JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UNAUMIZWA NA MAMBO YALIYOPITA? FANYA YAFUATAYO (SEHEMU 1)

- Jifunze kusamehe na kusahau, kutokuwa tayari kusamehe kutakufanya uendelee kuumizwa na mambo yaliyopita na kushindwa kuendelea na maisha yako

- Jiruhusu kusikia maumivu, linapokukuta jambo la kuumiza kama kufiwa ni vyema ukaruhusu maumivu kwa wakati ule ili yaishe kutofanya hivyo kutasababisha uumie kwa muda mrefu zaidi

#JamiiForums #Msongo
UNAUMIZWA NA MAMBO YALIYOPITA? FANYA YAFUATAYO (SEHEMU 2)

- Kubaliana na hali halisi acha kutamani mambo yawe kama yalivyokuwa awali

- Usijilaumu sana unapofanya makosa, tumia hiyo kama nafasi ya kujifunza

#JamiiForums #Msongo
BULAYA: FIDIA YA WANAOHARIBIWA MALI NA WANYAMAPORI NI NDOGO. KUNA DOUBLE STANDARD

- Amesema kumekuwa na 'Double Standard' ambapo mifugo inapoingia hifadhini fidia kubwa hotozwa lakini wanyamapori wanapoharibu mali za wananchi fidia yake ni kidogo

Soma > https://jamii.app/BulayaBungeni
UCL: REAL MADRID KUKABILIANA NA CHELSEA NUSU FAINALI

- Real Madrid itakuwa nyumbani kuialika Chelsea katika dimba la Estadio Alfredo Di Stefano, majira ya saa 4:00 usiku

- Katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya timu hizo zimekutana mara 3, Chelsea imeshinda michezo 2 na kutoka sare mchezo mmoja

#JamiiForums #JFSports
MAANDAMANO YA KUPINGA UTAWALA WA JESHI YAIBUKA CHAD

- Waandamanaji wanataka Utawala wa Kiraia kurejeshwa kufuatia kifo cha Rais Deby

- Baadhi ya Wapinzani wameita kitendo cha Jeshi kuchukua madaraka kuwa Mapinduzi na kuwataka Wananchi kuandamana

Soma > https://jamii.app/ChadProtests
MBEYA: MIILI NA KICHWA VYAOKOTWA KWENYE HIFADHI

> Polisi Wilayani Mbarali wamethibitisha kuokota miili miwili na kichwa ktk Hifadhi ya Taifa ya Ruaha

> Aidha, imetaarifiwa kuna Familia zinadai ndugu zao wanne kutoonekana kwa siku kadhaa

Soma - https://jamii.app/MiiliVichwaRuaha
NDUGAI AHOJI KWANINI FEDHA ZINAKWAMA WIZARANI

- Spika wa Bunge, Job Ndugai amehoji kwanini Fedha zinazokuja kwa ajili ya Mazingira zinakwama Wizara ya Fedha

- Amtaka Waziri kujiandaa akisema, "Siku ya Wizara yake nitakamata Shilingi mimi mwenyewe"

Soma https://jamii.app/SpikaWizaraFedha
VPL: SIMBA YAENDELEA KUJIKITA KILELENI MWA MSIMAMO WA LIGI

- Simba imeendelea kujitengenezea nafasi nzuri kileleni mwa Msimamo wa Ligi Kuu baada ya kuitandika Dodoma Jiji goli 3-1

- Magoli ya Simba yamefungwa na C. Mugalu 8' 68', L. Miquissone 56' huku goli la Dodoma Jiji likifungwa na C. Mkangala 29'

- Kwa matokeo hayo Simba inafikisha alama 61 ikiwa ni alama 4 juu ya Yanga inayoshika nafasi ya pili kwa alama 57

#JamiiForums #JFSports
UCL: CHELSEA YATOSHANA NGUVU NA MADRID

Mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kati ya Real Madrid dhidi ya Chelsea umemalizika kwa sare ya 1-1
-
Mchezo wa marudiano utapigwa Jumatano ijayo ya tarehe 5 Mei 2021 katika Dimba la Stamford Bridge

#JamiiForums #JFSports #UEFA
MHADHIRI TUDARCo ADAI FIDIA KWA KUWEKEWA MAZINGIRA MAGUMU ILI AACHISHWE KAZI

> Dkt. Kamanija amefungua kesi ya madai Baraza la Usuluhishi wa Migogoro ya Kazi akidai fidia ya Tsh. Milioni 130

> Kamanjina ni kati ya Waanzilishi wa Kitivo cha Sheria

Soma https://jamii.app/MizengweKazini
BURKINA FASO: WAANDISHI WAWILI WA HISPANIA WAUAWA

- Wanahabari hao walitekwa nyara karibu na eneo la Hifadhi ya asili Mashariki mwa Burkina Faso

- Vyombo vya Usalama vimesema raia wa #Ireland pia ameuawa ingawa hilo halijathibitishwa rasmi

Soma - https://jamii.app/WaandishiBurkinaFaso
WHO: WIMBI LA MAAMBUKIZI INDIA NI MATOKEO YA MIKUSANYIKO

- Shirika la Afya limesema wimbi hilo ni matokeo ya mikusanyiko ya watu, viwango vidogo vya Chanjo na uwepo wa aina mpya za Virusi

- Visa 17,997,267 vya Corona vimerekodiwa na vifo ni 201,187

Soma https://jamii.app/WHOCoronaIndia
SERIKALI YATENGA BILIONI 2 KAMA FIDIA KWA WATAKAOVAMIWA NA WANYAMAPORI

- Serikali imesema itawafidiwa Wananchi kulingana na uharibifu utakaojitokeza

> Matukio ya uvamizi wa Wanyamapori yamekuwa yakiripotiwa katika maeneo mbalimbali Nchini

Soma - https://jamii.app/Bilioni2Fidia
SOMALIA: RAIS ATOA RAI YA KUFANYIKA UCHAGUZI BAADA YA KUONGEZEWA MUDA MADARAKANI

-
Kitendo cha Wabunge kumuongezea Rais miaka 2 kiliibua sintofahamu huku Mataifa yakitishia vikwazo

- Kumekuwa na mvutano tangu Februari baada ya muda wa Rais kumalizika

Soma - https://jamii.app/RaisUchaguziSomalia