JamiiForums
βœ”
54K subscribers
34.1K photos
2.27K videos
31K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 Kifungu cha 37, inaeleza mhusika wa taarifa ana Haki ya kulipwa fidia kutoka kwa mkusanyaji au mchakataji wa Taarifa iwapo atapata madhara kwa sababu za ukiukwaji wa masharti ya Sheria hiyo

Endapo Tume itajiridhisha na maombi ya mhusika wa taarifa kuwa amepata madhara katika mazingira yanayompatia haki ya kulipwa fidia inaweza kuamuru kurekebishwa, kuzuiwa, kufutwa au kuharibiwa kwa taarifa hizo.

Soma: https://jamii.app/SheriaTaarifaBinafsi2022

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
Kumbuka kulinda taarifa zako na usikubali kuziweka wazi au kumpa mtu mwingine bila kujua lengo na matumizi ya taarifa zako

Usipolinda taarifa zako zinaweza kutumika katika Matukio ya Uhalifu kama vile Uwizi na Utapeli wa Mtandaoni

Mjadala zaidi https://jamii.app/PrivacyIsPower

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya 2022 Kifungu cha 61 inaeleza Mtu kuharibu, kufuta, kupotosha, kuficha au kubadilisha Taarifa Binafsi kinyume na Sheria ni kosa

Endapo atakapotiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua Tsh. 100,000 na isiyozidi Tsh. Milioni 10 au kifungo kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja

Soma: https://jamii.app/SheriaTaarifaBinafsi2022

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa na Indo-Pacific Center for Civil Society Resilience, jumla ya Nchi 7 katika Bara la Asia na Oceania (Indo - Pacific region) zilipitia changamoto ya kuzimwa kwa mtandao na kuminywa kwa Uhuru wa Kujieleza Mtandaoni

Nchi zilizofanyiwa Utafiti ni Cambodia, Fiji, Malaysia, Pakistan, Sri Lanka, Taiwan na Thailand

Baadhi ya matukio yaliyojitokeza ni pamoja na ukusanyaji wa Taarifa Binafsi za Watu Mitandaoni, Gharama kubwa za Kanuni za Usalama wa Mtandao na kupelekea kuminywa kwa Uhuru wa Utumiaji Mtandao

Soma https://jamii.app/DigitalThreatsIndoPacific

#DigitalThreats #DigitalSecurity #DataPrivacy #DataProtection #IndoPacificRegion
πŸ‘1
MOROGORO: Wateja wa Nyumba za Wageni wamejulishwa kuwa hawatakiwi kuandika taarifa za wanapotoka au wanapoelekea katika Vitabu vya nyumba hizo, kwa kuwa kufanya hivyo ni kukiuka Sheria ya Taarifa Binafsi

Mkurugenzi wa Usajili na Uzingatiaji wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa (#PDPC), Stephen Wangwe amesema Watu wanatakiwa kujua Sheria ya #TaarifaBinafsi ili wasiingie matatizoni, kwa kuwa taarifa hizi hazina uhusiano na wao kufika katika nyumba hizo

Aidha, amesema tangu kuanza kutumika kwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, mtu anapoona taarifa zake zimetumika bila ridhaa yake anaruhusiwa kulalamika kisha hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika au mhusika

Soma https://jamii.app/PDPCMarch1

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
πŸ‘2
MOROGORO: Washereheshaji wenye tabia ya kusambaza picha za Watu kama hawajapata idhini ya wahusika au mhusika wametakiwa kuwa makini kwa kuwa kufanya hivyo wanavunja Sheria

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Dkt. Emmanuel Mkilia akishiriki Warsha kuhusu dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi amesema kuna baadhi ya mambo ambayo yanafanywa na mtu au Watu na hawataki yasambazwe kwa kuwa kufanya hivyo ni kuingilia faragha ya mtu

Anaseme β€œUnakuta umeenda kwenye sherehe, wale MC wanakupiga picha mnato au video baadaye unaonekana Mtandaoni ukiwa umejiachia, ni muhimu kupata ridhaa ya Mtu kabla ya kutumia taarifa zake kama jina, picha, namba za simu, makazi, anuani, taarifa za kifedha na afya.”

Soma https://jamii.app/TaarifaBinafsiSheria

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
πŸ‘3
Ripoti ya Freedom House na Article 19 inaonesha wasiwasi miongoni mwa Wananchi juu ya juhudi za Serikali kudhibiti nafasi ya Kidijitali ambapo ilidhihirishwa na amri ndogo ya awali ya kuanzishwa kwa Lango la Mtandao la Kitaifa (National Internet Gateway - NIG)

Japo utekelezaji wa NIG uliopangwa kuanza Februari 16, 2022, ulizuiwa, Wananchi wanahofia kwani NIG ingekusanya Taarifa za Mtandao, kuwa na mamlaka ya kuzima mtandao, kuhifadhi taarifa kwa mwaka mmoja na kuzitoa kwa mamlaka inapohitajika, na Watoa Huduma wa Mawasiliano wasiotii wangepewa adhabu kali.

Soma https://jamii.app/DigitalThreatsIndoPacific

#DigitalThreats #DigitalSecurity #DataPrivacy #DataProtection #IndoPacificRegion #DigitalThreats
πŸ‘1
Mashirika, Taasisi na Watu Binafsi wametakiwa kuwa makini wanapotumia Taarifa Binafsi za Watu, kwani kufanya hivyo bila idhini ya mhusika au Wahusika ni kinyume cha Sheria na adhabu yake kwa Mchakataji wa Taarifa (Mtu au Taasisi) inaweza kufika hadi Faini ya Tsh. Milioni 100

Mkurugenzi wa Tafiti za Ulinzi wa Taarifa na Teknolojia wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Dkt. Noe Nnko amesema faini hiyo ipo Kipengele cha 47 cha Faini za Kiutawala kinachoeleza Tume inaweza kuchukua hatua ya kutoza faini na kiwango cha juu hicho.”

Ameongeza "Taasisi zinapaswa kuwa na Afisa wa Taarifa Binafsi aliyefundishwa kutunza taarifa za Watu kwa usahihi. Mbali na faini pia kuna fidia kwa mwathirika itakayopimwa kulingana na madhara atakayopata ya kifaragha.”

Soma https://jamii.app/FineDataPrivacy

#JamiiForums #DataProtection #UlinziWaTaarifaBinafsi #UlinziWaFaragha #DataPrivacy #DigitalRights #TaarifaZakoMaishaYako
πŸ‘2❀1
Ripoti ya Freedom House na Article 19 inaonesha wasiwasi miongoni mwa Wananchi wa Malaysia juu ya juhudi za Serikali kudhibiti nafasi ya Kidigitali na kuzuia Uhuru wa Kujieleza hasa kwa Waandishi wa Habari ilidhihirishwa na Muswada wa Usalama Mtandaoni wa Mwaka 2024

Kupitia mradi wa 'Sinar' ambalo ni shirika lisilo la Kiserikali waligundua madhara yatakayojitokeza na kuchapisha ripoti za kimataifa ambazo zilichochea uhamasishaji nchini humo ambapo Wataalamu wa IT na wajasiriamali waliwasilisha pingamizi juu ya mabadiliko ya Muswada huo kwa Serikali

Soma https://jamii.app/DigitalThreatsIndoPacific

#DigitalThreats #DigitalSecurity #DataPrivacy #DataProtection #IndoPacificRegion #DigitalThreats