JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Aliyekuwa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA), James Mbowe akizungumzia kuhusu uamuzi wake wa kuhamia Chama cha Ukombozi wa Umma (#CHAUMMA) Agosti 6, 2025, pia amesema yule ambaye aliahidi kumsaidia Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, yaani Godbless Lema, kwa sasa yupo Nchini #Canada na familia yake.

Soma https://jamii.app/JamesMbowe

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFSiasa #JFMatukio #UchaguziMkuu2025
😁2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Simon Mayeka amezungumzia kitendo cha baadhi ya Watu kuonekana wakishangilia taarifa za kifo cha aliyewahi kuwa Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Yustino Ndugai, kwamba kitendo hicho kimewashangaza wengi.

Amesema hayo akiwa msibani nje ya nyumba ya marehemu Ndugai, eneo la Njedengwa na kuongeza “Baada ya kumpumzisha ndugu yetu, tutakwenda kuongea na vijana wale kuonesha kwamba ule sio ustaarabu wa Kitanzania na ni utamaduni ambao hatujawahi kuuona Tanzania.”

Soma https://jamii.app/DCKongwa

#JamiiForums #JFMatukio #JamiiAfrica
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
MBEYA: Agosti 7, 2025, usafiri wa magari ya abiria kutoka Jiji la Mbeya kuelekea Wilaya ya Kyela ulitatizika kwa saa kadhaa baada ya madereva wa gari za abiri kugoma wakipinga faini kubwa, usumbufu na manyanyaso wanayopata kutoka kwa baadhi ya maafisa wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (#LATRA).

Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Mbeya na Kyela, George Aziz Mwankejela amesema walikubali kurejea kazini baada ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Solomon Itunda kuwaomba warejee kwenye kazi na kuahidi kufuatilia kwa karibu changamoto walizowasilisha ili zipatiwe ufumbuzi wa kudumu.

Soma zaidi https://jamii.app/MaderevaKyela

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #JFHuduma #JFMatukio
2
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Akizungumza kwenye ibada ya mazishi ya mwili wa Spika Mstaafu Job Yustino Ndugai, leo Agosti 10, 2025 kwenye Viwanja vya Bunge, Spika Tulia amegusia kauli za baadhi ya Watu waliomkebehi na kutoa maneno yalioumiza familia ya Hayati Ndugai.

Amesema Watu wengi wanaelewa kazi kubwa aliyoifanya Ndugai kwenye utumishi wake kuliko wale wanaomkashifu na kusema mambo yasiyopendeza.

Kushiriki kwenye mjadala bofya https://jamii.app/TuliaMsibaNdugai

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio #RIPNdugai
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
KATAVI: Wakulima wa zao la tumbaku kutoka Chama Cha Msingi Cha Ushirika Cha Wakulima wa Tumbaku Mpanda Kati, Manispaa ya Mpanda wamelalamika kutolipwa fedha zao licha ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kutoa maagizo kuwa kabla ya Sikukuu ya Nanenane Wakulima wote wawe wamelipwa.

Wakulima hao wamefika Ofisi ya Chama hicho kufikisha malalamiko yao ambapo pia wamesema kuna nyongeza ya makato ya fedha ya 3% kinyume na utaratibu wa vikao.

Akijibu madai hayo Meneja wa Chama hicho, Zaituni Tembo amekiri Wakulima hao kutolipwa na kufafanua kuwa makato wanayosema ni makubaliano ya Bima ya Mkopo kutoka Benki ya NMB ambayo waliafikiana katika vikao vya Wakulima tofauti na benki waliyokuwa wakifanya nayo kazi awali.

Zaidi soma https://jamii.app/MpandaKati

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio #JFEconomy #Accountability
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Hali ilivyokuwa leo Agosti 12, 2025 wakati wa usikilizwaji wa kesi inayomhusu Mwenyekiti wa #CHADEMA, #TunduLissu katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo, Dar es Salaam, ambapo baadhi ya Askari magereza walionekana wakiwa wanaimarisha ulinzi.

Zaidi Soma https://jamii.app/MaaskariKuvaaKininja

#JamiiAfrica #JamiiForums #HakiZaBinadamu #Utawala #JFMatukio
2
DAR: Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA, #TunduLissu inaendelea leo Agosti 13, 2025 ambapo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franco Kiswaga anatarajiwa kutoa uamuzi wa hoja zilizowasilishwa na pande mbili katika kesi hiyo.

Uamuzi huo unasomwa baada ya upande wa Lissu kupinga ombi la Jamhuri la kuahirisha mara kwa mara shauri hilo bila kuchukua uamuzi wa kulipeleka Mahakama Kuu endapo wana nia ya kuendelea nalo.

Ikumbukwe kuwa Mahakama Kuu – Masijala ya Dar es Salaam, Agosti 4, 2025, ilikubali ombi la upande wa Jamhuri la kuficha majina na taarifa nyingine za mashahidi wa upande wa mashtaka katika kesi ya uhaini inayomkabili Lissu.

Zaidi https://jamii.app/LissuUhainiKusikilizwaLeo

#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights #JFMatukio #HumanRights
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
ZANZIBAR: Wananchi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mjini Mkoani Mjini Magharibi ikiwemo Jang'ombe Lofi, Michenzani na Kisonge wamebomolewa na kuvunjiwa Vibanda, Maduka yao na sehemu za biashara na Watendaji wa Baraza la Manispaa la Mjini.

Aidha, Mkurugenzi Baraza la Manispaa Mjini, Hassanat Attai Masoud akitolea ufafanuzi wa uamuzi huo Agosti 12, 2025 amesema Wananchi hao wamepewa taarifa muda kuhusu maeneo waliyojenga bila ya ruhusa na kuzidi katika eneo la barabara na kuacha kufanya biashara katika maeneo ambayo hayajaruhusiwa.

Soma zaidi https://jamii.app/BomoaBomoaZanzibar

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMatukio #Governance
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) akivutana na Askari Polisi katika Mahakama ya Kisutu kabla ya kuanza kwa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, #TunduLissu, inayoendelea leo Agosti 13, 2025.

Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/MvutanoPolisiKisutu

#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights #JFMatukio #HumanRights
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Kabla ya kuanza kutajwa kwa Shauri la Uhaini linalomhusu Mwenyekiti wa #CHADEMA, #TunduLissu, leo Agosti 13, 2025 kumetokea hali ya mvutano kati ya Mwandishi wa Habari na baadhi ya Askari Polisi wakati wa kuingia katika Mahakama ya Kisutu, baadaye Mwandishi huyo aliruhusiwa kuingia.

Zaidi soma https://jamii.app/MwandishiKisutu

#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMatukio
2🔥1