JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa na Indo-Pacific Center for Civil Society Resilience, jumla ya Nchi 7 katika Bara la Asia na Oceania (Indo - Pacific region) zilipitia changamoto ya kuzimwa kwa mtandao na kuminywa kwa Uhuru wa Kujieleza Mtandaoni

Nchi zilizofanyiwa Utafiti ni Cambodia, Fiji, Malaysia, Pakistan, Sri Lanka, Taiwan na Thailand

Baadhi ya matukio yaliyojitokeza ni pamoja na ukusanyaji wa Taarifa Binafsi za Watu Mitandaoni, Gharama kubwa za Kanuni za Usalama wa Mtandao na kupelekea kuminywa kwa Uhuru wa Utumiaji Mtandao

Soma https://jamii.app/DigitalThreatsIndoPacific

#DigitalThreats #DigitalSecurity #DataPrivacy #DataProtection #IndoPacificRegion
👍1
Ripoti ya Freedom House na Article 19 inaonesha wasiwasi miongoni mwa Wananchi juu ya juhudi za Serikali kudhibiti nafasi ya Kidijitali ambapo ilidhihirishwa na amri ndogo ya awali ya kuanzishwa kwa Lango la Mtandao la Kitaifa (National Internet Gateway - NIG)

Japo utekelezaji wa NIG uliopangwa kuanza Februari 16, 2022, ulizuiwa, Wananchi wanahofia kwani NIG ingekusanya Taarifa za Mtandao, kuwa na mamlaka ya kuzima mtandao, kuhifadhi taarifa kwa mwaka mmoja na kuzitoa kwa mamlaka inapohitajika, na Watoa Huduma wa Mawasiliano wasiotii wangepewa adhabu kali.

Soma https://jamii.app/DigitalThreatsIndoPacific

#DigitalThreats #DigitalSecurity #DataPrivacy #DataProtection #IndoPacificRegion #DigitalThreats
👍1
Ripoti ya Freedom House na Article 19 inaonesha wasiwasi miongoni mwa Wananchi wa Malaysia juu ya juhudi za Serikali kudhibiti nafasi ya Kidigitali na kuzuia Uhuru wa Kujieleza hasa kwa Waandishi wa Habari ilidhihirishwa na Muswada wa Usalama Mtandaoni wa Mwaka 2024

Kupitia mradi wa 'Sinar' ambalo ni shirika lisilo la Kiserikali waligundua madhara yatakayojitokeza na kuchapisha ripoti za kimataifa ambazo zilichochea uhamasishaji nchini humo ambapo Wataalamu wa IT na wajasiriamali waliwasilisha pingamizi juu ya mabadiliko ya Muswada huo kwa Serikali

Soma https://jamii.app/DigitalThreatsIndoPacific

#DigitalThreats #DigitalSecurity #DataPrivacy #DataProtection #IndoPacificRegion #DigitalThreats
Ripoti ya Freedom House na Article 19 inaonesha wasiwasi miongoni mwa Wananchi wa Pakistan juu ya juhudi za Serikali kwenye kudhibiti nafasi ya Kidigitali na kuzuia Uhuru wa Kujieleza Mtandaoni kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa 2024 kupitia Sheria ya Kuzuia Uhalifu wa Kidijitali (PECA) ya 2022

Kupitia jitihada za Shirikisho la Waandishi wa Habari la Pakistan (PFUJ) Mahakama Kuu ya Islamabad ilitangaza kuwa Sheria hiyo ni kinyume na Katiba na kuagiza Serikali ipitie tena Sheria ya Udhalilishaji ya 2002 na kufanya mapendekezo mapya

Soma https://jamii.app/DigitalThreatsIndoPacific

#DigitalThreats #DigitalSecurity #DataPrivacy #DataProtection #IndoPacificRegion #DigitalThreats
Ripoti ya Freedom House na Article 19 imeonesha wasiwasi miongoni mwa Wananchi wa Sri Lanka, juu ya juhudi za Serikali kwenye kuzuia Uhuru wa Kujieleza Mtandaoni kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa 2024, kupitia Sheria ya Usalama Mtandaoni (OSA) ya 2023

Sheria hii ilipingwa vikali kutokana na kutoa ruhusa ya Upatikanaji wa mifumo ya kompyuta na taarifa binafsi bila ridhaa ya mhusika

Kupitia jitihada za Vyama kama vile Asia Internet Coalition na Global Network Initiative na mashirika mengine ya ndani na nje ya Sri Lanka, Sheria hiyo ilifanyiwa mabadiliko

Soma https://jamii.app/DigitalThreatsIndoPacific

#DigitalThreats #DigitalSecurity #DataPrivacy #DataProtection #IndoPacificRegion #DigitalThreats
Ripoti ya Freedom House na Article 19 ilionesha wasiwasi miongoni mwa Wananchi wa Taiwan baada ya Wizara ya Mambo ya Ndani kuanzisha mpango wa kubadilisha vitambulisho vya Taifa kuwa vya Kidigitali

Mpango huo ulizua taharuki kutokana na hofu ya uvujaji na matumizi mabaya ya Taarifa Binafsi, pamoja na hatari ya uwezekano wa udukuzi wa Taarifa

Vikundi na Taasisi mbalimbali walishinikiza Serikali kuboresha ulinzi na matumizi ya Taarifa binafsi pamoja na kuanzisha Taasisi huru ya kulinda taarifa binafsi

Soma https://jamii.app/DigitalThreatsIndoPacific

#DigitalThreats #DigitalSecurity #DataPrivacy #DataProtection #IndoPacificRegion #DigitalThreats
Ripoti ya Freedom House na Article 19 imeonesha wasiwasi miongoni mwa Wananchi wa Thailand juu ya juhudi za Serikali kudhibiti Vyombo vya Habari na kuzuia mtandao kupitia Sera ya "Single Gateway"

Sera hii ilipingwa vikali na Asasi za Kiraia na Wadau wa Teknolojia, kutokana na kutoa ruhusa ya kukandamiza Uhuru wa Kujielezea, matumizi ya mtandao n.k, ambapo jitihada zao zilizaa matunda kwa kufanikiwa kuzuia Sera hiyo kupitishwa

Soma https://jamii.app/DigitalThreatsIndoPacific

#DigitalThreats #DigitalSecurity #DataPrivacy #DataProtection #IndoPacificRegion #DigitalThreats