JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa #CHADEMA, #TunduLissu inaendelea leo Agosti 13, 2025 ambapo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franco Kiswaga anatarajiwa kutoa uamuzi wa hoja zilizowasilishwa na pande mbili katika kesi hiyo.

Uamuzi huo unasomwa baada ya upande wa Lissu kupinga ombi la Jamhuri la kuahirisha mara kwa mara shauri hilo bila kuchukua uamuzi wa kulipeleka Mahakama Kuu endapo wana nia ya kuendelea nalo.

Ikumbukwe kuwa Mahakama Kuu – Masijala ya Dar es Salaam, Agosti 4, 2025, ilikubali ombi la upande wa Jamhuri la kuficha majina na taarifa nyingine za mashahidi wa upande wa mashtaka katika kesi ya uhaini inayomkabili Lissu.

Zaidi https://jamii.app/LissuUhainiKusikilizwaLeo

#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights #JFMatukio #HumanRights
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) akivutana na Askari Polisi katika Mahakama ya Kisutu kabla ya kuanza kwa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, #TunduLissu, inayoendelea leo Agosti 13, 2025.

Kushiriki mjadala bofya https://jamii.app/MvutanoPolisiKisutu

#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights #JFMatukio #HumanRights
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga ametoa ombi kuwa kesi ya uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, #TunduLissu inayoendelea katika Mahakama ya Kisutu isiendelee kuonyeshwa mubashara (LIVE) kupitia Vyombo vya Habari ili kulinda mashahidi, amesema hayo leo Agosti 13, 2025 wakati wa mchakato wa kesi ulipokuwa ukiendelea.

Soma zaidi https://jamii.app/LissuUhainiKusikilizwaLeo

#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights #JFMatukio #HumanRights
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franco Kiswaga ameahirisha kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA), Tundu Lissu, hadi Agosti 18, 2025, ili kutoa amri kuhusu ombi na pingamizi la urushaji wa moja kwa moja wa mwenendo wa shauri hilo.

Uamuzi huo umefuata baada ya upande wa Jamhuri kuomba kesi hiyo isirushwe mubashara kwa lengo la kulinda utambulisho wa mashahidi raia, ombi ambalo limepingwa na upande wa utetezi.

Zaidi soma https://jamii.app/KesiLissuYasogezwaMbeleTena

#JamiiForums #JamiiAfrica #CivilRights #JFMatukio #HumanRights
2
GEITA: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Jeshi la Polisi kuchunguza tukio analodai limetokea katika Hifadhi ya Msitu Kigosi, akidai kijana mwenye umri wa Miaka 20+ ameuawa kwa kupigwa risasi na Askari wa Hifadhi, jana Agosti 13, 2025.

Anadai Familia ya marehemu ilitoa taarifa Polisi ambao walifika na kuuchukua mwili huo kisha wakaambiwa wakauchukue mwili leo Agosti 13, 2025 kwa ajili ya mazishi lakini familia haitaki kufanya hivyo hadi itakapopewa majibu juu ya hatua zilizochukuliwa.

Alipotafutwa Meneja Uhusiano wa TFS, Johary Kachwamba amesema “Tumepata taarifa kuhusu tukio hilo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inafanya kikao leo (Agosti 14, 2025) itajadili kubaini ukweli wake, kukiwa na taarifa zaidi tutatoa mrejesho.”

Jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Safia Jongo zinaendelea.

Soma zaidi https://jamii.app/KijanaAuawaGeita

#JamiiForums #JamiiAfrica #Accoutability #Governance #HumanRights #CivilRights #JFMdau2025
Kauli za Chuki si maoni ya kawaida wala sio kigezo cha Uhuru wa kujieleza.

Ni kauli zinazoweza kuharibu Heshima ya Mtu, kuathiri Afya ya Akili na kuleta taharuki kwenye Jamii.

Je, umewahi kukutana na kauli za chuki zinazokuhusu mtandaoni? Ulijisikiaje na ulichukua hatua gani?

Tembelea Jukwaa la JamiiForums.com kushiriki katika mijadala mingine.

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #KauliZaChuki #StopHateSpeech #DigitalPeace #NoToHateSpeech #ResponsiblePosting #JamiiYenyeUelewa
2
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema kimepokea taarifa kutoka kwa Wananchi wa Wilaya ya Mkuranga - Pwani kuhusu kushikiliwa kwa Vijana wanne kwa zaidi ya siku 26 bila kufikishwa Mahakamani au kupewa haki yao ya dhamana kwa makosa ambayo yana dhamana Kisheria.

Taarifa ya LHRC iliyotolewa leo Agosti 15, 2025 imesema inatoa wito kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mkuranga kuhakikisha vijana wote wanaoshikiliwa wanaachiliwa bila masharti yoyote na kama kuna tuhuma za kijinai dhidi yao wafikishwe Mahakamani kwa mujibu wa Sheria.

Pia, LHRC imeeleza “Ibara ya 13(6) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema ni marufuku kwa Mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama Mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo.

Soma zaidi https://jamii.app/LHRCAgosti15

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #Governance
1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Akizungumza leo Agosti 15, 2025 Askofu Gwajima amesema kuwa Mwenyekiti wa #CHADEMA Tundu Lissu kuendelea kukaa Magereza sio picha nzuri.

Zaidi https://jamii.app/LissuMagerezaPichaMbaya

#JamiiForums #JamiiAfrica #HumanRights #Governance #KuelekeaUchaguzi2025
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Aliyekuwa Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima akizungumza kwa njia ya Mtandao, leo Agosti 15, 2025 ameomba mamlaka zifungulie Makanisa ya Ufufuo na Uzima nchini kote na kutoa tahadhari kwamba yasipofunguliwa ndani ya siku 10 atarudi tena na kutoa neno ambalo Watu watastaajabu.

Soma Zaidi https://jamii.app/GwajimaKujipendekeza

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #HakiZaBinadamu
1
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Aliyekuwa Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima akizungumza kwa njia ya Mtandao, leo Agosti 15, 2025 amehoji kuhusu jaribio la kumuua Padre Fr. Kitima, akidai mpaka sasa hakuna aliyefikishwa Mahakamani.

Soma zaidi https://jamii.app/JaribioKitimaGwajima

#JamiiAfrica #JamiiForums #HumanRights #HakiZaBinadamu