Mdau wa JamiiForums.com kutoka Kijiji cha Kikunde Wilayani #Kilindi anadai wanufaika wa Mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (#TASAF) wanapata wakati mgumu kupata malipo yao hasa Wazee
Anadai Wazee wamekuwa wakitumikishwa kufanya kazi za kusafisha na kurekebisha Barabara za Mitaa ndio wanapata malipo. Anashauri Mamlaka za juu zifuatilie kinachoendelea katika mradi huo akidai waathirika wengi hawana sauti ya kueleza malalamiko yao
Soma https://jamii.app/TasafTanga
#JFUwajibikaji23 #JFHuduma #Governance

👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
WAZIRI SIMBACHAWENE: TUNAFUATILIA MADAI YA WANUFAIKA WA TASAF KUTOLIPWA
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (#TASAF) Wilaya ya #Moshi Mjini na Moshi Vijijini Mkoani #Kilimanjaro hawajalipwa stahiki zao tangu Desemba 2022, hoja hiyo imejadiliwa #Bungeni pia
Mbunge Shally Raymond ameuliza “Kaya za Kilimanjaro kuna Wanufaika wa TASAF ambao walipata ajira za muda lakini baada ya kutimiza majukumu hawajalipwa kwa vipindi viwili, je, ni lini Serikali itatoa malipo hayo?”
Akijibu hoja, Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Boniface Simbachawene amesema “Kwa kuwa hiyo ni taarifa, nimeisikia kutoka kwake, tunaenda kulifanyia kazi."
#JFUwajibikaji23 #Governance #JamiiForums

❤2👍1
TASAF: WANAOFANYA KAZI KWENYE MIRADI YA AJIRA ZA MUDA NI WENYE MIAKA 18 - 65
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umekiri kuchelewa kwa malipo kwa wanufaika lakini yameanza kutolewa sehemu zote Nchini kuanzia Juni 5, 2023
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha #TASAF, Zuhura Mdungi amesema "Malipo ya Serikali yapo tofauti na yale ya binafsi, kawaida huwa wanalipwa kila baada ya Miezi miwili. Pia, tutafungua ukurasa wetu ndani ya JamiiForums.com tuwe tunatoa taarifa na kujibu hoja za Wadau pindi kunapokuwa na uhitaji huo.”
Soma https://jamii.app/TASAFMalipo
#JFUwajibikaji23 #Governance

ARUSHA: Mdau wa JamiiForums.com amedai Mfuko wa Maendeleo ya Jamii wa Kunusuru Kaya Masikini #TASAF unawapatia Fedha Vijana wenye nguvu na kujiweza badala ya wahitaji ambao ni Wazee wasiojiweza, na Kaya Masikini
Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkirowa, Kata ya Lemara iliyopo Halmashauri ya Jiji la Arusha, Albert Joseph, amesema ni kweli suala hilo lipo Mtaani kwake na kudai amejaribu kulitafutia ufumbuzi kwa kushirikisha Mfuko huo lakini alijibiwa kuwa TASAF wana vigezo vyao
Pia, Diwani wa Kata ya #Lemara, Naboth Paulo Silasi, amesema tatizo kama hilo halipo kwenye Kata yake tu, bali ni sehemu kubwa ya #Arusha, ameona upendeleo katika utoaji wa Fedha hizo huku walengwa wakikosa
Soma https://jamii.app/ArushaTASAF
#JFHuduma #Accountability

👍3❤2👏2
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, ametoa Siku 30 za Uchunguzi kwa uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF), ili kubaini zilipo fedha zilizolipwa bila kuwafikia walengwa na kufahamu kiwango halisi cha fedha zilizopotea kwa mtindo huo
Ni baada ya Wadau wa JamiiForums.com kulalamikia uwepo wa Mazingira 'tata' ya ulipaji kwa wanufaika wa #TASAF, ambapo walidai kuwa malipo yanafanyika kwa wasio wanufaika halisi, katika Mikoa kadhaa Nchini ikiwemo #Arusha na #Tanga
Soma https://jamii.app/SimbachaweneTASAF
#SocialJustice #JFHuduma #JFUwajibikaji #KemeaRushwa #JamiiForums

