JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: Ofisi ya Msajili wa Ndoa imeanza rasmi zoezi la kuchapisha taarifa za Wanandoa watarajiwa kama majina yao, picha pamoja na sehemu watakazofanyia harusi Mtandaoni kupitia tovuti ya Serikali ya eCitizen

Kabla ya utaratibu huu mpya wa kuweka taarifa Mtandaoni, Wanandoa walitakiwa kuwasilisha Notisi ya Ndoa (Notice of Marriage) ambayo ilikuwa inabandikwa kwa siku 21 katika mlango wa Ofisi ya Msajili wa Ndoa, ili kutoa fursa kwa yeyote mwenye pingamizi la Kisheria kuwasilisha malalamiko yake

Wakati lengo la hatua hiyo limetajwa kuwa ni kuongeza uwazi na kurahisisha huduma kwa Wanandoa, baadhi ya Wakenya kupitia Mitandao ya Kijamii walilalamika, wakidai hatua hiyo inakiuka Sheria inayolinda Taarifa Binafsi za Wananchi kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya Kenya

Kupata taarifa zaidi soma https://jamii.app/MsajiliKenya

#JamiiAfrica #JamiiForums #DataPrivacy #DigitalRights #UlinziWaTaarifaBinafsi
1
Denmark itakuwa Nchi ya kwanza Ulaya kutoa Hakimiliki kwa raia wake juu ya matumizi ya Sura, miili na Sauti zao ili kukabiliana na video na sauti za kughushi "deepfakes" za Akili Unde zenye maudhui ya ngono, utapeli na propaganda za Kisiasa

Pendekezo hilo itamaanisha kuwa Mtu akichakachua au kutumia taarifa zako kutengeneza video, sauti au picha bandia bila ruhusa unaweza kudai ziondolowe na hata kulipwa fidia

Sheria hiyo inatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika rasmi kabla ya mwisho wa Mwaka 2025 na iwapo majukwaa ya #Teknolojia yatashindwa kuondoa maudhui yatakayoripotiwa yatakabiliwa na faini kubwa

Mdau unadhani Sheria kama hii inaweza kutumika kwa Nchi za Afrika?

Mjadala zaidi https://jamii.app/DenmarkFightsDeepfakes

#JamiiAfrica #JamiiForums #DataPrivacy #DataProtection #DigitalRights
👍21
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwenyekiti wa #CHADEMA, #TunduLissu amefika katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo kwa ajili ya shauri la maombi ya jinai ya kutaka Mahakama hiyo kufanya marejeo juu ya maombi ya Jamhuri kutaka kuficha mashahidi katika kesi ya Uchochezi inayomkabili ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Lissu anakabiliwa na kesi ya kuchapisha taarifa za uwongo katika Mtandao wa YouTube, kinyume na Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao Namba 14 ya Mwaka 2015.

‎Kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa ushahidi, upande wa mashtaka ulifungua maombi Mahakama ya Kisutu ukiomba mahakama iamuru baadhi ya mashahidi wake kutokuwekwa wazi wakati wakitoa ushahidi kwenye kesi hiyo wala taarifa za utambulisho wake kuwekwa wazi, upande wa Lissu ulipinga hilo.

Soma https://jamii.app/MashahidiKufichwaLissu

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio #CivilRights #DigitalRights
Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (#JAB) imewapiga marufuku Watangazaji wa Kipindi cha Genge la Gen Tok kinachorushwa na redio ya Mjini FM, kwa tuhuma za kukiuka haki za faragha na kumlazimisha aliyekuwa mgeni wao, Dogo Paten, kutoa Taarifa Binafsi bila ridhaa yake.

Bodi imewazuia Watangazaji wote wa kipindi hicho kujihusisha na kazi za habari kuanzia leo Julai 18, 2025 hadi watakapokamilisha matakwa ya Kisheria, yakiwemo kuwa na sifa za kitaaluma na kupata Ithibati ya Kitaaluma ya habari.

Uamuzi huo umetolewa siku mbili baada ya mahojiano kati ya Watangazaji hao na Dogo Paten, ambapo msanii huyo alikataa kujibu maswali kuhusu elimu yake, kitendo kilichosababisha baadhi yao kutoa kauli zilizotafsiriwa na wengi kama kejeli.

Soma zaidi https://jamii.app/BodiYaIthibatiWatangazaji

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #DataPrivacy #DigitalRights
👍1
ARUSHA: Waendeshaji Akaunti ya Mtandaoni ya “Wachokonozi”, Jackson Kabalo na Joseph Mrindoko leo Julai 21, 2025 wameachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha baada ya upande wa Jamhuri kueleza haupo tayari kuendelea na shauri hilo kwa sababu ambazo hawakuziweka wazi.

