JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) limetoa Onyo kwa wanaotumia Nembo ya Baraza hilo kupotosha Misamiati ya #Kiswahili na kusambaza Mtandaoni

Atakayebainika atalipa faini isiyopungua Milioni 5 au kifungo Miaka 3 jela ama vyote kwa pamoja

Soma - https://jamii.app/UpotoshajiBAKITA
#Lugha
Unatamkaje neno 'Nakupenda' kwa lugha ya Kabila lenu?

#JamiiForums #Maisha #Lugha
1👍1
🔥3🤣31😁1
Pamoja na utaalamu wako wa kuzungumza Lugha fulani kwa Ufasaha, inawezekana kuna Neno au Maneno yanakutatiza kutamka mpaka sasa

Tuambie Mdau, huwa unakwama kutamka Neno gani mara kwa mara?

#JamiiForums #Lugha #JFLugha
Siku ya Kimataifa ya Tafsiri huadhimishwa Septemba 30 kila Mwaka ikiwa na lengo la kuwaenzi Wataalamu wa Lugha, kuyaleta Mataifa Pamoja, Kuwezesha Mazungumzo, Maelewano na Ushirikiano, Kuchangia Maendeleo na Kuimarisha Amani na Usalama Duniani

Mei 24, 2017, Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) lilipitisha azimio namba 71/288 kuhusu wajibu wa Wataalamu wa Lugha katika kuunganisha Mataifa na hivyo ikatangazwa Septemba 30 kuwa Siku ya Kimataifa ya Tafsiri

Soma https://jamii.app/ITD2023

#JamiiForums #SikuYaWatafsiri #Lugha #InternationalTranslationDay #ITD2023
👏2
Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Mama husherehekewa Februari 21 kila Mwaka ili kukuza utofauti wa #Lugha na Tamaduni na kuhamasisha ufahamu wa urithi wa Lugha na Tamaduni Duniani kote

Siku hii inakumbuka Maandamano ya Watumiaji wa Lugha ya Kibengali Mwaka 1952 Nchini #Bangladesh, ambapo Wanafunzi na wanaharakati walitaka kutambuliwa kwa Lugha yao mama kama moja ya Lugha rasmi (Kibengali)

Je, unaijua Lugha Mama yako?

Soma https://jamii.app/LughaMama2024

#JamiiForums #MotherLanguageDay2024
👍6
Siku ya #Lugha ya Kiingereza Duniani (World English Language Day) ilianzishwa na #UNESCO kwa lengo la kusherehekea Umuhimu wa Kiingereza kama mojawapo ya Lugha za Kimataifa zinazotumiwa Duniani kote

Lengo la Siku hii ni kukuza uelewa wa umuhimu wa Lugha za kimataifa na kuzisherehekea kama chombo cha #Mawasiliano na kujenga Tamaduni.

Neno gani la Kiingereza ni Mtihani kwako kulitamka vizuri?

Mjadala zaidi https://jamii.app/WorldEnglishDay2024

#JamiiForums #WorldEnglishLanguageDay
1👍1