❤1👍1
Katika usimamizi wa Matumizi kwa Mwaka wa fedha 2022/23, Ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ulibaini #TANROADS, #MOEST na TASAF hazikutoza kodi ya zuio yenye thamani ya Tsh. 1,118,230,367
Wakati huohuo #TASAF na TANROADS zilitoza kodi ya zuio lakini hazikuwasilishwa Mamlaka ya Mapato (TRA) kiasi cha Tsh. 5,216,572,492
Jumla ya kodi za zuio ambazo hazijatozwa na hazijawasilishwa TRA ni Tsh. 6,334,802,859.
Soma https://jamii.app/CAGMiradi24
#JamiiForums #RipotiYaCAG24 #Governance #RipotiUkaguziMiradi

👍3
Rais #SamiaSuluhuHassan amemteua Shedrack Salmin Mziray kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), awali alikuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani (TASAF)
Taarifa ya #TASAF imeeleza uteuzi huo ulianza Julai 3, 2024 licha ya taarifa kutolewa jana Julai 18, 2024 na kuwa Mziray alianza kukaimu nafasi aliyoteuliwa Julai 1, 2023 baada ya kustaafu kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji, Ladislaus Joseph Mwamanga
Moja ya changamoto atakazokutana nazo ni malalamiko kuhusu Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini wa TASAF ambao umekuwa ukilalamikiwa na Wadau wa JamiiForums.com kuwa utaratibu sio mzuri na hauwanufaishi walengwa
Soma https://jamii.app/ShedrackMziray
#Governance #JamiiForums #Accountability

Mdau wa JamiiForums.com amesema uamuzi wa Serikali kupeleka Mradi wa Kusaidia Kaya Masikini (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea ni mzuri, japokuwa changamoto kubwa ipo kwa wasimamizi wa mfuko ambao wamekuwa na utata kwa wanufaika
Mdau ameeleza kuna Watu ambao ikifika muda wao wa kwenda kuchukua fedha za #TASAF hawazipati na ukifika muda wa wao kwenda kuhoji pia hawapewi majibu ya kueleweka
Aidha, mdau ametoa wito kwa Viongozi wa juu wanaokwenda kufanya ziara wasiishie Ofisini, bali waitishe Mikutano ya hadhara na kuruhusu wanufaika wazungumze ili kusikia changamoto za mpango huo
Soma https://jamii.app/RuvumaTASAF
#JamiiForums #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability #Governance #Uwajibikaji
Mdau ameeleza kuna Watu ambao ikifika muda wao wa kwenda kuchukua fedha za #TASAF hawazipati na ukifika muda wa wao kwenda kuhoji pia hawapewi majibu ya kueleweka
Aidha, mdau ametoa wito kwa Viongozi wa juu wanaokwenda kufanya ziara wasiishie Ofisini, bali waitishe Mikutano ya hadhara na kuruhusu wanufaika wazungumze ili kusikia changamoto za mpango huo
Soma https://jamii.app/RuvumaTASAF
#JamiiForums #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability #Governance #Uwajibikaji
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
KILIMANJARO: Mtia nia wa Ubunge Jimbo la Moshi Vijijini kupitia #CCM, Felista Njau, amedai kuwa baadhi ya watendaji Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (#TASAF) wamekuwa wakipokea hongo na kuwapa msaada wasio walengwa. Akijinadi mbele ya wananchi, ameahidi kuhakikisha fedha hizo zinafika kwa walengwa halali endapo atachaguliwa.
Aidha, wadau mbalimbali wa JamiiForums.com kwa nyakati tofauti wamekuwa wakilalamikia ubabaishaji unaofanywa na TASAF, ikiwemo masharti magumu ya upatikanaji wa msaada, kufanyishwa kazi kabla ya malipo, na kuondolewa kwa walengwa halali kwa madai ya kujimudu.
Soma https://jamii.app/NjauTasaf
#JamiiAfrica #JamiiForums #Demokrasia #UchaguziMkuu2025

❤2