Mara baada ya kuachiwa huru, walikamatwa tena na kupelekwa Mahakama ya Wilaya ya Meru, wakasomewa upya mashtaka yaleyale ya awali. Baada ya Hakimu kusikiliza hoja za pande zote, ameitaka Jamhuri kukamilisha upelelezi kabla ya Agosti 13, 2025 ambapo shauri litasikilizwa.

Watuhumiwa wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ambapo wanatuhumiwa kuchapisha taarifa za uongo kwa njia ya Mtandao na kutoa maudhui Mtandaoni bila kuwa na leseni.

Zaidi soma https://jamii.app/WachokoziWaachiwaWakamatwa

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio #DigitalRights #CivilRights
Tafiti iliyofanyika nchini Marekani inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya Vijana wanatumia Akili Unde (Artificial Intelligence -#AI) kwa ushauri wa mahusiano, kama rafiki wa karibu zaidi ya Uhalisia na Msaada kitaaluma.

Ripoti mpya kutoka Shirika la Common Sense Media 2025 inaonyesha zaidi 70% ya Vijana tayari wametumia #AI kama rafiki, huku nusu yao wakiitumia mara kwa mara, takriban 31% wamesema mazungumzo yao na AI yanaridhisha hata zaidi ya yale na marafiki wa kweli. Sababu kubwa ni AI hupatikana muda wote, haikuhukumu na hujibu kihisia, ikitoa hisia ya kuwa na rafiki wa karibu.

Aidha, ripoti hiyo inashauri kuwe na uangalizi zaidi na kuwahimiza Vijana kujenga 'mahusiano' halisi badala ya kutegemea marafiki wa Kidijitali (AI).

Je, Vijana wanabadilisha mahusiano ya kweli na ya Kibinadamu kuwa bandia?

Soma zaidi https://jamii.app/VijanaAkiliUnde

#JamiiAfrica #JamiiForums #Elimu #DigitalRights #JFDigitali
3🔥1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ZANZIBAR: Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (#PDPC), Innocent Mungy ameeleza umuhimu wa Tume kusimamia ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa kusema "Tunalinda zisiende kwenye mikono isiyo sawa, isiyoruhusiwa kuwa na matumizi ya hizo taarifa."

Ameeleza hayo wakati wa mafunzo maalum Julai19, 2025, yakihusisha Maafisa Habari wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC).

Soma zaidi https://jamii.app/PDPCTaarifaBinafsi

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #PersonalDataProtection #DataPrivacy #DigitalRights
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ZANZIBAR: Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Khalid Salumu Mohamed amesema "Zamani taarifa tulikuwa tunatunza kwenye makaratasi hivyo zilikuwa hazisambai kwa kasi lakini sasa hivi kuna ukuaji wa Teknolojia ya kisasa, taarifa zinasambaa haraka sana."

Ameyasema hayo wakati akifungua rasmi mafunzo ya Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa Maafisa Habari na Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Zanzibar, Julai 19, 2025.

Soma https://jamii.app/TuweMakiniUlinziFaragha

#JamiiForums #JamiiAfrica #DataProtection #DataPrivacy #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (#CCM), Amos Makalla ametangaza kuwa kesho Julai 26, 2025 wanatarajia kufanya Mkutano Mkuu Maalum wa #CCM Taifa ambao utatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu Halmashauri Kuu Taifa kupitia njia ya Mtandao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Julai 25, 2025 ameeleza ajenda kuu ya kikao ni Marekebisho Madogo ya Katiba huku akiweka bayana kuhusiana na tetesi zinazoendelea kwenye Mitandao ya kijamii juu ya uwepo wa mkutano huo, kwamba kwa sasa maandalizi yake yamekamilika katika ngazi zote za wilaya na Mikoa.

Soma zaidi https://jamii.app/MkutanoCCM

#JamiiAfrica #JamiiForums #DigitalRights #Uchaguzi2025 #Siasa #Democracy
1
Akiandika kupitia akaunti yake ndani ya JamiiForums.com, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amewataka baadhi ya Wababa wajitafakari kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ya malezi.

Amesema "Tunzeni Watoto wenu tafadhali. Unakuta Wababa wengine mmejaaliwa afya njema kabisa, kazi ya heshima ofisi ya umma au binafsi tena na cheo juu, wengine na biashara za kipato kabisa, kutwa mashtaka ya kutotunza Watoto, watoto wanalia na kujuta."

Gwajima anahoji "Hivi kweli tuanze kuwatuma Maafisa Ustawi wa Jamii huko ofisini kwenu na mwisho mabosi wenu wajue, halafu mje mtulaumu? Wengine mnapelekwa Mahakamani na hukumu ikitoka hamtekelezi hadi mivutano."

Soma zaidi https://jamii.app/WababaKutelekezaWatoto

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #DigitalRights #Accountability #Maisha #ChildRights #Malezi