATAIFA WATAKIWA KUKAA KARANTINI

Wasafiri wanaoingia Nchini humo watatakiwa kupimwa #COVID19 na kukaa Karantini kwa gharama zao

Serikali imeweka amri ya Raia kutokuwa nje kuanzia saa tatu usiku hadi saa 12 asubuhi

Soma - https://jamii.app/ZimbabweCurfew

#UVIKO3
USIWE SEHEMU YA UPOTOSHAJI KUHUSU COVID-19 NA CHANJO

Kufuatia usambaaji wa taarifa zisizo sahihi, Shirika la Afya Duniani (WHO) linashauri kila mmoja kuepuka kuwa sehemu ya upotoshaji

Taarifa za kupotosha zinaweza kueneza wasiwasi na hofu

Soma https://jamii.app/ChanjoUpotoshaji

#UVIKO3
UZALISHAJI WA POMBE YA BANANA WASITISHWA KWA KUTOKIDHI VIWANGO VYA UBORA

Uchunguzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) umebaini haifai kwa matumizi ya binadamu kutokana na kuongezewa kiwango kikubwa cha kemikali ya Asetic Acid

Soma - https://jamii.app/BananaMarufuku

#JFLeo
MICHEZO: Timu ya #Tanzania ya Watu wenye Ulemavu, Tembo Warriors imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Soka ya Bara la Afrika kwa wenye Ulemavu (CANAF 2021)

Imepata tiketi ya kushiriki Mashindano ya Dunia yatakayofanyika Uturuki 2022

Soma - https://jamii.app/KombeDunia2022

#JFSports
Rushwa ya Ngono inapotolewa Ofisini au sehemu za kutolea huduma husababisha madhara ikiwemo kukwamisha upatikanaji wa Haki, mtendewa kukosa huduma muhimu, kuongeza idadi ya wenye Magonjwa ya Zinaa

Vilevile Rushwa ya Ngono inadhoofisha nguvu kazi ya Wanawake, kuwakosesha Wanawake na Wasichana kipato binafsi, na kuzorotesha Maendeleo na Uchumi wa Nchi

Soma - https://jamii.app/RushwaMapenzi
#16DaysOfActivism
MSUMBIJI: VIJANA ZAIDI YA 100 WATEKWA NA WAPIGANAJI

Watu wenye silaha wamewateka nyara zaidi ya vijana katika Kijiji cha Naulala kilichopo Mkoa wa Niassa na kuchoma makazi

Taifa hilo limekuwa likikabiliana na waasi tangu Oktoba mwaka 2017

Soma - https://jamii.app/Msumbiji100
#JFLeo
Ili kuzuia Ukatili wa Kingono kwa Watoto, Mzazi/Mlezi hakikisha unadhibiti maudhui anayotazama kwenye Televisheni

Mshiriki wa 'Stories Of Change' anasema anasema mzuie Mtoto kuhudhuria Ngoma za mikesha (vigodoro) kwakuwa zinachochea vitendo vya Ngono. Tambua mazingira anayocheza Mtoto pamoja na anaocheza nao kama ni salama kwake

Ikiwezekana Mtoto asilale na wageni waliomzidi umri mkubwa Chumba kimoja

Soma - https://jamii.app/UkatiliKingonoSOC

#StoriesOfChange
Baadhi ya Wachangiaji ndani ya JamiiForums wamezua Mjadala kuhusu 'Homeworks' nyingi wanazopewa Watoto toka Shuleni hasa kipindi cha likizo

Baadhi wanaona ni jambo la manufaa kwani humpa nafasi Mzazi kushiriki katika maendeleo ya Mtoto huku wengine wakiona ni kumtesa Mtoto kipindi anachotakiwa kupumzika

Ikiwa wewe ni Mzazi, Mlezi au Mwalimu ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika Desemba 2, 2021 kupitia Clubhouse

#JamiiForums #Malezi
Takwimu zilizokusanywa na UNITAID na WHO kwa pamoja zinaonesha kati ya Mwaka 2015 na 2020, idadi ya Nchi zilizo na Sera za kujipima VVU imeongezeka kutoka Mataifa 6 hadi 88 - na Mataifa mengine 31 yanaandaa Sera hizo

Kujipima VVU kumesaidia kufikia idadi ya Watu wengi wakiwemo Wanaume na Vijana ambao wana uwezekano mdogo wa kufika Vituo vya Afya na walikuwa na viwango vya chini vya upimaji.

#WorldAIDSDay #JamiiForums
MDAU: MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUEPUKA TALAKA

Kutopuuza shida na haja za Mwenza wako hata kama ni mambo madogo madogo

Anashauri kuepuka mazingira yote yanayoweza kufanya utumbukie katika vishawishi vya kuvunja uaminifu

Anasisitiza kuepuka kuanzisha mijadala itakayoleta mabishano yasiyo ya lazima

Soma Makala yake - https://jamii.app/NdoaTalaka

#StoriesOfChange
WHATSAPP NA iMESSAGE ZABAINIKA KUTOA TAARIFA NYINGI ZA WATUMIAJI

Kwa maombi ya kawaida, #WhatsApp huwatumia FBI taarifa kila baada ya dakika 15 hata kwa watumiaji wa iPhone

Signal na Telegram zimetajwa kutotoa taarifa nyingi

Soma - https://jamii.app/TaarifaWatumiaji

#DataProtection